83) Sūrat Al-Muţaffifīn

Printed format

83) سُورَة المُطَفِّفِين

Waylun Lilmuţaffifīna 1. Ole wao hao wapunjao! وَيْل ٌ لِلْمُطَفِّفِينَ
Al-Ladhīna 'Idhā Aktālū `Alá An-Nāsi Yastawfūna 2. Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe. الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ
Wa 'Idhā Kālūhum 'Aw Wazanūhum Yukhsirūna 3. Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza. وَإِذَا كَالُوهُمْ أَوْ وَزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ
'Alā Yažunnu 'Ūla'ika 'Annahum Mabthūna 4. Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa أَلاَ يَظُنُّ أُولَئِكَ أَنَّهُمْ مَبْعُوثُونَ
Liyawmin `Ažīmin 5. Katika Siku iliyo kuu, لِيَوْمٍ عَظِيم ٍ
Yawma Yaqūmu An-Nāsu Lirabbi Al-`Ālamīna 6. Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote? يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ
Kallā 'Inna Kitāba Al-Fujjāri Lafī Sijjīnin 7. Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin. كَلاَّ إِنَّ كِتَابَ الفُجَّارِ لَفِي سِجِّين ٍ
Wa Mā 'Adrāka Mā Sijjīnun 8. Unajua nini Sijjin? وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّين ٌ
Kitābun Marqūmun 9. Kitabu kilicho andikwa. كِتَاب ٌ مَرْقُوم ٌ
Waylun Yawma'idhin Lilmukadhdhibīna 10. Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha! وَيْل ٌ يَوْمَئِذ ٍ لِلْمُكَذِّبِينَ
Al-Ladhīna Yukadhdhibūna Biyawmi Ad-Dīni 11. Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo. الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ
Wa Mā Yukadhdhibu Bihi 'Illā Kullu Mu`tadin 'Athīmin 12. Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi. وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إلاَّ كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيم ٍ
'Idhā Tutlá `Alayhi 'Āyātunā Qāla 'Asāţīru Al-'Awwalīna 13. Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale! إِذَا تُتْلَى عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الأَوَّلِينَ
Kallā Bal Rāna `Alá Qulūbihim Mā Kānū Yaksibūna 14. Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma. كَلاَّ بَلْ رَانَ عَلَى قُلُوبِهِمْ مَا كَانُوا يَكْسِبُونَ
Kallā 'Innahum `An Rabbihim Yawma'idhin Lamaĥjūbūna 15. Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi. كَلاَّ إِنَّهُمْ عَنْ رَبِّهِمْ يَوْمَئِذ ٍ لَمَحْجُوبُونَ
Thumma 'Innahum Laşālū Al-Jaĥīmi 16. Kisha wataingia Motoni! ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُوا الْجَحِيمِ
Thumma Yuqālu Hādhā Al-Ladhī Kuntum Bihi Tukadhdhibūna 17. Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha. ثُمَّ يُقَالُ هَذَا الَّذِي كُنتُمْ بِه ِِ تُكَذِّبُونَ
Kallā 'Inna Kitāba Al-'Abrāri Lafī `Illīyīna 18. Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin. كَلاَّ إِنَّ كِتَابَ الأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ
Wa Mā 'Adrāka Mā `Illīyūna 19. Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin? وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ
Kitābun Marqūmun 20. Kitabu kilicho andikwa. كِتَاب ٌ مَرْقُوم ٌ
Yash/haduhu Al-Muqarrabūna 21. Wanakishuhudia walio karibishwa. يَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ
'Inna Al-'Abrāra Lafī Na`īmin 22. Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema. إِنَّ الأَبْرَارَ لَفِي نَعِيم ٍ
`Alá Al-'Arā'iki Yanžurūna 23. Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia. عَلَى الأَرَائِكِ يَنظُرُونَ
Ta`rifu Fī Wujūhihim Nađrata An-Na`īmi 24. Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema, تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ
Yusqawna Min Raĥīqin Makhtūmin 25. Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri, يُسْقَوْنَ مِنْ رَحِيق ٍ مَخْتُوم ٍ
Khitāmuhu Miskun Wa Fī Dhālika Falyatanāfasi Al-Mutanāfisūna 26. Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana. خِتَامُه ُُ مِسْك ٌ وَفِي ذَلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ
Wa Mizājuhu Min Tasnīmin 27. Na mchanganyiko wake ni Tasniim, وَمِزَاجُه ُُ مِنْ تَسْنِيم ٍ
`Aynāan Yashrabu Bihā Al-Muqarrabūna 28. Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa. عَيْنا ً يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ
'Inna Al-Ladhīna 'Ajramū Kānū Mina Al-Ladhīna 'Āmanū Yađĥakūna 29. Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini. إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ
Wa 'Idhā Marrū Bihim Yataghāmazūna 30. Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana. وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ
Wa 'Idhā Anqalabū 'Ilá 'Ahlihimu Anqalabū Fakihīna 31. Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi. وَإِذَا انقَلَبُوا إِلَى أَهْلِهِمُ انقَلَبُوا فَكِهِينَ
Wa 'Idhā Ra'awhum Qālū 'Inna Hā'uulā' Lađāllūna 32. Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea. وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَاؤُلاَء لَضَالُّونَ
Wa Mā 'Ursilū `Alayhim Ĥāfižīna 33. Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ
Fālyawma Al-Ladhīna 'Āmanū Mina Al-Kuffāri Yađĥakūna 34. Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri, فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ
`Alá Al-'Arā'iki Yanžurūna 35. Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia. عَلَى الأَرَائِكِ يَنظُرُونَ
Hal Thūwiba Al-Kuffāru Mā Kānū Yaf`alūna 36. Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda?  * هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ
Next Sūrah