55) Sūrat Ar-Raĥmān

Printed format

55) سُورَة الرَّحمَان

Ar-Raĥmānu 1. Arrah'man, Mwingi wa Rehema الرَّحمَانُ
`Allama Al-Qur'āna 2. Amefundisha Qur'ani. عَلَّمَ الْقُرْآنَ
Khalaqa Al-'Insāna 3. Amemuumba mwanaadamu, خَلَقَ الإِنسَانَ
`Allamahu Al-Bayāna 4. Akamfundisha kubaini. عَلَّمَهُ الْبَيَانَ
Ash-Shamsu Wa Al-Qamaru Biĥusbānin 5. Jua na mwezi huenda kwa hisabu. الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ بِحُسْبَان ٍ
Wa An-Najmu Wa Ash-Shajaru Yasjudāni 6. Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea. وَالنَّجْمُ وَالشَّجَرُ يَسْجُدَانِ
Wa As-Samā'a Rafa`ahā Wa Wađa`a Al-Mīzāna 7. Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani, وَالسَّمَاءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ الْمِيزَانَ
'Allā Taţghaw Fī Al-Mīzāni 8. Ili msidhulumu katika mizani. أَلاَّ تَطْغَوْا فِي الْمِيزَانِ
Wa 'Aqīmū Al-Wazna Bil-Qisţi Wa Lā Tukhsirū Al-Mīzāna 9. Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani. وَأَقِيمُوا الْوَزْنَ بِالْقِسْطِ وَلاَ تُخْسِرُوا الْمِيزَانَ
Wa Al-'Arđa Wađa`ahā Lil'anāmi 10. Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe. وَالأَرْضَ وَضَعَهَا لِلأَنَامِ
Fīhā Fākihatun Wa An-Nakhlu Dhātu Al-'Akmāmi 11. Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba. فِيهَا فَاكِهَة ٌ وَالنَّخْلُ ذَاتُ الأَكْمَامِ
Wa Al-Ĥabbu Dhū Al-`Aşfi Wa Ar-Rayĥānu 12. Na nafaka zenye makapi, na rehani. وَالْحَبُّ ذُو الْعَصْفِ وَالرَّيْحَانُ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 13. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Khalaqa Al-'Insāna Min Şalşālin Kālfakhkhāri 14. Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo.. خَلَقَ الإِنسَانَ مِنْ صَلْصَال ٍ كَالْفَخَّارِ
Wa Khalaqa Al-Jānna Minrijin Min Nārin 15. Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto. وَخَلَقَ الْجَانَّ مِنْ مَارِج ٍ مِنْ نَار ٍ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 16. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Rabbu Al-Mashriqayni Wa Rabbu Al-Maghribayni 17. Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili. رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 18. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Maraja Al-Baĥrayni Yaltaqiyāni 19. Anaziendesha bahari mbili zikutane; مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ
Baynahumā Barzakhun Lā Yabghiyāni 20. Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane. بَيْنَهُمَا بَرْزَخ ٌ لاَ يَبْغِيَانِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 21. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Yakhruju Minhumā Al-Lu'ulu'uu Wa Al-Marjānu 22. Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani. يَخْرُجُ مِنْهُمَا اللُّؤْلُؤُ وَالْمَرْجَانُ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 23. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Wa Lahu Al-Jawāri Al-Munsha'ātu Fī Al-Baĥri Kāl'a`lāmi 24. Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima. وَلَهُ الْجَوَارِ الْمُنشَآتُ فِي الْبَحْرِ كَالأَعْلاَمِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 25. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Kullu Man `Alayhā Fānin 26. Kila kilioko juu yake kitatoweka. كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَان ٍ
Wa Yabqá Wajhu Rabbika Dhū Al-Jalāli Wa Al-'Ikrāmi 27. Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu. وَيَبْقَى وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلاَلِ وَالإِكْرَامِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 28. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Yas'aluhu Man As-Samāwāti Wa Al-'Arđi Kulla Yawmin Huwa Fī Sha'nin 29. Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo. يَسْأَلُه ُُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْن ٍ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 30. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Sanafrughu Lakum 'Ayyuhā Ath-Thaqalāni 31. Tutakuhisabuni enyi makundi mawili. سَنَفْرُغُ لَكُمْ أَيُّهَا الثَّقَلاَنِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 32. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Yā Ma`shara Al-Jinni Wa Al-'Insi 'Ini Astaţa`tum 'An Tanfudhū Min 'Aqţāri As-Samāwāti Wa Al-'Arđi Fānfudhū Lā Tanfudhūna 'Illā Bisulţānin 33. Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka. يَامَعْشَرَ الْجِنِّ وَالإِنسِ إِنِ اسْتَطَعْتُمْ أَنْ تَنفُذُوا مِنْ أَقْطَارِ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ فَانفُذُوا لاَ تَنفُذُونَ إِلاَّ بِسُلْطَان ٍ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 34. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Yursalu `Alaykumā Shuwāžun Min Nārin Wa Nuĥāsun Falā Tantaşirāni 35. Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda. يُرْسَلُ عَلَيْكُمَا شُوَاظ ٌ مِنْ نَار ٍ وَنُحَاس ٌ فَلاَ تَنتَصِرَانِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 36. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Fa'idhā Anshaqqati As-Samā'u Fakānat Wardatan Kālddihāni 37. Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta. فَإِذَا انشَقَّتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ وَرْدَة ً كَالدِّهَانِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 38. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Fayawma'idhin Lā Yus'alu `An Dhanbihi 'Insun Wa Lā Jānnun 39. Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini. فَيَوْمَئِذ ٍ لاَ يُسْأَلُ عَنْ ذَنْبِهِ~ِ إِنس ٌ وَلاَ جَانّ ٌ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 40. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Yu`rafu Al-Mujrimūna Bisīmāhum Fayu'ukhadhu Bin-Nawāşī Wa Al-'Aqdāmi 41. Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu. يُعْرَفُ الْمُجْرِمُونَ بِسِيمَاهُمْ فَيُؤْخَذُ بِالنَّوَاصِي وَالأَقْدَامِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 42. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Hadhihi Jahannamu Allatī Yukadhdhibu Bihā Al-Mujrimūna 43. Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha. هَذِه ِِ جَهَنَّمُ الَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا الْمُجْرِمُونَ
Yaţūfūna Baynahā Wa Bayna Ĥamīmin 'Ānin 44. Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka. يَطُوفُونَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ حَمِيم ٍ آن ٍ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 45. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Wa Liman Khāfa Maqāma Rabbihi Jannatāni 46. Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili. وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّه ِِ جَنَّتَانِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 47. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Dhawātā 'Afnānin 48. Bustani zenye matawi yaliyo tanda. ذَوَاتَا أَفْنَان ٍ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 49. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Fīhimā `Aynāni Tajriyāni 50. Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita. فِيهِمَا عَيْنَانِ تَجْرِيَانِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 51. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Fīhimā Min Kulli Fākihatin Zawjāni 52. Humo katika kila matunda zimo namna mbili. فِيهِمَا مِنْ كُلِّ فَاكِهَة ٍ زَوْجَانِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 53. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Muttaki'īna `Alá Furushin Baţā'inuhā Min 'Istabraqin Wa Janá Al-Jannatayni Dānin 54. Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu. مُتَّكِئِينَ عَلَى فُرُش ٍ بَطَائِنُهَا مِنْ إِسْتَبْرَق ٍ وَجَنَى الْجَنَّتَيْنِ دَان ٍ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 55. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Fīhinna Qāşirātu Aţ-Ţarfi Lam Yaţmithhunna 'Insun Qablahum Wa Lā Jānnun 56. Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini. فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنْس ٌ قَبْلَهُمْ وَلاَ جَانّ ٌ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 57. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Ka'annahunna Al-Yāqūtu Wa Al-Marjānu 58. Kama kwamba wao ni yakuti na marijani. كَأَنَّهُنَّ الْيَاقُوتُ وَالْمَرْجَانُ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 59. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha. فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Hal Jazā'u Al-'Iĥsāni 'Illā Al-'Iĥsānu 60. Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani? هَلْ جَزَاءُ الإِحْسَانِ إِلاَّ الإِحْسَانُ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 61. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Wa Min Dūnihimā Jannatāni 62. Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili. وَمِنْ دُونِهِمَا جَنَّتَانِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 63. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Mud/hāmmatāni 64. Za kijani kibivu. مُدْهَامَّتَانِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 65. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Fīhimā `Aynāni Nađđākhatāni 66. Na chemchem mbili zinazo furika. فِيهِمَا عَيْنَانِ نَضَّاخَتَانِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 67. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Fīhimā Fākihatun Wa Nakhlun Wa Rummānun 68. Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga. فِيهِمَا فَاكِهَة ٌ وَنَخْل ٌ وَرُمَّان ٌ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 69. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Fīhinna Khayrātun Ĥisānun 70. Humo wamo wanawake wema wazuri. فِيهِنَّ خَيْرَاتٌ حِسَان ٌ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 71. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Ĥūrun Maqşūrātun Al-Khiyāmi 72. Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema. حُور ٌ مَقْصُورَات ٌ فِي الْخِيَامِ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 73. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Lam Yaţmithhunna 'Insun Qablahum Wa Lā Jānnun 74. Hajawagusa mtu wala jini kabla yao. لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنس ٌ قَبْلَهُمْ وَلاَ جَانّ ٌ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 75. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Muttaki'īna `Alá Rafrafin Khrin Wa `Abqarīyin Ĥisānin 76. Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri. مُتَّكِئِينَ عَلَى رَفْرَفٍ خُضْر ٍ وَعَبْقَرِيٍّ حِسَان ٍ
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbikumā Tukadhdhibāni 77. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Tabāraka Asmu Rabbika Dhī Al-Jalāli Wa Al-'Ikrāmi 78. Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.  تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلاَلِ وَالإِكْرَامِ
Next Sūrah