50) Sūrat Qāf

Printed format

50) سُورَة قَاف

Qāf Wa Al-Qur'āni Al-Majīdi 1. Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu! قَاف وَالْقُرْآنِ الْمَجِيدِ
Bal `Ajibū 'An Jā'ahum Mundhirun Minhum Faqāla Al-Kāfirūna Hādhā Shay'un `Ajībun 2. Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema makafiri: Hili ni jambo la ajabu! بَلْ عَجِبُوا أَنْ جَاءَهُمْ مُنْذِر ٌ مِنْهُمْ فَقَالَ الْكَافِرُونَ هَذَا شَيْءٌ عَجِيب ٌ
'A'idhā Mitnā Wa Kunnā Turābāan Dhālika Raj`un Ba`īdun 3. Ati tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali! أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابا ً ذَلِكَ رَجْع ٌ بَعِيد ٌ
Qad `Alimnā Mā Tanquşu Al-'Arđu Minhum Wa `Indanā Kitābun Ĥafīžun 4. Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinacho punguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinacho hifadhi yote. قَدْ عَلِمْنَا مَا تَنْقُصُ الأَرْضُ مِنْهُمْ وَعِنْدَنَا كِتَابٌ حَفِيظ ٌ
Bal Kadhdhabū Bil-Ĥaqqi Lammā Jā'ahum Fahum Fī 'Amrin Marījin 5. Lakini waliikanusha Haki ilipo wajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mkorogo. بَلْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ فَهُمْ فِي أَمْر ٍ مَرِيج ٍ
'Afalam Yanžurū 'Ilá As-Samā'i Fawqahum Kayfa Banaynāhā Wa Zayyannāhā Wa Mā Lahā Min Furūjin 6. Je! Hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyo zijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa. أَفَلَمْ يَنْظُرُوا إِلَى السَّمَاءِ فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَاهَا وَزَيَّنَّاهَا وَمَا لَهَا مِنْ فُرُوج ٍ
Wa Al-'Arđa Madadnāhā Wa 'Alqaynā Fīhā Rawāsiya Wa 'Anbatnā Fīhā Min Kulli Zawjin Bahījin 7. Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna. وَالأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْبَتْنَا فِيهَا مِنْ كُلِّ زَوْج ٍ بَهِيج ٍ
Tabşiratan Wa Dhikrá Likulli `Abdin Munībin 8. Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea. تَبْصِرَة ً وَذِكْرَى لِكُلِّ عَبْد ٍ مُنِيب ٍ
Wa Nazzalnā Mina As-Samā'i Mā'an Mubārakāan Fa'anbatnā Bihi Jannātin Wa Ĥabba Al-Ĥaşīdi 9. Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyo barikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka za kuvunwa. وَنَزَّلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاء ً مُبَارَكا ً فَأَنْبَتْنَا بِه ِِ جَنَّات ٍ وَحَبَّ الْحَصِيدِ
Wa An-Nakhla Bāsiqātin Lahā Ţal`un Nađīdun 10. Na mitende mirefu yenye makole yaliyo zaa kwa wingi, وَالنَّخْلَ بَاسِقَات ٍ لَهَا طَلْع ٌ نَضِيد ٌ
Rizqāan Lil`ibādi Wa 'Aĥyaynā Bihi Baldatan Maytāan Kadhālika Al-Khurūju 11. Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyo kuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyo kuwa ufufuaji. رِزْقا ً لِلْعِبَادِ وَأَحْيَيْنَا بِه ِِ بَلْدَة ً مَيْتا ً كَذَلِكَ الْخُرُوجُ
Kadhdhabat Qablahum Qawmu Nūĥin Wa 'Aşĥābu Ar-Rassi Wa Thamūdu 12. Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na wakaazi wa Rassi na Thamudi. كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوح ٍ وَأَصْحَابُ الرَّسِّ وَثَمُودُ
Wa `Ādun Wa Fir`awnu Wa 'Ikhwānu Lūţin 13. Na A'di na Firauni na kaumu ya Lut'i. وَعَاد ٌ وَفِرْعَوْنُ وَإِخْوَانُ لُوط ٍ
Wa 'Aşĥābu Al-'Aykati Wa Qawmu Tubba`in Kullun Kadhdhaba Ar-Rusula Faĥaqqa Wa`īdi 14. Na wakaazi wa Machakani, na watu wa Tubbaa'. Wote hao waliwakanusha Mitume, kwa hivyo onyo likathibitika juu yao. وَأَصْحَابُ الأَيْكَةِ وَقَوْمُ تُبَّع ٍ كُلّ ٌ كَذَّبَ الرُّسُلَ فَحَقَّ وَعِيدِ
'Afa`ayīnā Bil-Khalqi Al-'Awwali Bal Hum Fī Labsin Min Khalqin Jadīdin 15. Kwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza. Bali wao wamo katika shaka tu juu ya umbo jipya. أَفَعَيِينَا بِالْخَلْقِ الأَوَّلِ بَلْ هُمْ فِي لَبْس ٍ مِنْ خَلْق ٍ جَدِيد ٍ
Wa Laqad Khalaq Al-'Insāna Wa Na`lamu Mā Tuwaswisu Bihi Nafsuhu Wa Naĥnu 'Aqrabu 'Ilayhi Min Ĥabli Al-Warīdi 16. Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake. وَلَقَدْ خَلَقْنَا الإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِه ِِ نَفْسُه ُُ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ
'Idh Yatalaqqá Al-Mutalaqqiyāni `Ani Al-Yamīni Wa `Ani Ash-Shimāli Qa`īdun 17. Wanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na kushotoni. إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيد ٌ
Mā Yalfižu Min Qawlin 'Illā Ladayhi Raqībun `Atīdun 18. Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari. مَا يَلْفِظُ مِنْ قَوْل ٍ إِلاَّ لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيد ٌ
Wa Jā'at Sakratu Al-Mawti Bil-Ĥaqqi Dhālika Mā Kunta Minhu Taĥīdu 19. Na uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyo kuwa ukiyakimbia. وَجَاءَتْ سَكْرَةُ الْمَوْتِ بِالْحَقِّ ذَلِكَ مَا كُنْتَ مِنْهُ تَحِيدُ
Wa Nufikha Fī Aş-Şūri Dhālika Yawmu Al-Wa`īdi 20. Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi. وَنُفِخَ فِي الصُّورِ ذَلِكَ يَوْمُ الْوَعِيدِ
Wa Jā'at Kullu Nafsin Ma`ahā Sā'iqun Wa Shahīdun 21. Na kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji na shahidi. وَجَاءَتْ كُلُّ نَفْس ٍ مَعَهَا سَائِق ٌ وَشَهِيد ٌ
Laqad Kunta Fī Ghaflatin Min Hādhā Fakashafnā `Anka Ghā'aka Fabaşaruka Al-Yawma Ĥadīdun 22. (Aambiwe): Kwa hakika ulikuwa umeghafilika na haya; basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali. لَقَدْ كُنْتَ فِي غَفْلَة ٍ مِنْ هَذَا فَكَشَفْنَا عَنْكَ غِطَاءَكَ فَبَصَرُكَ الْيَوْمَ حَدِيد ٌ
Wa Qāla Qarīnuhu Hādhā Mā Ladayya `Atīdun 23. Na mwenzake atasema: Huyu niliye naye mimi kesha tayarishwa. وَقَالَ قَرِينُه ُُ هَذَا مَا لَدَيَّ عَتِيد ٌ
'Alqiyā Fī Jahannama Kulla Kaffārin `Anīdin 24. Mtupeni katika Jahannamu kila kafiri mwenye inda, أَلْقِيَا فِي جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيد ٍ
Mannā`in Lilkhayri Mu`tadin Murībin 25. Akatazaye kheri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka, مَنَّاع ٍ لِلْخَيْرِ مُعْتَد ٍ مُرِيب ٍ
Al-Ladhī Ja`ala Ma`a Allāhi 'Ilahāan 'Ākhara Fa'alqiyāhu Fī Al-`Adhābi Ash-Shadīdi 26. Aliye weka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali. الَّذِي جَعَلَ مَعَ اللَّهِ إِلَها ً آخَرَ فَأَلْقِيَاه ُُ فِي الْعَذَابِ الشَّدِيدِ
Qāla Qarīnuhu Rabbanā Mā 'Aţghaytuhu Wa Lakin Kāna Fī Đalālin Ba`īdin 27. Mwenzake aseme: Ee Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali. قَالَ قَرِينُه ُُ رَبَّنَا مَا أَطْغَيْتُه ُُ وَلَكِنْ كَانَ فِي ضَلاَل ٍ بَعِيد ٍ
Qāla Lā Takhtaşimū Ladayya Wa Qad Qaddamtu 'Ilaykum Bil-Wa`īdi 28. (Mwenyezi Mungu) aseme: Msigombane mbele yangu. Nilikuleteeni mbele onyo langu. قَالَ لاَ تَخْتَصِمُوا لَدَيَّ وَقَدْ قَدَّمْتُ إِلَيْكُمْ بِالْوَعِيدِ
Mā Yubaddalu Al-Qawlu Ladayya Wa Mā 'Anā Bižallāmin Lil`abīdi 29. Mbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja wangu. مَا يُبَدَّلُ الْقَوْلُ لَدَيَّ وَمَا أَنَا بِظَلاَّم ٍ لِلْعَبِيدِ
Yawma Naqūlu Lijahannama Hal Amtala'ti Wa Taqūlu Hal Min Mazīdin 30. Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada? يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلْ امْتَلَأْتِ وَتَقُولُ هَلْ مِنْ مَزِيد ٍ
Wa 'Uzlifati Al-Jannatu Lilmuttaqīna Ghayra Ba`īdin 31. Na Pepo italetwa karibu kwa ajili ya wachamngu, haitakuwa mbali. وَأُزْلِفَتِ الْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ غَيْرَ بَعِيد ٍ
dhā Mā Tū`adūna Likulli 'Awwābin Ĥafīžin 32. Haya ndiyo mnayo ahidiwa kwa kila mwenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu na akajilinda. هَذَا مَا تُوعَدُونَ لِكُلِّ أَوَّابٍ حَفِيظ ٍ
Man Khashiya Ar-Raĥmana Bil-Ghaybi Wa Jā'a Biqalbin Munībin 33. Mwenye kumwogopa Mwingi wa Rehema hali kuwa hamwoni, na akaja kwa moyo ulio elekea- مَنْ خَشِيَ الرَّحْمَنَ بِالْغَيْبِ وَجَاءَ بِقَلْب ٍ مُنِيب ٍ
Adkhulūhā Bisalāmin Dhālika Yawmu Al-Khulūdi 34. (Ataambiwa) ingieni kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya daima dawamu. ادْخُلُوهَا بِسَلاَم ٍ ذَلِكَ يَوْمُ الْخُلُودِ
Lahum Mā Yashā'ūna Fīhā Wa Ladaynā Mazīdun 35. Humo watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada. لَهُمْ مَا يَشَاءُونَ فِيهَا وَلَدَيْنَا مَزِيد ٌ
Wa Kam 'Ahlaknā Qablahum Min Qarnin Hum 'Ashaddu Minhum Baţshāan Fanaqqabū Fī Al-Bilādi Hal Min Maĥīşin 36. Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao walio kuwa na nguvu zaidi kuliko hawa! Nao walitanga tanga katika nchi nyingi. Je! Walipata pa kukimbilia? وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُمْ مِنْ قَرْنٍ هُمْ أَشَدُّ مِنْهُمْ بَطْشا ً فَنَقَّبُوا فِي الْبِلاَدِ هَلْ مِنْ مَحِيص ٍ
'Inna Fī Dhālika Ladhikrá Liman Kāna Lahu Qalbun 'Aw 'Alqá As-Sam`a Wa Huwa Shahīdun 37. Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia. إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَه ُُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيد ٌ
Wa Laqad Khalaq As-Samāwāti Wa Al-'Arđa Wa Mā Baynahumā Fī Sittati 'Ayyāmin Wa Mā Massanā Min Lughūbin 38. Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina yao mnamo siku sita; na wala hayakutugusa machofu. وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّام ٍ وَمَا مَسَّنَا مِنْ لُغُوب ٍ
Fāşbir `Alá Mā Yaqūlūna Wa Sabbiĥ Biĥamdi Rabbika Qabla Ţulū`i Ash-Shamsi Wa Qabla Al-Ghurūbi 39. Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa. فَاصْبِرْ عَلَى مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ
Wa Mina Al-Layli Fasabbiĥhu Wa 'Adbāra As-Sujūdi 40. Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu. وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَأَدْبَارَ السُّجُودِ
Wa Astami` Yawma Yunādi Al-Munādi Min Makānin Qarībin 41. Na sikiliza siku atapo nadi mwenye kunadi kutoka pahala karibu. وَاسْتَمِعْ يَوْمَ يُنَادِ الْمُنَادِ مِنْ مَكَان ٍ قَرِيب ٍ
Yawma Yasma`ūna Aş-Şayĥata Bil-Ĥaqqi Dhālika Yawmu Al-Khurūji 42. Siku watakapo sikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kufufuka. يَوْمَ يَسْمَعُونَ الصَّيْحَةَ بِالْحَقِّ ذَلِكَ يَوْمُ الْخُرُوجِ
'Innā Naĥnu Nuĥyī Wa Numītu Wa 'Ilaynā Al-Maşīru 43. Hakika Sisi tunahuisha na tunafisha, na kwetu Sisi ndio marejeo. إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَإِلَيْنَا الْمَصِيرُ
Yawma Tashaqqaqu Al-'Arđu `Anhum Sirā`āan Dhālika Ĥashrun `Alaynā Yasīrun 44. Siku itapo wapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi. يَوْمَ تَشَقَّقُ الأَرْضُ عَنْهُمْ سِرَاعا ً ذَلِكَ حَشْرٌ عَلَيْنَا يَسِير ٌ
Naĥnu 'A`lamu Bimā Yaqūlūna Wa Mā 'Anta `Alayhim Bijabbārin Fadhakkir Bil-Qur'āni Man Yakhāfu Wa`īdi 45. Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur'ani anaye liogopa onyo. *   نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ وَمَا أَنْتَ عَلَيْهِمْ بِجَبَّار ٍ فَذَكِّرْ بِالْقُرْآنِ مَنْ يَخَافُ وَعِيدِ
Next Sūrah