23) Sūrat Al-Mu'uminūna

Printed format

23) سُورَة الْمُؤْمِنُونَ

Qad 'Aflaĥa Al-Mu'uminūna 1. HAKIKA wamefanikiwa Waumini, قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ
Al-Ladhīna Hum Fī Şalātihim Khāshi`ūna 2. Ambao ni wanyenyekevu katika Sala zao, الَّذِينَ هُمْ فِي صَلاَتِهِمْ خَاشِعُونَ
Wa Al-Ladhīna Hum `Ani Al-Laghwi Mu`rūna 3. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi, وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ
Wa Al-Ladhīna Hum Lilzzakāati Fā`ilūna 4. Na ambao wanatoa Zaka, وَالَّذِينَ هُمْ لِلزَّكَاةِ فَاعِلُونَ
Wa Al-Ladhīna Hum Lifurūjihim Ĥāfižūna 5.Na ambao wanazilinda tupu zao, وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ
'Illā `Alá 'Azwājihim 'W Mā Malakat 'Aymānuhum Fa'innahum Ghayru Malūmīna 6. Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. إِلاَّ عَلَى أَزْوَاجِهِمْ أوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ
Famani Abtaghá Warā'a Dhālika Fa'ūlā'ika Humu Al-`Ādūna 7. Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka. فَمَنِ ابْتَغَى وَرَاءَ ذَلِكَ فَأُوْلَائِكَ هُمُ الْعَادُونَ
Wa Al-Ladhīna Hum Li'mānātihim Wa `Ahdihim Rā`ūna 8. Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao, وَالَّذِينَ هُمْ لِأمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ
Wa Al-Ladhīna Hum `Alá Şalawātihim Yuĥāfižūna 9. Na ambao Sala zao wanazihifadhi - وَالَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ
'Ūlā'ika Humu Al-Wārithūna 10. Hao ndio warithi, أُوْلَائِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ
Al-Ladhīna Yarithūna Al-Firdawsa Hum Fīhā Khālidūna 11. Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo. الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ
Wa Laqad Khalaq Al-'Insāna Min Sulālatin Min Ţīnin 12. Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo. وَلَقَدْ خَلَقْنَا الإِنسَانَ مِنْ سُلاَلَة ٍ مِنْ طِين ٍ
Thumma Ja`alnāhu Nuţfatan Fī Qarārin Makīnin 13. Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. ثُمَّ جَعَلْنَاه ُُ نُطْفَة ً فِي قَرَار ٍ مَكِين ٍ
Thumma Khalaq An-Nuţfata `Alaqatan Fakhalaq Al-`Alaqata Muđghatan Fakhalaq Al-Muđghata `Ižāmāan Fakasawnā Al-`Ižāma Laĥmāan Thumma 'Ansha'nāhu Khalqāan 'Ākhara Fatabāraka Allāhu 'Aĥsanu Al-Khāliqīna 14. Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji. ثُمَّ خَلَقْنَا النُّطْفَةَ عَلَقَة ً فَخَلَقْنَا الْعَلَقَةَ مُضْغَة ً فَخَلَقْنَا الْمُضْغَةَ عِظَاما ً فَكَسَوْنَا الْعِظَامَ لَحْما ً ثُمَّ أَنشَأْنَاه ُُ خَلْقا ً آخَرَ فَتَبَارَكَ اللَّهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ
Thumma 'Innakum Ba`da Dhālika Lamayyitūna 15. Kisha hakika nyinyi baada ya hayo mtakufa. ثُمَّ إِنَّكُمْ بَعْدَ ذَلِكَ لَمَيِّتُونَ
Thumma 'Innakum Yawma Al-Qiyāmati Tub`athūna 16. Kisha hakika nyinyi Siku ya Kiyama mtafufuliwa. ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ تُبْعَثُونَ
Wa Laqad Khalaqnā Fawqakum Sab`a Ţarā'iqa Wa Mā Kunnā `Ani Al-Khalqi Ghāfilīna 17. Na kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe. وَلَقَدْ خَلَقْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعَ طَرَائِقَ وَمَا كُنَّا عَنِ الْخَلْقِ غَافِلِينَ
Wa 'Anzalnā Mina As-Samā'i Mā'an Biqadarin Fa'askannāhu Fī Al-'Arđi Wa 'Innā `Alá Dhahābin Bihi Laqādirūna 18. Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa. وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاء ً بِقَدَر ٍ فَأَسْكَنَّاه ُُ فِي الأَرْضِ وَإِنَّا عَلَى ذَهَاب ٍ بِه ِِ لَقَادِرُونَ
Fa'ansha'nā Lakum Bihi Jannātin Min Nakhīlin Wa 'A`nābin Lakum Fīhā Fawākihu Kathīratun Wa Minhā Ta'kulūna 19. Kwa maji hayo tukakufanyieni bustani za mitende na mizabibu, mnapata humo matunda mengi, na katika hayo mnakula; فَأَنشَأْنَا لَكُمْ بِه ِِ جَنَّات ٍ مِنْ نَخِيل ٍ وَأَعْنَاب ٍ لَكُمْ فِيهَا فَوَاكِه ُُ كَثِيرَة ٌ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ
Wa Shajaratan Takhruju Min Ţūri Saynā'a Tanbutu Bid-Duhni Wa Şibghin Lil'ākilīna 20. Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unatoa mafuta na kuwa kitoweo kwa walao. وَشَجَرَة ً تَخْرُجُ مِنْ طُورِ سَيْنَاءَ تَنْبُتُ بِالدُّهْنِ وَصِبْغ ٍ لِلآكِلِينَ
Wa 'Inna Lakum Al-'An`āmi La`ibratan Nusqīkum Mimmā Fī Buţūnihā Wa Lakum Fīhā Manāfi`u Kathīratun Wa Minhā Ta'kulūna 21. Na hakika mnayo mazingatio makubwa katika nyama hoa - tunakunywesheni katika vile viliomo matumboni mwao, na nyinyi mnapata katika hao manufaa mengi, na pia mnawala. وَإِنَّ لَكُمْ فِي الأَنعَامِ لَعِبْرَة ً نُسقِيكُمْ مِمَّا فِي بُطُونِهَا وَلَكُمْ فِيهَا مَنَافِعُ كَثِيرَة ٌ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ
Wa `Alayhā Wa `Alá Al-Fulki Tuĥmalūna 22. Na juu yao na juu ya marikebu mnabebwa. وَعَلَيْهَا وَعَلَى الْفُلْكِ تُحْمَلُونَ
Wa Laqad 'Arsalnā Nūĥāan 'Ilá Qawmihi Faqāla Yā Qawmi A`budū Allāha Mā Lakum Min 'Ilahin Ghayruhu 'Afalā Tattaqūna 23. Na hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu asiye kuwa Yeye. Basi je! Hamwogopi? وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحا ً إِلَى قَوْمِه ِِ فَقَالَ يَاقَوْمِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُمْ مِنْ إِلَه ٍٍ غَيْرُهُ~ُ أَفَلاَ تَتَّقُونَ
Faqāla Al-Mala'u Al-Ladhīna Kafarū Min Qawmihi Mā Hādhā 'Illā Basharun Mithlukum Yurīdu 'An Yatafađđala `Alaykum Wa Law Shā'a Allāhu La'anzala Malā'ikatan Mā Sami`nā Bihadhā Fī 'Ābā'inā Al-'Awwalīna 24. Walisema wale wakuu walio kufuru katika watu wake: Huyu si chochote ila ni mtu tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu amependa basi yakini angeli teremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa baba zetu wa zamani. فَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ قَوْمِه ِِ مَا هَذَا إِلاَّ بَشَر ٌ مِثْلُكُمْ يُرِيدُ أَنْ يَتَفَضَّلَ عَلَيْكُمْ وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَأَنزَلَ مَلاَئِكَة ً مَا سَمِعْنَا بِهَذَا فِي آبَائِنَا الأَوَّلِينَ
'In Huwa 'Illā Rajulun Bihi Jinnatun Fatarabbaşū Bihi Ĥattá Ĥīnin 25. Huyu si lolote ila ni mtu mwenye wazimu. Basi mngojeeni tu kwa muda. إِنْ هُوَ إِلاَّ رَجُل ٌ بِه ِِ جِنَّة ٌ فَتَرَبَّصُوا بِه ِِ حَتَّى حِين ٍ
Qāla Rabbi Anşurnī Bimā Kadhdhabūni 26. Akasema (Nuhu): Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa kuwa wamenikanusha. قَالَ رَبِّ انصُرْنِي بِمَا كَذَّبُونِ
Fa'awĥaynā 'Ilayhi 'Ani Aşna`i Al-Fulka Bi'a`yuninā Wa Waĥyinā Fa'idhā Jā'a 'Amrunā Wa Fāra At-Tannūru Fāsluk Fīhā Min Kullin Zawjayni Athnayni Wa 'Ahlaka 'Illā Man Sabaqa `Alayhi Al-Qawlu Minhum Wa Lā Tukhāţibnī Fī Al-Ladhīna Žalamū 'Innahum Mughraqūna 27. Tukampa wahyi: Unda jahazi mbele ya macho yetu na uwongozi wetu! Basi itapo fika amri yetu na ikafurika tanuri, hapo waingize ndani yake wa kila namna dume na jike, na ahali zako, isipo kuwa yule ambaye katika wao juu yake imekwisha tangulia kauli. Wala usinitajie hao walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa. فَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِ أَنِ اصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا فَإِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ فَاسْلُكْ فِيهَا مِنْ كُلّ ٍ زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلاَّ مَنْ سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ مِنْهُمْ وَلاَ تُخَاطِبْنِي فِي الَّذِينَ ظَلَمُوا إِنَّهُمْ مُغْرَقُونَ
Fa'idhā Astawayta 'Anta Wa Man Ma`aka `Alá Al-Fulki Faquli Al-Ĥamdu Lillāhi Al-Ladhī Najjānā Mina Al-Qawmi Až-Žālimīna 28. Basi utakapo tulia wewe na walio pamoja nawe humo marikebuni, sema: Alhamdulillahi Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, aliye tuokoa na watu madhaalimu! فَإِذَا اسْتَوَيْتَ أَنْتَ وَمَنْ مَعَكَ عَلَى الْفُلْكِ فَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي نَجَّانَا مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
Wa Qul Rabbi 'Anzilnī Munzalāan Mubārakāan Wa 'Anta Khayru Al-Munzilīna 29. Na sema: Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora wa wateremshaji. وَقُلْ رَبِّ أَنزِلْنِي مُنْزَلا ً مُبَارَكا ً وَأَنْتَ خَيْرُ الْمُنزِلِينَ
'Inna Fī Dhālika La'āyātin Wa 'In Kunnā Lamubtalīna 30. Hakika katika hayo yapo mazingatio. Na kwa yakini Sisi ni wenye kuwafanyia mtihani. إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَات ٍ وَإِنْ كُنَّا لَمُبْتَلِينَ
Thumma 'Ansha'nā Min Ba`dihim Qarnāan 'Ākharīna 31. Kisha baada yao tukaanzisha kizazi kingine. ثُمَّ أَنشَأْنَا مِنْ بَعْدِهِمْ قَرْنا ً آخَرِينَ
Fa'arsalnā Fīhim Rasūlāan Minhum 'Ani A`budū Allāha Mā Lakum Min 'Ilahin Ghayruhu 'Afalā Tattaqūna 32. Tukawapelekea Mtume miongoni mwao, kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu asiye kuwa Yeye. Jee, hamwogopi? فَأَرْسَلْنَا فِيهِمْ رَسُولا ً مِنْهُمْ أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُمْ مِنْ إِلَه ٍٍ غَيْرُهُ~ُ أَفَلاَ تَتَّقُونَ
Wa Qāla Al-Mala'u Min Qawmihi Al-Ladhīna Kafarū Wa Kadhdhabū Biliqā'i Al-'Ākhirati Wa 'Atrafnāhum Al-Ĥayāati Ad-Dunyā Mā Hādhā 'Illā Basharun Mithlukum Ya'kulu Mimmā Ta'kulūna Minhu Wa Yashrabu Mimmā Tashrabūna 33. Na wakubwa katika watu wake walio kufuru na wakakanusha mkutano wa Akhera, na tukawadekeza kwa starehe katika maisha ya dunia, walisema: Huyu si chochote ila ni binaadamu kama nyinyi; anakula mlacho, na anakunywa mnywacho. وَقَالَ الْمَلَأُ مِنْ قَوْمِهِ الَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِلِقَاءِ الآخِرَةِ وَأَتْرَفْنَاهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا مَا هَذَا إِلاَّ بَشَر ٌ مِثْلُكُمْ يَأْكُلُ مِمَّا تَأْكُلُونَ مِنْهُ وَيَشْرَبُ مِمَّا تَشْرَبُونَ
Wa La'in 'Aţa`tum Basharāan Mithlakum 'Innakum 'Idhāan Lakhāsirūna 34. Na nyinyi mkimt'ii mtu kama nyinyi basi hakika mtakuwa khasarani. وَلَئِنْ أَطَعْتُمْ بَشَرا ً مِثْلَكُمْ إِنَّكُمْ إِذا ً لَخَاسِرُونَ
'Aya`idukum 'Annakum 'Idhā Mittum Wa Kuntum Turābāan Wa `Ižāmāan 'Annakum Mukhrajūna 35. Hivyo anakuahidini ati ya kwamba mtakapo kufa na mkawa udongo na mifupa kuwa mtatolewa? أَيَعِدُكُمْ أَنَّكُمْ إِذَا مِتُّمْ وَكُنتُمْ تُرَابا ً وَعِظَاماً أَنَّكُمْ مُخْرَجُونَ
Hayhāta Hayhāta Limā Tū`adūna 36. Hayawi! Hayawi hayo mnayo ahidiwa. هَيْهَاتَ هَيْهَاتَ لِمَا تُوعَدُونَ
'In Hiya 'Illā Ĥayātunā Ad-Dunyā Namūtu Wa Naĥyā Wa Mā Naĥnu Bimabthīna 37. Hapana ila uhai wetu wa duniani tu, tunakufa na kuishi basi. Wala sisi hatutafufuliwa. إِنْ هِيَ إِلاَّ حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ
'In Huwa 'Illā Rajulun Aftará `Alá Allāhi Kadhibāan Wa Mā Naĥnu Lahu Bimu'uminīna 38. Huyu si lolote ila ni mtu anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, wala sisi sio wa kumuamini. إِنْ هُوَ إِلاَّ رَجُل ٌ افْتَرَى عَلَى اللَّهِ كَذِبا ً وَمَا نَحْنُ لَه ُُ بِمُؤْمِنِينَ
Qāla Rabbi Anşurnī Bimā Kadhdhabūni 39. Akasema: Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa sababu wananikanusha. قَالَ رَبِّ انصُرْنِي بِمَا كَذَّبُونِ
Qāla `Ammā Qalīlin Layuşbiĥunna Nādimīna 40. (Mwenyezi Mungu) akasema: Baada ya muda mchache watakuwa wenye kujuta. قَالَ عَمَّا قَلِيل ٍ لَيُصْبِحُنَّ نَادِمِينَ
Fa'akhadhat/humu Aş-Şayĥatu Bil-Ĥaqqi Faja`alnāhum Ghuthā'an Fabu`dāan Lilqawmi Až-Žālimīna 41. Basi ukawanyakua ukelele kwa haki, na tukawafanya kama takataka zinazo elea juu ya maji. Ikapotelea mbali kaumu ya madhaalimu! فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ بِالْحَقِّ فَجَعَلْنَاهُمْ غُثَاء ً فَبُعْدا ً لِلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
Thumma 'Ansha'nā Min Ba`dihim Qurūnāan 'Ākharīna 42. Kisha tukaleta baada yao vizazi vingine. ثُمَّ أَنشَأْنَا مِنْ بَعْدِهِمْ قُرُونا ً آخَرِينَ
Mā Tasbiqu Min 'Ummatin 'Ajalahā Wa Mā Yasta'khirūna 43. Hapana umma uwezao kutanguliza ajali yake wala kuikawiza. مَا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ
Thumma 'Arsalnā Rusulanā Tatrā Kulla Mā Jā'a 'Ummatan Rasūluhā Kadhdhabūhu Fa'atba`nā Ba`đahum Ba`đāan Wa Ja`alnāhum 'Aĥādītha Fabu`dāan Liqawmin Lā Yu'uminūna 44. Kisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipo wafikia Mtume wao walimkanusha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya ni hadithi za kusimuliwa. Wakapotelea mbali watu wasio amini. ثُمَّ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا تَتْرَا كُلَّ مَا جَاءَ أُمَّة ً رَسُولُهَا كَذَّبُوه ُُ فَأَتْبَعْنَا بَعْضَهُمْ بَعْضا ً وَجَعَلْنَاهُمْ أَحَادِيثَ فَبُعْدا ً لِقَوْم ٍ لاَ يُؤْمِنُونَ
Thumma 'Arsalnā Mūsá Wa 'Akhāhu Hārūna Bi'āyātinā Wa Sulţānin Mubīnin 45. Kisha tukamtuma Musa na nduguye, Haaruni, pamoja na ishara zetu na hoja zilizo wazi. ثُمَّ أَرْسَلْنَا مُوسَى وَأَخَاه ُُ هَارُونَ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَان ٍ مُبِين ٍ
'Ilá Fir`awna Wa Mala'ihi Fāstakbarū Wa Kānū Qawmāan `Ālīna 46. Kumwendea Firauni na wakuu wake. Lakini walijivuna, nao walikuwa watu majeuri. إِلَى فِرْعَوْنَ وَمَلَئِه ِِ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْماً عَالِينَ
Faqālū 'Anu'uminu Libasharayni Mithlinā Wa Qawmuhumā Lanā `Ābidūna 47. Wakasema: Je, tuwaamini wanaadamu wawili hawa kama sisi, na ambao watu wao ni watumwa wetu? فَقَالُوا أَنُؤْمِنُ لِبَشَرَيْنِ مِثْلِنَا وَقَوْمُهُمَا لَنَا عَابِدُونَ
Fakadhdhabūhumā Fakānū Mina Al-Muhlakīna 48. Basi wakawakanusha, na wakawa miongoni mwa walio angamizwa. فَكَذَّبُوهُمَا فَكَانُوا مِنَ الْمُهْلَكِينَ
Wa Laqad 'Ātaynā Mūsá Al-Kitāba La`allahum Yahtadūna 49. Na hakika tulimpa Musa Kitabu ili wapate kuongoka. وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ
Wa Ja`alnā Abna Maryama Wa 'Ummahu 'Āyatan Wa 'Āwaynāhumā 'Ilá Rabwatin Dhāti Qarārin Wa Ma`īnin 50. Na tukamfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ni Ishara, na tukawapa makimbilio kwenda mahali palipo inuka penye utulivu na chemchem za maji. وَجَعَلْنَا ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ آيَة ً وَآوَيْنَاهُمَا إِلَى رَبْوَة ٍ ذَاتِ قَرَار ٍ وَمَعِين ٍ
Yā 'Ayyuhā Ar-Rusulu Kulū Mina Aţ-Ţayyibāti Wa A`malū Şāliĥāan 'Innī Bimā Ta`malūna `Alīmun 51. Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayo yatenda. يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحا ً إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيم ٌ
Wa 'Inna Hadhihi 'Ummatukum 'Ummatan Wāĥidatan Wa 'Anā Rabbukum Fa Attaqūni 52. Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi. وَإِنَّ هَذِهِ~ِ أُمَّتُكُمْ أُمَّة ً وَاحِدَة ً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ
Fataqaţţa`ū 'Amrahum Baynahum Zuburāan Kullu Ĥizbin Bimā Ladayhim Farūna 53. Lakini walikatiana jambo lao mapande mbali mbali. Kila kundi likifurahia kwa waliyo nayo. فَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُمْ بَيْنَهُمْ زُبُرا ً كُلُّ حِزْب ٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ
FadharhumGhamratihim Ĥattá Ĥīnin 54. Basi waache katika ghafla yao kwa muda. فَذَرْهُمْ فِي غَمْرَتِهِمْ حَتَّى حِين ٍ
'Ayaĥsabūna 'Annamā Numidduhum Bihi Min Mālin Wa Banīna 55. Je! Wanadhani ya kuwa kwa vile tunavyo wapa mali na watoto أَيَحْسَبُونَ أَنَّمَا نُمِدُّهُمْ بِه ِِ مِنْ مَال ٍ وَبَنِينَ
Nusāri`u Lahum Al-Khayrāti Bal Lā Yash`urūna 56. Ndio tunawahimizia kheri? Lakini wenyewe hawatambui. نُسَارِعُ لَهُمْ فِي الْخَيْرَاتِ بَل لاَ يَشْعُرُونَ
'Inna Al-Ladhīna Hum Min Khashyati Rabbihim Mushfiqūna 57. Kwa hakika hao ambao kwa kumwogopa Mola wao Mlezi wananyenyekea, إِنَّ الَّذِينَ هُمْ مِنْ خَشْيَةِ رَبِّهِمْ مُشْفِقُونَ
Wa Al-Ladhīna Hum Bi'āyāti Rabbihim Yu'uminūna 58. Na wale ambao Ishara za Mola wao Mlezi wanaziamini, وَالَّذِينَ هُمْ بِآيَاتِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ
Wa Al-Ladhīna Hum Birabbihim Lā Yushrikūna 59. Na wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi, وَالَّذِينَ هُمْ بِرَبِّهِمْ لاَ يُشْرِكُونَ
Wa Al-Ladhīna Yu'utūna Mā 'Ātaw Wa Qulūbuhum Wa Jilatun 'Annahum 'Ilá Rabbihim Rāji`ūna 60. Na wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinagopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi, وَالَّذِينَ يُؤْتُونَ مَا آتَوا وَقُلُوبُهُمْ وَجِلَةٌ أَنَّهُمْ إِلَى رَبِّهِمْ رَاجِعُونَ
'Ūlā'ika Yusāri`ūna Fī Al-Khayrāti Wa Hum Lahā Sābiqūna 61. Basi wote hao ndio wanao kimbilia katika mambo ya kheri, na ndio watakao tangulia kuyafikia. أُوْلَائِكَ يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَهُمْ لَهَا سَابِقُونَ
Wa Lā Nukallifu Nafsāan 'Illā Wus`ahā Wa Ladaynā Kitābun Yanţiqu Bil-Ĥaqqi Wa Hum Lā Yužlamūn 62. Na hatuilazimishi nafsi ila kwa kadri ya uwezo wake. Na tunacho kitabu kisemacho kweli. Nao hawatadhulumiwa. وَلاَ نُكَلِّفُ نَفْسا ً إِلاَّ وُسْعَهَا وَلَدَيْنَا كِتَاب ٌ يَنطِقُ بِالْحَقِّ وَهُمْ لاَ يُظْلَمُون
Bal QulūbuhumGhamratin Min Hādhā Wa Lahum 'A`mālun Min Dūni Dhālika Hum Lahā `Āmilūna 63. Lakini nyoyo zao zimeghafilika na hayo, na wanavyo vitendo vinginevyo wanavyo vifanya. بَلْ قُلُوبُهُمْ فِي غَمْرَة ٍ مِنْ هَذَا وَلَهُمْ أَعْمَال ٌ مِنْ دُونِ ذَلِكَ هُمْ لَهَا عَامِلُونَ
Ĥattá 'Idhā 'Akhadhnā Mutrafīhim Bil-`Adhābi 'Idhā Hum Yaj'arūna 64. Hata tutakapo watia katika adhabu wale walio dekezwa kwa starehe kati yao, hapo ndipo watapo yayatika. حَتَّى إِذَا أَخَذْنَا مُتْرَفِيهِمْ بِالْعَذَابِ إِذَا هُمْ يَجْأَرُونَ
Lā Taj'arū Al-Yawma 'Innakum Minnā Lā Tunşarūna 65. Msiyayatike leo! Hakika nyinyi hamtanusurika nasi. لاَ تَجْأَرُوا الْيَوْمَ إِنَّكُمْ مِنَّا لاَ تُنصَرُونَ
Qad Kānat 'Āyātī Tutlá `Alaykum Fakuntum `Alá 'A`qābikum Tankişūna 66. Hakika zilikuwa Aya zangu mkisomewa, nanyi mkirudi nyuma juu ya visigino vyenu, قَدْ كَانَتْ آيَاتِي تُتْلَى عَلَيْكُمْ فَكُنتُمْ عَلَى أَعْقَابِكُمْ تَنكِصُونَ
Mustakbirīna Bihi Sāmirāan Tahjurūna 67. Na huku mkitakabari na usiku mkiizungumza (Qur'ani) kwa dharau. مُسْتَكْبِرِينَ بِه ِِ سَامِرا ً تَهْجُرُونَ
'Afalam Yaddabbarū Al-Qawla 'Am Jā'ahum Mā Lam Ya'ti 'Ābā'ahumu Al-'Awwalīna 68. Je, hawakuifikiri kauli, au yamewajia yasiyo wafikia baba zao wa zamani? أَفَلَمْ يَدَّبَّرُوا الْقَوْلَ أَمْ جَاءَهُمْ مَا لَمْ يَأْتِ آبَاءَهُمُ الأَوَّلِينَ
'Am Lam Ya`rifū Rasūlahum Fahum Lahu Munkirūna 69. Au hawakumjua Mtume wao, ndio maana wanamkataa? أَمْ لَمْ يَعْرِفُوا رَسُولَهُمْ فَهُمْ لَه ُُ مُنكِرُونَ
'Am Yaqūlūna Bihi Jinnatun Bal Jā'ahum Bil-Ĥaqqi Wa 'Aktharuhum Lilĥaqqi Kārihūna 70. Au wanasema: Ana wazimu? Bali amewajia kwa Haki, na wengi wao wanaichukia Haki. أَمْ يَقُولُونَ بِه ِِ جِنَّة ٌ بَلْ جَاءَهُمْ بِالْحَقِّ وَأَكْثَرُهُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ
Wa Lawi Attaba`a Al-Ĥaqqu 'Ahwā'ahum Lafasadati As-Samāwātu Wa Al-'Arđu Wa Man Fīhinna Bal 'Ataynāhum Bidhikrihim Fahum `An Dhikrihim Mu`rūna 71. Na lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao. وَلَوِ اتَّبَعَ الْحَقُّ أَهْوَاءَهُمْ لَفَسَدَتِ السَّمَاوَاتُ وَالأَرْضُ وَمَنْ فِيهِنَّ بَلْ أَتَيْنَاهُمْ بِذِكْرِهِمْ فَهُمْ عَنْ ذِكْرِهِمْ مُعْرِضُونَ
'Am Tas'aluhum Kharjāan Fakharāju Rabbika Khayrun Wa Huwa Khayru Ar-Rāziqīna 72. Au unawaomba ujira? Lakini ujira wa Mola wako Mlezi ni bora, na Yeye ndiye Mbora wa wanao ruzuku. أَمْ تَسْأَلُهُمْ خَرْجا ً فَخَرَاجُ رَبِّكَ خَيْر ٌ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ
Wa 'Innaka Latad`ūhum 'Ilá Şirāţin Mustaqīmin 73. Na kwa yakini wewe unawaita kwenye Njia Iliyo Nyooka. وَإِنَّكَ لَتَدْعُوهُمْ إِلَى صِرَاط ٍ مُسْتَقِيم ٍ
Wa 'Inna Al-Ladhīna Lā Yu'uminūna Bil-'Ākhirati `Ani Aş-Şirāţi Lanākibūna 74. Na hakika wale wasio iamini Akhera wanajitenga na Njia hiyo. وَإِنَّ الَّذِينَ لاَ يُؤْمِنُونَ بِالآخِرَةِ عَنِ الصِّرَاطِ لَنَاكِبُونَ
Wa Law Raĥimnāhum Wa Kashafnā Mā Bihim Min Đurrin Lalajjū Fī Ţughyānihim Ya`mahūna 75. Na lau tungeli warehemu na tukawaondolea shida waliyo nayo bila ya shaka wangeli endelea katika upotofu wao vile vile, wakitangatanga. وَلَوْ رَحِمْنَاهُمْ وَكَشَفْنَا مَا بِهِمْ مِنْ ضُرّ ٍ لَلَجُّوا فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ
Wa Laqad 'Akhadhnāhum Bil-`Adhābi Famā Astakānū Lirabbihim Wa Mā Yatađarra`ūna 76. Na hakika tuliwatia adhabu kali; lakini hawakuelekea kwa Mola wao Mlezi wala hawakunyenyekea. وَلَقَدْ أَخَذْنَاهُمْ بِالْعَذَابِ فَمَا اسْتَكَانُوا لِرَبِّهِمْ وَمَا يَتَضَرَّعُونَ
Ĥattá 'Idhā Fataĥnā `Alayhim Bābāan Dhā `Adhābin Shadīdin 'Idhā Hum Fīhi Mublisūna 77. Mpaka tulipo wafungulia mlango wa adhabu kali, hapo ndipo wakawa wenye kukata tamaa. حَتَّى إِذَا فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَابا ً ذَا عَذَاب ٍ شَدِيد ٍ إِذَا هُمْ فِيه ِِ مُبْلِسُونَ
Wa Huwa Al-Ladhī 'Ansha'a Lakumu As-Sam`a Wa Al-'Abşāra Wa Al-'Af'idata Qalīlāan Mā Tashkurūna 78. Na Yeye ndiye aliye kuumbieni kusikia na kuona na nyoyo za kufahamu. Ni kuchache mno kushukuru kwenu. وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالأَبْصَارَ وَالأَفْئِدَةَ قَلِيلا ً مَا تَشْكُرُونَ
Wa Huwa Al-Ladhī Dhara'akum Al-'Arđi Wa 'Ilayhi Tuĥsharūna 79. Na Yeye ndiye aliye kuenezeni katika ardhi, na kwake Yeye mtakusanywa. وَهُوَ الَّذِي ذَرَأَكُمْ فِي الأَرْضِ وَإِلَيْهِ تُحْشَرُونَ
Wa Huwa Al-Ladhī Yuĥyī Wa Yumītu Wa Lahu Akhtilāfu Al-Layli Wa An-Nahāri 'Afalā Ta`qilūna 80. Na Yeye ndiye anaye huisha na kufisha, na yake Yeye mabadiliko ya usiku na mchana. Basi je! Hamfahamu? وَهُوَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ وَلَهُ اخْتِلاَفُ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ أَفَلاَ تَعْقِلُونَ
Bal Qālū Mithla Mā Qāla Al-'Awwalūna 81. Bali wanasema kama walivyo sema watu wa kwanza. بَلْ قَالُوا مِثْلَ مَا قَالَ الأَوَّلُونَ
Qālū 'A'idhā Mitnā Wa Kunnā Turābāan Wa `Ižāmāan 'A'innā Lamabthūna 82. Walisema: Je! Tukisha kufa tukawa udongo na mifupa ndio tutafufuliwa? قَالُوا أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابا ً وَعِظَاماً أَئِنَّا لَمَبْعُوثُونَ
Laqad Wu`idnā Naĥnu Wa 'Ābā'uunā Hādhā Min Qablu 'In Hādhā 'Illā 'Asāţīru Al-'Awwalīna 83. Tuliahidiwa haya sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni visa vya uwongo vya watu wa zamani. لَقَدْ وُعِدْنَا نَحْنُ وَآبَاؤُنَا هَذَا مِنْ قَبْلُ إِنْ هَذَا إِلاَّ أَسَاطِيرُ الأَوَّلِينَ
Qul Limani Al-'Arđu Wa Man Fīhā 'In Kuntum Ta`lamūna 84. Sema: Ni ya nani ardhi na viliomo ndani yake, kama nyinyi mnajua? قُلْ لِمَنِ الأَرْضُ وَمَنْ فِيهَا إِنْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
Sayaqūlūna Lillāhi Qul 'Afalā Tadhakkarūna 85. Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu! Sema: Basi, je, hamkumbuki? سَيَقُولُونَ لِلَّهِ قُلْ أَفَلاَ تَذَكَّرُونَ
Qul Man Rabbu As-Samāwāti As-Sab`i Wa Rabbu Al-`Arshi Al-`Ažīmi 86. Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu saba na Mola Mlezi wa A'rshi Kuu? قُلْ مَنْ رَبُّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ وَرَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ
Sayaqūlūna Lillāhi Qul 'Afalā Tattaqūna 87. Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, hamwogopi? سَيَقُولُونَ لِلَّهِ قُلْ أَفَلاَ تَتَّقُونَ
Qul Man Biyadihi Malakūtu Kulli Shay'in Wa Huwa Yujīru Wa Lā Yujāru `Alayhi 'In Kuntum Ta`lamūn 88. Sema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu, naye ndiye anaye linda, wala hakilindwi asicho taka, kama mnajua? قُلْ مَنْ بِيَدِه ِِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْء ٍ وَهُوَ يُجِيرُ وَلاَ يُجَارُ عَلَيْهِ إِنْ كُنتُمْ تَعْلَمُون
Sayaqūlūna Lillāhi Qul Fa'annā Tusĥarūna 89. Watasema: (Ufalme huo) ni wa Mwenyezi Mungu. Sema: Basi vipi mnadanganyika? سَيَقُولُونَ لِلَّهِ قُلْ فَأَنَّا تُسْحَرُونَ
Bal 'Ataynāhum Bil-Ĥaqqi Wa 'Innahum Lakādhibūna 90. Bali tumewaletea Haki, na kwa yakini hao ni waongo. بَلْ أَتَيْنَاهُمْ بِالْحَقِّ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ
Attakhadha Allāhu Min Waladin Wa Mā Kāna Ma`ahu Min 'Ilahin 'Idhāan Ladhahaba Kullu 'Ilahin Bimā Khalaqa Wa La`alā Ba`đuhum `Alá Ba`đin Subĥāna Allāhi `Ammā Yaşifūna 91. Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu. مَا اتَّخَذَ اللَّهُ مِنْ وَلَد ٍ وَمَا كَانَ مَعَه ُُ مِنْ إِلَهٍ~ ٍ إِذا ً لَذَهَبَ كُلُّ إِلَه ٍ ٍ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلاَ بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْض ٍ سُبْحَانَ اللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ
`Ālimi Al-Ghaybi Wa Ash-Shahādati Fata`ālá `Ammā Yushrikūna 92. Mjuzi wa siri na dhaahiri, na ametukuka juu ya hayo wanayo mshirikisha nayo. عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَتَعَالَى عَمَّا يُشْرِكُونَ
Qul Rabbi 'Immā Turiyannī Mā Yū`adūna 93. Sema: Mola wangu Mlezi! Ukinionyesha adhabu waliyo ahidiwa, قُلْ رَبِّ إِمَّا تُرِيَنِّي مَا يُوعَدُونَ
Rabbi Falā Taj`alnī Fī Al-Qawmi Až-Žālimīna 94. Mola wangu Mlezi! Usinijaalie katika watu madhaalimu hao. رَبِّ فَلاَ تَجْعَلْنِي فِي الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
Wa 'Innā `Alá 'An Nuriyaka Mā Na`iduhum Laqādirūna 95. Na hakika Sisi ni waweza wa kukuonyeshsa tuliyo waahidi. وَإِنَّا عَلَى أَنْ نُرِيَكَ مَا نَعِدُهُمْ لَقَادِرُونَ
Adfa` Bi-Atī Hiya 'Aĥsanu As-Sayyi'ata Naĥnu 'A`lamu Bimā Yaşifūna 96. Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunajua wayasemayo. ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ السَّيِّئَةَ نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَصِفُونَ
Wa Qul Rabbi 'A`ūdhu Bika Min Hamazāti Ash-Shayāţīni 97. Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani. وَقُلْ رَبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ
Wa 'A`ūdhu Bika Rabbi 'An Yaĥđurūni 98. Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie. وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَنْ يَحْضُرُونِ
Ĥattá 'Idhā Jā'a 'Aĥadahumu Al-Mawtu Qāla Rabbi Arji`ūni 99. Mpaka yanapo mfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe. حَتَّى إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِع