Ţā-Sīn Tilka 'Āyātu Al-Qur'āni Wa Kitābin Mubīnin  | 1. T'aa Siin. (T'.S.), Hizi ni Aya za Qur'ani
na Kitabu kinacho bainisha; | طَا-سِين تِلْكَ آيَاتُ الْقُرْآنِ وَكِتَاب ٍ مُبِين ٍ |
Hudáan Wa Bushrá Lilmu'uminīna  | 2. Uwongofu na bishara kwa Waumini, | هُدى ً وَبُشْرَى لِلْمُؤْمِنِينَ |
Al-Ladhīna Yuqīmūna Aş-Şalāata Wa Yu'utūna Az-Zakāata Wa Hum Bil-'Ākhirati Hum Yūqinūna  | 3. Ambao wanashika Sala, na wanatoa Zaka, na Akhera
wana yakini nayo. | الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلاَةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ بِالآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ |
'Inna Al-Ladhīna Lā Yu'uminūna Bil-'Ākhirati Zayyannā Lahum 'A`mālahum Fahum Ya`mahūna  | 4. Kwa hakika wale wasio iamini Akhera tumewapambia
vitendo vyao, kwa hivyo wanatangatanga ovyo. | إِنَّ الَّذِينَ لاَ يُؤْمِنُونَ بِالآخِرَةِ زَيَّنَّا لَهُمْ أَعْمَالَهُمْ فَهُمْ يَعْمَهُونَ |
'Ūlā'ika Al-Ladhīna Lahum Sū'u Al-`Adhābi Wa Hum Fī Al-'Ākhirati Humu Al-'Akhsarūna  | 5. Hao ndio watapata adhabu mbaya kabisa, na hao
katika Akhera ndio watapata khasara zaidi. | أُوْلَائِكَ الَّذِينَ لَهُمْ سُوءُ الْعَذَابِ وَهُمْ فِي الآخِرَةِ هُمُ الأَخْسَرُونَ |
Wa 'Innaka Latulaqqá Al-Qur'āna Min Ladun Ĥakīmin `Alīmin  | 6. Na hakika wewe unafundishwa Qur'ani inayo tokana
kwake Mwenye hikima Mwenye kujua. | وَإِنَّكَ لَتُلَقَّى الْقُرْآنَ مِنْ لَدُنْ حَكِيمٍ عَلِيم ٍ |
'Idh Qāla Mūsá Li'hlihi 'Innī 'Ānastu Nārāan Sa'ātīkum Minhā Bikhabarin 'Aw 'Ātīkum Bishihābin Qabasin La`allakum Taşţalūna  | 7. (Kumbuka) Musa alipo waambia ahali zake: Hakika
nimeona moto, nitakwenda nikuleteeni khabari, au nitakuleteeni kijinga
kinacho waka ili mpate kuota moto. | إِذْ قَالَ مُوسَى لِأهْلِهِ~ِ إِنِّي آنَسْتُ نَارا ً سَآتِيكُمْ مِنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ آتِيكُمْ بِشِهَاب ٍ قَبَس ٍ لَعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ |
Falammā Jā'ahā Nūdiya 'An Būrika Man Fī An-Nāri Wa Man Ĥawlahā Wa Subĥāna Allāhi Rabbi Al-`Ālamīna  | 8. Basi alipo fika ilinadiwa: Amebarikiwa aliomo
katika moto huu na walioko pembezoni mwake. Na ametakasika Mwenyezi Mungu,
Mola Mlezi wa walimwengu wote. | فَلَمَّا جَاءَهَا نُودِيَ أَنْ بُورِكَ مَنْ فِي النَّارِ وَمَنْ حَوْلَهَا وَسُبْحَانَ اللَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ |
Yā Mūsá 'Innahu 'Anā Allāhu Al-`Azīzu Al-Ĥakīmu  | 9. Ewe Musa! Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu,
Mwenye nguvu, Mwenye hikima. | يَا مُوسَى إِنَّهُ~ُ أَنَا اللَّهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ |
Wa 'Alqi `Aşāka Falammā Ra'āhā Tahtazzu Ka'annahā Jānnun Wallá Mudbirāan Wa Lam Yu`aqqib Yā Mūsá Lā Takhaf 'Innī Lā Yakhāfu Ladayya Al-Mursalūna  | 10. Na itupe fimbo yako! Alipo iona ikitikisika
kama nyoka, aligeuka nyuma wala hakungoja. Ewe Musa! Usikhofu! Hakika hawakhofu
mbele yangu Mitume. | وَأَلْقِ عَصَاكَ فَلَمَّا رَآهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَانّ ٌ وَلَّى مُدْبِرا ً وَلَمْ يُعَقِّبْ يَا مُوسَى لاَ تَخَفْ إِنِّي لاَ يَخَافُ لَدَيَّ الْمُرْسَلُونَ |
'Illā Man Žalama Thumma Baddala Ĥusnāan Ba`da Sū'in Fa'innī Ghafūrun Raĥīmun  | 11. Lakini aliye dhulumu, kisha akabadilisha
wema baada ya ubaya, basi Mimi ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. | إِلاَّ مَنْ ظَلَمَ ثُمَّ بَدَّلَ حُسْنا ً بَعْدَ سُوء ٍ فَإِنِّي غَفُور ٌ رَحِيم ٌ |
Wa 'Adkhil Yadaka Fī Jaybika Takhruj Bayđā'a Min Ghayri Sū'in Fī Tis`i 'Āyātin 'Ilá Fir`awna Wa Qawmihi 'Innahum Kānū Qawmāan Fāsiqīna  | 12. Na ingiza mkono wako katika mfuko wako, utatoka
mweupe bila ya maradhi. Ni katika Ishara tisa za kumpelekea Firauni na
kaumu yake. Hakika hao walikuwa watu waovu. | وَأَدْخِلْ يَدَكَ فِي جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوء ٍ فِي تِسْعِ آيَات ٍ إِلَى فِرْعَوْنَ وَقَوْمِهِ~ِ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْما ً فَاسِقِينَ |
Falammā Jā'at/hum 'Āyātunā Mubşiratan Qālū Hādhā Siĥrun Mubīnun  | 13. Basi zilipo wafikia Ishara zetu hizo zenye
kuonyesha, wakasema: Huu ni uchawi dhaahiri. | فَلَمَّا جَاءَتْهُمْ آيَاتُنَا مُبْصِرَة ً قَالُوا هَذَا سِحْر ٌ مُبِين ٌ |
Wa Jaĥadū Bihā Wa Astayqanat/hā 'Anfusuhum Žulmāan Wa `Ulūwāan Fānžur Kayfa Kāna `Āqibatu Al-Mufsidīna  | 14. Na wakazikataa kwa dhulma na kujivuna, na
hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo. Basi angalia ulikuwaje mwisho
wa mafisadi! | وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنْفُسُهُمْ ظُلْما ً وَعُلُوّا ً فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ |
Wa Laqad 'Ātaynā Dāwūda Wa Sulaymāna `Ilmāan Wa Qālā Al-Ĥamdu Lillāhi Al-Ladhī Fađđalanā `Alá Kathīrin Min `Ibādihi Al-Mu'uminīna  | 15. Na hakika tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu,
na wakasema: Alhamdu Lillahi, Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu aliye
tufadhilisha kuliko wengi katika waja wake Waumini. | وَلَقَدْ آتَيْنَا دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ عِلْما ً وَقَالاَ الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي فَضَّلَنَا عَلَى كَثِير ٍ مِنْ عِبَادِهِ الْمُؤْمِنِينَ |
Wa Waritha Sulaymānu Dāwūda Wa Qāla Yā 'Ayyuhā An-Nāsu `Ullimnā Manţiqa Aţ-Ţayri Wa 'Ūtīnā Min Kulli Shay'in 'Inna Hādhā Lahuwa Al-Fađlu Al-Mubīnu  | 16. Na Sulaiman alimrithi Daudi, na akasema:
Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege, na tumepewa kila kitu. Hakika hii
ni fadhila iliyo dhaahiri. | وَوَرِثَ سُلَيْمَانُ دَاوُودَ وَقَالَ يَاأَيُّهَا النَّاسُ عُلِّمْنَا مَنطِقَ الطَّيْرِ وَأُوتِينَا مِنْ كُلِّ شَيْء ٍ إِنَّ هَذَا لَهُوَ الْفَضْلُ الْمُبِينُ |
Wa Ĥushira Lisulaymāna Junūduhu Mina Al-Jinni Wa Al-'Insi Wa Aţ-Ţayri Fahum Yūza`ūna  | 17. Na alikusanyiwa Sulaiman majeshi yake ya
majini, na watu, na ndege; nayo yakapangwa kwa nidhamu. | وَحُشِرَ لِسُلَيْمَانَ جُنُودُه ُُ مِنَ الْجِنِّ وَالإِنْسِ وَالطَّيْرِ فَهُمْ يُوزَعُونَ |
Ĥattá 'Idhā 'Ataw `Alá Wādī An-Namli Qālat Namlatun Yā 'Ayyuhā An-Namlu Adkhulū Masākinakum Lā Yaĥţimannakum Sulaymānu Wa Junūduhu Wa Hum Lā Yash`urūna  | 18. Mpaka walipo fika kwenye bonde la wadudu
chungu, alisema mdudu chungu mmoja: Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani
mwenu, asikupondeni Sulaiman na majeshi yake bila ya wao kutambua. | حَتَّى إِذَا أَتَوْا عَلَى وَادِي النَّمْلِ قَالَتْ نَمْلَة ٌ يَاأَيُّهَا النَّمْلُ ادْخُلُوا مَسَاكِنَكُمْ لاَ يَحْطِمَنَّكُمْ سُلَيْمَانُ وَجُنُودُه ُُ وَهُمْ لاَ يَشْعُرُونَ |
Fatabassama Đāĥikāan Min Qawlihā Wa Qāla Rabbi 'Awzi`nī 'An 'Ashkura Ni`mataka Allatī 'An`amta `Alayya Wa `Alá Wa A-Dayya Wa 'An 'A`mala Şāliĥāan Tarđāhu Wa 'Adkhilnī Biraĥmatika Fī `Ibādika Aş-Şāliĥīna  | 19. Basi (Sulaiman) akatabasamu akacheka kwa
neno hili, na akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako
uliyo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo,
na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema. | فَتَبَسَّمَ ضَاحِكا ً مِنْ قَوْلِهَا وَقَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَى وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحا ً تَرْضَاه ُُ وَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ |
Wa Tafaqqada Aţ-Ţayra Faqāla Mā Lī Lā 'Ará Al-Hud/huda 'Am Kāna Mina Al-Ghā'ibīna  | 20. Na akawakagua ndege, na akasema: Imekuwaje,
mbona simwoni Hud-hud, au amekuwa miongoni mwa walio ghibu? | وَتَفَقَّدَ الطَّيْرَ فَقَالَ مَا لِي لاَ أَرَى الْهُدْهُدَ أَمْ كَانَ مِنَ الْغَائِبِينَ |
La'u`adhdhibannahu `Adhābāan Shadīdāan 'Aw La'adhbaĥannahu 'Aw Laya'tiyanī Bisulţānin Mubīnin  | 21. Kwa yakini nitamuadhibu kwa adhabu kali,
au nitamchinja, au aniletee hoja ya kutosha. | لَأُعَذِّبَنَّه ُُ عَذَابا ً شَدِيداً أَوْ لَأَذْبَحَنَّهُ~ُ أَوْ لَيَأْتِيَنِي بِسُلْطَان ٍ مُبِين ٍ |
Famakatha Ghayra Ba`īdin Faqāla 'Aĥaţtu Bimā Lam Tuĥiţ Bihi Wa Ji'tuka Min Saba'iin Binaba'iin Yaqīnin  | 22. Basi (Hud-hud) akakaa si mbali na akasema:
Nimegundua usilo gundua wewe, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na
nakuletea khabari za yakini. | فَمَكَثَ غَيْرَ بَعِيد ٍ فَقَالَ أَحَطتُ بِمَا لَمْ تُحِطْ بِه ِِ وَجِئْتُكَ مِنْ سَبَإ ٍ بِنَبَإ ٍ يَقِين ٍ |
'Innī Wa Jadttu Amra'atan Tamlikuhum Wa 'Ūtiyat Min Kulli Shay'in Wa Lahā `Arshun `Ažīmun  | 23. Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala,
naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa. | إِنِّي وَجَدتُّ امْرَأَة ً تَمْلِكُهُمْ وَأُوتِيَتْ مِنْ كُلِّ شَيْء ٍ وَلَهَا عَرْشٌ عَظِيم ٌ |
Wa Jadtuhā Wa Qawmahā Yasjudūna Lilshshamsi Min Dūni Allāhi Wa Zayyana Lahumu Ash-Shayţānu 'A`mālahum Faşaddahum `Ani As-Sabīli Fahum Lā Yahtadūna  | 24. Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia
jua badala ya Mwenyezi Mungu; na Shet'ani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia
Njia. Kwa hivyo hawakuongoka, | وَجَدْتُهَا وَقَوْمَهَا يَسْجُدُونَ لِلشَّمْسِ مِنْ دُونِ اللَّهِ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ فَهُمْ لاَ يَهْتَدُونَ |
'Allā Yasjudū Lillāhi Al-Ladhī Yukhriju Al-Khab'a Fī As-Samāwāti Wa Al-'Arđi Wa Ya`lamu Mā Tukhfūna Wa Mā Tu`linūna  | 25. Na hawamsujudii Mwenyezi Mungu ambaye huyatoa
yaliyo fichikana katika mbingu na ardhi, na anayajua mnayo yaficha na mnayo
yatangaza. | أَلاَّ يَسْجُدُوا لِلَّهِ الَّذِي يُخْرِجُ الْخَبْءَ فِي السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُخْفُونَ وَمَا تُعْلِنُونَ |
Allāhu Lā 'Ilāha 'Illā Huwa Rabbu Al-`Arshi Al-`Ažīmi  | 26. Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Mola
Mlezi wa A'rshi tukufu.. | اللَّهُ لاَ إِلَهَ~َ إِلاَّ هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ |
Qāla Sananžuru 'Aşadaqta 'Am Kunta Mina Al-Kādhibīna  | 27. Akasema (Sulaiman): Tutatazama umesema kweli
au wewe ni miongoni mwa waongo. | قَالَ سَنَنظُرُ أَصَدَقْتَ أَمْ كُنتَ مِنَ الْكَاذِبِينَ |
Adh/hab Bikitābī Hādhā Fa'alqih 'Ilayhim Thumma Tawalla `Anhum Fānžur Mādhā Yarji`ūna  | 28. Nenda na barua yangu hii na uwafikishie,
kisha waache na utazame watarejesha nini. | اذْهَب بِكِتَابِي هَذَا فَأَلْقِه إِلَيْهِمْ ثُمَّ تَوَلَّ عَنْهُمْ فَانظُرْ مَاذَا يَرْجِعُونَ |
Qālat Yā 'Ayyuhā Al-Mala'u 'Innī 'Ulqiya 'Ilayya Kitābun Karīmun  | 29. (Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika
nimeletewa barua tukufu. | قَالَتْ يَا أَيُّهَا المَلَأُ إِنِّي أُلْقِيَ إِلَيَّ كِتَاب ٌ كَرِيم ٌ |
'Innahu Min Sulaymāna Wa 'Innahu Bismi Allāhi Ar-Raĥmāni Ar-Raĥīmi  | 30. Imetoka kwa Sulaiman nayo ni: Kwa jina la
Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. | إِنَّه ُُ مِنْ سُلَيْمَانَ وَإِنَّه ُُ بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ |
'Allā Ta`lū `Alayya Wa 'Tūnī Muslimīna  | 31. Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi
mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri. | أَلاَّ تَعْلُوا عَلَيَّ وَأْتُونِي مُسْلِمِينَ |
Qālat Yā 'Ayyuhā Al-Mala'u 'Aftūnī Fī 'Amrī Mā Kuntu Qāţi`atan 'Amrāan Ĥattá Tash/hadūni  | 32. Akasema: Enyi wahishimiwa! Nipeni shauri
katika jambo langu hili, kwani mimi sikati shauri yoyote mpaka mhudhurie. | قَالَتْ يَاأَيُّهَا المَلَأُ أَفْتُونِي فِي أَمْرِي مَا كُنتُ قَاطِعَةً أَمْراً حَتَّى تَشْهَدُونِ |
Qālū Naĥnu 'Ūlū Qūwatin Wa 'Ūlū Ba'sin Shadīdin Wa Al-'Amru 'Ilayki Fānžurī Mādhā Ta'murīna  | 33. Wakasema: Sisi ni wenye nguvu na wakali kwa
vita; na amri iko kwako, basi tazama ni nini unaamrisha. | قَالُوا نَحْنُ أُوْلُوا قُوَّة ٍ وَأُولُوا بَأْس ٍ شَدِيد ٍ وَالأَمْرُ إِلَيْكِ فَانظُرِي مَاذَا تَأْمُرِينَ |
Qālat 'Inna Al-Mulūka 'Idhā Dakhalū Qaryatan 'Afsadūhā Wa Ja`alū 'A`izzata 'Ahlihā 'Adhillatan Wa Kadhalika Yaf`alūna  | 34. Akasema: Hakika wafalme wanapo uingia mji
wanauharibu, na wanawafanya wale watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo
ndivyo watendavyo. | قَالَتْ إِنَّ الْمُلُوكَ إِذَا دَخَلُوا قَرْيَةً أَفْسَدُوهَا وَجَعَلُوا أَعِزَّةَ أَهْلِهَا أَذِلَّة ً وَكَذَلِكَ يَفْعَلُونَ |
Wa 'Innī Mursilatun 'Ilayhim Bihadīyatin Fanāžiratun Bima Yarji`u Al-Mursalūna  | 35. Lakini mimi nitawapelekea zawadi, nami nitangoja
watakayo rudi nayo wajumbe. | وَإِنِّي مُرْسِلَة ٌ إِلَيْهِمْ بِهَدِيَّة ٍ فَنَاظِرَة ٌ بِمَ يَرْجِعُ الْمُرْسَلُونَ |
Falammā Jā'a Sulaymāna Qāla 'Atumiddūnani Bimālin Famā 'Ātāniya Allāhu Khayrun Mimmā 'Ātākum Bal 'Antum Bihadīyatikum Tafraĥūna  | 36. Basi alipo fika (mjumbe) kwa Sulaiman, alisema
(Sulaiman): Hivyo ndio nyinyi mnanisaidia kwa mali? Aliyo nipa Mwenyezi
Mungu ni bora zaidi kuliko aliyo kupeni nyinyi. Lakini nyinyi mnafurahia
hii zawadi yenu. | فَلَمَّا جَاءَ سُلَيْمَانَ قَالَ أَتُمِدُّونَنِ بِمَال ٍ فَمَا آتَانِيَ اللَّهُ خَيْر ٌ مِمَّا آتَاكُمْ بَلْ أَنْتُمْ بِهَدِيَّتِكُمْ تَفْرَحُونَ |
Arji` 'Ilayhim Falana'tiyannahum Bijunūdin Lā Qibala Lahum Bihā Wa Lanukhrijannahum Minhā 'Adhillatan Wa Hum Şāghirūna  | 37. Rejea kwao! Kwa yakini sisi tutawajia kwa
majeshi wasio yaweza kuyakabili. Na hakika tutawatoa humo na hali wao wamekuwa
madhalili na wanyonge. | ارْجِعْ إِلَيْهِمْ فَلَنَأْتِيَنَّهُمْ بِجُنُود ٍ لاَ قِبَلَ لَهُمْ بِهَا وَلَنُخْرِجَنَّهُمْ مِنْهَا أَذِلَّة ً وَهُمْ صَاغِرُونَ |
Qāla Yā 'Ayyuhā Al-Mala'u 'Ayyukum Ya'tīnī Bi`arshihā Qabla 'An Ya'tūnī Muslimīna  | 38. Akasema: Enyi wahishimiwa! Ni nani kati yenu
atakaye niletea kiti chake cha enzi kabla hawajanijia nao wamekwisha salimu
amri. | قَالَ يَاأَيُّهَا المَلَأُ أَيُّكُمْ يَأْتِينِي بِعَرْشِهَا قَبْلَ أَنْ يَأْتُونِي مُسْلِمِينَ |
Qāla `Ifrytun Mina Al-Jinni 'Anā 'Ātīka Bihi Qabla 'An Taqūma Min Maqāmika Wa 'Innī `Alayhi Laqawīyun 'Amīnun  | 39. Akasema: Afriti, katika majini: Mimi nitakuletea
kabla hujainuka pahala pako hapo. Na mimi kwa hakika nina nguvu na muaminifu. | قَالَ عِفْريت ٌ مِنَ الْجِنِّ أَنَا آتِيكَ بِه ِِ قَبْلَ أَنْ تَقُومَ مِنْ مَقَامِكَ وَإِنِّي عَلَيْهِ لَقَوِيٌّ أَمِين ٌ |
Qāla Al-Ladhī `Indahu `Ilmun Mina Al-Kitābi 'Anā 'Ātīka Bihi Qabla 'An Yartadda 'Ilayka Ţarfuka Falammā Ra'āhu Mustaqirrāan `Indahu Qāla Hādhā Min Fađli Rabbī Liyabluwanī 'A'ashkuru 'Am 'Akfuru Wa Man Shakara Fa'innamā Yashkuru Linafsihi Wa Man Kafara Fa'inna Rabbī Ghanīyun Karīmun  | 40. Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea
kabla ya kupepesa jicho lako. Basi alipo kiona kimewekwa mbele yake, akasema:
Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru
au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa
ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na
Karimu. | قَالَ الَّذِي عِنْدَه ُُ عِلْم ٌ مِنَ الْكِتَابِ أَنَا آتِيكَ بِه ِِ قَبْلَ أَنْ يَرْتَدَّ إِلَيْكَ طَرْفُكَ فَلَمَّا رَآهُ مُسْتَقِرّاً عِنْدَه ُُ قَالَ هَذَا مِنْ فَضْلِ رَبِّي لِيَبْلُوَنِي أَأَشْكُرُ أَمْ أَكْفُرُ وَمَنْ شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِه ِِ وَمَنْ كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّي غَنِيّ ٌ كَرِيم ٌ |
Qāla Nakkirū Lahā `Arshahā Nanžur 'Atahtadī 'Am Takūnu Mina Al-Ladhīna Lā Yahtadūna  | 41. Akasema: Mgeuzieni kiti chake cha enzi hiki,
tuone ataongoka, au atakuwa miongoni mwa wasio ongoka. | قَالَ نَكِّرُوا لَهَا عَرْشَهَا نَنظُرْ أَتَهْتَدِي أَمْ تَكُونُ مِنَ الَّذِينَ لاَ يَهْتَدُونَ |
Falammā Jā'at Qīla 'Ahakadhā `Arshuki Qālat Ka'annahu Huwa Wa 'Ūtīnā Al-`Ilma Min Qablihā Wa Kunnā Muslimīna  | 42. Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti
chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman
na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na
tukawa Waislamu. | فَلَمَّا جَاءَتْ قِيلَ أَهَكَذَا عَرْشُكِ قَالَتْ كَأَنَّه ُُ هُوَ وَأُوتِينَا الْعِلْمَ مِنْ قَبْلِهَا وَكُنَّا مُسْلِمِينَ |
Wa Şaddahā Mā Kānat Ta`budu Min Dūni Allāhi 'Innahā Kānat Min Qawmin Kāfirīna  | 43. Na yale aliyo kuwa akiyaabudu badala ya Mwenyezi
Mungu yalimzuilia. Hakika yeye (Malkia) alikuwa katika kaumu ya makafiri. | وَصَدَّهَا مَا كَانَتْ تَعْبُدُ مِنْ دُونِ اللَّهِ إِنَّهَا كَانَتْ مِنْ قَوْم ٍ كَافِرِينَ |
Qīla Lahā Adkhulī Aş-Şarĥa Falammā Ra'at/hu Ĥasibat/hu Lujjatan Wa Kashafat `An Sāqayhā Qāla 'Innahu Şarĥun Mumarradun Min Qawārīra Qālat Rabbi 'Innī Žalamtu Nafsī Wa 'Aslamtu Ma`a Sulaymāna Lillāhi Rabbi Al-`Ālamīna  | 44. Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba.
Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake.
(Sulaiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema
(Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea
pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. | قِيلَ لَهَا ادْخُلِي الصَّرْحَ فَلَمَّا رَأَتْهُ حَسِبَتْهُ لُجَّة ً وَكَشَفَتْ عَنْ سَاقَيْهَا قَالَ إِنَّه ُُ صَرْح ٌ مُمَرَّد ٌ مِنْ قَوَارِيرَ قَالَتْ رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي وَأَسْلَمْتُ مَعَ سُلَيْمَانَ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ |
Wa Laqad 'Arsalnā 'Ilá Thamūda 'Akhāhum Şāliĥāan 'Ani A`budū Allāha Fa'idhā Hum Farīqāni Yakhtaşimūna  | 45. Na kwa kina Thamud tulimtuma ndugu yao Saleh
kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu. Basi wakawa makundi mawili yanayo
gombana. | وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَى ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحاً أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ فَإِذَا هُمْ فَرِيقَانِ يَخْتَصِمُونَ |
Qāla Yā Qawmi Lima Tasta`jilūna Bis-Sayyi'ati Qabla Al-Ĥasanati Lawlā Tastaghfirūna Allāha La`allakum Turĥamūna  | 46. Akasema: Enyi watu wangu! Kwa nini mnauhimiza
uwovu kabla ya wema? Kwa nini hamuombi msamaha kwa Mwenyezi Mungu ili mrehemewe? | قَالَ يَاقَوْمِ لِمَ تَسْتَعْجِلُونَ بِالسَّيِّئَةِ قَبْلَ الْحَسَنَةِ لَوْلاَ تَسْتَغْفِرُونَ اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ |
Qālū Aţţayyarnā Bika Wa Biman Ma`aka Qāla Ţā'irukum `Inda Allāhi Bal 'Antum Qawmun Tuftanūna  | 47. Wakasema: Tuna kisirani nawe na wale walio
pamoja nawe. Yeye akasema: Uaguzi wa ukorofi wenu uko kwa Mwenyezi Mungu;
lakini nyinyi ni watu mnao jaribiwa. | قَالُوا اطَّيَّرْنَا بِكَ وَبِمَنْ مَعَكَ قَالَ طَائِرُكُمْ عِنْدَ اللَّهِ بَلْ أَنْتُمْ قَوْم ٌ تُفْتَنُونَ |
Wa Kāna Fī Al-Madīnati Tis`atu Rahţin Yufsidūna Fī Al-'Arđi Wa Lā Yuşliĥūna  | 48. Na walikuwamo mjini watu tisa wakifanya ufisadi
katika nchi wala hawafanyi la maslaha. | وَكَانَ فِي الْمَدِينَةِ تِسْعَةُ رَهْط ٍ يُفْسِدُونَ فِي الأَرْضِ وَلاَ يُصْلِحُونَ |
Qālū Taqāsamū Billāhi Lanubayyitannahu Wa 'Ahlahu Thumma Lanaqūlanna Liwalīyihi Mā Shahidnā Mahlika 'Ahlihi Wa 'Innā Laşādiqūna  | 49. Wakasema: Apishaneni kwa Mwenyezi Mungu tutamshambulia
usiku yeye na ahali zake; kisha tutamwambia mrithi wake: Sisi hatukuona
maangamizo ya watu wake, na sisi bila ya shaka tunasema kweli. | قَالُوا تَقَاسَمُوا بِاللَّهِ لَنُبَيِّتَنَّه ُُ وَأَهْلَه ُُ ثُمَّ لَنَقُولَنَّ لِوَلِيِّه ِِ مَا شَهِدْنَا مَهْلِكَ أَهْلِه ِِ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ |
Wa Makarū Makrāan Wa Makarnā Makrāan Wa Hum Lā Yash`urūna  | 50. Basi wakapanga mipango yao, na Sisi tukapanga
mipango yetu, na wao hawatambui. | وَمَكَرُوا مَكْرا ً وَمَكَرْنَا مَكْرا ً وَهُمْ لاَ يَشْعُرُونَ |
Fānžur Kayfa Kāna `Āqibatu Makrihim 'Annā Dammarnāhum Wa Qawmahum 'Ajma`īna  | 51. Basi angalia ulivyo kuwa mwisho wa mipango
yao, ya kwamba tuliwaangamiza wao pamoja na watu wao wote. | فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ مَكْرِهِمْ أَنَّا دَمَّرْنَاهُمْ وَقَوْمَهُمْ أَجْمَعِينَ |
Fatilka Buyūtuhum Khāwiyatan Bimā Žalamū 'Inna Fī Dhālika La'āyatan Liqawmin Ya`lamūna  | 52. Basi hizo nyumba zao ni tupu kwa sababu ya
walivyo dhulumu. Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara kwa watu wanao
jua. | فَتِلْكَ بُيُوتُهُمْ خَاوِيَة ً بِمَا ظَلَمُوا إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَة ً لِقَوْم ٍ يَعْلَمُونَ |
Wa 'Anjaynā Al-Ladhīna 'Āmanū Wa Kānū Yattaqūna  | 53. Na tukawaokoa wale walio amini na walio kuwa
wanamchamngu. | وَأَنجَيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ |
Wa Lūţāan 'Idh Qāla Liqawmihi 'Ata'tūna Al-Fāĥishata Wa 'Antum Tubşirūna  | 54. Na Lut'i alipo waambia watu wake: Je! Mnafanya
uchafu nanyi mnaona? | وَلُوطا ً إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ~ِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ وَأَنْتُمْ تُبْصِرُونَ |
'A'innakum Lata'tūna Ar-Rijāla Shahwatan Min Dūni An-Nisā' Bal 'Antum Qawmun Tajhalūna  | 55. Hivyo nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio
badala ya wanawake? Hakika nyinyi ni watu mnao fanya ujinga kabisa! | أَئِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَة ً مِنْ دُونِ النِسَاء بَلْ أَنْتُمْ قَوْم ٌ تَجْهَلُونَ |
Famā Kāna Jawāba Qawmihi 'Illā 'An Qālū 'Akhrijū 'Āla Lūţin Min Qaryatikum 'Innahum 'Unāsun Yataţahharūna  | 56. Basi haikuwa jawabu ya watu wake ila ni kusema:
Wafukuzeni wafwasi wa Lut'i katika mji wenu. Hao ni watu wanao jitia usafi. | فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ~ِ إِلاَّ أَنْ قَالُوا أَخْرِجُوا آلَ لُوط ٍ مِنْ قَرْيَتِكُمْ إِنَّهُمْ أُنَاس ٌ يَتَطَهَّرُونَ |
Fa'anjaynāhu Wa 'Ahlahu 'Illā Amra'atahu Qaddarnāhā Mina Al-Ghābirīna  | 57. Basi tukamwokoa yeye na ahali zake, isipo
kuwa mkewe; tukamkadiria katika walio baki nyuma. | فَأَنجَيْنَاه ُُ وَأَهْلَهُ~ُ إِلاَّ امْرَأَتَه ُُ قَدَّرْنَاهَا مِنَ الْغَابِرِينَ |
Wa 'Amţarnā `Alayhim Maţarāan Fasā'a Maţaru Al-Mundharīna  | 58. Na tukawanyeshea mvua. Ni ovu kweli kweli
hiyo mvua ya walio kwisha onywa. | وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِمْ مَطَرا ً فَسَاءَ مَطَرُ الْمُنذَرِينَ |
Quli Al-Ĥamdu Lillāhi Wa Salāmun `Alá `Ibādihi Al-Ladhīna Aşţafá 'Āālllahu Khayrun 'Ammā Yushrikūna  | 59. Sema: Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa ni kwa
Mwenyezi Mungu! Na amani ishuke juu ya waja wake alio wateuwa. Je! Mwenyezi
Mungu ni bora, au wale wanao washirikisha naye? | قُلِ الْحَمْدُ لِلَّهِ وَسَلاَمٌ عَلَى عِبَادِهِ الَّذِينَ اصْطَفَى آاللَّهُ خَيْرٌ أَمَّا يُشْرِكُونَ |
'Amman Khalaqa As-Samāwāti Wa Al-'Arđa Wa 'Anzala Lakum Mina As-Samā'i Mā'an Fa'anbatnā Bihi Ĥadā'iqa Dhāta Bahjatin Mā Kāna Lakum 'An Tunbitū Shajarahā 'A'ilahun Ma`a Allāhi Bal Hum Qawmun Ya`dilūna  | 60. AU NANI yule aliye ziumba mbingu na ardhi,
na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani
zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu
pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu walio potoka. | أَمَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَأَنزَلَ لَكُمْ مِنَ السَّمَاءِ مَاء ً فَأَنْبَتْنَا بِه ِِ حَدَائِقَ ذَاتَ بَهْجَة ٍ مَا كَانَ لَكُمْ أَنْ تُنْبِتُوا شَجَرَهَا أَءِلَه ٌ ٌ مَعَ اللَّهِ بَلْ هُمْ قَوْم ٌ يَعْدِلُونَ |
'Amman Ja`ala Al-'Arđa Qarārāan Wa Ja`ala Khilālahā 'Anhārāan Wa Ja`ala Lahā Rawāsiya Wa Ja`ala Bayna Al-Baĥrayni Ĥājizāan 'A'ilahun Ma`a Allāhi Bal 'Aktharuhum Lā Ya`lamūna  | 61. Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa
kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina
ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali
wengi wao hawajui. | أَمَّنْ جَعَلَ الأَرْضَ قَرَارا ً وَجَعَلَ خِلاَلَهَا أَنْهَارا ً وَجَعَلَ لَهَا رَوَاسِيَ وَجَعَلَ بَيْنَ الْبَحْرَيْنِ حَاجِزاً أَءِلَه ٌ ٌ مَعَ اللَّهِ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لاَ يَعْلَمُونَ |
'Amman Yujību Al-Muđţarra 'Idhā Da`āhu Wa Yakshifu As-Sū'a Wa Yaj`alukum Khulafā'a Al-'Arđi 'A'ilahun Ma`a Allāhi Qalīlāan Mā Tadhakkarūna  | 62. Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale
anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je!
Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia. | أَمَّنْ يُجِيبُ الْمُضطَرَّ إِذَا دَعَاه ُُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الأَرْضِ أَءِلَه ٌ ٌ مَعَ اللَّهِ قَلِيلا ً مَا تَذَكَّرُونَ |
'Amman Yahdīkum Fī Žulumāti Al-Barri Wa Al-Baĥri Wa Man Yursilu Ar-Riyāĥa Bushrāan Bayna Yaday Raĥmatihi 'A'ilahun Ma`a Allāhi Ta`ālá Allāhu `Ammā Yushrikūna  | 63. Au nani yule anaye kuongoeni katika giza
la bara na bahari, na akazipeleka pepo kuleta bishara kabla ya rehema zake?
Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya
wanao washirikisha naye. | أَمَّنْ يَهْدِيكُمْ فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَمَنْ يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرا ً بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ~ِ أَءِلَه ٌ ٌ مَعَ اللَّهِ تَعَالَى اللَّهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ |
'Amman Yabda'u Al-Khalqa Thumma Yu`īduhu Wa Man Yarzuqukum Mina As-Samā'i Wa Al-'Arđi 'A'ilahun Ma`a Allāhi Qul Hātū Burhānakum 'In Kuntum Şādiqīna  | 64. Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha?
Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu
pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema
kweli. | أَمَّنْ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُه ُُ وَمَنْ يَرْزُقُكُمْ مِنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ أَءِلَه ٌ ٌ مَعَ اللَّهِ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِنْ كُنتُمْ صَادِقِينَ |
Qul Lā Ya`lamu Man Fī As-Samāwāti Wa Al-'Arđi Al-Ghayba 'Illā Allāhu Wa Mā Yash`urūna 'Ayyāna Yub`athūna  | 65. Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye
ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Wala wao hawajui lini watafufuliwa. | قُلْ لاَ يَعْلَمُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ الْغَيْبَ إِلاَّ اللَّهُ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ |
Bal Addāraka `Ilmuhum Fī Al-'Ākhirati Bal Hum Fī Shakkin Minhā Bal Hum Minhā `Amūna  | 66. Kwani huo ujuzi wao umefikilia kuijua Akhera?
Bali wao wamo katika shaka nayo tu, bali wao ni vipofu nayo. | بَلْ ادَّارَكَ عِلْمُهُمْ فِي الآخِرَةِ بَلْ هُمْ فِي شَكّ ٍ مِنْهَا بَلْ هُمْ مِنْهَا عَمُونَ |
Wa Qāla Al-Ladhīna Kafarū 'A'idhā Kunnā Turābāan Wa 'Ābā'uunā 'A'innā Lamukhrajūna  | 67. Na wakasema walio kufuru: Tutapo kuwa mchanga,
sisi na baba zetu, hivyo kweli tutakuja tolewa? | وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَئِذَا كُنَّا تُرَابا ً وَآبَاؤُنَا أَئِنَّا لَمُخْرَجُونَ |
Laqad Wu`idnā Hādhā Naĥnu Wa 'Ābā'uunā Min Qablu 'In Hādhā 'Illā 'Asāţīru Al-'Awwalīna  | 68. Haya haya tuliahidiwa sisi na baba zetu zamani.
Hayakuwa haya ila ni hadithi za uwongo za watu wa kale. | لَقَدْ وُعِدْنَا هَذَا نَحْنُ وَآبَاؤُنَا مِنْ قَبْلُ إِنْ هَذَا إِلاَّ أَسَاطِيرُ الأَوَّلِينَ |
Qul Sīrū Fī Al-'Arđi Fānžurū Kayfa Kāna `Āqibatu Al-Mujrimīna  | 69. Sema: Nendeni katika ardhi, na tazameni ulikuwaje
mwisho wa wakosefu. | قُلْ سِيرُوا فِي الأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِينَ |
Wa Lā Taĥzan `Alayhim Wa Lā Takun Fī Đayqin Mimmā Yamkurūna  | 70. Wala usiwahuzunukie wala usiwe katika dhiki
kwa sababu ya hila zao wanazo zifanya. | وَلاَ تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلاَ تَكُنْ فِي ضَيْق ٍ مِمَّا يَمْكُرُونَ |
Wa Yaqūlūna Matá Hādhā Al-Wa`du 'In Kuntum Şādiqīna  | 71. Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa
mnasema kweli? | وَيَقُولُونَ مَتَى هَذَا الْوَعْدُ إِنْ كُنتُمْ صَادِقِينَ |
Qul `Asá 'An Yakūna Radifa Lakum Ba`đu Al-Ladhī Tasta`jilūna  | 72. Sema: Asaa ni karibu kukufikieni sehemu ya
yale mnayo yahimiza. | قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ رَدِفَ لَكُمْ بَعْضُ الَّذِي تَسْتَعْجِلُونَ |
Wa 'Inna Rabbaka Ladhū Fađlin `Alá An-Nāsi Wa Lakinna 'Aktharahum Lā Yashkurūna  | 73. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye fadhila
kwa watu, lakini wengi wao hawashukuru. | وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لاَ يَشْكُرُونَ |
Wa 'Inna Rabbaka Laya`lamu Mā Tukinnu Şudūruhum Wa Mā Yu`linūna  | 74. Na hakika Mola wako Mlezi anayajua yanayo
ficha vifua vyao na wanayo yatangaza. | وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ |
Wa Mā Min Ghā'ibatin Fī As-Samā'i Wa Al-'Arđi 'Illā Fī Kitābin Mubīnin  | 75. Na hakuna siri katika mbingu na ardhi ila
imo katika Kitabu kinacho bainisha. | وَمَا مِنْ غَائِبَة ٍ فِي السَّمَاءِ وَالأَرْضِ إِلاَّ فِي كِتَا< |