76) Sūrat Al-'Inn

Printed format

76) سُورَة الإنسَان

Hal 'Atá `Alá Al-'Insāni Ĥīnun Mina Ad-Dahri Lam Yakun Shay'āan Madhkūrāan 1. Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa. هَلْ أَتَى عَلَى الإِنسَانِ حِين ٌ مِنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُنْ شَيْئا ً مَذْكُورا ً
'Innā Khalaq Al-'Insāna Min Nuţfatin 'Amshājin Nabtalīhi Faja`alnāhu Samī`āan Başīrāan 2. Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona. إِنَّا خَلَقْنَا الإِنسَانَ مِنْ نُطْفَةٍ أَمْشَاج ٍ نَبْتَلِيه ِِ فَجَعَلْنَاه ُُ سَمِيعا ً بَصِيرا ً
'Innā Hadaynāhu As-Sabīla 'Immā Shākirāan Wa 'Immā Kafūrāan 3. Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru. إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرا ً وَإِمَّا كَفُورا ً
'Innā 'A`tadnā Lilkāfirīna Salāsilāan Wa 'Aghlālāan Wa Sa`īrāan 4. Hakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali. إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَلاَسِلا ً وَأَغْلاَلا ً وَسَعِيرا ً
'Inna Al-'Abrāra Yashrabūna Min Ka'sin Kāna Mizājuhā Kāfūrāan 5. Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyo changanyika na kafuri, إِنَّ الأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِنْ كَأْس ٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورا ً
`Aynāan Yashrabu Bihā `Ibādu Allāhi Yufajjirūnahā Tafjīrāan 6. Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi. عَيْنا ً يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ اللَّهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرا ً
Yūfūna Bin-Nadhri Wa Yakhāfūna Yawmāan Kāna Sharruhu Mustaţīrāan 7. Wanatimiza ahadi, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana, يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْما ً كَانَ شَرُّه ُُ مُسْتَطِيرا ً
Wa Yuţ`imūna Aţ-Ţa`āma `Alá Ĥubbihi Miskīnāan Wa Yatīmāan Wa 'Asīrāan 8. Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa. وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَى حُبِّه ِِ مِسْكِينا ً وَيَتِيما ً وَأَسِيرا ً
'Innamā Nuţ`imukum Liwajhi Allāhi Lā Nurīdu Minkum Jazā'an Wa Lā Shukūrāan 9. Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّهِ لاَ نُرِيدُ مِنْكُمْ جَزَاء ً وَلاَ شُكُورا ً
'Innā Nakhāfu Min Rabbinā Yawmāan `Abūsāan Qamţarīrāan 10. Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu. إِنَّا نَخَافُ مِنْ رَبِّنَا يَوْماً عَبُوسا ً قَمْطَرِيرا ً
Fawaqāhumu Allāhu Sharra Dhālika Al-Yawmi Wa Laqqāhum Nađratan Wa Surūrāan 11. Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha. فَوَقَاهُمُ اللَّهُ شَرَّ ذَلِكَ الْيَوْمِ وَلَقَّاهُمْ نَضْرَة ً وَسُرُورا ً
Wa Jazāhum Bimā Şabarū Jannatan Wa Ĥarīrāan 12. Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri. وَجَزَاهُمْ بِمَا صَبَرُوا جَنَّة ً وَحَرِيرا ً
Muttaki'īna Fīhā `Alá Al-'Arā'iki Lā Yarawna Fīhā Shamsāan Wa Lā Zamharīrāan 13. Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali. مُتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الأَرَائِكِ لاَ يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسا ً وَلاَ زَمْهَرِيرا ً
Wa Dāniyatan `Alayhim Žilāluhā Wa Dhullilat Quţūfuhā Tadhlīlāan 14. Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini. وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلاَلُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلا ً
Wa Yuţāfu `Alayhim Bi'āniyatin Min Fiđđatin Wa 'Akwābin Kānat Qawārīra 15. Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae, وَيُطَافُ عَلَيْهِمْ بِآنِيَة ٍ مِنْ فِضَّة ٍ وَأَكْوَاب ٍ كَانَتْ قَوَارِيرَ
Qawārīra Min Fiđđatin Qaddarūhā Taqdīrāan 16. Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo. قَوَارِيرَ مِنْ فِضَّة ٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرا ً
Wa Yusqawna Fīhā Ka'sāan Kāna Mizājuhā Zanjabīlāan 17. Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi. وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسا ً كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلا ً
`Aynāan Fīhā Tusammá Salsabīlāan 18. Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil. عَيْنا ً فِيهَا تُسَمَّى سَلْسَبِيلا ً
Wa Yaţūfu `Alayhim Wildānun Mukhalladūna 'Idhā Ra'aytahum Ĥasibtahum Lu'ulu'uāan Manthūrāan 19. Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizo tawanywa. وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَان ٌ مُخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤا ً مَنثُورا ً
Wa 'Idhā Ra'ayta Thamma Ra'ayta Na`īmāan Wa Mulkāan Kabīrāan 20. Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa. وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيما ً وَمُلْكا ً كَبِيرا ً
`Āliyahum Thiyābu Sundusin Khuđrun Wa 'Istabraqun Wa Ĥullū 'Asāwira Min Fiđđatin Wa Saqāhum Rabbuhum Sharābāan Ţahūrāan 21. Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya at'ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa. عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْر ٌ وَإِسْتَبْرَق ٌ وَحُلُّوا أَسَاوِرَ مِنْ فِضَّة ٍ وَسَقَاهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابا ً طَهُورا ً
'Inna Hādhā Kāna Lakum Jazā'an Wa Kāna Sa`yukum Mashkūrāan 22. Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa. إِنَّ هَذَا كَانَ لَكُمْ جَزَاء ً وَكَانَ سَعْيُكُمْ مَشْكُورا ً
'Innā Naĥnu Nazzalnā `Alayka Al-Qur'āna Tanzīlāan 23. Hakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani kidogo kidogo. إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ تَنْزِيلا ً
Fāşbir Liĥukmi Rabbika Wa Lā Tuţi` Minhum 'Āthimāan 'Aw Kafūrāan 24. Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimt'ii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru. فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلاَ تُطِعْ مِنْهُمْ آثِماً أَوْ كَفُورا ً
Wa Adhkur Asma Rabbika Bukratan Wa 'Aşīlāan 25. Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni; وَاذْكُرْ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَة ً وَأَصِيلا ً
Wa Mina Al-Layli Fāsjud Lahu Wa Sabbiĥhu Laylāan Ţawīlāan 26. Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati mrefu. وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَه ُُ وَسَبِّحْهُ لَيْلا ً طَوِيلا ً
'Inna Hā'uulā' Yuĥibbūna Al-`Ājilata Wa Yadharūna Warā'ahum Yawmāan Thaqīlāan 27. Kwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na wanaiacha nyuma yao siku nzito. إِنَّ هَاؤُلاَء يُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَاءَهُمْ يَوْما ً ثَقِيلا ً
Naĥnu Khalaqnāhum Wa Shadadnā 'Asrahum Wa 'Idhā Shi'nā Baddalnā 'Amthālahum Tabdīlāan 28. Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao. نَحْنُ خَلَقْنَاهُمْ وَشَدَدْنَا أَسْرَهُمْ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَا أَمْثَالَهُمْ تَبْدِيلا ً
'Inna Hadhihi Tadhkiratun Faman Shā'a Attakhadha 'Ilá Rabbihi Sabīlāan 29. Hakika haya ni mawaidha; basi anaye taka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi. إِنَّ هَذِه ِِ تَذْكِرَة ٌ فَمَنْ شَاءَ اتَّخَذَ إِلَى رَبِّه ِِ سَبِيلا ً
Wa Mā Tashā'ūna 'Illā 'An Yashā'a Allāhu 'Inna Allāha Kāna `Alīmāan Ĥakīmāan 30. Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ilimu, Mwenye hikima. وَمَا تَشَاءُونَ إِلاَّ أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيماً حَكِيما ً
Yudkhilu Man Yashā'u Fī Raĥmatihi Wa Až-Žālimīna 'A`adda Lahum `Adhābāan 'Alīmāan 31. Humuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu.  * يُدْخِلُ مَنْ يَشَاءُ فِي رَحْمَتِه ِِ وَالظَّالِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَاباً أَلِيما ً
Next Sūrah