75) Sūrat Al-Qiyāmah

Printed format

75) سُورَة الْقِيَامَه

Lā 'Uqsimu Biyawmi Al-Qiyāmahi 1. Ninaapa kwa Siku ya Kiyama! لاَ أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ
Wa Lā 'Uqsimu Bin-Nafsi Al-Lawwāmahi 2. Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu! وَلاَ أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ
'Ayaĥsabu Al-'Insānu 'Allan Najma`a `Ižāmahu 3. Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? أَيَحْسَبُ الإِنسَانُ أَلَّنْ نَجْمَعَ عِظَامَهُ
Balá Qādirīna `Alá 'An Nusawwiya Banānahu 4. Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake! بَلَى قَادِرِينَ عَلَى أَنْ نُسَوِّيَ بَنَانَهُ
Bal Yurīdu Al-'Insānu Liyafjura 'Amāmahu 5. Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake. بَلْ يُرِيدُ الإِنسَانُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُ
Yas'alu 'Ayyāna Yawmu Al-Qiyāmahi 6. Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama? يَسْأَلُ أَيَّانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ
Fa'idhā Bariqa Al-Başaru 7. Basi jicho litapo dawaa, فَإِذَا بَرِقَ الْبَصَرُ
Wa Khasafa Al-Qamaru 8. Na mwezi utapo patwa, وَخَسَفَ الْقَمَرُ
Wa Jumi`a Ash-Shamsu Wa Al-Qamaru 9. Na likakusanywa jua na mwezi, وَجُمِعَ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ
Yaqūlu Al-'Insānu Yawma'idhin 'Ayna Al-Mafarru 10. Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio? يَقُولُ الإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ الْمَفَرُّ
Kallā Lā Wazara 11. La! Hapana pa kukimbilia! كَلاَّ لاَ وَزَرَ
'Ilá Rabbika Yawma'idhin Al-Mustaqarru 12. Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu. إِلَى رَبِّكَ يَوْمَئِذ ٍ الْمُسْتَقَرُّ
Yunabba'u Al-'Insānu Yawma'idhin Bimā Qaddama Wa 'Akhkhara 13. Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha. يُنَبَّأُ الإِنسَانُ يَوْمَئِذ ٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ
Bali Al-'Insānu `Alá Nafsihi Başīrahun 14. Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake. بَلِ الإِنسَانُ عَلَى نَفْسِه ِِ بَصِيرَة ٌ
Wa Law 'Alqá Ma`ādhīrahu 15. Na ingawa atatoa chungu ya udhuru. وَلَوْ أَلْقَى مَعَاذِيرَهُ
Lā Tuĥarrik Bihi Lisānaka Lita`jala Bihi 16. Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka. لاَ تُحَرِّكْ بِه ِِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ
'Inna `Alaynā Jam`ahu Wa Qur'ānahu 17. Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha. إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَه ُُ وَقُرْآنَهُ
Fa'idhā Qara'nāhu Fa Attabi` Qur'ānahu 18. Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake. فَإِذَا قَرَأْنَاه ُُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ
Thumma 'Inna `Alaynā Bayānahu 19. Kisha ni juu yetu kuubainisha. ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ
Kallā Bal Tuĥibbūna Al-`Ājilaha 20. Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani, كَلاَّ بَلْ تُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ
Wa Tadharūna Al-'Ākhiraha 21. Na mnaacha maisha ya Akhera. وَتَذَرُونَ الآخِرَةَ
Wujūhun Yawma'idhin Nāđirahun 22. Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara, وُجُوه ٌ ٌ يَوْمَئِذ ٍ نَاضِرَة ٌ
'Ilá Rabbihā Nāžirahun 23. Zinamwangallia Mola wao Mlezi. إِلَى رَبِّهَا نَاظِرَة ٌ
Wa Wujūhun Yawma'idhin Bāsirahun 24. Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana. وَوُجُوه ٌ ٌ يَوْمَئِذ ٍ بَاسِرَة ٌ
Tažunnu 'An Yuf`ala Bihā Fāqirahun 25. Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo. تَظُنُّ أَنْ يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَة ٌ
Kallā 'Idhā Balaghati At-Tarāqī 26. La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo, كَلاَّ إِذَا بَلَغَتِ التَّرَاقِي
Wa Qīla Man Rāqin 27. Na pakasemwa: Nani wa kumganga? وَقِيلَ مَنْ رَاق ٍ
Wa Žanna 'Annahu Al-Firāqu 28. Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki; وَظَنَّ أَنَّهُ الْفِرَاقُ
Wa At-Taffati As-Sāqu Bis-Sāqi 29. Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi, وَالْتَفَّتِ السَّاقُ بِالسَّاقِ
'Ilá Rabbika Yawma'idhin Al-Masāqu 30. Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi! إِلَى رَبِّكَ يَوْمَئِذ ٍ الْمَسَاقُ
Falā Şaddaqa Wa Lā Şallá 31. Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali. فَلاَ صَدَّقَ وَلاَ صَلَّى
Wa Lakin Kadhdhaba Wa Tawallá 32. Bali alikanusha, na akageuka. وَلَكِنْ كَذَّبَ وَتَوَلَّى
Thumma Dhahaba 'Ilá 'Ahlihi Yatamaţţá 33. Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao. ثُمَّ ذَهَبَ إِلَى أَهْلِه ِِ يَتَمَطَّى
'Awlá Laka Fa'awlá 34. Ole wako, ole wako! أَوْلَى لَكَ فَأَوْلَى
Thumma 'Awlá Laka Fa'awlá 35. Kisha Ole wako, ole wako! ثُمَّ أَوْلَى لَكَ فَأَوْلَى
'Ayaĥsabu Al-'Insānu 'An Yutraka Sudáan 36. Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure? أَيَحْسَبُ الإِنسَانُ أَنْ يُتْرَكَ سُدى ً
'Alam Yaku Nuţfatan Min Manīyin Yumná 37. Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa? أَلَمْ يَكُ نُطْفَة ً مِنْ مَنِيّ ٍ يُمْنَى
Thumma Kāna `Alaqatan Fakhalaqa Fasawwá 38. Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo. ثُمَّ كَانَ عَلَقَة ً فَخَلَقَ فَسَوَّى
Faja`ala Minhu Az-Zawjayni Adh-Dhakara Wa Al-'Unthá 39. Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke. فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالأُنثَى
'Alaysa Dhālika Biqādirin `Alá 'An Yuĥyiya Al-Mawtá 40. Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu? *   أَلَيْسَ ذَلِكَ بِقَادِرٍ عَلَى أَنْ يُحْيِيَ الْمَوْتَى
Next Sūrah