54) Sūrat Al-Qamar

Printed format

54) سُورَة القَمَر

Aqtarabati As-Sā`atu Wa Anshaqqa Al-Qamaru 1. Saa imekaribia, na mwezi umepasuka! اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانْشَقَّ الْقَمَرُ
Wa 'In Yaraw 'Āyatan Yu`riđū Wa Yaqūlū Siĥrun Mustamirrun 2. Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea. وَإِنْ يَرَوْا آيَة ً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْر ٌ مُسْتَمِرّ ٌ
Wa Kadhdhabū Wa Attaba`ū 'Ahwā'ahum Wa Kullu 'Amrin Mustaqirrun 3. Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti. وَكَذَّبُوا وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ وَكُلُّ أَمْر ٍ مُسْتَقِرّ ٌ
Wa Laqad Jā'ahum Mina Al-'Anbā'i Mā Fīhi Muzdajarun 4. Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio. وَلَقَدْ جَاءَهُمْ مِنَ الأَنْبَاءِ مَا فِيه ِِ مُزْدَجَر ٌ
Ĥikmatun Bālighatun Famā Tughni An-Nudhuru 5. Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu! حِكْمَة ٌ بَالِغَة ٌ فَمَا تُغْنِ النُّذُرُ
Fatawalla `Anhum Yawma Yad`u Ad-Dā`i 'Ilá Shay'in Nukurin 6. Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha; فَتَوَلَّ عَنْهُمْ يَوْمَ يَدْعُ الدَّاعِ إِلَى شَيْء ٍ نُكُر ٍ
Khushsha`āan 'Abşāruhum Yakhrujūna Mina Al-'Ajthi Ka'annahum Jarādun Muntashirun 7. Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika, خُشَّعاً أَبْصَارُهُمْ يَخْرُجُونَ مِنَ الأَجْدَاثِ كَأَنَّهُمْ جَرَاد ٌ مُنتَشِر ٌ
Muhţi`īna 'Ilá Ad-Dā`i Yaqūlu Al-Kāfirūna Hādhā Yawmun `Asirun 8. Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu. مُهْطِعِينَ إِلَى الدَّاعِ يَقُولُ الْكَافِرُونَ هَذَا يَوْمٌ عَسِر ٌ
Kadhdhabat Qablahum Qawmu Nūĥin Fakadhdhabū `Abdanā Wa Qālū Majnūnun Wa Azdujira 9. Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa. كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوح ٍ فَكَذَّبُوا عَبْدَنَا وَقَالُوا مَجْنُون ٌ وَازْدُجِرَ
Fada`ā Rabbahu 'Annī Maghlūbunntaşir 10. Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru! فَدَعَا رَبَّهُ~ُ أَنِّي مَغْلُوب ٌ فَانْتَصِرْ
Fafataĥnā 'Abwāba As-Samā'i Bimā'in Munhamirin 11. Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika. فَفَتَحْنَا أَبْوَابَ السَّمَاءِ بِمَاء ٍ مُنْهَمِر ٍ
Wa Fajjarnā Al-'Arđa `Uyūnāan Fāltaqá Al-Mā'u `Alá 'Amrin Qad Qudira 12. Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa. وَفَجَّرْنَا الأَرْضَ عُيُونا ً فَالْتَقَى الْمَاءُ عَلَى أَمْر ٍ قَدْ قُدِرَ
Wa Ĥamalnāhu `Alá Dhāti 'Alwāĥin Wa Dusurin 13. Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba. وَحَمَلْنَاه ُُ عَلَى ذَاتِ أَلْوَاح ٍ وَدُسُر ٍ
Tajrī Bi'a`yuninā Jazā'an Liman Kāna Kufira 14.Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa. تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا جَزَاء ً لِمَنْ كَانَ كُفِرَ
Wa Laqad Taraknāhā 'Āyatan Fahal Min Muddakirin 15. Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye kumbuka? وَلَقَدْ تَرَكْنَاهَا آيَة ً فَهَلْ مِنْ مُدَّكِر ٍ
Fakayfa Kāna `Adhābī Wa Nudhuri 16. Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu. فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
Wa Laqad Yassarnā Al-Qur'āna Lildhdhikri Fahal Min Muddakirin 17. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka? وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِر ٍ
Kadhdhabat `Ādun Fakayfa Kāna `Adhābī Wa Nudhuri 18. Kina A'di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu? كَذَّبَتْ عَاد ٌ فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
'Innā 'Arsalnā `Alayhim Rīĥāan Şarşarāan Fī Yawmi Naĥsin Mustamirrin 19. Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo, إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحا ً صَرْصَرا ً فِي يَوْمِ نَحْس ٍ مُسْتَمِرّ ٍ
Tanzi`u An-Nāsa Ka'annahum 'A`jāzu Nakhlin Munqa`irin 20. Ukiwang'oa watu kama vigogo vya mitende vilio ng'olewa. تَنزِعُ النَّاسَ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْل ٍ مُنْقَعِر ٍ
Fakayfa Kāna `Adhābī Wa Nudhuri 21. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu? فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
Wa Laqad Yassarnā Al-Qur'āna Lildhdhikri Fahal Min Muddakirin 22. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anaye kumbuka? وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِر ٍ
Kadhdhabat Thamūdu Bin-Nudhuri 23. Thamudi waliwakanusha Waonyaji. كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِالنُّذُرِ
Faqālū 'Abasharāan Minnā Wāĥidāan Nattabi`uhu 'Innā 'Idhāan Lafī Đalālin Wa Su`urin 24. Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa! فَقَالُوا أَبَشَرا ً مِنَّا وَاحِدا ً نَتَّبِعُهُ~ُ إِنَّا إِذا ً لَفِي ضَلاَل ٍ وَسُعُر ٍ
'A'uulqiya Adh-Dhikru `Alayhi Min Bayninā Bal Huwa Kadhdhābun 'Ashirun 25. Ni yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi! أَؤُلْقِيَ الذِّكْرُ عَلَيْهِ مِنْ بَيْنِنَا بَلْ هُوَ كَذَّابٌ أَشِر ٌ
Saya`lamūna Ghadāan Mani Al-Kadhdhābu Al-'Ashiru 26. Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi. سَيَعْلَمُونَ غَدا ً مَنِ الْكَذَّابُ الأَشِرُ
'Innā Mursilū An-Nāqati Fitnatan Lahum Fārtaqibhum Wa Aşţabir 27. Hakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame tu na ustahamili. إِنَّا مُرْسِلُو النَّاقَةِ فِتْنَة ً لَهُمْ فَارْتَقِبْهُمْ وَاصْطَبِرْ
Wa Nabbi'hum 'Anna Al-Mā'a Qismatun Baynahum Kullu Shirbin Muĥtađarun 28. Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliye khusika. وَنَبِّئْهُمْ أَنَّ الْمَاءَ قِسْمَة ٌ بَيْنَهُمْ كُلُّ شِرْب ٍ مُحْتَضَر ٌ
Fanādaw Şāĥibahum Fata`āţá Fa`aqara 29. Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja. فَنَادَوْا صَاحِبَهُمْ فَتَعَاطَى فَعَقَرَ
Fakayfa Kāna `Adhābī Wa Nudhuri 30. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu! فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
'Innā 'Arsalnā `Alayhim Şayĥatan Wāĥidatan Fakānū Kahashīmi Al-Muĥtažiri 31. Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea uwa. إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ صَيْحَة ً وَاحِدَة ً فَكَانُوا كَهَشِيمِ الْمُحْتَظِرِ
Wa Laqad Yassarnā Al-Qur'āna Lildhdhikri Fahal Min Muddakirin 32. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye? وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِر ٍ
Kadhdhabat Qawmu Lūţin Bin-Nudhuri 33. Kaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji. كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوط ٍ بِالنُّذُرِ
'Innā 'Arsalnā `Alayhim Ĥāşibāan 'Illā 'Āla Lūţin Najjaynāhum Bisaĥarin 34. Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri. إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ حَاصِبا ً إِلاَّ آلَ لُوط ٍ نَجَّيْنَاهُمْ بِسَحَر ٍ
Ni`matan Min `Indinā Kadhālika Najzī Man Shakara 35. Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye shukuru. نِعْمَة ً مِنْ عِنْدِنَا كَذَلِكَ نَجْزِي مَنْ شَكَرَ
Wa Laqad 'Andharahum Baţshatanā Fatamāraw Bin-Nudhuri 36. Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo. وَلَقَدْ أَنذَرَهُمْ بَطْشَتَنَا فَتَمَارَوْا بِالنُّذُرِ
Wa Laqad Rāwadūhu `An Đayfihi Faţamasnā 'A`yunahum Fadhūqū `Adhābī Wa Nudhuri 37. Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu! وَلَقَدْ رَاوَدُوه ُُ عَنْ ضَيْفِه ِِ فَطَمَسْنَا أَعْيُنَهُمْ فَذُوقُوا عَذَابِي وَنُذُرِ
Wa Laqad Şabbaĥahum Bukratan `Adhābun Mustaqirrun 38. Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea. وَلَقَدْ صَبَّحَهُمْ بُكْرَةً عَذَاب ٌ مُسْتَقِرّ ٌ
Fadhūqū `Adhābī Wa Nudhuri 39. Basi onjeni adhabu na maonyo yangu! فَذُوقُوا عَذَابِي وَنُذُرِ
Wa Laqad Yassarnā Al-Qur'āna Lildhdhikri Fahal Min Muddakirin 40. Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka? وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِر ٍ
Wa Laqad Jā'a 'Āla Fir`awna An-Nudhuru 41. Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni. وَلَقَدْ جَاءَ آلَ فِرْعَوْنَ النُّذُرُ
Kadhdhabū Bi'āyātinā Kullihā Fa'akhadhnāhum 'Akhdha `Azīzin Muqtadirin 42. Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo shika Mwenye nguvu Mwenye uweza. كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كُلِّهَا فَأَخَذْنَاهُمْ أَخْذَ عَزِيز ٍ مُقْتَدِر ٍ
'Akuffārukum Khayrun Min 'Ūla'ikum 'Am Lakum Barā'atun Az-Zuburi 43. Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani? أَكُفَّارُكُمْ خَيْر ٌ مِنْ أُوْلَئِكُمْ أَمْ لَكُمْ بَرَاءَة ٌ فِي الزُّبُرِ
'Am Yaqūlūna Naĥnu Jamī`un Muntaşirun 44. Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu. أَمْ يَقُولُونَ نَحْنُ جَمِيع ٌ مُنْتَصِر ٌ
Sayuhzamu Al-Jam`u Wa Yuwallūna Ad-Dubura 45. Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma. سَيُهْزَمُ الْجَمْعُ وَيُوَلُّونَ الدُّبُرَ
Bali As-Sā`atu Maw`iduhum Wa As-Sā`atu 'Ad/há Wa 'Amarru 46. Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi. بَلِ السَّاعَةُ مَوْعِدُهُمْ وَالسَّاعَةُ أَدْهَى وَأَمَرُّ
'Inna Al-Mujrimīna Fī Đalālin Wa Su`urin 47. Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu. إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي ضَلاَل ٍ وَسُعُر ٍ
Yawma Yusĥabūna Fī An-Nāri `Alá Wujūhihim Dhūqū Massa Saqara 48. Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu! يَوْمَ يُسْحَبُونَ فِي النَّارِ عَلَى وُجُوهِهِمْ ذُوقُوا مَسَّ سَقَرَ
'Innā Kulla Shay'in Khalaqnāhu Biqadarin 49. Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo. إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاه ُُ بِقَدَر ٍ
Wa Mā 'Amrunā 'Illā Wāĥidatun Kalamĥin Bil-Başari 50. Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho. وَمَا أَمْرُنَا إِلاَّ وَاحِدَة ٌ كَلَمْح ٍ بِالْبَصَرِ
Wa Laqad 'Ahlaknā 'Ashyā`akum Fahal Min Muddakirin 51. Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka? وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا أَشْيَاعَكُمْ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِر ٍ
Wa Kullu Shay'in Fa`alūhu Fī Az-Zuburi 52. Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni. وَكُلُّ شَيْء ٍ فَعَلُوه ُُ فِي الزُّبُرِ
Wa Kullu Şaghīrin Wa Kabīrin Mustaţarun 53. Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa. وَكُلُّ صَغِير ٍ وَكَبِير ٍ مُسْتَطَر ٌ
'Inna Al-Muttaqīna Fī Jannātin Wa Naharin 54. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito. إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّات ٍ وَنَهَر ٍ
Fī Maq`adi Şidqin `Inda Malīkin Muqtadirin 55. Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza. *   فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ عِنْدَ مَلِيك ٍ مُقْتَدِر ٍ
Next Sūrah