Yā 'Ayyuhā An-Nāsu Attaqū Rabbakum 'Inna Zalzalata As-Sā`ati Shay'un `Ažīmun  | 1. Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika tetemeko
la Saa (ya Kiyama) ni jambo kuu. | يَاأَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيم ٌ |
Yawma Tarawnahā Tadh/halu Kullu Murđi`atin `Ammā 'Arđa`at Wa Tađa`u Kullu Dhāti Ĥamlin Ĥamlahā Wa Tará An-Nāsa Sukārá Wa Mā Hum Bisukārá Wa Lakinna `Adhāba Allāhi Shadīdun  | 2. Siku mtapo iona, kila mwenye kunyonyesha atamsahau
amnyonyeshaye, na kila mwenye mimba ataharibu mimba yake. Na utaona watu
wamelewa, na kumbe hawakulewa. Lakini adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali. | يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارَى وَمَا هُمْ بِسُكَارَى وَلَكِنَّ عَذَابَ اللَّهِ شَدِيد ٌ |
Wa Mina An-Nāsi Man Yujādilu Fī Allāhi Bighayri `Ilmin Wa Yattabi`u Kulla Shayţānin Marīdin  | 3. Na miongoni mwa watu wapo wanao bishana juu
ya Mwenyezi Mungu bila ya ilimu, na wanamfuata kila shet'ani aliye asi. | وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يُجَادِلُ فِي اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْم ٍ وَيَتَّبِعُ كُلَّ شَيْطَان ٍ مَرِيد ٍ |
Kutiba `Alayhi 'Annahu Man Tawallāhu Fa'annahu Yuđilluhu Wa Yahdīhi 'Ilá `Adhābi As-Sa`īri  | 4. Ameandikiwa kwamba anaye mfanya kuwa rafiki,
basi huyo hakika atampoteza na atamwongoza kwenye adhabu ya Moto mkali. | كُتِبَ عَلَيْهِ أَنَّه ُُ مَنْ تَوَلاَّه ُُ فَأَنَّه ُُ يُضِلُّه ُُ وَيَهْدِيهِ~ِ إِلَى عَذَابِ السَّعِيرِ |
Yā 'Ayyuhā An-Nāsu 'In Kuntum Fī Raybin Mina Al-Ba`thi Fa'innā Khalaqnākum Min Turābin Thumma Min Nuţfatin Thumma Min `Alaqatin Thumma Min Muđghatin Mukhallaqatin Wa Ghayri Mukhallaqatin Linubayyina Lakum Wa Nuqirru Fī Al-'Arĥāmi Mā Nashā'u 'Ilá 'Ajalin Musammáan Thumma Nukhrijukum Ţiflāan Thumma Litablughū 'Ashuddakum Wa Minkum Man Yutawaffá Wa Minkum Man Yuraddu 'Ilá 'Ardhali Al-`Umuri Likaylā Ya`lama Min Ba`di `Ilmin Shay'āan Wa Tará Al-'Arđa Hāmidatan Fa'idhā 'Anzalnā `Alayhā Al-Mā'a Ahtazzat Wa Rabat Wa 'Anbatat Min Kulli Zawjin Bahījin  | 5. Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa
basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na
manii, kisha kutokana na kipande cha damu ilio gandana, kisha kutokana
na kipande cha nyama chenye umbo na kisicho kuwa na umbo, ili tukubainishieni.
Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio
wekwa. Kisha tunakutoeni kwa hali ya mtoto mchanga, kisha mfikie kutimia
akili. Na wapo katika nyinyi wanao kufa, na wapo katika nyinyi wanao rudishwa
kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijua.
Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake
husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri. | يَاأَيُّهَا النَّاسُ إِنْ كُنْتُمْ فِي رَيْب ٍ مِنَ الْبَعْثِ فَإِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ تُرَاب ٍ ثُمَّ مِنْ نُطْفَة ٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَة ٍ ثُمَّ مِنْ مُضْغَة ٍ مُخَلَّقَة ٍ وَغَيْرِ مُخَلَّقَة ٍ لِنُبَيِّنَ لَكُمْ وَنُقِرُّ فِي الأَرْحَامِ مَا نَشَاءُ إِلَى أَجَل ٍ مُسَمّى ً ثُمَّ نُخْرِجُكُمْ طِفْلا ً ثُمَّ لِتَبْلُغُوا أَشُدَّكُمْ وَمِنْكُمْ مَنْ يُتَوَفَّى وَمِنْكُمْ مَنْ يُرَدُّ إِلَى أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْلاَ يَعْلَمَ مِنْ بَعْدِ عِلْم ٍ شَيْئا ً وَتَرَى الأَرْضَ هَامِدَة ً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ وَأَنْبَتَتْ مِنْ كُلِّ زَوْج ٍ بَهِيج ٍ |
Dhālika Bi'anna Allāha Huwa Al-Ĥaqqu Wa 'Annahu Yuĥyī Al-Mawtá Wa 'Annahu `Alá Kulli Shay'in Qadīrun  | 6. Hayo ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye
Haki, na kwamba hakika Yeye ndiye mwenye kuhuisha wafu, na kwamba hakika
Yeye ni Muweza wa kila kitu. | ذَلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّه ُُ يُحْيِي الْمَوْتَى وَأَنَّه ُُ عَلَى كُلِّ شَيْء ٍ قَدِير ٌ |
Wa 'Anna As-Sā`ata 'Ātiyatun Lā Rayba Fīhā Wa 'Anna Allāha Yab`athu Man Fī Al-Qubūri  | 7. Na kwamba hakika Saa itakuja hapana shaka kwa
hilo, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini. | وَأَنَّ السَّاعَةَ آتِيَة ٌ لاَ رَيْبَ فِيهَا وَأَنَّ اللَّهَ يَبْعَثُ مَنْ فِي الْقُبُورِ |
Wa Mina An-Nāsi Man Yujādilu Fī Allāhi Bighayri `Ilmin Wa Lā Hudáan Wa Lā Kitābin Munīrin  | 8. Na katika watu wapo wanao bishana juu ya Mwenyezi
Mungu bila ya ilimu, wala uwongofu, wala Kitabu chenye nuru. | وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يُجَادِلُ فِي اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْم ٍ وَلاَ هُدى ً وَلاَ كِتَاب ٍ مُنِير ٍ |
Thāniya `Iţfihi Liyuđilla `An Sabīli Allāhi Lahu Fī Ad-Dunyā Khizyun Wa Nudhīquhu Yawma Al-Qiyāmati `Adhāba Al-Ĥarīqi  | 9. Anaye geuza shingo yake ili kupoteza watu waache
Njia ya Mwenyezi Mungu. Duniani atapata hizaya, na Siku ya Kiyama tutamwonjesha
adhabu ya kuungua. | ثَانِيَ عِطْفِه ِِ لِيُضِلَّ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ لَه ُُ فِي الدُّنْيَا خِزْي ٌ وَنُذِيقُه ُُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَذَابَ الْحَرِيقِ |
Dhālika Bimā Qaddamat Yadāka Wa 'Anna Allāha Laysa Bižallāmin Lil`abīdi  | 10. (Ataambiwa): Hayo ni kwa sababu ya iliyo
tanguliza mikono yako. Na hakika Mwenyezi Mungu si dhaalimu kwa waja. | ذَلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ يَدَاكَ وَأَنَّ اللَّهَ لَيْسَ بِظَلاَّم ٍ لِلْعَبِيدِ |
Wa Mina An-Nāsi Man Ya`budu Allāha `Alá Ĥarfin Fa'in 'Aşābahu Khayrun Aţma'anna Bihi Wa 'In 'Aşābat/hu Fitnatun Anqalaba `Alá Wajhihi Khasira Ad-Dunyā Wa Al-'Ākhirata Dhālika Huwa Al-Khusrānu Al-Mubīnu  | 11. Na katika watu wapo wanao muabudu Mwenyezi
Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na ukimfikia msukosuko
hugeuza uso wake. Amekhasiri dunia na Akhera; hiyo ndiyo khasara iliyo
wazi. | وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَعْبُدُ اللَّهَ عَلَى حَرْف ٍ فَإِنْ أَصَابَه ُُ خَيْر ٌ اطْمَأَنَّ بِه ِِ وَإِنْ أَصَابَتْهُ فِتْنَة ٌ انقَلَبَ عَلَى وَجْهِه ِِ خَسِرَ الدُّنْيَا وَالآخِرَةَ ذَلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ |
Yad`ū Min Dūni Allāhi Mā Lā Yađurruhu Wa Mā Lā Yanfa`uhu Dhālika Huwa Ađ-Đalālu Al-Ba`īdu  | 12. Badala ya Mwenyezi Mungu, yeye huomba kisicho
mdhuru wala kumnufaisha. Huko ndiko kupotolea mbali! | يَدْعُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ مَا لاَ يَضُرُّه ُُ وَمَا لاَ يَنْفَعُه ُُ ذَلِكَ هُوَ الضَّلاَلُ الْبَعِيدُ |
Yad`ū Laman Đarruhu 'Aqrabu Min Naf`ihi Labi'sa Al-Mawlá Wa Labi'sa Al-`Ashīru  | 13. Humuomba yule ambaye bila ya shaka dhara
yake ipo karibu zaidi kuliko nafuu yake. Kwa hakika huyo ni mlinzi muovu,
na rafiki muovu. | يَدْعُوا لَمَنْ ضَرُّهُ~ُ أَقْرَبُ مِنْ نَفْعِه ِِ لَبِئْسَ الْمَوْلَى وَلَبِئْسَ الْعَشِيرُ |
'Inna Allāha Yudkhilu Al-Ladhīna 'Āmanū Wa `Amilū Aş-Şāliĥāti Jannātin Tajrī Min Taĥtihā Al-'Anhāru 'Inna Allāha Yaf`alu Mā Yurīdu  | 14. Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini
na wakatenda mema katika Bustani zipitazo mito kati yake. Hakika Mwenyezi
Mungu hutenda atakayo. | إِنَّ اللَّهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّات ٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الأَنْهَارُ إِنَّ اللَّهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ |
Man Kāna Yažunnu 'An Lan Yanşurahu Allāhu Fī Ad-Dunyā Wa Al-'Ākhirati Falyamdud Bisababin 'Ilá As-Samā'i Thumma Liyaqţa` Falyanžur Hal Yudh/hibanna Kayduhu Mā Yaghīžu  | 15. Anaye dhani kwamba Mwenyezi Mungu hatamnusuru
(Mtume) katika dunia na Akhera na afunge kamba kwenye dari kisha aikate.
Atazame je hila yake itaondoa hayo yaliyo mkasirisha? | مَنْ كَانَ يَظُنُّ أَنْ لَنْ يَنصُرَهُ اللَّهُ فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ فَلْيَمْدُدْ بِسَبَب ٍ إِلَى السَّمَاءِ ثُمَّ لِيَقْطَعْ فَلْيَنظُرْ هَلْ يُذْهِبَنَّ كَيْدُه ُُ مَا يَغِيظُ |
Wa Kadhalika 'Anzalnāhu 'Āyātin Bayyinātin Wa 'Anna Allāha Yahdī Man Yurīdu  | 16. Na namna hivi tumeiteremsha (Qur'ani) kuwa
ni Aya zilizo wazi, na hakika Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. | وَكَذَلِكَ أَنزَلْنَاهُ آيَات ٍ بَيِّنَات ٍ وَأَنَّ اللَّهَ يَهْدِي مَنْ يُرِيدُ |
'Inna Al-Ladhīna 'Āmanū Wa Al-Ladhīna Hādū Wa Aş-Şābi'īna Wa An-Naşārá Wa Al-Majūsa Wa Al-Ladhīna 'Ashrakū 'Inna Allāha Yafşilu Baynahum Yawma Al-Qiyāmati 'Inna Allāha `Alá Kulli Shay'in Shahīdun  | 17. Hakika walio amini, na ambao ni Mayahudi
na Wasabai na Wakristo na Majusi na wale walio shiriki - hakika Mwenyezi
Mungu atawapambanua baina yao Siku ya Kiyama. Hakika Mwenyezi Mungu ni
Shahidi wa kila kitu. | إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئِينَ وَالنَّصَارَى وَالْمَجُوسَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا إِنَّ اللَّهَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْء ٍ شَهِيد ٌ |
'Alam Tará 'Anna Allāha Yasjudu Lahu Man Fī As-Samāwāti Wa Man Fī Al-'Arđi Wa Ash-Shamsu Wa Al-Qamaru Wa An-Nujūmu Wa Al-Jibālu Wa Ash-Shajaru Wa Ad-Dawābbu Wa Kathīrun Mina An-Nāsi Wa Kathīrun Ĥaqqa `Alayhi Al-`Adhābu Wa Man Yuhini Allāhu Famā Lahu Min Mukrimin 'Inna Allāha Yaf`alu Mā Yashā'u  | 18. Je! Huoni kwamba vinamsujudia Mwenyezi Mungu
viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na jua, na mwezi, na nyota, na
milima, na miti, na wanyama, na wengi miongoni mwa watu. Na wengi imewastahiki
adhabu. Na anaye fedheheshwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumhishimu. Hakika
Mwenyezi Mungu hutenda apendayo. | أَلَمْ تَرَى أَنَّ اللَّهَ يَسْجُدُ لَه ُُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَمَنْ فِي الأَرْضِ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ وَالنُّجُومُ وَالْجِبَالُ وَالشَّجَرُ وَالدَّوَابُّ وَكَثِير ٌ مِنَ النَّاسِ وَكَثِيرٌ حَقَّ عَلَيْهِ الْعَذَابُ وَمَنْ يُهِنِ اللَّهُ فَمَا لَه ُُ مِنْ مُكْرِم ٍ إِنَّ اللَّهَ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ |
Hadhāni Khaşmāni Akhtaşamū Fī Rabbihim Fa-Al-Ladhīna Kafarū Quţţi`at Lahum Thiyābun Min Nārin Yuşabbu Min Fawqi Ru'ūsihimu Al-Ĥamīmu  | 19. Hawa wagomvi wawili walio gombana kwa ajili
ya Mola wao Mlezi. Basi walio kufuru watakatiwa nguo za moto, na yatamiminwa
juu ya vichwa vyao maji yanayo chemka. | هَذَانِ خَصْمَانِ اخْتَصَمُوا فِي رَبِّهِمْ فَالَّذِينَ كَفَرُوا قُطِّعَتْ لَهُمْ ثِيَاب ٌ مِنْ نَار ٍ يُصَبُّ مِنْ فَوْقِ رُءُوسِهِمُ الْحَمِيمُ |
Yuşharu Bihi Mā Fī Buţūnihim Wa Al-Julūdu  | 20. Kwa maji hayo vitayayushwa viliomo matumboni
mwao, na ngozi zao pia. | يُصْهَرُ بِه ِِ مَا فِي بُطُونِهِمْ وَالْجُلُودُ |
Wa Lahum Maqāmi`u Min Ĥadīdin  | 21. Na kwa ajili yao yatakuwapo marungu ya chuma. | وَلَهُمْ مَقَامِعُ مِنْ حَدِيد ٍ |
Kullamā 'Arādū 'An Yakhrujū Minhā Min Ghammin 'U`īdū Fīhā Wa Dhūqū `Adhāba Al-Ĥarīqi  | 22. Kila wakitaka kutoka humo kwa sababu ya uchungu
watarudishwa humo humo, na wataambiwa: Onjeni adhabu ya kuungua! | كُلَّمَا أَرَادُوا أَنْ يَخْرُجُوا مِنْهَا مِنْ غَمٍّ أُعِيدُوا فِيهَا وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ |
'Inna Allāha Yudkhilu Al-Ladhīna 'Āmanū Wa `Amilū Aş-Şāliĥāti Jannātin Tajrī Min Taĥtihā Al-'Anhāru Yuĥallawna Fīhā Min 'Asāwira Min Dhahabin Wa Lu'ulu'uāan Wa Libāsuhum Fīhā Ĥarīrun  | 23. Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini
na wakatenda mema katika Bustani zipitiwazo na mito kati yake. Watapambwa
humo kwa mapambo ya mikononi ya dhahabu na lulu. Na mavazi yao humo ni
hariri. | إِنَّ اللَّهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّات ٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الأَنْهَارُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِنْ ذَهَب ٍ وَلُؤْلُؤا ً وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِير ٌ |
Wa Hudū 'Ilá Aţ-Ţayyibi Mina Al-Qawli Wa Hudū 'Ilá Şirāţi Al-Ĥamīdi  | 24. Na wataongozwa kwenye maneno mazuri, na wataongozwa
kwenye Njia ya Msifiwa. | وَهُدُوا إِلَى الطَّيِّبِ مِنَ الْقَوْلِ وَهُدُوا إِلَى صِرَاطِ الْحَمِيدِ |
'Inna Al-Ladhīna Kafarū Wa Yaşuddūna `An Sabīli Allāhi Wa Al-Masjidi Al-Ĥarāmi Al-Ladhī Ja`alnāhu Lilnnāsi Sawā'an Al-`Ākifu Fīhi Wa Al-Bādi Wa Man Yurid Fīhi Bi'ilĥādin Bižulmin Nudhiqhu Min `Adhābin 'Alīmin  | 25. Hakika wale walio kufuru na wakazuilia Njia
ya Mwenyezi Mungu na Msikiti Mtakatifu, ambao tumeufanya kwa ajili ya watu
wote sawasawa, kwa wakaao humo na wageni. Na kila atakaye taka kufanya
upotofu humo kwa dhulma, basi tutamwonjesha adhabu chungu. | إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَيَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ الَّذِي جَعَلْنَاه ُُ لِلنَّاسِ سَوَاء ً الْعَاكِفُ فِيه ِِ وَالْبَادِ وَمَنْ يُرِدْ فِيه ِِ بِإِلْحَاد ٍ بِظُلْم ٍ نُذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيم ٍ |
Wa 'Idh Bawwa'nā Li'ibrāhīma Makāna Al-Bayti 'An Lā Tushrik Bī Shay'āan Wa Ţahhir Baytiya Lilţţā'ifīna Wa Al-Qā'imīna Wa Ar-Rukka`i As-Sujūdi  | 26. Na pale tulipomweka Ibrahim pahala penye
ile Nyumba tukamwambia: Usinishirikishe na chochote; na isafishe Nyumba
yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu, na wanao kaa hapo kwa ibada,
na wanao rukuu, na wanao sujudu. | وَإِذْ بَوَّأْنَا لِإبْرَاهِيمَ مَكَانَ الْبَيْتِ أَنْ لاَ تُشْرِكْ بِي شَيْئا ً وَطَهِّرْ بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْقَائِمِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ |
Wa 'Adhdhin Fī An-Nāsi Bil-Ĥajji Ya'tūka Rijālāan Wa `Alá Kulli Đāmirin Ya'tīna Min Kulli Fajjin `Amīqin  | 27. Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu
na juu ya kila ngamia aliye konda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali. | وَأَذِّنْ فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالا ً وَعَلَى كُلِّ ضَامِر ٍ يَأْتِينَ مِنْ كُلِّ فَجٍّ عَمِيق ٍ |
Liyash/hadū Manāfi`a Lahum Wa Yadhkurū Asma Allāhi Fī 'Ayyāmin Ma`lūmātin `Alá Mā Razaqahum Min Bahīmati Al-'An`ām Fakulū Minhā Wa 'Aţ`imū Al-Bā'isa Al-Faqīra  | 28. Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina
la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya nyama hoa alio waruzuku. Basi
kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri. | لِيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّام ٍ مَعْلُومَاتٍ عَلَى مَا رَزَقَهُمْ مِنْ بَهِيمَةِ الأَنعَام فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ |
Thumma Liyaqđū Tafathahum Wa Līūfū Nudhūrahum Wa Līaţţawwafū Bil-Bayti Al-`Atīqi  | 29. Kisha wajisafishe taka zao, na waondoe nadhiri
zao, na waizunguke Nyumba ya Kale. | ثُمَّ لِيَقْضُوا تَفَثَهُمْ وَلْيُوفُوا نُذُورَهُمْ وَلْيَطَّوَّفُوا بِالْبَيْتِ الْعَتِيقِ |
Dhālika Wa Man Yu`ažžim Ĥurumāti Allāhi Fahuwa Khayrun Lahu `Inda Rabbihi Wa 'Uĥillat Lakumu Al-'An`ām 'Illā Mā Yutlá `Alaykum Fājtanibū Ar-Rijsa Mina Al-'Awthāni Wa Ajtanibū Qawla Az-Zūri  | 30. Ndio hivyo iwe! Na anaye vitukuza vitakatifu
vya Mwenyezi Mungu basi hayo ndiyo kheri yake mbele ya Mola wake Mlezi.
Na mmehalalishiwa nyama hoa ila wale mlio somewa. Basi jiepusheni na uchafu
wa masanamu, na jiepusheni na usemi wa uwongo. | ذَلِكَ وَمَنْ يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّهِ فَهُوَ خَيْر ٌ لَه ُُ عِنْدَ رَبِّه ِِ وَأُحِلَّتْ لَكُمُ الأَنعَام إِلاَّ مَا يُتْلَى عَلَيْكُمْ فَاجْتَنِبُوا الرِّجْسَ مِنَ الأَوْثَانِ وَاجْتَنِبُوا قَوْلَ الزُّورِ |
Ĥunafā'a Lillāhi Ghayra Mushrikīna Bihi Wa Man Yushrik Billāhi Faka'annamā Kharra Mina As-Samā'i Fatakhţafuhu Aţ-Ţayru 'Aw Tahwī Bihi Ar-Rīĥu Fī Makānin Saĥīqin  | 31. Kwa kumtakasikia Imani Mwenyezi Mungu, bila
ya kumshirikisha. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu ni kama kwamba ameporomoka
kutoka mbinguni, kisha ndege wakamnyakua au upepo ukamtupa pahala mbali. | حُنَفَاءَ لِلَّهِ غَيْرَ مُشْرِكِينَ بِه ِِ وَمَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ السَّمَاءِ فَتَخْطَفُهُ الطَّيْرُ أَوْ تَهْوِي بِهِ الرِّيحُ فِي مَكَان ٍ سَحِيق ٍ |
Dhālika Wa Man Yu`ažžim Sha`ā'ira Allāhi Fa'innahā Min Taqwá Al-Qulūbi  | 32. Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi
Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo. | ذَلِكَ وَمَنْ يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِنْ تَقْوَى الْقُلُوبِ |
Lakum Fīhā Manāfi`u 'Ilá 'Ajalin Musammáan Thumma Maĥilluhā 'Ilá Al-Bayti Al-`Atīqi  | 33. Katika hao nyinyi mna manufaa mpaka muda
maalumu. Kisha pahala pa kuchinjiwa kwake ni kwenye Nyumba ya Kale. | لَكُمْ فِيهَا مَنَافِعُ إِلَى أَجَل ٍ مُسَمّى ً ثُمَّ مَحِلُّهَا إِلَى الْبَيْتِ الْعَتِيقِ |
Wa Likulli 'Ummatin Ja`alnā Mansakāan Liyadhkurū Asma Allāhi `Alá Mā Razaqahum Min Bahīmati Al-'An`āmi Fa'ilahukum 'Ilahun Wāĥidun Falahu 'Aslimū Wa Bashshiri Al-Mukhbitīna  | 34. Na kila umma tumewafanyia mahala pa kuchinjia
mihanga ya ibada ili walitaje jina la Mwenyezi Mungu juu ya vile walivyo
ruzukiwa katika wanyama wa mifugo. Basi Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Jisalimishieni
kwake tu, na wabashirie wanyenyekevu, | وَلِكُلِّ أُمَّة ٍ جَعَلْنَا مَنْسَكا ً لِيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَى مَا رَزَقَهُمْ مِنْ بَهِيمَةِ الأَنعَامِ فَإِلَهُكُمْ إِلَه ٌ ٌ وَاحِد ٌ فَلَهُ~ُ أَسْلِمُوا وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ |
Al-Ladhīna 'Idhā Dhukira Allāhu Wajilat Qulūbuhum Wa Aş-Şābirīna `Alá Mā 'Aşābahum Wa Al-Muqīmī Aş-Şalāati Wa Mimmā Razaqnāhum Yunfiqūna  | 35. Ambao, anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao
hutetemeka, na wanao vumilia kwa yanao wasibu, na wanao shika Sala, na
wanatoa katika tulivyo waruzuku. | الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَالصَّابِرِينَ عَلَى مَا أَصَابَهُمْ وَالْمُقِيمِي الصَّلاَةِ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ |
Wa Al-Budna Ja`alnāhā Lakum Min Sha`ā'iri Allāhi Lakum Fīhā Khayrun Fādhkurū Asma Allāhi `Alayhā Şawāffa Fa'idhā Wajabat Junūbuhā Fakulū Minhā Wa 'Aţ`imū Al-Qāni`a Wa Al-Mu`tarra Kadhālika Sakhkharnāhā Lakum La`allakum Tashkurūna  | 36. Na ngamia wa sadaka tumekufanyieni kuwa ni
kudhihirisha matukuzo kwa Mwenyezi Mungu; kwa hao mna kheri nyingi. Basi
litajeni jina la Mwenyezi Mungu juu yao wanapo simama kwa safu. Na waangukapo
ubavu kuleni katika hao na walisheni walio kinai na wanao lazimika kuomba.
Ndio kama hivi tumewafanya hawa wanyama dhalili kwenu ili mpate kushukuru. | وَالْبُدْنَ جَعَلْنَاهَا لَكُمْ مِنْ شَعَائِرِ اللَّهِ لَكُمْ فِيهَا خَيْر ٌ فَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَيْهَا صَوَافَّ فَإِذَا وَجَبَتْ جُنُوبُهَا فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْقَانِعَ وَالْمُعْتَرَّ كَذَلِكَ سَخَّرْنَاهَا لَكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ |
Lan Yanāla Allāha Luĥūmuhā Wa Lā Dimā'uuhā Wa Lakin Yanāluhu At-Taqwá Minkum Kadhālika Sakhkharahā Lakum Litukabbirū Allāha `Alá Mā Hadākum Wa Bashshiri Al-Muĥsinīna  | 37. Nyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala
damu zao, lakini unamfikia uchamngu wenu. Namna hivi tumewadhalilisha kwenu
ili mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa alivyo kuongoeni. Na wabashirie wafanyao
mema. | لَنْ يَنَالَ اللَّهَ لُحُومُهَا وَلاَ دِمَاؤُهَا وَلَكِنْ يَنَالُهُ التَّقْوَى مِنْكُمْ كَذَلِكَ سَخَّرَهَا لَكُمْ لِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَبَشِّرِ الْمُحْسِنِينَ |
'Inna Allāha Yudāfi`u `Ani Al-Ladhīna 'Āmanū 'Inna Allāha Lā Yuĥibbu Kulla Khawwānin Kafūrin  | 38. Hakika Mwenyezi Mungu huwakinga walio amini.
Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila khaini mwingi wa kukanya mema. | إِنَّ اللَّهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ اللَّهَ لاَ يُحِبُّ كُلَّ خَوَّان ٍ كَفُور ٍ |
'Udhina Lilladhīna Yuqātalūna Bi'annahum Žulimū Wa 'Inna Allāha `Alá Naşrihim Laqadīrun  | 39. Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita
kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia
- | أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا وَإِنَّ اللَّهَ عَلَى نَصْرِهِمْ لَقَدِير ٌ |
Al-Ladhīna 'Ukhrijū Min Diyārihim Bighayri Ĥaqqin 'Illā 'An Yaqūlū Rabbunā Allāhu Wa Lawlā Daf`u Allāhi An-Nāsa Ba`đahum Biba`đin Lahuddimat Şawāmi`u Wa Biya`un Wa Şalawātun Wa Masājidu Yudhkaru Fīhā Asmu Allāhi Kathīrāan Wa Layanşuranna Allāhu Man Yanşuruhu 'Inna Allāha Laqawīyun `Azīzun  | 40. Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo
haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau
kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli
vunjwa nymba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo
ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka
Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu
ni Mwenye nguvu Mtukufu. | الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِنْ دِيَارِهِمْ بِغَيْرِ حَقّ ٍ إِلاَّ أَنْ يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّهُ وَلَوْلاَ دَفْعُ اللَّهِ النَّاسَ بَعْضَهُمْ بِبَعْض ٍ لَهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَبِيَع ٌ وَصَلَوَات ٌ وَمَسَاجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا اسْمُ اللَّهِ كَثِيرا ً وَلَيَنصُرَنَّ اللَّهُ مَنْ يَنصُرُهُ~ُ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيز ٌ |
Al-Ladhīna 'In Makkannāhum Fī Al-'Arđi 'Aqāmū Aş-Şalāata Wa 'Ātaw Az-Zakāata Wa 'Amarū Bil-Ma`rūfi Wa Nahaw `Ani Al-Munkari Wa Lillahi `Āqibatu Al-'Umūri  | 41. Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi
husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya.
Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote. | الَّذِينَ إِنْ مَكَّنَّاهُمْ فِي الأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلاَةَ وَآتَوْا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنْكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الأُمُورِ |
Wa 'In Yukadhdhibūka Faqad Kadhdhabat Qablahum Qawmu Nūĥin Wa `Ādun Wa Thamūdu  | 42. Na wakikukanusha basi walikwisha kanusha
kabla yao watu wa Nuhu, na kina A'ad na kina Thamud, | وَإِنْ يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوح ٍ وَعَاد ٌ وَثَمُودُ |
Wa Qawmu 'Ibrāhīma Wa Qawmu Lūţin  | 43. Na watu wa Ibrahim na watu wa Lut'i | وَقَوْمُ إِبْرَاهِيمَ وَقَوْمُ لُوط ٍ |
Wa 'Aşĥābu Madyana Wa Kudhdhiba Mūsá Fa'amlaytu Lilkāfirīna Thumma 'Akhadhtuhum Fakayfa Kāna Nakīri  | 44. Na watu wa Madiana. Na Musa pia alikanushwa.
Nikawapa muda makafiri, kisha nikawatia mkononi. Basi ilikuwaje adhabu
yangu! | وَأَصْحَابُ مَدْيَنَ وَكُذِّبَ مُوسَى فَأَمْلَيْتُ لِلْكَافِرِينَ ثُمَّ أَخَذْتُهُمْ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ |
Faka'ayyin Min Qaryatin 'Ahlaknāhā Wa Hiya Žālimatun Fahiya Khāwiyatun `Alá `Urūshihā Wa Bi'rin Mu`aţţalatin Wa Qaşrin Mashīdin  | 45. Miji mingapi tuliiangamiza iliyo kuwa ikidhulumu,
ikawa imebaki magofu, na visima vilivyo achwa, na majumba yaliyo kuwa madhubuti? | فَكَأَيِّنْ مِنْ قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا وَهِيَ ظَالِمَة ٌ فَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَى عُرُوشِهَا وَبِئْر ٍ مُعَطَّلَة ٍ وَقَصْر ٍ مَشِيد ٍ |
'Afalam Yasīrū Fī Al-'Arđi Fatakūna Lahum Qulūbun Ya`qilūna Bihā 'Aw 'Ādhānun Yasma`ūna Bihā Fa'innahā Lā Ta`má Al-'Abşāru Wa Lakin Ta`má Al-Qulūbu Allatī Fī Aş-Şudūri  | 46. Je! Hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa
na nyoyo zao za kuzingatia, au masikio ya kusikilia? Kwani hakika si macho
yanayo pofuka, lakini zinazo pofuka ni nyoyo ziliomo vifuani. | أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الأَرْضِ فَتَكُونَ لَهُمْ قُلُوب ٌ يَعْقِلُونَ بِهَا أَوْ آذَان ٌ يَسْمَعُونَ بِهَا فَإِنَّهَا لاَ تَعْمَى الأَبْصَارُ وَلَكِنْ تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ |
Wa Yasta`jilūnaka Bil-`Adhābi Wa Lan Yukhlifa Allāhu Wa`dahu Wa 'Inna Yawmāan `Inda Rabbika Ka'alfi Sanatin Mimmā Ta`uddūna  | 47. Na wanakuhimiza ulete adhabu, lakini Mwenyezi
Mungu hatakwenda kinyume na ahadi yake kabisa. Na hakika siku moja kwa
Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu mnavyo hisabu nyinyi. | وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِالْعَذَابِ وَلَنْ يُخْلِفَ اللَّهُ وَعْدَه ُُ وَإِنَّ يَوْماً عِنْدَ رَبِّكَ كَأَلْفِ سَنَة ٍ مِمَّا تَعُدُّونَ |
Wa Ka'ayyin Min Qaryatin 'Amlaytu Lahā Wa Hiya Žālimatun Thumma 'Akhadhtuhā Wa 'Ilayya Al-Maşīru  | 48. Na miji mingapi niliipa muda na hali ilikuwa
imedhulumu, na kisha nikaitia mkononi? Na kwangu Mimi ndio marudio yote. | وَكَأَيِّنْ مِنْ قَرْيَةٍ أَمْلَيْتُ لَهَا وَهِيَ ظَالِمَة ٌ ثُمَّ أَخَذْتُهَا وَإِلَيَّ الْمَصِيرُ |
Qul Yā 'Ayyuhā An-Nāsu 'Innamā 'Anā Lakum Nadhīrun Mubīnun  | 49. Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni mwonyaji
kwenu niliye dhaahiri. | قُلْ يَاأَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا أَنَا لَكُمْ نَذِير ٌ مُبِين ٌ |
Fa-Al-Ladhīna 'Āmanū Wa `Amilū Aş-Şāliĥāti Lahum Maghfiratun Wa Rizqun Karīmun  | 50. Basi walio amini na wakatenda mema watapata
maghfira na riziki za ukarimu. | فَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ مَغْفِرَة ٌ وَرِزْق ٌ كَرِيم ٌ |
Wa Al-Ladhīna Sa`aw Fī 'Āyātinā Mu`ājizīna 'Ūlā'ika 'Aşĥābu Al-Jaĥīmi  | 51. Na wanao jitahidi kuzipinga Aya zetu hao
ndio watu wa Motoni. | وَالَّذِينَ سَعَوْا فِي آيَاتِنَا مُعَاجِزِينَ أُوْلَائِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ |
Wa Mā 'Arsalnā Min Qablika Min Rasūlin Wa Lā Nabīyin 'Illā 'Idhā Tamanná 'Alqá Ash-Shayţānu Fī 'Umnīyatihi Fayansakhu Allāhu Mā Yulqī Ash-Shayţānu Thumma Yuĥkimu Allāhu 'Āyātihi Wa Allāhu `Alīmun Ĥakīmun  | 52. Na hatukumtuma kabla yako Mtume wala Nabii
ila anapo soma, Shet'ani hutumbukiza katika masomo yake. Lakini Mwenyezi
Mungu huyaondoa anayo yatia Shet'ani; kisha Mwenyezi Mungu huzithibitisha
Aya zake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. | وَمَا أَرْسَلْنَا مِنْ قَبْلِكَ مِنْ رَسُول ٍ وَلاَ نَبِيّ ٍ إِلاَّ إِذَا تَمَنَّى أَلْقَى الشَّيْطَانُ فِي أُمْنِيَّتِه ِِ فَيَنْسَخُ اللَّهُ مَا يُلْقِي الشَّيْطَانُ ثُمَّ يُحْكِمُ اللَّهُ آيَاتِه ِِ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيم ٌ |
Liyaj`ala Mā Yulqī Ash-Shayţānu Fitnatan Lilladhīna Fī Qulūbihim Marađun Wa Al-Qāsiyati Qulūbuhum Wa 'Inna Až-Žālimīna Lafī Shiqāqin Ba`īdin  | 53. Hayo ni ili alifanye lile analo litia Shet'ani
liwe ni fitna kwa wale wenye maradhi ndani ya nyoyo zao, na wale ambao
nyoyo zao ni ngumu. Na hakika madhaalimu wamo katika mfarakano wa mbali. | لِيَجْعَلَ مَا يُلْقِي الشَّيْطَانُ فِتْنَة ً لِلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَض ٌ وَالْقَاسِيَةِ قُلُوبُهُمْ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ لَفِي شِقَاق ٍ بَعِيد ٍ |
Wa Liya`lama Al-Ladhīna 'Ūtū Al-`Ilma 'Annahu Al-Ĥaqqu Min Rabbika Fayu'uminū Bihi Fatukhbita Lahu Qulūbuhum Wa 'Inna Allāha Lahādi Al-Ladhīna 'Āmanū 'Ilá Şirāţin Mustaqīmin  | 54. Na ili walio pewa ilimu wajue kuwa hayo ni
Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi na waamini, na zipate kutua nyoyo zao.
Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye waongoa wenye kuamini kwenye Njia
Iliyo Nyooka. | وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ فَيُؤْمِنُوا بِه |