53) Sūrat An-Najm

Printed format

53) سُورَة النَّجْم

Wa An-Najmi 'Idhā Hawá 1. Naapa kwa nyota inapo tua, وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَى
Mā Đalla Şāĥibukum Wa Mā Ghawá 2. Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea. مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَى
Wa Mā Yanţiqu `Ani Al-Hawá 3. Wala hatamki kwa matamanio. وَمَا يَنْطِقُ عَنِ الْهَوَى
'In Huwa 'Illā Waĥyun Yūĥá 4. Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa; إِنْ هُوَ إِلاَّ وَحْي ٌ يُوحَى
`Allamahu Shadīdu Al-Quwá 5. Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu, عَلَّمَه ُُ شَدِيدُ الْقُوَى
Dhū Mirratin Fāstawá 6. Mwenye kutua, akatulia, ذُو مِرَّة ٍ فَاسْتَوَى
Wa Huwa Bil-'Ufuqi Al-'A`lá 7. Naye yuko juu kabisa upeo wa macho. وَهُوَ بِالأُفُقِ الأَعْلَى
Thumma Danā Fatadallá 8. Kisha akakaribia na akateremka. ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّى
Fakāna Qāba Qawsayni 'Aw 'Adná 9. Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi. فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَى
Fa'awĥá 'Ilá `Abdihi Mā 'Awĥá 10. Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia. فَأَوْحَى إِلَى عَبْدِه ِِ مَا أَوْحَى
Mā Kadhaba Al-Fu'uādu Mā Ra'á 11. Moyo haukusema uwongo uliyo yaona. مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَى
'Afatumārūnahu `Alá Mā Yará 12. Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona? أَفَتُمَارُونَه ُُ عَلَى مَا يَرَى
Wa Laqad Ra'āhu Nazlatan 'Ukh 13. Na akamwona mara nyingine, وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَى
`Inda Sidrati Al-Muntahá 14. Penye Mkunazi wa mwisho. عِنْدَ سِدْرَةِ الْمُنْتَهَى
`Indahā Jannatu Al-Ma'wá 15. Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa. عِنْدَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَى
'Idh Yaghshá As-Sidrata Mā Yaghshá 16. Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika. إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَى
Mā Zāgha Al-Başaru Wa Mā Ţaghá 17. Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka. مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَى
Laqad Ra'á Min 'Āyāti Rabbihi Al-Kub 18. Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi. لَقَدْ رَأَى مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَى
'Afara'aytumu Al-Lāta Wa Al-`Uzzá 19. Je! Mmemuona Lata na Uzza? أَفَرَأَيْتُمُ اللاَّتَ وَالْعُزَّى
Wa Manāata Ath-Thālithata Al-'Ukh 20. Na Manaat, mwingine wa tatu? وَمَنَاةَ الثَّالِثَةَ الأُخْرَى
'Alakumu Adh-Dhakaru Wa Lahu Al-'Unthá 21. Je! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake? أَلَكُمُ الذَّكَرُ وَلَهُ الأُنثَى
Tilka 'Idhāan Qismatun Đīzá 22. Huo ni mgawanyo wa dhulma! تِلْكَ إِذا ً قِسْمَة ٌ ضِيزَى
'In Hiya 'Illā 'Asmā'un Sammaytumūhā 'Antum Wa 'Ābā'uukum Mā 'Anzala Allāhu Bihā Min Sulţānin 'In Yattabi`ūna 'Illā Až-Žanna Wa Mā Tahwá Al-'Anfusu Wa Laqad Jā'ahum Min Rabbihimu Al-Hudá 23. Hayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi. إِنْ هِيَ إِلاَّ أَسْمَاء ٌ سَمَّيْتُمُوهَا أَنْتُمْ وَآبَاؤُكُمْ مَا أَنزَلَ اللَّهُ بِهَا مِنْ سُلْطَان ٍ إِنْ يَتَّبِعُونَ إِلاَّ الظَّنَّ وَمَا تَهْوَى الأَنْفُسُ وَلَقَدْ جَاءَهُمْ مِنْ رَبِّهِمُ الْهُدَى
'Am Lil'insāni Mā Tamanná 24. Ati mtu anakipata kila anacho kitamani? أَمْ لِلإِنسَانِ مَا تَمَنَّى
Falillāhi Al-'Ākhiratu Wa Al-'Ū 25. Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera. فَلِلَّهِ الآخِرَةُ وَالأُولَى
Wa Kam Min Malakin As-Samāwāti Lā TughShafā`atuhum Shay'āan 'Illā Min Ba`di 'An Ya'dhana Allāhu Liman Yashā'u Wa Yarđá 26. Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia. وَكَمْ مِنْ مَلَك ٍ فِي السَّمَاوَاتِ لاَ تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئا ً إِلاَّ مِنْ بَعْدِ أَنْ يَأْذَنَ اللَّهُ لِمَنْ يَشَاءُ وَيَرْضَى
'Inna Al-Ladhīna Lā Yu'uminūna Bil-'Ākhirati Layusammūna Al-Malā'ikata Tasmiyata Al-'Unthá 27. Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike. إِنَّ الَّذِينَ لاَ يُؤْمِنُونَ بِالآخِرَةِ لَيُسَمُّونَ الْمَلاَئِكَةَ تَسْمِيَةَ الأُنْثَى
Wa Mā Lahum Bihi Min `Ilmin 'In Yattabi`ūna 'Illā Až-Žanna Wa 'Inna Až-Žanna Lā Yughnī Mina Al-Ĥaqqi Shay'āan 28. Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki. وَمَا لَهُمْ بِه ِِ مِنْ عِلْم ٍ إِنْ يَتَّبِعُونَ إِلاَّ الظَّنَّ وَإِنَّ الظَّنَّ لاَ يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئا ً
Fa'a`riđ `An Man Tawallá `An Dhikrinā Wa Lam Yurid 'Illā Al-Ĥayāata Ad-Dun 29. Basi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia. فَأَعْرِضْ عَنْ مَنْ تَوَلَّى عَنْ ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلاَّ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا
Dhālika Mablaghuhum Mina Al-`Ilmi 'Inna Rabbaka Huwa 'A`lamu Biman Đalla `An Sabīlihi Wa Huwa 'A`lamu Bimani Ahtadá 30. Huo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuongoka. ذَلِكَ مَبْلَغُهُمْ مِنَ الْعِلْمِ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنْ ضَلَّ عَنْ سَبِيلِه ِِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اهْتَدَى
Wa Lillahi Mā Fī As-Samāwāti Wa Mā Fī Al-'Arđi Liyajziya Al-Ladhīna 'Asā'ū Bimā `Amilū Wa Yajziya Al-Ladhīna 'Aĥsanū Bil-Ĥusná 31. Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema. وَلِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ أَسَاءُوا بِمَا عَمِلُوا وَيَجْزِيَ الَّذِينَ أَحْسَنُوا بِالْحُسْنَى
Al-Ladhīna Yajtanibūna Kabā'ira Al-'Ithmi Wa Al-Fawāĥisha 'Illā Al-Lamama 'Inna Rabbaka Wāsi`u Al-Maghfirati Huwa 'A`lamu Bikum 'Idh 'Ansha'akum Mina Al-'Arđi Wa 'Idh 'Antum 'Ajinnatun Fī Buţūni 'Ummahātikum Falā Tuzakkū 'Anfusakum Huwa 'A`lamu Bimani Attaqá 32. Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu. الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلاَّ اللَّمَمَ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُمْ مِنَ الأَرْضِ وَإِذْ أَنْتُمْ أَجِنَّة ٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ فَلاَ تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَى
'Afara'ayta Al-Ladhī Tawallá 33. Je! Umemwona yule aliye geuka? أَفَرَأَيْتَ الَّذِي تَوَلَّى
Wa 'A`ţá Qalīlāan Wa 'Akdá 34. Na akatoa kidogo, kisha akajizuia? وَأَعْطَى قَلِيلا ً وَأَكْدَى
'A`indahu `Ilmu Al-Ghaybi Fahuwa Yará 35. Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona? أَعِنْدَه ُُ عِلْمُ الْغَيْبِ فَهُوَ يَرَى
'Am Lam Yunabba' Bimā Fī Şuĥufi Mūsá 36. Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa? أَمْ لَمْ يُنَبَّأْ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَى
Wa 'Ibrāhīma Al-Ladhī Wa Ffá 37. Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi? وَإِبْرَاهِيمَ الَّذِي وَفَّى
'Allā Taziru Wāziratun Wizra 'Ukh 38. Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine? أَلاَّ تَزِرُ وَازِرَة ٌ وِزْرَ أُخْرَى
Wa 'An Laysa Lil'insāni 'Illā Mā Sa`á 39. Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe? وَأَنْ لَيْسَ لِلإِنسَانِ إِلاَّ مَا سَعَى
Wa 'Anna Sa`yahu Sawfa Yurá 40. Na kwamba vitendo vyake vitaonekana? وَأَنَّ سَعْيَه ُُ سَوْفَ يُرَى
Thumma Yujzāhu Al-Jazā'a Al-'Awfá 41. Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu. ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاءَ الأَوْفَى
Wa 'Anna 'Ilá Rabbika Al-Muntahá 42. Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho. وَأَنَّ إِلَى رَبِّكَ الْمُنْتَهَى
Wa 'Annahu Huwa 'Ađĥaka Wa 'Ab 43. Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio. وَأَنَّه ُُ هُوَ أَضْحَكَ وَأَبْكَى
Wa 'Annahu Huwa 'Amāta Wa 'Aĥyā 44. Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha. وَأَنَّه ُُ هُوَ أَمَاتَ وَأَحْيَا
Wa 'Annahu Khalaqa Az-Zawjayni Adh-Dhakara Wa Al-'Unthá 45. Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike وَأَنَّه ُُ خَلَقَ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالأُنْثَى
Min Nuţfatin 'Idhā Tumná 46. Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa. مِنْ نُطْفَة ٍ إِذَا تُمْنَى
Wa 'Anna `Alayhi An-Nash'ata Al-'Ukh 47. Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine. وَأَنَّ عَلَيْهِ النَّشْأَةَ الأُخْرَى
Wa 'Annahu Huwa 'Aghná Wa 'Aqná 48. Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha. وَأَنَّه ُُ هُوَ أَغْنَى وَأَقْنَى
Wa 'Annahu Huwa Rabbu Ash-Shi`rá 49. Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra. وَأَنَّه ُُ هُوَ رَبُّ الشِّعْرَى
Wa 'Annahu 'Ahlaka `Ādāan Al-'Ū 50. Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza, وَأَنَّهُ~ُ أَهْلَكَ عَادا ً الأُولَى
Wa Thamūda Famā 'Ab 51. Na Thamudi hakuwabakisha, وَثَمُودَ فَمَا أَبْقَى
Wa Qawma Nūĥin Min Qablu 'Innahum Kānū Hum 'Ažlama Wa 'Aţghá 52. Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi; وَقَوْمَ نُوح ٍ مِنْ قَبْلُ إِنَّهُمْ كَانُوا هُمْ أَظْلَمَ وَأَطْغَى
Wa Al-Mu'utafikata 'Ahwá 53. Na miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua. وَالْمُؤْتَفِكَةَ أَهْوَى
Faghashshāhā Mā Ghashshá 54. Vikaifunika vilivyo funika. فَغَشَّاهَا مَا غَشَّى
Fabi'ayyi 'Ālā'i Rabbika Tatamārá 55. Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka? فَبِأَيِّ آلاَءِ رَبِّكَ تَتَمَارَى
dhā Nadhīrun Mina An-Nudhuri Al-'Ū 56. Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani. هَذَا نَذِير ٌ مِنَ النُّذُرِ الأُولَى
'Azifati Al-'Āzifahu 57. Kiyama kimekaribia! أَزِفَتِ الآزِفَةُ
Laysa Lahā Min Dūni Allāhi Kāshifahun 58. Hapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu. لَيْسَ لَهَا مِنْ دُونِ اللَّهِ كَاشِفَة ٌ
'Afamin Hādhā Al-Ĥadīthi Ta`jabūna 59. Je! Mnayastaajabia maneno haya? أَفَمِنْ هَذَا الْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ
Wa Tađĥakūna Wa Lā Tabkūna 60. Na mnacheka, wala hamlii? وَتَضْحَكُونَ وَلاَ تَبْكُونَ
Wa 'Antum Sāmidūna 61. Nanyi mmeghafilika? وَأَنْتُمْ سَامِدُونَ
Fāsjudū Lillāhi Wa A`budū 62. Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu. *   فَاسْجُدُوا لِلَّهِ وَاعْبُدُوا
Next Sūrah