88) Sūrat Al-Ghāshiyah

Printed format

88) سُورَة الْغَاشِيَه

Hal 'Atāka Ĥadīthu Al-Ghāshiyahi 1. Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza? هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ
Wujūhun Yawma'idhin Khāshi`ahun 2. Siku hiyo nyuso zitainama, وُجُوه ٌ ٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَة ٌ
`Āmilatun Nāşibahun 3. Zikifanya kazi, nazo taabani. عَامِلَة ٌ نَاصِبَة ٌ
Taşlá Nārāan Ĥāmiyahan 4. Ziingie katika Moto unao waka - تَصْلَى نَاراً حَامِيَة ً
Tusqá Min `Aynin 'Āniyahin 5. Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka. تُسْقَى مِنْ عَيْن ٍ آنِيَة ٍ
Laysa Lahum Ţa`āmun 'Illā Min Đarī`in 6. Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba. لَيْسَ لَهُمْ طَعَام ٌ إِلاَّ مِنْ ضَرِيع ٍ
Lā Yusminu Wa Lā Yughnī Min Jū`in 7. Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa. لاَ يُسْمِنُ وَلاَ يُغْنِي مِنْ جُوع ٍ
Wujūhun Yawma'idhin Nā`imahun 8. Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu. وُجُوه ٌ ٌ يَوْمَئِذ ٍ نَاعِمَة ٌ
Lisa`yihā Rāđiyahun 9. Zitakuwa radhi kwa juhudi yao, لِسَعْيِهَا رَاضِيَة ٌ
Fī Jannatin `Āliyahin 10. Katika Bustani ya juu. فِي جَنَّةٍ عَالِيَة ٍ
Lā Tasma`u Fīhā Lāghiyahan 11. Hawatasikia humo upuuzi. لاَ تَسْمَعُ فِيهَا لاَغِيَة ً
Fīhā `Aynunriyahun 12. Humo imo chemchem inayo miminika. فِيهَا عَيْن ٌ جَارِيَة ٌ
Fīhā Sururun Marfū`ahun 13. Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa, فِيهَا سُرُر ٌ مَرْفُوعَة ٌ
Wa 'Akwābun Mawđū`ahun 14. Na bilauri zilizo pangwa, وَأَكْوَاب ٌ مَوْضُوعَة ٌ
Wa Namāriqu Maşfūfahun 15. Na matakia safu safu, وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَة ٌ
Wa Zarābīyu Mabthūthahun 16. Na mazulia yaliyo tandikwa. وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَة ٌ
'Afalā Yanžurūna 'Ilá Al-'Ibili Kayfa Khuliqat 17. Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa? أَفَلاَ يَنْظُرُونَ إِلَى الإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ
Wa 'Ilá As-Samā'i Kayfa Rufi`at 18. Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa? وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ
Wa 'Ilá Al-Jibāli Kayfa Nuşibat 19. Na milima jinsi ilivyo thibitishwa? وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ
Wa 'Ilá Al-'Arđi Kayfa Suţiĥat 20. Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa? وَإِلَى الأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ
Fadhakkir 'Innamā 'Anta Mudhakkirun 21. Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji. فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنْتَ مُذَكِّر ٌ
Lasta `Alayhim Bimusayţirin 22. Wewe si mwenye kuwatawalia. لَسْتَ عَلَيْهِمْ بِمُسَيْطِر ٍ
'Illā Man Tawallá Wa Kafara 23. Lakini anaye rudi nyuma na kukataa, إِلاَّ مَنْ تَوَلَّى وَكَفَرَ
Fayu`adhdhibuhu Allāhu Al-`Adhāba Al-'Akbara 24. Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa! فَيُعَذِّبُهُ اللَّهُ الْعَذَابَ الأَكْبَرَ
'Inna 'Ilaynā 'Īābahum 25. Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao. إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ
Thumma 'Inna `Alaynā Ĥisābahum 26. Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!  * ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُمْ
Next Sūrah