77) Sūratālmursalāt

Printed format

77) سُورَةَالْمُرْسَلاَت

Wa Al-Mursalāti `Urfāan 1. Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole! وَالْمُرْسَلاَتِ عُرْفا ً
Fāl`āşifāti `Aşfāan 2. Na zinazo vuma kwa kasi! فَالْعَاصِفَاتِ عَصْفا ً
Wa An-Nāshirāti Nashan 3. Na zikaeneza maeneo yote! وَالنَّاشِرَاتِ نَشْرا ً
Fālfāriqāti Farqāan 4. Na zinazo farikisha zikatawanya! فَالْفَارِقَاتِ فَرْقا ً
Fālmulqiyāti Dhikrāan 5. Na zinazo peleka mawaidha! فَالْمُلْقِيَاتِ ذِكْرا ً
`Udhrāan 'Aw Nudhan 6. Kwa kuudhuru au kuonya, عُذْراً أَوْ نُذْرا ً
'Innamā Tū`adūna Lawāqi`un 7. Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa! إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَاقِع ٌ
Fa'idhā An-Nujūmu Ţumisat 8. Wakati nyota zitakapo futwa, فَإِذَا النُّجُومُ طُمِسَتْ
Wa 'Idhā As-Samā'u Furijat 9. Na mbingu zitakapo pasuliwa, وَإِذَا السَّمَاءُ فُرِجَتْ
Wa 'Idhā Al-Jibālu Nusifat 10. Na milima itakapo peperushwa, وَإِذَا الْجِبَالُ نُسِفَتْ
Wa 'Idhā Ar-Rusulu 'Uqqitat 11. Na Mitume watakapo wekewa wakati wao, وَإِذَا الرُّسُلُ أُقِّتَتْ
L'ayyi Yawmin 'Ujjilat 12. Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo? لأَيِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ
Liyawmi Al-Faşli 13. Kwa siku ya kupambanua! لِيَوْمِ الْفَصْلِ
Wa Mā 'Adrāka Mā Yawmu Al-Faşli 14. Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini? وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الْفَصْلِ
Waylun Yawma'idhin Lilmukadhdhibīna 15. Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْل ٌ يَوْمَئِذ ٍ لِلْمُكَذِّبِينَ
'Alam Nuhliki Al-'Awwalīna 16. Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia? أَلَمْ نُهْلِكِ الأَوَّلِينَ
Thumma Nutbi`uhumu Al-'Ākhirīna 17. Kisha tukawafuatilizia walio fuatia? ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ الآخِرِينَ
Kadhālika Naf`alu Bil-Mujrimīna 18. Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu! كَذَلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ
Waylun Yawma'idhin Lilmukadhdhibīna 19. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْل ٌ يَوْمَئِذ ٍ لِلْمُكَذِّبِينَ
'Alam Nakhluqkum Min Mā'in Mahīnin 20. Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa? أَلَمْ نَخْلُقْكُمْ مِنْ مَاء ٍ مَهِين ٍ
Faja`alnāhu Fī Qarārin Makīnin 21. Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti? فَجَعَلْنَاه ُُ فِي قَرَار ٍ مَكِين ٍ
'Ilá Qadarin Ma`lūmin 22. Mpaka muda maalumu? إِلَى قَدَر ٍ مَعْلُوم ٍ
Faqadarnā Fani`ma Al-Qādirūna 23. Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria. فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ
Waylun Yawma'idhin Lilmukadhdhibīna 24. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْل ٌ يَوْمَئِذ ٍ لِلْمُكَذِّبِينَ
'Alam Naj`ali Al-'Arđa Kifātāan 25. Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya أَلَمْ نَجْعَلِ الأَرْضَ كِفَاتا ً
'Aĥyā'an Wa 'Amwātāan 26. Walio hai na maiti? أَحْيَاء ً وَأَمْوَاتا ً
Wa Ja`alnā Fīhā Rawāsiya Shāmikhātin Wa 'Asqaynākum Mā'an Furātāan 27. Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu? وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَات ٍ وَأَسْقَيْنَاكُمْ مَاء ً فُرَاتا ً
Waylun Yawma'idhin Lilmukadhdhibīna 28. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْل ٌ يَوْمَئِذ ٍ لِلْمُكَذِّبِينَ
Anţaliqū 'Ilá Mā Kuntum Bihi Tukadhdhibūna 29. Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha! انطَلِقُوا إِلَى مَا كُنتُمْ بِه ِِ تُكَذِّبُونَ
Anţaliqū 'Ilá Žillin Dhī Thalāthi Shu`abin 30. Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu! انطَلِقُوا إِلَى ظِلّ ٍ ذِي ثَلاَثِ شُعَب ٍ
Lā Žalīlin Wa Lā Yughnī Mina Al-Lahabi 31. Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako. لاَ ظَلِيل ٍ وَلاَ يُغْنِي مِنَ اللَّهَبِ
'Innahā Tarmī Bishararin Kālqaşri 32. Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَر ٍ كَالْقَصْرِ
Ka'annahu Jimālatun Şufrun 33. Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano! كَأَنَّه ُُ جِمَالَة ٌ صُفْر ٌ
Waylun Yawma'idhin Lilmukadhdhibīna 34. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْل ٌ يَوْمَئِذ ٍ لِلْمُكَذِّبِينَ
dhā Yawmu Lā Yanţiqūna 35. Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu, هَذَا يَوْمُ لاَ يَنطِقُونَ
Wa Lā Yu'udhanu Lahum Faya`tadhirūna 36. Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru. وَلاَ يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ
Waylun Yawma'idhin Lilmukadhdhibīna 37. Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! وَيْل ٌ يَوْمَئِذ ٍ لِلْمُكَذِّبِينَ
dhā Yawmu Al-Faşli Jama`nākum Wa Al-'Awwalīna 38. Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia. هَذَا يَوْمُ الْفَصْلِ جَمَعْنَاكُمْ وَالأَوَّلِينَ
Fa'in Kāna Lakum Kaydun Fakīdūni 39. Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi! فَإِنْ كَانَ لَكُمْ كَيْد ٌ فَكِيدُونِ
Waylun Yawma'idhin Lilmukadhdhibīna 40. Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! وَيْل ٌ يَوْمَئِذ ٍ لِلْمُكَذِّبِينَ
'Inna Al-Muttaqīna Fī Žilālin Wa `Uyūnin 41. Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem, إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلاَل ٍ وَعُيُون ٍ
Wa Fawākiha Mimmā Yashtahūna 42. Na matunda wanayo yapenda, وَفَوَاكِه ََ مِمَّا يَشْتَهُونَ
Kulū Wa Ashrabū Hanī'āan Bimā Kuntum Ta`malūna 43. Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئا ً بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
'Innā Kadhālika Naj Al-Muĥsinyna 44. Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema. إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنينَ
Waylun Yawma'idhin Lilmukadhdhibīna 45. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْل ٌ يَوْمَئِذ ٍ لِلْمُكَذِّبِينَ
Kulū Wa Tamatta`ū Qalīlāan 'Innakum Mujrimūna 46. Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu! كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلا ً إِنَّكُمْ مُجْرِمُونَ
Waylun Yawma'idhin Lilmukadhdhibīna 47. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْل ٌ يَوْمَئِذ ٍ لِلْمُكَذِّبِينَ
Wa 'Idhā Qīla Lahumu Arka`ū Lā Yarka`ūna 48. Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami. وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لاَ يَرْكَعُونَ
Waylun Yawma'idhin Lilmukadhdhibīna 49. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْل ٌ يَوْمَئِذ ٍ لِلْمُكَذِّبِينَ
Fabi'ayyi Ĥadīthin Ba`dahu Yu'uminūna 50. Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?  * فَبِأَيِّ حَدِيث ٍ بَعْدَه ُُ يُؤْمِنُونَ
Next Sūrah