73) Sūrat Al-Muzzammil

Printed format

73) سُورَة المُزَّمِّل

Yā 'Ayyuhā Al-Muzzammilu 1. Ewe uliye jifunika! يَاأَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ
Qumi Al-Layla 'Illā Qalīlāan 2. Kesha usiku kucha, ila kidogo tu! قُمِ اللَّيْلَ إِلاَّ قَلِيلا ً
Nişfahu 'Aw Anquş Minhu Qalīlāan 3. Nusu yake, au ipunguze kidogo. نِصْفَهُ~ُ أَوْ انْقُصْ مِنْهُ قَلِيلا ً
'Aw Zid `Alayhi Wa Rattili Al-Qur'āna Tartīlāan 4. Au izidishe - na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo. أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلا ً
'Innā Sanulqī `Alayka Qawlāan Thaqīlāan 5. Hakika Sisi tutakuteremshia kauli nzito. إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلا ً ثَقِيلا ً
'Inna Nāshi'ata Al-Layli Hiya 'Ashaddu Waţ'āan Wa 'Aqwamu Qīlāan 6. Hakika kuamka usiku kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi. إِنَّ نَاشِئَةَ اللَّيْلِ هِيَ أَشَدُّ وَطْئا ً وَأَقْوَمُ قِيلا ً
'Inna Laka Fī Aalnnahāri Sabĥāan Ţawīlāan 7. Kwani hakika mchana una shughuli nyingi. إِنَّ لَكَ فِي اَلنَّهَارِ سَبْحا ً طَوِيلا ً
Wa Adhkur Asma Rabbika Wa Tabattal 'Ilayhi Tabtīlāan 8. Na lidhukuru jina la Mola wako Mlezi, na ujitolee kwake kwa ukamilifu. وَاذْكُرْ اسْمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلْ إِلَيْهِ تَبْتِيلا ً
Rabbu Al-Mashriqi Wa Al-Maghribi Lā 'Ilāha 'Illā Huwa Fa Attakhidh/hu Wa Kīlāan 9. Mola Mlezi wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipo kuwa Yeye, basi mfanye kuwa Mtegemewa wako. رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ لاَ إِلَهَ~َ إِلاَّ هُوَ فَاتَّخِذْهُ وَكِيلا ً
Wa Aşbir `Alá Mā Yaqūlūna Wa Ahjurhum Hajrāan Jamīlāan 10. Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kwa vizuri. وَاصْبِرْ عَلَى مَا يَقُولُونَ وَاهْجُرْهُمْ هَجْرا ً جَمِيلا ً
Wa Dharnī Wa Al-Mukadhdhibīna 'Ū An-Na`mati Wa Mahhilhum Qalīlāan 11. Na niache Mimi na hao wanao kanusha, walio neemeka; na wape muhula kidogo! وَذَرْنِي وَالْمُكَذِّبِينَ أُولِي النَّعْمَةِ وَمَهِّلْهُمْ قَلِيلا ً
'Inna Ladaynā 'Ankālāan Wa Jaĥīmāan 12. Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unao waka kwa ukali kabisa! إِنَّ لَدَيْنَا أَنكَالا ً وَجَحِيما ً
Wa Ţa`āmāan Dhā Ghuşşatin Wa `Adhābāan 'Alīmāan 13. Na chakula kinacho kwama kooni, na adhabu inayo umiza. وَطَعَاما ً ذَا غُصَّة ٍ وَعَذَاباً أَلِيما ً
Yawma Tarjufu Al-'Arđu Wa Al-Jibālu Wa Kānati Al-Jibālu Kathībāan Mahīlāan 14. Siku ambayo ardhi itatikiswa na milima pia, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga! يَوْمَ تَرْجُفُ الأَرْضُ وَالْجِبَالُ وَكَانَتِ الْجِبَالُ كَثِيبا ً مَهِيلا ً
'Innā 'Arsalnā 'Ilaykum Rasūlāan Shāhidāan `Alaykum Kamā 'Arsalnā 'Ilá Fir`awna Rasūlāan 15. Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu, kama tulivyo mtuma Mtume kwa Firauni. إِنَّا أَرْسَلْنَا إِلَيْكُمْ رَسُولا ً شَاهِداً عَلَيْكُمْ كَمَا أَرْسَلْنَا إِلَى فِرْعَوْنَ رَسُولا ً
Fa`aşá Fir`awnu Ar-Rasūla Fa'akhadhnāhu 'Akhdhāan Wabīlāan 16. Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamshika mshiko wa mateso. فَعَصَى فِرْعَوْنُ الرَّسُولَ فَأَخَذْنَاهُ~ُ أَخْذا ً وَبِيلا ً
Fakayfa Tattaqūna 'In Kafartum Yawmāan Yaj`alu Al-Wildāna Shībāan 17. Basi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi? فَكَيْفَ تَتَّقُونَ إِنْ كَفَرْتُمْ يَوْما ً يَجْعَلُ الْوِلْدَانَ شِيبا ً
As-Samā'u Munfaţirun Bihi Kāna Wa`duhu Maf`ūlāan 18. Hapo mbingu zitapasuka! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa. السَّمَاءُ مُنْفَطِر ٌ بِه ِِ كَانَ وَعْدُه ُُ مَفْعُولا ً
'Inna Hadhihi Tadhkiratun Faman Shā'a Attakhadha 'Ilá Rabbihi Sabīlāan 19. Kwa hakika hili ni kumbusho. Mwenye kutaka atashika njia ya kwendea kwa Mola wake Mlezi. إِنَّ هَذِه ِِ تَذْكِرَة ٌ فَمَنْ شَاءَ اتَّخَذَ إِلَى رَبِّه ِِ سَبِيلا ً
'Inna Rabbaka Ya`lamu 'Annaka Taqūmu 'Adná Min Thuluthayi Al-Layli Wa Nişfahu Wa Thuluthahu Wa Ţā'ifatun Mina Al-Ladhīna Ma`aka Wa Allāhu Yuqaddiru Al-Layla Wa An-Nahāra `Alima 'An Lan Tuĥşūhu Fatāba `Alaykumqra'ū Mā Tayassara Mina Al-Qur'āni `Alima 'An Sayakūnu Minkum Marđá Wa 'Ākharūna Yađribūna Fī Al-'Arđi Yabtaghūna Min Fađli Allāhi Wa 'Ākharūna Yuqātilūna Fī Sabīli Allāhi Fāqra'ū Mā Tayassara Minhu Wa 'Aqīmū Aş-Şalāata Wa 'Ā Az-Zakāata Wa 'Aqriđū Allāha Qarđāan Ĥasanāan Wa Mā Tuqaddimū Li'nfusikum Min Khayrin Tajidūhu `Inda Allāhi Huwa Khayrāan Wa 'A`žama 'Ajrāan Wa Astaghfirū Allāha 'Inna Allāha Ghafūrun Raĥīmun 20. Hakika Mola wako Mlezi anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur'ani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na mshike Sala, na toeni Zaka, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema. Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. *   إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَى مِنْ ثُلُثَيِ اللَّيْلِ وَنِصْفَه ُُ وَثُلُثَه ُُ وَطَائِفَة ٌ مِنَ الَّذِينَ مَعَكَ وَاللَّهُ يُقَدِّرُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ عَلِمَ أَنْ لَنْ تُحْصُوه ُُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ عَلِمَ أَنْ سَيَكُونُ مِنْكُمْ مَرْضَى وَآخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِي الأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِنْ فَضْلِ اللَّهِ وَآخَرُونَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ وَأَقِيمُوا الصَّلاَةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَقْرِضُوا اللَّهَ قَرْضاً حَسَنا ً وَمَا تُقَدِّمُوا لِأنْفُسِكُمْ مِنْ خَيْر ٍ تَجِدُوه ُُ عِنْدَ اللَّهِ هُوَ خَيْرا ً وَأَعْظَمَ أَجْرا ً وَاسْتَغْفِرُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ غَفُور ٌ رَحِيم ٌ
Next Sūrah