68) Sūrat Al-Qalam

Printed format

68) سُورَة القَلَم

n Wa Al-Qalami Wa Mā Yasţurūna 1. Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo, نُون وَالْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ
Mā 'Anta Bini`mati Rabbika Bimajnūnin 2. Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu. مَا أَنْتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُون ٍ
Wa 'Inna Laka La'ajrāan Ghayra Mamnūnin 3. Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika. وَإِنَّ لَكَ لَأَجْراً غَيْرَ مَمْنُون ٍ
Wa 'Innaka La`alá Khuluqin `Ažīmin 4. Na hakika wewe una tabia tukufu. وَإِنَّكَ لَعَلى خُلُقٍ عَظِيم ٍ
Fasatubşiru Wa Yubşirūna 5. Karibu utaona, na wao wataona, فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ
Bi'ayyyikumu Al-Maftūnu 6. Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu. بِأَيّيِكُمُ الْمَفْتُونُ
'Inna Rabbaka Huwa 'A`lamu Biman Đalla `An Sabīlihi Wa Huwa 'A`lamu Bil-Muhtadīna 7. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka. إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنْ ضَلَّ عَنْ سَبِيلِه ِِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ
Falā Tuţi`i Al-Mukadhdhibīna 8. Basi usiwat'ii wanao kadhibisha. فَلاَ تُطِعِ الْمُكَذِّبِينَ
Wa Ddū Law Tud/hinu Fayud/hinūna 9. Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie. وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ
Wa Lā Tuţi` Kulla Ĥallāfin Mahīnin 10. Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa, وَلاَ تُطِعْ كُلَّ حَلاَّف ٍ مَهِين ٍ
Hammāzin Mashshā'in Binamīmin 11. Mtapitapi, apitaye akifitini, هَمَّاز ٍ مَشَّاء ٍ بِنَمِيم ٍ
Mannā`in Lilkhayri Mu`tadin 'Athīmin 12. Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi, مَنَّاع ٍ لِلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيم ٍ
`Utullin Ba`da Dhālika Zanīmin 13. Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu. عُتُلّ ٍ بَعْدَ ذَلِكَ زَنِيم ٍ
'An Kāna Dhā Mālin Wa Banīna 14. Ati kwa kuwa ana mali na watoto! أَنْ كَانَ ذَا مَال ٍ وَبَنِينَ
'Idhā Tutlá `Alayhi 'Āyātunā Qāla 'Asāţīru Al-'Awwalīna 15. Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani! إِذَا تُتْلَى عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الأَوَّلِينَ
Sanasimuhu `Alá Al-Khurţūmi 16. Tutamtia kovu juu ya pua yake. سَنَسِمُه ُُ عَلَى الْخُرْطُومِ
'Innā Balawnāhum Kamā Balawnā 'Aşĥāba Al-Jannati 'Idh 'Aqsamū Layaşrimunnahā Muşbiĥīna 17. Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi. إِنَّا بَلَوْنَاهُمْ كَمَا بَلَوْنَا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ
Wa Lā Yastathnūna 18. Wala hawakusema: Mungu akipenda! وَلاَ يَسْتَثْنُونَ
Faţāfa `Alayhā Ţā'ifun Min Rabbika Wa Hum Nā'imūna 19. Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala! فَطَافَ عَلَيْهَا طَائِف ٌ مِنْ رَبِّكَ وَهُمْ نَائِمُونَ
Fa'aşbaĥat Kālşşarīmi 20. Likawa kama usiku wa giza. فَأَصْبَحَتْ كَالصَّرِيمِ
Fatanādaw Muşbiĥīna 21. Asubuhi wakaitana. فَتَنَادَوا مُصْبِحِينَ
'Ani Aghdū `Alá Ĥarthikum 'In Kuntum Şārimīna 22. Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna. أَنِ اغْدُوا عَلَى حَرْثِكُمْ إِنْ كُنتُمْ صَارِمِينَ
nţalaqū Wa Hum Yatakhāfatūna 23. Basi walikwenda na huku wakinong'onezana, فَانطَلَقُوا وَهُمْ يَتَخَافَتُونَ
'An Lā Yadkhulannahā Al-Yawma `Alaykum Miskīnun 24. Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni. أَنْ لاَ يَدْخُلَنَّهَا الْيَوْمَ عَلَيْكُمْ مِسْكِين ٌ
Waghadaw `Alá Ĥardin Qādirīna 25. Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo. وَغَدَوْا عَلَى حَرْد ٍ قَادِرِينَ
Falammā Ra'awhā Qālū 'Innā Lađāllūna 26. Basi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea! فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوا إِنَّا لَضَالُّونَ
Bal Naĥnu Maĥrūmūna 27. Bali tumenyimwa! بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ
Qāla 'Awsaţuhum 'Alam 'Aqul Lakum Lawlā Tusabbiĥūna 28. Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu? قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُلْ لَكُمْ لَوْلاَ تُسَبِّحُونَ
Qālū Subĥāna Rabbinā 'Innā Kunnā Žālimīna 29. Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu. قَالُوا سُبْحَانَ رَبِّنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ
Fa'aqbala Ba`đuhum `Alá Ba`đin Yatalāwamūna 30. Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao. فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْض ٍ يَتَلاَوَمُونَ
Qālū Yā Waylanā 'Innā Kunnā Ţāghīna 31. Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka! قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ
`Asá Rabbunā 'An Yubdilanā Khayrāan Minhā 'Innā 'Ilá Rabbinā Rāghibūna 32. Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. عَسَى رَبُّنَا أَنْ يُبْدِلَنَا خَيْرا ً مِنْهَا إِنَّا إِلَى رَبِّنَا رَاغِبُونَ
Kadhālika Al-`Adhābu Wa La`adhābu Al-'Ākhirati 'Akbaru Law Kānū Ya`lamūna 33. Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua! كَذَلِكَ الْعَذَابُ وَلَعَذَابُ الآخِرَةِ أَكْبَرُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ
'Inna Lilmuttaqīna `Inda Rabbihim Jannāti An-Na`īmi 34. Hakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi. إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِنْدَ رَبِّهِمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ
'Afanaj`alu Al-Muslimīna Kālmujrimīna 35. Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ
Mā Lakum Kayfa Taĥkumūna 36. Mna nini? Mnahukumu vipi? مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ
'Am Lakum Kitābun Fīhi Tadrusūna 37. Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma? أَمْ لَكُمْ كِتَاب ٌ فِيه ِِ تَدْرُسُونَ
'Inna Lakum Fīhi Lamā Takhayyarūna 38. Kuwa mtapata humo mnayo yapenda? إِنَّ لَكُمْ فِيه ِِ لَمَا تَخَيَّرُونَ
'Am Lakum 'Aymānun `Alaynā Bālighatun 'Ilá Yawmi Al-Qiyāmati 'Inna Lakum Lamā Taĥkumūna 39. Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayo jihukumia? أَمْ لَكُمْ أَيْمَانٌ عَلَيْنَا بَالِغَة ٌ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ إِنَّ لَكُمْ لَمَا تَحْكُمُونَ
Salhum 'Ayyuhum Bidhālika Za`īmun 40. Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya? سَلْهُم أَيُّهُمْ بِذَلِكَ زَعِيم ٌ
'Am Lahum Shurakā'u Falya'tū Bishurakā'ihim 'In Kānū Şādiqīna 41. Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli. أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ فَلْيَأْتُوا بِشُرَكَائِهِمْ إِنْ كَانُوا صَادِقِينَ
Yawma Yukshafu `An Sāqin Wa Yud`awna 'Ilá As-Sujūdi Falā Yastaţī`ūna 42. Siku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza, يَوْمَ يُكْشَفُ عَنْ سَاق ٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ فَلاَ يَسْتَطِيعُونَ
Khāshi`atan 'Abşāruhum Tarhaquhum Dhillatun Wa Qad Kānū Yud`awna 'Ilá As-Sujūdi Wa Hum Sālimūna 43. Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima - خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّة ٌ وَقَدْ كَانُوا يُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ وَهُمْ سَالِمُونَ
Fadharnī Wa Man Yukadhdhibu Bihadhā Al-Ĥadīthi Sanastadrijuhum Min Ĥaythu Lā Ya`lamūna 44. Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua. فَذَرْنِي وَمَنْ يُكَذِّبُ بِهَذَا الْحَدِيثِ سَنَسْتَدْرِجُهُمْ مِنْ حَيْثُ لاَ يَعْلَمُونَ
Wa 'Umlī Lahum 'Inna Kaydī Matīnun 45. Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara. وَأُمْلِي لَهُمْ إِنَّ كَيْدِي مَتِين ٌ
'Am Tas'aluhum 'Ajrāan Fahum Min Maghramin Muthqalūna 46. Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo? أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرا ً فَهُمْ مِنْ مَغْرَم ٍ مُثْقَلُونَ
'Am `Indahumu Al-Ghaybu Fahum Yaktubūna 47. Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika? أَمْ عِنْدَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ
Fāşbir Liĥukmi Rabbika Wa Lā Takun Kaşāĥibi Al-Ĥūti 'Idh Nādá Wa Huwa Makžūmun 48. Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa. فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلاَ تَكُنْ كَصَاحِبِ الْحُوتِ إِذْ نَادَى وَهُوَ مَكْظُوم ٌ
Lawlā 'An Tadārakahu Ni`matun Min Rabbihi Lanubidha Bil-`Arā'i Wa Huwa Madhmūmun 49. Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa. لَوْلاَ أَنْ تَدَارَكَه ُُ نِعْمَة ٌ مِنْ رَبِّه ِِ لَنُبِذَ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ مَذْمُوم ٌ
jtabāhu Rabbuhu Faja`alahu Mina Aş-Şāliĥīna 50. Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema. فَاجْتَبَاه ُُ رَبُّه ُُ فَجَعَلَه ُُ مِنَ الصَّالِحِينَ
Wa 'In Yakādu Al-Ladhīna Kafarū Layuzliqūnaka Bi'abşārihim Lammā Sami`ū Adh-Dhikra Wa Yaqūlūna 'Innahu Lamajnūnun 51. Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu. وَإِنْ يَكَادُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَيُزْلِقُونَكَ بِأَبْصَارِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا الذِّكْرَ وَيَقُولُونَ إِنَّه ُُ لَمَجْنُون ٌ
Wa Mā Huwa 'Illā Dhikrun Lil`ālamīna 52. Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. *   وَمَا هُوَ إِلاَّ ذِكْر ٌ لِلْعَالَمِينَ
Next Sūrah