52) Sūrat Aţ-Ţūr

Printed format

52) سُورَة الطُّور

Wa Aţūri 1. Naapa kwa mlima wa T'ur, وَالطُّورِ
Wa Kitābin Masţūrin 2. Na Kitabu kilicho andikwa وَكِتَاب ٍ مَسْطُور ٍ
Fī Raqqin Manshūrin 3. Katika ngozi iliyo kunjuliwa, فِي رَقّ ٍ مَنْشُور ٍ
Wa Al-Bayti Al-Ma`mūri 4. Na kwa Nyumba iliyo jengwa, وَالْبَيْتِ الْمَعْمُورِ
Wa As-Saqfi Al-Marfū`i 5. Na kwa dari iliyo nyanyuliwa, وَالسَّقْفِ الْمَرْفُوعِ
Wa Al-Baĥri Al-Masjūri 6. Na kwa bahari iliyo jazwa, وَالْبَحْرِ الْمَسْجُورِ
'Inna `Adhāba Rabbika Lawāqi`un 7. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea. إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَاقِع ٌ
Mā Lahu Min Dāfi`in 8. Hapana wa kuizuia. مَا لَه ُُ مِنْ دَافِع ٍ
Yawma Tamūru As-Samā'u Mawrāan 9. Siku zitakapo tikisika mbingu kwa mtikiso, يَوْمَ تَمُورُ السَّمَاءُ مَوْرا ً
Wa Tasīru Al-Jibālu Sayrāan 10. Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa. وَتَسِيرُ الْجِبَالُ سَيْرا ً
Fawaylun Yawma'idhin Lilmukadhdhibīna 11. Basi ole wao siku hiyo hao wanao kadhibisha, فَوَيْل ٌ يَوْمَئِذ ٍ لِلْمُكَذِّبِينَ
Al-Ladhīna HumKhawđin Yal`abūna 12. Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi. الَّذِينَ هُمْ فِي خَوْض ٍ يَلْعَبُونَ
Yawma Yuda``ūna 'Ilá Nāri Jahannama Da``āan 13. Siku watapo sukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu, يَوْمَ يُدَعُّونَ إِلَى نَارِ جَهَنَّمَ دَعّا ً
Hadhihi An-Nāru Allatī Kuntum Bihā Tukadhdhibūna 14. (Waambiwe): Huu ndio ule Moto mlio kuwa mkiukanusha! هَذِهِ النَّارُ الَّتِي كُنتُمْ بِهَا تُكَذِّبُونَ
'Afasiĥrun Hādhā 'Am 'Antum Lā Tubşirūna 15. Je! Huu ni uchawi, au hamwoni tu? أَفَسِحْرٌ هَذَا أَمْ أَنْتُمْ لاَ تُبْصِرُونَ
Aşlawhā Fāşbirū 'Aw Lā Taşbirū Sawā'un `Alaykum 'Innamā Tujzawna Mā Kuntum Ta`malūna 16. Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyo kuwa mkiyatenda. اصْلَوْهَا فَاصْبِرُوا أَوْ لاَ تَصْبِرُوا سَوَاءٌ عَلَيْكُمْ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
'Inna Al-Muttaqīna Fī Jannātin Wa Na`īmin 17. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na neema, إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّات ٍ وَنَعِيم ٍ
Fākihīna Bimā 'Ātāhum Rabbuhum Wa Waqāhum Rabbuhum `Adhāba Al-Jaĥīmi 18. Wakifurahi kwa yale aliyo wapa Mola wao Mlezi. Na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni. فَاكِهِينَ بِمَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ وَوَقَاهُمْ رَبُّهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ
Kulū Wa Ashrabū Hanī'āan Bimā Kuntum Ta`malūna 19. Kuleni na kunyweni kwa raha kabisa kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyatenda. كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئا ً بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Muttaki'īna `Alá Sururin Maşfūfatin Wa Zawwajnāhum Biĥūrin `Īnin 20. Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza mahuru-l-aini. مُتَّكِئِينَ عَلَى سُرُر ٍ مَصْفُوفَة ٍ وَزَوَّجْنَاهُمْ بِحُورٍ عِين ٍ
Wa Al-Ladhīna 'Āmanū Wa Attaba`at/hum Dhurrīyatuhum Bi'īmānin 'Alĥaqnā Bihim Dhurrīyatahum Wa Mā 'Alatnāhum Min `Amalihim Min Shay'in Kullu Amri'in Bimā Kasaba Rahīnun 21. Na walio amini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima atapata alicho kichuma. وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُمْ بِإِيمَانٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَا أَلَتْنَاهُمْ مِنْ عَمَلِهِمْ مِنْ شَيْء ٍ كُلُّ امْرِئ ٍ بِمَا كَسَبَ رَهِين ٌ
Wa 'Amdadnāhum Bifākihatin Wa Laĥmin Mimmā Yashtahūna 22. Na tutawapa matunda, na nyama kama watavyo penda. وَأَمْدَدْنَاهُمْ بِفَاكِهَة ٍ وَلَحْم ٍ مِمَّا يَشْتَهُونَ
Yatanāza`ūna Fīhā Ka'sāan Lā Laghwun Fīhā Wa Lā Ta'thīmun 23. Watapeana humo bilauri zisio na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi. يَتَنَازَعُونَ فِيهَا كَأْسا ً لاَ لَغْو ٌ فِيهَا وَلاَ تَأْثِيم ٌ
Wa Yaţūfu `Alayhim Ghilmānun Lahum Ka'annahum Lu'ulu'uun Maknūnun 24. Iwe wanawapitia watumishi wao kama kwamba ni lulu zilizomo katika chaza. وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ غِلْمَان ٌ لَهُمْ كَأَنَّهُمْ لُؤْلُؤ ٌ مَكْنُون ٌ
Wa 'Aqbala Ba`đuhum `Alá Ba`đin Yatasā'alūna 25. Wataelekeana wakiulizana. وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْض ٍ يَتَسَاءَلُونَ
Qālū 'Innā Kunnā Qablu Fī 'Ahlinā Mushfiqīna 26. Waseme: Tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa; قَالُوا إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِي أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ
Famanna Allāhu `Alaynā Wa Waqānā `Adhāba As-Samūmi 27. Basi Mwenyezi Mungu akatufanyia hisani na akatulinda na adhabu ya upepo wa Moto. فَمَنَّ اللَّهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ
'Innā Kunnā Min Qablu Nad`ūhu 'Innahu Huwa Al-Barru Ar-Raĥīmu 28. Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwenye kurehemu. إِنَّا كُنَّا مِنْ قَبْلُ نَدْعُوهُ~ُ إِنَّه ُُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ
Fadhakkir Famā 'Anta Bini`mati Rabbika Bikāhinin Wa Lā Majnūnin 29. Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu. فَذَكِّرْ فَمَا أَنْتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِكَاهِن ٍ وَلاَ مَجْنُون ٍ
'Am Yaqūlūna Shā`irun Natarabbaşu Bihi Rayba Al-Manūni 30. Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari. أَمْ يَقُولُونَ شَاعِر ٌ نَتَرَبَّصُ بِه ِِ رَيْبَ الْمَنُونِ
Qul Tarabbaşū Fa'innī Ma`akum Mina Al-Mutarabbişīna 31. Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia. قُلْ تَرَبَّصُوا فَإِنِّي مَعَكُمْ مِنَ الْمُتَرَبِّصِينَ
'Am Ta'muruhum 'Aĥlāmuhum Bihadhā 'Am Hum Qawmun Ţāghūna 32. Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu? أَمْ تَأْمُرُهُمْ أَحْلاَمُهُمْ بِهَذَا أَمْ هُمْ قَوْم ٌ طَاغُونَ
'Am Yaqūlūna Taqawwalahu Bal Lā Yu'uminūna 33. Au ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini! أَمْ يَقُولُونَ تَقَوَّلَه ُُ بَل لاَ يُؤْمِنُونَ
Falya'tū Biĥadīthin Mithlihi 'In Kānū Şādiqīna 34. Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli. فَلْيَأْتُوا بِحَدِيث ٍ مِثْلِهِ~ِ إِنْ كَانُوا صَادِقِينَ
'Am Khuliqū Min Ghayri Shay'in 'Am Humu Al-Khāliqūna 35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ
'Am Khalaqū As-Samāwāti Wa Al-'Arđa Bal Lā Yūqinūna 36. Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini. أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ بَل لاَ يُوقِنُونَ
'Am `Indahum Khazā'inu Rabbika 'Am Humu Al-Musayţirūna 37. Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka? أَمْ عِنْدَهُمْ خَزَائِنُ رَبِّكَ أَمْ هُمُ الْمُسَيْطِرُونَ
'Am Lahum Sullamun Yastami`ūna Fīhi Falya'ti Mustami`uhum Bisulţānin Mubīnin 38. Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi! أَمْ لَهُمْ سُلَّم ٌ يَسْتَمِعُونَ فِيه ِِ فَلْيَأْتِ مُسْتَمِعُهُمْ بِسُلْطَان ٍ مُبِين ٍ
'Am Lahu Al-Banātu Wa Lakumu Al-Banūna 39. Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana? أَمْ لَهُ الْبَنَاتُ وَلَكُمُ الْبَنُونَ
'Am Tas'aluhum 'Ajrāan Fahum Min Maghramin Muthqalūna 40. Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama? أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرا ً فَهُمْ مِنْ مَغْرَم ٍ مُثْقَلُونَ
'Am `Indahumu Al-Ghaybu Fahum Yaktubūna 41. Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wameandika? أَمْ عِنْدَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ
'Am Yurīdūna Kaydāan Fa-Al-Ladhīna Kafarū Humu Al-Makīdūna 42. Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao walio kufuru ndio watakao tegeka. أَمْ يُرِيدُونَ كَيْدا ً فَالَّذِينَ كَفَرُوا هُمُ الْمَكِيدُونَ
'Am Lahum 'Ilahun Ghayru Allāhi Subĥāna Allāhi `Ammā Yushrikūna 43. Au wanae mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Subhanallah! Ametaksika Mwenyezi Mungu na hao wanao washirikisha naye. أَمْ لَهُمْ إِلَه ٌٌ غَيْرُ اللَّهِ سُبْحَانَ اللَّهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ
Wa 'In Yaraw Kisfāan Mina As-Samā'i Sāqiţāan Yaqūlū Saĥābun Markūmun 44. Na hata wange ona pande linatoka mbinguni linaanguka wange sema: Ni mawingu yaliyo bebana. وَإِنْ يَرَوْا كِسْفا ً مِنَ السَّمَاءِ سَاقِطا ً يَقُولُوا سَحَاب ٌ مَرْكُوم ٌ
Fadharhum Ĥattá Yulāqū Yawmahumu Al-Ladhī Fīhi Yuş`aqūna 45. Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapo hilikishwa. فَذَرْهُمْ حَتَّى يُلاَقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي فِيه ِِ يُصْعَقُونَ
Yawma Lā Yughnī `Anhum Kayduhum Shay'āan Wa Lā Hum Yunşarūna 46. Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa. يَوْمَ لاَ يُغْنِي عَنْهُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئا ً وَلاَ هُمْ يُنصَرُونَ
Wa 'Inna Lilladhīna Žalamū `Adhābāan Dūna Dhālika Wa Lakinna 'Aktharahum Lā Ya`lamūna 47. Na hakika walio dhulumu watapata adhabu nyengine isiyo kuwa hii, lakini wengi wao hawajui. وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا عَذَابا ً دُونَ ذَلِكَ وَلَكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لاَ يَعْلَمُونَ
Wa Aşbir Liĥukmi Rabbika Fa'innaka Bi'a`yuninā Wa Sabbiĥ Biĥamdi Rabbika Ĥīna Taqūmu 48. Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo simama, وَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ
Wa Mina Al-Layli Fasabbiĥhu Wa 'Idbāra An-Nujūmi 49. Na usiku pia mtakase, na zinapo kuchwa nyota. *   وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَإِدْبَارَ النُّجُومِ
Next Sūrah