82) Sūrat Al-'Infiţār | Printed format | 82) سُورَة الإنفِطَار |
| 'Idhā As-Samā'u Anfaţarat | 1. Mbingu itapo chanika, | إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ |
| Wa 'Idhā Al-Kawākibu Antatharat | 2. Na nyota zitapo tawanyika, | وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ |
| Wa 'Idhā Al-Biĥāru Fujjirat | 3. Na bahari zitakapo pasuliwa, | وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ |
| Wa 'Idhā Al-Qubūru Bu`thirat | 4. Na makaburi yatapo fukuliwa, | وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ |
| `Alimat Nafsun Mā Qaddamat Wa 'Akhkharat | 5. Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma. | عَلِمَتْ نَفْس ٌ مَا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ |
| Yā 'Ayyuhā Al-'Insānu Mā Gharraka Birabbika Al-Karīmi | 6. Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? | يَاأَيُّهَا الإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ |
| Al-Ladhī Khalaqaka Fasawwāka Fa`adalaka | 7. Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha, | الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ |
| Fī 'Ayyi Şūratin Mā Shā'a Rakkabaka | 8. Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga. | فِي أَيِّ صُورَة ٍ مَا شَاءَ رَكَّبَكَ |
| Kallā Bal Tukadhdhibūna Bid-Dīni | 9. Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo. | كَلاَّ بَلْ تُكَذِّبُونَ بِالدِّينِ |
| Wa 'Inna `Alaykum Laĥāfižīna | 10. Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu, | وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ |
| Kirāmāan Kātibīna | 11. Waandishi wenye hishima, | كِرَاما ً كَاتِبِينَ |
| Ya`lamūna Mā Taf`alūna | 12. Wanayajua mnayo yatenda. | يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ |
| 'Inna Al-'Abrāra Lafī Na`īmin | 13. Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema, | إِنَّ الأَبْرَارَ لَفِي نَعِيم ٍ |
| Wa 'Inna Al-Fujjāra Lafī Jaĥīmin | 14. Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni; | وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيم ٍ |
| Yaşlawnahā Yawma Ad-Dīni | 15. Wataingia humo Siku ya Malipo. | يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ |
| Wa Mā Hum `Anhā Bighā'ibīna | 16. Na hawatoacha kuwamo humo. | وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ |
| Wa Mā 'Adrāka Mā Yawmu Ad-Dīni | 17. Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? | وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ |
| Thumma Mā 'Adrāka Mā Yawmu Ad-Dīni | 18. Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? | ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ |
| Yawma Lā Tamliku Nafsun Linafsin Shay'āan Wa Al-'Amru Yawma'idhin Lillāhi | 19. Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu. * | يَوْمَ لاَ تَمْلِكُ نَفْس ٌ لِنَفْس ٍ شَيْئا ً وَالأَمْرُ يَوْمَئِذ ٍ لِلَّهِ |