74) Sūrat Al-Muddaththir

Printed format

74) سُورَة المُدَّثِّر

Yā 'Ayyuhā Al-Muddaththiru 1. Ewe uliye jigubika! يَاأَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ
Qum Fa'andhir 2. Simama uonye! قُمْ فَأَنذِرْ
Wa Rabbaka Fakabbir 3. Na Mola wako Mlezi mtukuze! وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ
Wa Thiyābaka Faţahhir 4. Na nguo zako, zisafishe. وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ
Wa Ar-Rujza Fāhjur 5. Na yaliyo machafu yahame! وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ
Wa Lā Tamnun Tastakthiru 6. Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa. وَلاَ تَمْنُنْ تَسْتَكْثِرُ
Wa Lirabbika Fāşbir 7. Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri! وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ
Fa'idhā Nuqira Fī An-Nāqūri 8. Basi litapo pulizwa barugumu, فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ
Fadhālika Yawma'idhin Yawmun `Asīrun 9. Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu. فَذَلِكَ يَوْمَئِذ ٍ يَوْمٌ عَسِير ٌ
`Alá Al-Kāfirīna Ghayru Yasīrin 10. Kwa makafiri haitakuwa nyepesi. عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِير ٍ
Dharnī Wa Man Khalaqtu Waĥīdāan 11. Niache peke yangu na niliye muumba; ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدا ً
Wa Ja`altu Lahu Mālāan Mamdūdāan 12. Na nikamjaalia awe na mali mengi, وَجَعَلْتُ لَه ُُ مَالا ً مَمْدُودا ً
Wa Banīna Shuhūdāan 13. Na wana wanao onekana, وَبَنِينَ شُهُودا ً
Wa Mahhadtu Lahu Tamhīdāan 14. Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa. وَمَهَّدْتُ لَه ُُ تَمْهِيدا ً
Thumma Yaţma`u 'An 'Azīda 15. Kisha anatumai nimzidishie! ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ
Kallā 'Innahu Kāna Li'yātinā `Anīdāan 16. Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu! كَلاَّ إِنَّه ُُ كَانَ لِأيَاتِنَا عَنِيدا ً
Sa'urhiquhu Şa`ūdāan 17. Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana. سَأُرْهِقُه ُُ صَعُودا ً
'Innahu Fakkara Wa Qaddara 18. Kwani hakika yeye alifikiri na akapima. إِنَّه ُُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ
Faqutila Kayfa Qaddara 19. Basi ameangamia! Vipi alivyo pima! فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ
Thumma Qutila Kayfa Qaddara 20. Tena ameangamia! Vipi alivyo pima! ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ
Thumma Nažara 21. Kisha akatazama, ثُمَّ نَظَرَ
Thumma `Abasa Wa Basara 22. Kisha akakunja kipaji, na akanuna. ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ
Thumma 'Adbara Wa Astakbara 23. Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari. ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ
Faqāla 'In Hādhā 'Illā Siĥrun Yu'utharu 24. Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa. فَقَالَ إِنْ هَذَا إِلاَّ سِحْر ٌ يُؤْثَرُ
'In Hādhā 'Illā Qawlu Al-Bashari 25. Haya si chochote ila kauli ya binaadamu. إِنْ هَذَا إِلاَّ قَوْلُ الْبَشَرِ
Sa'uşlīhi Saqara 26. Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar. سَأُصْلِيه ِِ سَقَرَ
Wa Mā 'Adrāka Mā Saqaru 27. Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar? وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ
Lā Tubqī Wa Lā Tadharu 28. Haubakishi wala hausazi. لاَ تُبْقِي وَلاَ تَذَرُ
Lawwāĥatun Lilbashari 29. Unababua ngozi iwe nyeusi. لَوَّاحَة ٌ لِلْبَشَرِ
`Alayhā Tis`ata `Ashara 30. Juu yake wapo kumi na tisa. عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ
Wa Mā Ja`alnā 'Aşĥāba An-Nāri 'Illā Malā'ikatan Wa Mā Ja`alnā `Iddatahum 'Illā Fitnatan Lilladhīna Kafarū Liyastayqina Al-Ladhīna 'Ū Al-Kitāba Wa Yazdāda Al-Ladhīna 'Āmanū 'Īmānāan Wa Lā Yartāba Al-Ladhīna 'Ū Al-Kitāba Wa Al-Mu'uminūna Wa Liyaqūla Al-Ladhīna Fī Qulūbihim Marađun Wa Al-Kāfirūna Mādhā 'Arāda Allāhu Bihadhā Mathalāan Kadhālika Yuđillu Allāhu Man Yashā'u Wa Yahdī Man Yashā'u Wa Mā Ya`lamu Junūda Rabbika 'Illā Huwa Wa Mā Hiya 'Illā Dhikrá Lilbashari 31. Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha walio kufuru, wapate kuwa na yakini walio pewa Kitabu, na wazidi Imani wale walio amini, wala wasiwe na shaka walio pewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anaye jua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu. وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلاَّ مَلاَئِكَة ً وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلاَّ فِتْنَة ً لِلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانا ً وَلاَ يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَض ٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّهُ بِهَذَا مَثَلا ً كَذَلِكَ يُضِلُّ اللَّهُ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي مَنْ يَشَاءُ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلاَّ هُوَ وَمَا هِيَ إِلاَّ ذِكْرَى لِلْبَشَرِ
Kallā Wa Al-Qamari 32. Hasha! Naapa kwa mwezi! كَلاَّ وَالْقَمَرِ
Wa Al-Layli 'Idh 'Adbara 33. Na kwa usiku unapo kucha! وَاللَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ
Wa Aş-Şubĥi 'Idhā 'Asfara 34. Na kwa asubuhi inapo pambazuka! وَالصُّبْحِ إِذَا أَسْفَرَ
'Innahā La'iĥdá Al-Kubari 35. Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa! إِنَّهَا لَإِحْدَى الْكُبَرِ
Nadhīrāan Lilbashari 36. Ni onyo kwa binaadamu, نَذِيرا ً لِلْبَشَرِ
Liman Shā'a Minkum 'An Yataqaddama 'Aw Yata'akhkhara 37. Kwa anaye taka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa. لِمَنْ شَاءَ مِنْكُمْ أَنْ يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ
Kullu Nafsin Bimā Kasabat Rahīnahun 38. Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyo yachuma. كُلُّ نَفْس ٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَة ٌ
'Illā 'Aşĥāba Al-Yamīni 39. Isipo kuwa watu wa kuliani. إِلاَّ أَصْحَابَ الْيَمِينِ
Fī Jannātin Yatasā'alūna 40. Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana فِي جَنَّات ٍ يَتَسَاءَلُونَ
`Ani Al-Mujrimīna 41. Khabari za wakosefu: عَنِ الْمُجْرِمِينَ
Mā Salakakum Fī Saqara 42. Ni nini kilicho kupelekeni Motoni? مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ
Qālū Lam Naku Mina Al-Muşallīna 43. Waseme: Hatukuwa miongoni walio kuwa wakisali. قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ
Wa Lam Naku Nuţ`imu Al-Miskīna 44. Wala hatukuwa tukiwalisha masikini. وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ
Wa Kunnā Nakhūđu Ma`a Al-Khā'iđīna 45. Na tulikuwa tukizama pamoja na walio zama katika maovu. وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ
Wa Kunnā Nukadhdhibu Biyawmi Ad-Dīni 46. Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo. وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ
Ĥattá 'Atānā Al-Yaqīnu 47. Mpaka yakini ilipo tufikia. حَتَّى أَتَانَا الْيَقِينُ
Famā Tanfa`uhum Shafā`atu Ash-Shāfi`īna 48. Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi. فَمَا تَنْفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ
Famā Lahum `Ani At-Tadhkirati Mu`rīna 49. Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili? فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ
Ka'annahum Ĥumurun Mustanfirahun 50. Kama kwamba wao ni mapunda walio timuliwa, كَأَنَّهُمْ حُمُر ٌ مُسْتَنْفِرَة ٌ
Farrat Min Qaswarahin 51. Wanao mkimbia simba! فَرَّتْ مِنْ قَسْوَرَة ٍ
Bal Yurīdu Kullu Amri'in Minhum 'An Yu'utá Şuĥufāan Munashsharahan 52. Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizo funuliwa. بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئ ٍ مِنْهُمْ أَنْ يُؤْتَى صُحُفا ً مُنَشَّرَة ً
Kallā Bal Lā Yakhāfūna Al-'Ākhiraha 53. Hasha! Kwani wao hawaiogopi Akhera? كَلاَّ بَلْ لاَ يَخَافُونَ الآخِرَةَ
Kallā 'Innahu Tadhkirahun 54. Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho! كَلاَّ إِنَّه ُُ تَذْكِرَة ٌ
Faman Shā'a Dhakarahu 55. Basi anaye taka atakumbuka. فَمَنْ شَاءَ ذَكَرَهُ
Wa Mā Yadhkurūna 'Illā 'An Yashā'a Allāhu Huwa 'Ahlu At-Taqwá Wa 'Ahlu Al-Maghfirahi 56. Na hawatakumbuka isipo kuwa Mwenyezi Mungu atake. Uchamngu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye. *   وَمَا يَذْكُرُونَ إِلاَّ أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَى وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ
Next Sūrah