90) Sūrat Al-Balad

Printed format

90) سُورَة البَلَد

Lā 'Uqsimu Bihadhā Al-Baladi 1. Naapa kwa Mji huu! لاَ أُقْسِمُ بِهَذَا الْبَلَدِ
Wa 'Anta Ĥillun Bihadhā Al-Baladi 2. Nawe unaukaa Mji huu. وَأَنْتَ حِلّ ٌ بِهَذَا الْبَلَدِ
Wa Wālidin Wa Mā Walada 3. Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. وَوَالِد ٍ وَمَا وَلَدَ
Laqad Khalaq Al-'Insāna Fī Kabadin 4. Hakika tumemuumba mtu katika taabu. لَقَدْ خَلَقْنَا الإِنسَانَ فِي كَبَد ٍ
'Ayaĥsabu 'An Lan Yaqdira `Alayhi 'Aĥadun 5. Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? أَيَحْسَبُ أَنْ لَنْ يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَد ٌ
Yaqūlu 'Ahlaktu Mālāan Lubadāan 6. Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالا ً لُبَدا ً
'Ayaĥsabu 'An Lam Yarahu 'Aĥadun 7. Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? أَيَحْسَبُ أَنْ لَمْ يَرَهُ~ُ أَحَد ٌ
'Alam Naj`al Lahu `Aynayni 8. Kwani hatukumpa macho mawili? أَلَمْ نَجْعَلْ لَه ُُ عَيْنَيْنِ
Wa Lisānāan Wa Shafatayni 9. Na ulimi, na midomo miwili? وَلِسَانا ً وَشَفَتَيْنِ
Wa Hadaynāhu An-Najdayni 10. Na tukambainishia zote njia mbili? وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ
Falā Aqtaĥama Al-`Aqabaha 11. Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. فَلاَ اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ
Wa Mā 'Adrāka Mā Al-`Aqabahu 12. Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ
Fakku Raqabahin 13. Kumkomboa mtumwa; فَكُّ رَقَبَة ٍ
'Aw 'Iţ`āmun Fī Yawmin Dhī Masghabahin 14. Au kumlisha siku ya njaa أَوْ إِطْعَام ٌ فِي يَوْم ٍ ذِي مَسْغَبَة ٍ
Yatīmāan Dhā Maqrabahin 15. Yatima aliye jamaa, يَتِيما ً ذَا مَقْرَبَة ٍ
'Aw Miskīnāan Dhā Matrabahin 16. Au masikini aliye vumbini. أَوْ مِسْكِينا ً ذَا مَتْرَبَة ٍ
Thumma Kāna Mina Al-Ladhīna 'Āmanū Wa Tawāşaw Biş-Şabri Wa Tawāşaw Bil-Marĥamahi 17. Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ
'Ūlā'ika 'Aşĥābu Al-Maymanahi 18. Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. أُوْلَائِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ
Wa Al-Ladhīna Kafarū Bi'āyātinā Hum 'Aşĥābu Al-Mash'amahi 19. Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا هُمْ أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ
`Alayhim Nārun Mu'uşadahun 20. Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.  * عَلَيْهِمْ نَار ٌ مُؤصَدَة ٌ
Next Sūrah