81) Sūrat At-Takwīr

Printed format

81) سُورَة التَّكوِير

'Idhā Ash-Shamsu Kūwirat 1. Jua litakapo kunjwa, إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ
Wa 'Idhā An-Nujūmu Ankadarat 2. Na nyota zikazimwa, وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ
Wa 'Idhā Al-Jibālu Suyyirat 3. Na milima ikaondolewa, وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ
Wa 'Idhā Al-`Ishāru `Uţţilat 4. Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe, وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ
Wa 'Idhā Al-Wuĥūshu Ĥushirat 5. Na wanyama wa mwituni wakakusanywa, وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ
Wa 'Idhā Al-Biĥāru Sujjirat 6. Na bahari zikawaka moto, وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ
Wa 'Idhā An-Nufūsu Zūwijat 7. Na nafsi zikaunganishwa, وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ
Wa 'Idhā Al-Maw'ūdatu Su'ilat 8. Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa, وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ
Bi'ayyi Dhanbin Qutilat 9. Kwa kosa gani aliuliwa? بِأَيِّ ذَنْب ٍ قُتِلَتْ
Wa 'Idhā Aş-Şuĥufu Nushirat 10. Na madaftari yatakapo enezwa, وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ
Wa 'Idhā As-Samā'u Kushiţat 11. Na mbingu itapo tanduliwa, وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ
Wa 'Idhā Al-Jaĥīmu Su``irat 12. Na Jahannamu itapo chochewa, وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ
Wa 'Idhā Al-Jannatu 'Uzlifat 13. Na Pepo ikasogezwa, وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ
`Alimat Nafsun Mā 'Aĥđarat 14. Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha. عَلِمَتْ نَفْس ٌ مَا أَحْضَرَتْ
Falā 'Uqsimu Bil-Khunnasi 15. Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma, فَلاَ أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ
Al-Jawāri Al-Kunnasi 16. Zinazo kwenda, kisha zikajificha, الْجَوَارِ الْكُنَّسِ
Wa Al-Layli 'Idhā `As`asa 17. Na kwa usiku unapo pungua, وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ
Wa Aş-Şubĥi 'Idhā Tanaffasa 18. Na kwa asubuhi inapo pambazuka, وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ
'Innahu Laqawlu Rasūlin Karīmin 19. Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu, إِنَّه ُُ لَقَوْلُ رَسُول ٍ كَرِيم ٍ
Dhī Qūwatin `Inda Dhī Al-`Arshi Makīnin 20. Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi, ذِي قُوَّةٍ عِنْدَ ذِي الْعَرْشِ مَكِين ٍ
Muţā`in Thamma 'Amīnin 21. Anaye t'iiwa, tena muaminifu. مُطَاع ٍ ثَمَّ أَمِين ٍ
Wa Mā Şāĥibukum Bimajnūnin 22. Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. وَمَا صَاحِبُكُمْ بِمَجْنُون ٍ
Wa Laqad Ra'āhu Bil-'Ufuqi Al-Mubīni 23. Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi. وَلَقَدْ رَآهُ بِالأُفُقِ الْمُبِينِ
Wa Mā Huwa `Alá Al-Ghaybi Biđanīnin 24. Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu. وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِين ٍ
Wa Mā Huwa Biqawli Shayţānin Rajīmin 25. Wala hii si kauli ya Shetani maluuni. وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَان ٍ رَجِيم ٍ
Fa'ayna Tadh/habūna 26. Basi mnakwenda wapi? فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ
'In Huwa 'Illā Dhikrun Lil`ālamīna 27. Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. إِنْ هُوَ إِلاَّ ذِكْر ٌ لِلْعَالَمِينَ
Liman Shā'a Minkum 'An Yastaqīma 28. Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa. لِمَنْ شَاءَ مِنْكُمْ أَنْ يَسْتَقِيمَ
Wa Mā Tashā'ūna 'Illā 'An Yashā'a Allāhu Rabbu Al-`Ālamīna 29. Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.  * وَمَا تَشَاءُونَ إِلاَّ أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ
Next Sūrah