70) Sūrat Al-Ma`ārij

Printed format

70) سُورَة المَعَارِج

Sa'ala Sā'ilun Bi`adhābin Wāqi`in 1. Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea, سَأَلَ سَائِل ٌ بِعَذَاب ٍ وَاقِع ٍ
Lilkāfiryna Laysa Lahu Dāfi`un 2. Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia - لِلْكَافِرينَ لَيْسَ لَه ُُ دَافِع ٌ
Mina Allāhi Dhī Al-Ma`āriji 3. Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja. مِنَ اللَّهِ ذِي الْمَعَارِجِ
Ta`ruju Al-Malā'ikatu Wa Ar-Rūĥu 'Ilayhi Fī Yawmin Kāna Miqdāruhu Khamsīna 'Alfa Sanahin 4. Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu! تَعْرُجُ الْمَلاَئِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْم ٍ كَانَ مِقْدَارُه ُُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَة ٍ
Fāşbir Şabrāan Jamīlāan 5. Basi subiri kwa subira njema. فَاصْبِرْ صَبْرا ً جَمِيلا ً
'Innahum Yarawnahu Ba`īdāan 6. Hakika wao wanaiona iko mbali, إِنَّهُمْ يَرَوْنَه ُُ بَعِيدا ً
Wa Narāhu Qarībāan 7. Na Sisi tunaiona iko karibu. وَنَرَاه ُُ قَرِيبا ً
Yawma Takūnu As-Samā'u Kālmuhli 8. Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa. يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ
Wa Takūnu Al-Jibālu Kāl`ihni 9. Na milima itakuwa kama sufi. وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ
Wa Lā Yas'alu Ĥamīmun Ĥamīmāan 10. Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. وَلاَ يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيما ً
Yubaşşarūnahum Yawaddu Al-Mujrimu Law Yaftadī Min `Adhābi Yawmi'idhin Bibanīhi 11. Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, يُبَصَّرُونَهُمْ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذ ٍ بِبَنِيهِ
Wa Şāĥibatihi Wa 'Akhīhi 12. Na mkewe, na nduguye, وَصَاحِبَتِه ِِ وَأَخِيهِ
Wa Faşīlatihi Allatī Tu'uwyhi 13. Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu, وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْويهِ
Wa Man Al-'Arđi Jamī`āan Thumma Yunjīhi 14. Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. وَمَنْ فِي الأَرْضِ جَمِيعا ً ثُمَّ يُنجِيهِ
Kallā 'Innahā Lažá 15. La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, كَلاَّ إِنَّهَا لَظَى
Nazzā`atan Lilshshawá 16. Unao babua ngozi ya kichwa! نَزَّاعَة ً لِلشَّوَى
Tad`ū Man 'Adbara Wa Tawallá 17. Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka. تَدْعُوا مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّى
Wa Jama`a Fa'aw`á 18. Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi. وَجَمَعَ فَأَوْعَى
'Inna Al-'Insāna Khuliqa Halū`āan 19. Hakika mtu ameumbwa na papara. إِنَّ الإِنسَانَ خُلِقَ هَلُوعا ً
'Idhā Massahu Ash-Sharru Jazū`āan 20. Inapo mgusa shari hupapatika. إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعا ً
Wa 'Idhā Massahu Al-Khayru Manū`āan 21. Na inapo mgusa kheri huizuilia. وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعا ً
'Illā Al-Muşallīna 22. Isipo kuwa wanao sali, إِلاَّ الْمُصَلِّينَ
Al-Ladhīna Hum `Alá Şalātihim Dā'imūna 23. Ambao wanadumisha Sala zao, الَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلاَتِهِمْ دَائِمُونَ
Wa Al-Ladhīna Fī 'Amwālihim Ĥaqqun Ma`lūmun 24. Na ambao katika mali yao iko haki maalumu وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقّ ٌ مَعْلُوم ٌ
Lilssā'ili Wa Al-Maĥrūmi 25. Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba; لِلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ
Wa Al-Ladhīna Yuşaddiqūna Biyawmi Ad-Dīni 26. Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo, وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ
Wa Al-Ladhīna Hum Min `Adhābi Rabbihim Mushfiqūna 27. Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. وَالَّذِينَ هُمْ مِنْ عَذَابِ رَبِّهِمْ مُشْفِقُونَ
'Inna `Adhāba Rabbihim Ghayru Ma'mūnin 28. Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo. إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُون ٍ
Wa Al-Ladhīna Hum Lifurūjihim Ĥāfižūna 29. Na ambao wanahifadhi tupu zao. وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ
'Illā `Alá 'Azwājihim 'Aw Mā Malakat 'Aymānuhum Fa'innahum Ghayru Malūmīna 30. Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi - إِلاَّ عَلَى أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ
Famani Abtaghá Warā'a Dhālika Fa'ūlā'ika Humu Al-`Ādūna 31. Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka. فَمَنِ ابْتَغَى وَرَاءَ ذَلِكَ فَأُوْلَائِكَ هُمُ الْعَادُونَ
Wa Al-Ladhīna Hum Li'mānātihim Wa `Ahdihim Rā`ūna 32. Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, وَالَّذِينَ هُمْ لِأمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ
Wa Al-Ladhīna Hum Bishahādātihim Qā'imūna 33. Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, وَالَّذِينَ هُمْ بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ
Wa Al-Ladhīna Hum `Alá Şalātihim Yuĥāfižūna 34. Na ambao wanazihifadhi Sala zao. وَالَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلاَتِهِمْ يُحَافِظُونَ
'Ūlā'ika Fī Jannātin Mukramūna 35. Hao ndio watakao hishimiwa Peponi. أُوْلَائِكَ فِي جَنَّات ٍ مُكْرَمُونَ
Famāli Al-Ladhīna Kafarū Qibalaka Muhţi`īna 36. Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu? فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ
`Ani Al-Yamīni Wa `Ani Ash-Shimāli `Izīna 37. Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto! عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ
'Ayaţma`u Kullu Amri'in Minhum 'An Yudkhala Jannata Na`īmin 38. Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema? أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئ ٍ مِنْهُمْ أَنْ يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيم ٍ
Kallā 'Innā Khalaqnāhum Mimmā Ya`lamūna 39. La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua. كَلاَّ إِنَّا خَلَقْنَاهُمْ مِمَّا يَعْلَمُونَ
Falā 'Uqsimu Birabbi Al-Mashāriqi Wa Al-Maghāribi 'Innā Laqādirūna 40. Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza فَلاَ أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ
`Alá 'An Nubaddila Khayrāan Minhum Wa Mā Naĥnu Bimasbūqīna 41. Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi. عَلَى أَنْ نُبَدِّلَ خَيْرا ً مِنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ
Fadharhum Yakhūđū Wa Yal`abū Ĥattá Yulāqū Yawmahumu Al-Ladhī Yū`adūna 42. Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa, فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّى يُلاَقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ
Yawma Yakhrujūna Mina Al-'Ajthi Sirā`āan Ka'annahum 'Ilá Nuşubin Yūfiđūna 43. Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo, يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الأَجْدَاثِ سِرَاعا ً كَأَنَّهُمْ إِلَى نُصُب ٍ يُوفِضُونَ
Khāshi`atan 'Abşāruhum Tarhaquhum Dhillatun Dhālika Al-Yawmu Al-Ladhī Kānū Yū`adūna 44. Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa. *   خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّة ٌ ذَلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ
Next Sūrah