69) Sūrat Al-Ĥāqqah

Printed format

69) سُورَة الحَاقَّه

Al-Ĥāqqahu 1. Tukio la haki. الْحَاقَّةُ
Al-Ĥāqqahu 2. Nini hilo Tukio la haki? مَا الْحَاقَّةُ
Wa Mā 'Adrāka Mā Al-Ĥāqqahu 3. Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki? وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحَاقَّةُ
Kadhdhabat Thamūdu Wa `Ādun Bil-Qāri`ahi 4. Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha. كَذَّبَتْ ثَمُودُ وَعَاد ٌ بِالْقَارِعَةِ
Fa'ammā Thamūdu Fa'uhlikū Biţ-Ţāghiyahi 5. Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno. فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهْلِكُوا بِالطَّاغِيَةِ
Wa 'Ammā `Ādun Fa'uhlikū Birīĥin Şarşarin `Ātiyahin 6. Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika. وَأَمَّا عَاد ٌ فَأُهْلِكُوا بِرِيح ٍ صَرْصَرٍ عَاتِيَة ٍ
Sakhkharahā `Alayhim Sab`a Layālin Wa Thamāniyata 'Ayyāmin Ĥusūmāan Fatará Al-Qawma Fīhā Şar`á Ka'annahum 'A`jāzu Nakhlin Khāwiyahin 7. Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani. سَخَّرَهَا عَلَيْهِمْ سَبْعَ لَيَال ٍ وَثَمَانِيَةَ أَيَّامٍ حُسُوما ً فَتَرَى الْقَوْمَ فِيهَا صَرْعَى كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ خَاوِيَة ٍ
Fahal Tará Lahum Min Bāqiyahin 8. Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki? فَهَلْ تَرَى لَهُمْ مِنْ بَاقِيَة ٍ
Wa Jā'a Fir`awnu Wa Man Qablahu Wa Al-Mu'utafikātu Bil-Khāţi'ahi 9. Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia. وَجَاءَ فِرْعَوْنُ وَمَنْ قَبْلَه ُُ وَالْمُؤْتَفِكَاتُ بِالْخَاطِئَةِ
Fa`aşaw Rasūla Rabbihim Fa'akhadhahum 'Akhdhatan Rābiyahan 10. Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu. فَعَصَوْا رَسُولَ رَبِّهِمْ فَأَخَذَهُمْ أَخْذَة ً رَابِيَة ً
'Innā Lammā Ţaghá Al-Mā'u Ĥamalnākum Al-Jāriyahi 11. Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina, إِنَّا لَمَّا طَغَى الْمَاءُ حَمَلْنَاكُمْ فِي الْجَارِيَةِ
Linaj`alahā Lakum Tadhkiratan Wa Ta`iyahā 'Udhunun Wā`iyahun 12. Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi. لِنَجْعَلَهَا لَكُمْ تَذْكِرَة ً وَتَعِيَهَا أُذُن ٌ وَاعِيَة ٌ
Fa'idhā Nufikha Fī Aş-Şūri Nafkhatun Wāĥidahun 13. Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu, فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ نَفْخَة ٌ وَاحِدَة ٌ
Wa Ĥumilati Al-'Arđu Wa Al-Jibālu Fadukkatā Dakkatan Wāĥidahan 14. Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja, وَحُمِلَتِ الأَرْضُ وَالْجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّة ً وَاحِدَة ً
Fayawma'idhin Waqa`ati Al-Wāqi`ahu 15. Siku hiyo ndio Tukio litatukia. فَيَوْمَئِذ ٍ وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ
Wa Anshaqqati As-Samā'u Fahiya Yawma'idhin Wa Ahiyahun 16. Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa. وَانشَقَّتِ السَّمَاءُ فَهِيَ يَوْمَئِذ ٍ وَاهِيَة ٌ
Wa Al-Malaku `Alá 'Arjā'ihā Wa Yaĥmilu `Arsha Rabbika Fawqahum Yawma'idhin Thamāniyahun 17. Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi. وَالْمَلَكُ عَلَى أَرْجَائِهَا وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذ ٍ ثَمَانِيَة ٌ
Yawma'idhin Tu`rađūna Lā Takhfá Minkum Khāfiyahun 18. Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu. يَوْمَئِذ ٍ تُعْرَضُونَ لاَ تَخْفَى مِنْكُمْ خَافِيَة ٌ
Fa'ammā Man 'Ūtiya Kitābahu Biyamīnihi Fayaqūlu Hā'uum Aqra'ū Kitābī 19. Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu! فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَه ُُ بِيَمِينِه ِِ فَيَقُولُ هَاؤُمْ اقْرَءُوا كِتَابِي
'Innī Žanantu 'Annī Mulāqin Ĥisābiyah 20. Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu. إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلاَقٍ حِسَابِيَه
Fahuwa Fī `Īshatin Rāđiyahin 21. Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza, فَهُوَ فِي عِيشَة ٍ رَاضِيَة ٍ
Fī Jannatin `Āliyahin 22. Katika Bustani ya juu, فِي جَنَّةٍ عَالِيَة ٍ
Quţūfuhā Dāniyahun 23. Matunda yake yakaribu. قُطُوفُهَا دَانِيَة ٌ
Kulū Wa Ashrabū Hanī'āan Bimā 'Aslaftum Al-'Ayyāmi Al-Khāliyahi 24. Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita. كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئا ً بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الأَيَّامِ الْخَالِيَةِ
Wa 'Ammā Man 'Ūtiya Kitābahu Bishimālihi Fayaqūlu Yā Laytanī Lam 'Ūta Kitābīh 25. Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu! وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَه ُُ بِشِمَالِه ِِ فَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيهْ
Wa Lam 'Adri Mā Ĥisābīh 26. Wala nisingeli jua nini hisabu yangu. وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيهْ
Yā Laytahā Kānati Al-Qāđiyaha 27. Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa. يَا لَيْتَهَا كَانَتِ الْقَاضِيَةَ
Mā 'Aghná `Annī Mālīh 28. Mali yangu hayakunifaa kitu. مَا أَغْنَى عَنِّي مَالِيهْ
Halaka `Annī Sulţānīh 29. Madaraka yangu yamenipotea. هَلَكَ عَنِّي سُلْطَانِيهْ
Khudhūhu Faghullūhu 30. (Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu! خُذُوه ُُ فَغُلُّوهُ
Thumma Al-Jaĥīma Şallūhu 31. Kisha mtupeni Motoni! ثُمَّ الْجَحِيمَ صَلُّوهُ
Thumma Fī Silsilatin Dhar`uhā Sab`ūna Dhirā`āan Fāslukūhu 32. Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini! ثُمَّ فِي سِلْسِلَة ٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعا ً فَاسْلُكُوهُ
'Innahu Kāna Lā Yu'uminu Billāhi Al-`Ažīmi 33. Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, إِنَّه ُُ كَانَ لاَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ الْعَظِيمِ
Wa Lā Yaĥuđđu `Alá Ţa`āmi Al-Miskīni 34. Wala hahimizi kulisha masikini. وَلاَ يَحُضُّ عَلَى طَعَامِ الْمِسْكِينِ
Falaysa Lahu Al-Yawma Hāhunā Ĥamīmun 35. Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu, فَلَيْسَ لَهُ الْيَوْمَ هَاهُنَا حَمِيم ٌ
Wa Lā Ţa`āmun 'Illā Min Ghislīnin 36. Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. وَلاَ طَعَام ٌ إِلاَّ مِنْ غِسْلِين ٍ
Lā Ya'kuluhu 'Illā Al-Khāţi'ūna 37. Chakula hicho hawakili ila wakosefu. لاَ يَأْكُلُهُ~ُ إِلاَّ الْخَاطِئُونَ
Falā 'Uqsimu Bimā Tubşirūna 38. Basi naapa kwa mnavyo viona, فَلاَ أُقْسِمُ بِمَا تُبْصِرُونَ
Wa Mā Lā Tubşirūna 39. Na msivyo viona, وَمَا لاَ تُبْصِرُونَ
'Innahu Laqawlu Rasūlin Karīmin 40. Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima. إِنَّه ُُ لَقَوْلُ رَسُول ٍ كَرِيم ٍ
Wa Mā Huwa Biqawli Shā`irin Qalīlāan Mā Tu'uminūna 41. Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini. وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِر ٍ قَلِيلا ً مَا تُؤْمِنُونَ
Wa Lā Biqawli Kāhinin Qalīlāan Mā Tadhakkarūna 42. Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka. وَلاَ بِقَوْلِ كَاهِن ٍ قَلِيلا ً مَا تَذَكَّرُونَ
Tanzīlun Min Rabbi Al-`Ālamīna 43. Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. تَنزِيل ٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ
Wa Law Taqawwala `Alaynā Ba`đa Al-'Aqāwīli 44. Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu, وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الأَقَاوِيلِ
La'akhadhnā Minhu Bil-Yamīni 45. Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia, لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ
Thumma Laqaţa`nā Minhu Al-Watīna 46. Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo! ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ
Famā Minkum Min 'Aĥadin `Anhu Ĥājizīna 47. Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia. فَمَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ
Wa 'Innahu Latadhkiratun Lilmuttaqīna 48. Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu. وَإِنَّه ُُ لَتَذْكِرَة ٌ لِلْمُتَّقِينَ
Wa 'Innā Lana`lamu 'Anna Minkum Mukadhdhibīna 49. Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha. وَإِنَّا لَنَعْلَمُ أَنَّ مِنْكُمْ مُكَذِّبِينَ
Wa 'Innahu Laĥasratun `Alá Al-Kāfirīna 50. Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa. وَإِنَّه ُُ لَحَسْرَةٌ عَلَى الْكَافِرِينَ
Wa 'Innahu Laĥaqqu Al-Yaqīni 51. Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini. وَإِنَّه ُُ لَحَقُّ الْيَقِينِ
Fasabbiĥ Biāsmi Rabbika Al-`Ažīmi 52. Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu. *   فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ
Next Sūrah