51) Sūrat Adh-Dhāriyāt

Printed format

51) سُورَة الذَّارِيَات

Wa Adh-Dhāriyāti Dharwan 1. Naapa kwa pepo zinazo tawanya, وَالذَّارِيَاتِ ذَرْوا ً
Fālĥāmilāti Wiqan 2. Na zinazo beba mizigo, فَالْحَامِلاَتِ وِقْرا ً
Fāljāriyāti Yusrāan 3. Na zinazo kwenda kwa wepesi. فَالْجَارِيَاتِ يُسْرا ً
Fālmuqassimāti 'Aman 4. Na zinazo gawanya kwa amri, فَالْمُقَسِّمَاتِ أَمْرا ً
'Innamā Tū`adūna Laşādiqun 5. Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli, إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِق ٌ
Wa 'Inna Ad-Dīna Lawāqi`un 6. Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea. وَإِنَّ الدِّينَ لَوَاقِع ٌ
Wa As-Samā'i Dhāti Al-Ĥubuki 7. Naapa kwa mbingu zenye njia, وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْحُبُكِ
'Innakum Lafī Qawlin Mukhtalifin 8. Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana. إِنَّكُمْ لَفِي قَوْل ٍ مُخْتَلِف ٍ
Yu'ufaku `Anhu Man 'Ufika 9. Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa. يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ
Qutila Al-Kharrāşūna 10. Wazushi wameangamizwa. قُتِلَ الْخَرَّاصُونَ
Al-Ladhīna HumGhamratin Sāhūna 11. Ambao wameghafilika katika ujinga. الَّذِينَ هُمْ فِي غَمْرَة ٍ سَاهُونَ
Yas'alūna 'Ayyāna Yawmu Ad-Dīni 12. Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo? يَسْأَلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ الدِّينِ
Yawma Hum `Alá An-Nāri Yuftanūna 13. Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni. يَوْمَ هُمْ عَلَى النَّارِ يُفْتَنُونَ
Dhūqū Fitnatakumdhā Al-Ladhī Kuntum Bihi Tasta`jilūna 14. Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza. ذُوقُوا فِتْنَتَكُمْ هَذَا الَّذِي كُنتُمْ بِه ِِ تَسْتَعْجِلُونَ
'Inna Al-Muttaqīna Fī Jannātin Wa `Uyūnin 15. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّات ٍ وَعُيُون ٍ
'Ākhidhīna Mā 'Ātāhum Rabbuhum 'Innahum Kānū Qabla Dhālika Muĥsinīna 16. Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema. آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَلِكَ مُحْسِنِينَ
Kānū Qalīlāan Mina Al-Layli Mā Yahja`ūna 17. Walikuwa wakilala kidogo tu usiku. كَانُوا قَلِيلا ً مِنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ
Wa Bil-'Asĥāri Hum Yastaghfirūna 18. Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira. وَبِالأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ
Wa Fī 'Amwālihim Ĥaqqun Lilssā'ili Wa Al-Maĥrūmi 19. Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba. وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقّ ٌ لِلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ
Wa Fī Al-'Arđi 'Āyātun Lilmūqinīna 20. Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini. وَفِي الأَرْضِ آيَات ٌ لِلْمُوقِنِينَ
Wa Fī 'Anfusikum 'Afalā Tubşirūna 21. Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni? وَفِي أَنفُسِكُمْ أَفَلاَ تُبْصِرُونَ
Wa Fī As-Samā'i Rizqukum Wa Mā Tū`adūna 22. Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa. وَفِي السَّمَاءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ
Fawarabbi As-Samā'i Wa Al-'Arđi 'Innahu Laĥaqqun Mithla Mā 'Annakum Tanţiqūna 23. Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema. فَوَرَبِّ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ إِنَّه ُُ لَحَقّ ٌ مِثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ
Hal 'Atāka Ĥadīthu Đayfi 'Ibrāhīma Al-Mukramīna 24. Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa? هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ
'Idh Dakhalū `Alayhi Faqālū Salāmāan Qāla Salāmun Qawmun Munkarūna 25. Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni. إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلاَما ً قَالَ سَلاَم ٌ قَوْم ٌ مُنكَرُونَ
Farāgha 'Ilá 'Ahlihi Fajā'a Bi`ijlin Samīnin 26. Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona. فَرَاغَ إِلَى أَهْلِه ِِ فَجَاءَ بِعِجْل ٍ سَمِين ٍ
Faqarrabahu 'Ilayhim Qāla 'Alā Ta'kulūna 27. Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli? فَقَرَّبَهُ~ُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلاَ تَأْكُلُونَ
Fa'awjasa Minhum Khīfatan Qālū Lā Takhaf Wa Bashsharūhu Bighulāmin `Alīmin 28. Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu. فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَة ً قَالُوا لاَ تَخَفْ وَبَشَّرُوه ُُ بِغُلاَمٍ عَلِيم ٍ
Fa'aqbalati Amra'atuhu Fī Şarratin Faşakkat Wajhahā Wa Qālat `Ajūzun `Aqīmun 29. Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa! فَأَقْبَلَتِ امْرَأَتُه ُُ فِي صَرَّة ٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيم ٌ
Qālū Kadhāliki Qāla Rabbuki 'Innahu Huwa Al-Ĥakīmu Al-`Alīmu 30. Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua. قَالُوا كَذَلِكِ قَالَ رَبُّكِ إِنَّه ُُ هُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ
Qāla Famā Khaţbukum 'Ayyuhā Al-Mursalūna 31. AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa? قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ
Qālū 'Innā 'Ursilnā 'Ilá Qawmin Mujrimīna 32. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu, قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَى قَوْم ٍ مُجْرِمِينَ
Linursila `Alayhim Ĥijāratan Min Ţīnin 33. Tuwatupie mawe ya udongo, لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَة ً مِنْ طِين ٍ
Musawwamatan `Inda Rabbika Lilmusrifīna 34. Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka. مُسَوَّمَةً عِنْدَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ
Fa'akhrajnā Man Kāna Fīhā Mina Al-Mu'uminīna 35. Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini. فَأَخْرَجْنَا مَنْ كَانَ فِيهَا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ
Famā Wajadnā Fīhā Ghayra Baytin Mina Al-Muslimīna 36. Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu! فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْت ٍ مِنَ الْمُسْلِمِينَ
Wa Taraknā Fīhā 'Āyatan Lilladhīna Yakhāfūna Al-`Adhāba Al-'Alīma 37. Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu. وَتَرَكْنَا فِيهَا آيَة ً لِلَّذِينَ يَخَافُونَ الْعَذَابَ الأَلِيمَ
Wa Fī Mūsá 'Idh 'Arsalnāhu 'Ilá Fir`awna Bisulţānin Mubīnin 38. Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi. وَفِي مُوسَى إِذْ أَرْسَلْنَاهُ~ُ إِلَى فِرْعَوْنَ بِسُلْطَان ٍ مُبِين ٍ
Fatawallá Biruknihi Wa Qāla Sāĥirun 'Aw Majnūnun 39. Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu! فَتَوَلَّى بِرُكْنِه ِِ وَقَالَ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُون ٌ
Fa'akhadhnāhu Wa Junūdahu Fanabadhnāhum Al-Yammi Wa Huwa Mulīmun 40. Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa. فَأَخَذْنَاه ُُ وَجُنُودَه ُُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ وَهُوَ مُلِيم ٌ
Wa Fī `Ādin 'Idh 'Arsalnā `Alayhimu Ar-Rīĥa Al-`Aqīma 41. Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi. وَفِي عَاد ٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الرِّيحَ الْعَقِيمَ
Mā Tadharu Min Shay'in 'Atat `Alayhi 'Illā Ja`alat/hu Kālrramīmi 42. Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka. مَا تَذَرُ مِنْ شَيْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلاَّ جَعَلَتْهُ كَالرَّمِيمِ
Wa Fī Thamūda 'Idh Qīla Lahum Tamatta`ū Ĥattá Ĥīnin 43. Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu. وَفِي ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا حَتَّى حِين ٍ
Fa`ataw `An 'Amri Rabbihim Fa'akhadhat/humu Aş-Şā`iqatu Wa Hum Yanžurūna 44. Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona. فَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ وَهُمْ يَنظُرُونَ
Famā Astaţā`ū Min Qiyāmin Wa Mā Kānū Muntaşirīna 45. Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea. فَمَا اسْتَطَاعُوا مِنْ قِيَام ٍ وَمَا كَانُوا مُنتَصِرِينَ
Wa Qawma Nūĥin Min Qablu 'Innahum Kānū Qawmāan Fāsiqīna 46. Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu. وَقَوْمَ نُوح ٍ مِنْ قَبْلُ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْما ً فَاسِقِينَ
Wa As-Samā'a Banaynāhā Bi'ayydin Wa 'Innā Lamūsi`ūna 47. Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua. وَالسَّمَاءَ بَنَيْنَاهَا بِأَيْيد ٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ
Wa Al-'Arđa Farashnāhā Fani`ma Al-Māhidūna 48. Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi! وَالأَرْضَ فَرَشْنَاهَا فَنِعْمَ الْمَاهِدُونَ
Wa Min Kulli Shay'in Khalaqnā Zawjayni La`allakum Tadhakkarūna 49. Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie. وَمِنْ كُلِّ شَيْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ
Fafirrū 'Ilá Allāhi 'Innī Lakum Minhu Nadhīrun Mubīnun 50. Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. فَفِرُّوا إِلَى اللَّهِ إِنِّي لَكُمْ مِنْهُ نَذِير ٌ مُبِين ٌ
Wa Lā Taj`alū Ma`a Allāhi 'Ilahāan 'Ākhara 'Innī Lakum Minhu Nadhīrun Mubīnun 51. Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. وَلاَ تَجْعَلُوا مَعَ اللَّهِ إِلَها ً آخَرَ إِنِّي لَكُمْ مِنْهُ نَذِير ٌ مُبِين ٌ
Kadhālika Mā 'Atá Al-Ladhīna Min Qablihim Min Rasūlin 'Illā Qālū Sāĥirun 'Aw Majnūnun 52. Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu. كَذَلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ مِنْ رَسُول ٍ إِلاَّ قَالُوا سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُون ٌ
'Atawāşaw Bihi Bal Hum Qawmun Ţāghūna 53. Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi. أَتَوَاصَوْا بِه ِِ بَلْ هُمْ قَوْم ٌ طَاغُونَ
Fatawalla `Anhum Famā 'Anta Bimalūmin 54. Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi. فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَا أَنْتَ بِمَلُوم ٍ
Wa Dhakkir Fa'inna Adh-Dhikrá Tanfa`u Al-Mu'uminīna 55. Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini. وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَى تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ
Wa Mā Khalaqtu Al-Jinna Wa Al-'Insa 'Illā Liya`budūni 56. Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi. وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالإِنسَ إِلاَّ لِيَعْبُدُونِ
Mā 'Urīdu Minhum Min Rizqin Wa Mā 'Urīdu 'An Yuţ`imūni 57. Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe. مَا أُرِيدُ مِنْهُمْ مِنْ رِزْق ٍ وَمَا أُرِيدُ أَنْ يُطْعِمُونِ
'Inna Allāha Huwa Ar-Razzāqu Dhū Al-Qūwati Al-Matīnu 58. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti. إِنَّ اللَّهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ
Fa'inna Lilladhīna Žalamū Dhanūbāan Mithla Dhanūbi 'Aşĥābihim Falā Yasta`jilūni 59. Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize. فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذَنُوبا ً مِثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَابِهِمْ فَلاَ يَسْتَعْجِلُونِ
Fawaylun Lilladhīna Kafarū Min Yawmihimu Al-Ladhī Yū`adūna 60. Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa. *   فَوَيْل ٌ لِلَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ يَوْمِهِمُ الَّذِي يُوعَدُونَ
Next Sūrah