56) Sūrat Al-Wāqi`ah

Printed format

56) سُورَة الوَاقِعَه

'Idhā Waqa`ati Al-Wāqi`ahu 1. Litakapo tukia hilo Tukio إِذَا وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ
Laysa Liwaq`atihā Kādhibahun 2. Hapana cha kukanusha kutukia kwake. لَيْسَ لِوَقْعَتِهَا كَاذِبَة ٌ
Khāfiđatun Rāfi`ahun 3. Literemshalo linyanyualo, خَافِضَة ٌ رَافِعَة ٌ
'Idhā Rujjati Al-'Arđu Rajjāan 4. Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso, إِذَا رُجَّتِ الأَرْضُ رَجّا ً
Wa Bussati Al-Jibālu Bassāan 5. Na milima itapo sagwasagwa, وَبُسَّتِ الْجِبَالُ بَسّا ً
Fakānat Habā'an Munbaththāan 6. Iwe mavumbi yanayo peperushwa, فَكَانَتْ هَبَاء ً مُنْبَثّا ً
Wa Kuntum 'Azwājāan Thalāthahan 7. Na nyinyi mtakuwa namna tatu:- وَكُنتُمْ أَزْوَاجا ً ثَلاَثَة ً
Fa'aşĥābu Al-Maymanati Mā 'Aşĥābu Al-Maymanahi 8. Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani? فَأَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ
Wa 'Aşĥābu Al-Mash'amati Mā 'Aşĥābu Al-Mash'amahi 9. Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni? وَأَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ
Wa As-Sābiqūna As-Sābiqūna 10. Na wa mbele watakuwa mbele. وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ
'Ūlā'ika Al-Muqarrabūna 11. Hao ndio watakao karibishwa أُوْلَائِكَ الْمُقَرَّبُونَ
Fī Jannāti An-Na`īmi 12. Katika Bustani zenye neema. فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ
Thullatun Mina Al-'Awwalīna 13. Fungu kubwa katika wa mwanzo, ثُلَّة ٌ مِنَ الأَوَّلِينَ
Wa Qalīlun Mina Al-'Ākhirīna 14. Na wachache katika wa mwisho. وَقَلِيل ٌ مِنَ الآخِرِينَ
`Alá Sururin Mawđūnahin 15. Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa. عَلَى سُرُر ٍ مَوْضُونَة ٍ
Muttaki'īna `Alayhā Mutaqābilīna 16. Wakiviegemea wakielekeana. مُتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ
Yaţūfu `Alayhim Wildānun Mukhalladūna 17. Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele, يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَان ٌ مُخَلَّدُونَ
Bi'akwābin Wa 'Abārīqa Wa Ka'sin Min Ma`īnin 18. Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi. بِأَكْوَاب ٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْس ٍ مِنْ مَعِين ٍ
Lā Yuşadda`ūna `Anhā Wa Lā Yunzifūna 19. Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa. لاَ يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلاَ يُنزِفُونَ
Wa Fākihatin Mimmā Yatakhayyarūna 20. Na matunda wayapendayo, وَفَاكِهَة ٍ مِمَّا يَتَخَيَّرُونَ
Wa Laĥmi Ţayrin Mimmā Yashtahūna 21. Na nyama za ndege kama wanavyo tamani. وَلَحْمِ طَيْر ٍ مِمَّا يَشْتَهُونَ
Wa Ĥūrun `Īnun 22. Na Mahurulaini, وَحُورٌ عِين ٌ
Ka'amthāli Al-Lu'ulu'ui Al-Maknūni 23. Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa. كَأَمْثَالِ اللُّؤْلُؤِ الْمَكْنُونِ
Jazā'an Bimā Kānū Ya`malūna 24. Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda. جَزَاء ً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Lā Yasma`ūna Fīhā Laghwan Wa Lā Ta'thīmāan 25. Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi, لاَ يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوا ً وَلاَ تَأْثِيما ً
'Illā Qīlāan Salāmāan Salāmāan 26. Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama. إِلاَّ قِيلا ً سَلاَما ً سَلاَما ً
Wa 'Aşĥābu Al-Yamīni Mā 'Aşĥābu Al-Yamīni 27. Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani? وَأَصْحَابُ الْيَمِينِ مَا أَصْحَابُ الْيَمِينِ
Fī Sidrin Makhđūdin 28. Katika mikunazi isiyo na miba, فِي سِدْر ٍ مَخْضُود ٍ
Wa Ţalĥin Manđūdin 29. Na migomba iliyo pangiliwa, وَطَلْح ٍ مَنْضُود ٍ
Wa Žillin Mamdūdin 30. Na kivuli kilicho tanda, وَظِلّ ٍ مَمْدُود ٍ
Wa Mā'in Maskūbin 31. Na maji yanayo miminika, وَمَاء ٍ مَسْكُوب ٍ
Wa Fākihatin Kathīrahin 32. Na matunda mengi, وَفَاكِهَة ٍ كَثِيرَة ٍ
Lā Maqţū`atin Wa Lā Mamnū`ahin 33. Hayatindikii wala hayakatazwi, لاَ مَقْطُوعَة ٍ وَلاَ مَمْنُوعَة ٍ
Wa Furushin Marfū`ahin 34. Na matandiko yaliyo nyanyuliwa. وَفُرُش ٍ مَرْفُوعَة ٍ
'Innā 'Ansha'nāhunna 'Inshā'an 35. Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya, إِنَّا أَنشَأْنَاهُنَّ إِنشَاء ً
Faja`alnāhunna 'Abkārāan 36. Na tutawafanya vijana, فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارا ً
`Urubāan 'Atrābāan 37. Wanapendana na waume zao, hirimu moja. عُرُباً أَتْرَابا ً
Li'aşĥābi Al-Yamīni 38. Kwa ajili ya watu wa kuliani. لِأَصْحَابِ الْيَمِينِ
Thullatun Mina Al-'Awwalīna 39. Fungu kubwa katika wa mwanzo, ثُلَّة ٌ مِنَ الأَوَّلِينَ
Wa Thullatun Mina Al-'Ākhirīna 40. Na fungu kubwa katika wa mwisho. وَثُلَّة ٌ مِنَ الآخِرِينَ
Wa 'Aşĥābu Ash-Shimāli Mā 'Aşĥābu Ash-Shimāli 41. Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni? وَأَصْحَابُ الشِّمَالِ مَا أَصْحَابُ الشِّمَالِ
Fī Samūmin Wa Ĥamīmin 42. Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka, فِي سَمُوم ٍ وَحَمِيم ٍ
Wa Žillin Min Yaĥmūmin 43. Na kivuli cha moshi mweusi, وَظِلّ ٍ مِنْ يَحْمُوم ٍ
Lā Bāridin Wa Lā Karīmin 44. Si cha kuburudisha wala kustarehesha. لاَ بَارِد ٍ وَلاَ كَرِيم ٍ
'Innahum Kānū Qabla Dhālika Mutrafīna 45. Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa. إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَلِكَ مُتْرَفِينَ
Wa Kānū Yuşirrūna `Alá Al-Ĥinthi Al-`Ažīmi 46. Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa, وَكَانُوا يُصِرُّونَ عَلَى الْحِنثِ الْعَظِيمِ
Wa Kānū Yaqūlūna 'A'idhā Mitnā Wa Kunnā Turābāan Wa `Ižāmāan 'A'innā Lamabthūna 47. Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa? وَكَانُوا يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابا ً وَعِظَاماً أَئِنَّا لَمَبْعُوثُونَ
'Awa 'Ābā'uunā Al-'Awwalūna 48. Au baba zetu wa zamani? أَوَ آبَاؤُنَا الأَوَّلُونَ
Qul 'Inna Al-'Awwalīna Wa Al-'Ākhirīna 49. Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho قُلْ إِنَّ الأَوَّلِينَ وَالآخِرِينَ
Lamajmū`ūna 'Ilá Mīqāti Yawmin Ma`lūmin 50. Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu. لَمَجْمُوعُونَ إِلَى مِيقَاتِ يَوْم ٍ مَعْلُوم ٍ
Thumma 'Innakum 'Ayyuhā Ađ-Đāllūna Al-Mukadhdhibūna 51. Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha, ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا الضَّالُّونَ الْمُكَذِّبُونَ
La'ākilūna Min Shajarin Min Zaqqūmin 52. Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu. لَآكِلُونَ مِنْ شَجَر ٍ مِنْ زَقُّوم ٍ
Famāli'ūna Minhā Al-Buţūna 53. Na kwa mti huo mtajaza matumbo. فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ
Fashāribūna `Alayhi Mina Al-Ĥamīmi 54. Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka. فَشَارِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ الْحَمِيمِ
Fashāribūna Shurba Al-Hīmi 55. Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu. فَشَارِبُونَ شُرْبَ الْهِيمِ
dhā Nuzuluhum Yawma Ad-Dīni 56. Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo. هَذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ الدِّينِ
Naĥnu Khalaqnākum Falawlā Tuşaddiqūna 57. Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki? نَحْنُ خَلَقْنَاكُمْ فَلَوْلاَ تُصَدِّقُونَ
'Afara'aytum Mā Tumnūna 58. Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza? أَفَرَأَيْتُمْ مَا تُمْنُونَ
'A'antum Takhluqūnahu 'Am Naĥnu Al-Khāliqūna 59. Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji? أَأَنْتُمْ تَخْلُقُونَهُ~ُ أَمْ نَحْنُ الْخَالِقُونَ
Naĥnu Qaddarnā Baynakumu Al-Mawta Wa Mā Naĥnu Bimasbūqīna 60. Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi نَحْنُ قَدَّرْنَا بَيْنَكُمُ الْمَوْتَ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ
`Alá 'An Nubaddila 'Amthālakum Wa Nunshi'akum Fī Mā Lā Ta`lamūna 61. Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua. عَلَى أَنْ نُبَدِّلَ أَمْثَالَكُمْ وَنُنْشِئَكُمْ فِي مَا لاَ تَعْلَمُونَ
Wa Laqad `Alimtumu An-Nash'ata Al-'Ūlá Falawlā Tadhkkarūna 62. Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki? وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ النَّشْأَةَ الأُولَى فَلَوْلاَ تَذكَّرُونَ
'Afara'aytum Mā Taĥruthūna 63. Je! Mnaona makulima mnayo yapanda? أَفَرَأَيْتُمْ مَا تَحْرُثُونَ
'A'antum Tazra`ūnahu 'Am Naĥnu Az-Zāri`ūna 64. Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha? أَأَنْتُمْ تَزْرَعُونَهُ~ُ أَمْ نَحْنُ الزَّارِعُونَ
Law Nashā'u Laja`alnāhu Ĥuţāmāan Fažalaltum Tafakkahūna 65. Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu, لَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَاه ُُ حُطَاما ً فَظَلَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ
'Innā Lamughramūna 66. Mkisema: Hakika sisi tumegharimika; إِنَّا لَمُغْرَمُونَ
Bal Naĥnu Maĥrūmūna 67. Bali sisi tumenyimwa. بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ
'Afara'aytumu Al-Mā'a Al-Ladhī Tashrabūna 68. Je! Mnayaona maji mnayo yanywa? أَفَرَأَيْتُمُ الْمَاءَ الَّذِي تَشْرَبُونَ
'A'antum 'Anzaltumūhu Mina Al-Muzni 'Am Naĥnu Al-Munzilūna 69. Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha? أَأَنْتُمْ أَنزَلْتُمُوه ُُ مِنَ الْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ الْمُنزِلُونَ
Law Nashā'u Ja`alnāhu 'Ujājāan Falawlā Tashkurūna 70. Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru? لَوْ نَشَاءُ جَعَلْنَاهُ~ُ أُجَاجا ً فَلَوْلاَ تَشْكُرُونَ
'Afara'aytumu An-Nāra Allatī Tūrūna 71. Je! Mnauona moto mnao uwasha? أَفَرَأَيْتُمُ النَّارَ الَّتِي تُورُونَ
'A'antum 'Ansha'tum Shajaratahā 'Am Naĥnu Al-Munshi'ūna 72. Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji? أَأَنْتُمْ أَنشَأْتُمْ شَجَرَتَهَا أَمْ نَحْنُ الْمُنشِئُونَ
Naĥnu Ja`alnāhā Tadhkiratan Wa Matā`āan Lilmuqwīna 73. Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani. نَحْنُ جَعَلْنَاهَا تَذْكِرَة ً وَمَتَاعا ً لِلْمُقْوِينَ
Fasabbiĥ Biāsmi Rabbika Al-`Ažīmi 74. Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu. فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ
Falā 'Uqsimu Bimawāqi`i An-Nujūmi 75. Basi naapa kwa maanguko ya nyota, فَلاَ أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ
Wa 'Innahu Laqasamun Law Ta`lamūna `Ažīmun 76. Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua! وَإِنَّه ُُ لَقَسَم ٌ لَوْ تَعْلَمُونَ عَظِيم ٌ
'Innahu Laqur'ānun Karīmun 77. Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu, إِنَّه ُُ لَقُرْآن ٌ كَرِيم ٌ
Fī Kitābin Maknūnin 78. Katika Kitabu kilicho hifadhiwa. فِي كِتَاب ٍ مَكْنُون ٍ
Lā Yamassuhu 'Illā Al-Muţahharūna 79. Hapana akigusaye ila walio takaswa. لاَ يَمَسُّهُ~ُ إِلاَّ الْمُطَهَّرُونَ
Tanzīlun Min Rabbi Al-`Ālamīna 80. Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. تَنزِيل ٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ
'Afabihadhā Al-Ĥadīthi 'Antum Mud/hinūna 81. Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza? أَفَبِهَذَا الْحَدِيثِ أَنْتُمْ مُدْهِنُونَ
Wa Taj`alūna Rizqakum 'Annakum Tukadhdhibūna 82. Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha? وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ
Falawlā 'Idhā Balaghati Al-Ĥulqūma 83. Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo, فَلَوْلاَ إِذَا بَلَغَتِ الْحُلْقُومَ
Wa 'Antum Ĥīna'idhin Tanžurūna 84. Na nyinyi wakati huo mnatazama! وَأَنْتُمْ حِينَئِذ ٍ تَنظُرُونَ
Wa Naĥnu 'Aqrabu 'Ilayhi Minkum Wa Lakin Lā Tubşirūna 85. Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi. وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْكُمْ وَلَكِنْ لاَ تُبْصِرُونَ
Falawlā 'In Kuntum Ghayra Madīnīna 86. Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu, فَلَوْلاَ إِنْ كُنتُمْ غَيْرَ مَدِينِينَ
Tarji`ūnahā 'In Kuntum Şādiqīna 87. Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli? تَرْجِعُونَهَا إِنْ كُنتُمْ صَادِقِينَ
Fa'ammā 'In Kāna Mina Al-Muqarrabīna 88. Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa, فَأَمَّا إِنْ كَانَ مِنَ الْمُقَرَّبِينَ
Farawĥun Wa Rayĥānun Wa Jannatu Na`īmin 89. Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema. فَرَوْح ٌ وَرَيْحَان ٌ وَجَنَّةُ نَعِيم ٍ
Wa 'Ammā 'In Kāna Min 'Aşĥābi Al-Yamīni 90. Na akiwa katika watu wa upande wa kulia, وَأَمَّا إِنْ كَانَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ
Fasalāmun Laka Min 'Aşĥābi Al-Yamīni 91. Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia. فَسَلاَم ٌ لَكَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ
Wa 'Ammā 'In Kāna Mina Al-Mukadhdhibīna Ađ-Đāllīna 92. Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu, وَأَمَّا إِنْ كَانَ مِنَ الْمُكَذِّبِينَ الضَّالِّينَ
Fanuzulun Min Ĥamīmin 93. Basi karamu yake ni maji yanayo chemka, فَنُزُل ٌ مِنْ حَمِيم ٍ
Wa Taşliyatu Jaĥīmin 94. Na kutiwa Motoni. وَتَصْلِيَةُ جَحِيم ٍ
'Inna Hādhā Lahuwa Ĥaqqu Al-Yaqīni 95. Hakika hii ndiyo haki yenye yakini. إِنَّ هَذَا لَهُوَ حَقُّ الْيَقِينِ
Fasabbiĥ Biāsmi Rabbika Al-`Ažīmi 96. Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa. *   فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ
Next Sūrah