44) Sūrat Ad-Dukhān

Printed format

44) سُورَة الدُّخَان

Ĥā-Mīm 1. H'a Mim حَا-مِيم
Wa Al-Kitābi Al-Mubīni 2. Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha, وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ
'Innā 'Anzalnāhu Fī Laylatin Mubārakatin 'Innā Kunnā Mundhirīna 3. Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji. إِنَّا أَنزَلْنَاه ُُ فِي لَيْلَة ٍ مُبَارَكَة ٍ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ
Fīhā Yufraqu Kullu 'Amrin Ĥakīmin 4. Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima, فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيم ٍ
'Amrāan Min `Indinā 'Innā Kunnā Mursilīna 5. Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma. أَمْرا ً مِنْ عِنْدِنَا إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ
Raĥmatan Min Rabbika 'Innahu Huwa As-Samī`u Al-`Alīmu 6. Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. رَحْمَة ً مِنْ رَبِّكَ إِنَّه ُُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
Rabbi As-Samāwāti Wa Al-'Arđi Wa Mā Baynahumā 'In Kuntum Mūqinīna 7. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini. رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا إِنْ كُنْتُمْ مُوقِنِينَ
Lā 'Ilāha 'Illā Huwa Yuĥyī Wa Yumītu Rabbukum Wa Rabbu 'Ābā'ikumu Al-'Awwalīna 8. Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo. لاَ إِلَهَ~َ إِلاَّ هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الأَوَّلِينَ
Bal HumShakkin Yal`abūna 9. Lakini wao wanacheza katika shaka. بَلْ هُمْ فِي شَكّ ٍ يَلْعَبُونَ
Fārtaqib Yawma Ta'tī As-Samā'u Bidukhānin Mubīnin 10. Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri, فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَان ٍ مُبِين ٍ
Yaghshá An-Nāsa Hādhā `Adhābun 'Alīmun 11. Utakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu! يَغْشَى النَّاسَ هَذَا عَذَابٌ أَلِيم ٌ
Rabbanā Akshif `Annā Al-`Adhāba 'Innā Mu'uminūna 12. Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. رَبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ
'Anná Lahumu Adh-Dhikrá Wa Qad Jā'ahum Rasūlun Mubīnun 13. Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha. أَنَّى لَهُمُ الذِّكْرَى وَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُول ٌ مُبِين ٌ
Thumma Tawallaw `Anhu Wa Qālū Mu`allamun Majnūnun 14. Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu. ثُمَّ تَوَلَّوْا عَنْهُ وَقَالُوا مُعَلَّم ٌ مَجْنُون ٌ
'Innā Kāshifū Al-`Adhābi Qalīlāan 'Innakum `Ā'idūna 15. Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile! إِنَّا كَاشِفُوا الْعَذَابِ قَلِيلا ً إِنَّكُمْ عَائِدُونَ
Yawma Nabţishu Al-Baţshata Al-Kubrá 'Innā Muntaqimūna 16. Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa. يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَى إِنَّا مُنتَقِمُونَ
Wa Laqad Fatannā Qablahum Qawma Fir`awna Wa Jā'ahum Rasūlun Karīmun 17. Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu. وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَاءَهُمْ رَسُول ٌ كَرِيم ٌ
'An 'Addū 'Ilayya `Ibāda Allāhi 'Innī Lakum Rasūlun 'Amīnun 18. Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu. أَنْ أَدُّوا إِلَيَّ عِبَادَ اللَّهِ إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِين ٌ
Wa 'An Lā Ta`lū `Alá Allāhi 'Innī 'Ātīkum Bisulţānin Mubīnin 19. Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi. وَأَنْ لاَ تَعْلُوا عَلَى اللَّهِ إِنِّي آتِيكُمْ بِسُلْطَان ٍ مُبِين ٍ
Wa 'Innī `Udhtu Birabbī Wa Rabbikum 'An Tarjumūni 20. Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe. وَإِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمْ أَنْ تَرْجُمُونِ
Wa 'In Lam Tu'uminū Lī Fā`tazilūni 21. Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami. وَإِنْ لَمْ تُؤْمِنُوا لِي فَاعْتَزِلُونِ
Fada`ā Rabbahu 'Anna Hā'uulā' Qawmun Mujrimūna 22. Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu. فَدَعَا رَبَّهُ~ُ أَنَّ هَاؤُلاَء قَوْم ٌ مُجْرِمُونَ
Fa'asri Bi`ibādī Laylāan 'Innakum Muttaba`ūna 23. Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa. فَأَسْرِ بِعِبَادِي لَيْلا ً إِنَّكُمْ مُتَّبَعُونَ
Wa Atruki Al-Baĥra Rahwan 'Innahum Jundun Mughraqūna 24. Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa. وَاتْرُكِ الْبَحْرَ رَهْوا ً إِنَّهُمْ جُند ٌ مُغْرَقُونَ
Kam Tarakū Min Jannātin Wa `Uyūnin 25. Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha! كَمْ تَرَكُوا مِنْ جَنَّات ٍ وَعُيُون ٍ
Wa Zurū`in Wa Maqāmin Karīmin 26. Na mimea na vyeo vitukufu! وَزُرُوع ٍ وَمَقَام ٍ كَرِيم ٍ
Wa Na`matin Kānū Fīhā Fākihīna 27. Na neema walizo kuwa wakijistareheshea! وَنَعْمَة ٍ كَانُوا فِيهَا فَاكِهِينَ
Kadhālika Wa 'Awrathnāhā Qawmāan 'Ākharīna 28. Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe. كَذَلِكَ وَأَوْرَثْنَاهَا قَوْما ً آخَرِينَ
Famā Bakat `Alayhimu As-Samā'u Wa Al-'Arđu Wa Mā Kānū Munžarīna 29. La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula. فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ
Wa Laqad Najjaynā Banī 'Isrā'īla Mina Al-`Adhābi Al-Muhīni 30. Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha, وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنَ الْعَذَابِ الْمُهِينِ
Min Fir`awna 'Innahu Kāna `Ālīāan Mina Al-Musrifīna 31. Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka. مِنْ فِرْعَوْنَ إِنَّه ُُ كَانَ عَالِيا ً مِنَ الْمُسْرِفِينَ
Wa Laqadi Akhtarnāhum `Alá `Ilmin `Alá Al-`Ālamīna 32. Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe. وَلَقَدِ اخْتَرْنَاهُمْ عَلَى عِلْمٍ عَلَى الْعَالَمِينَ
Wa 'Ātaynāhum Mina Al-'Āyāti Mā Fīhi Balā'un Mubīnun 33. Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi. وَآتَيْنَاهُمْ مِنَ الآيَاتِ مَا فِيه ِِ بَلاَء ٌ مُبِين ٌ
'Inna Hā'uulā' Layaqūlūna 34. Hakika hawa wanasema: إِنَّ هَاؤُلاَء لَيَقُولُونَ
'In Hiya 'Illā Mawtatunā Al-'Ūlá Wa Mā Naĥnu Bimunsharīna 35. Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi. إِنْ هِيَ إِلاَّ مَوْتَتُنَا الأُولَى وَمَا نَحْنُ بِمُنشَرِينَ
Fa'tū Bi'ābā'inā 'In Kuntum Şādiqīna 36. Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli. فَأْتُوا بِآبَائِنَا إِنْ كُنتُمْ صَادِقِينَ
'Ahum Khayrun 'Am Qawmu Tubba`in Wa Al-Ladhīna Min Qablihim 'Ahlaknāhum 'Innahum Kānū Mujrimīna 37. Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu. أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّع ٍ وَالَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ أَهْلَكْنَاهُمْ إِنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ
Wa Mā Khalaq As-Samāwāti Wa Al-'Arđa Wa Mā Baynahumā Lā`ibīna 38. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo. وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لاَعِبِينَ
Khalaqnāhumā 'Illā Bil-Ĥaqqi Wa Lakinna 'Aktharahum Lā Ya`lamūna 39. Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui. مَا خَلَقْنَاهُمَا إِلاَّ بِالْحَقِّ وَلَكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لاَ يَعْلَمُونَ
'Inna Yawma Al-Faşli Mīqātuhum 'Ajma`īna 40. Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote. إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ مِيقَاتُهُمْ أَجْمَعِينَ
Yawma Lā Yughnī Mawláan `An Mawláan Shay'āan Wa Lā Hum Yunşarūna 41. Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa. يَوْمَ لاَ يُغْنِي مَوْلىً عَنْ مَوْلى ً شَيْئا ً وَلاَ هُمْ يُنصَرُونَ
'Illā Man Raĥima Allāhu 'Innahu Huwa Al-`Azīzu Ar-Raĥīmu 42. Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. إِلاَّ مَنْ رَحِمَ اللَّهُ إِنَّه ُُ هُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ
'Inna Shajarata Az-Zaqqūmi 43. Hakika Mti wa Zaqqum, إِنَّ شَجَرَةَ الزَّقُّومِ
Ţa`āmu Al-'Athīmi 44. Ni chakula cha mwenye dhambi. طَعَامُ الأَثِيمِ
Kālmuhli Yaghlī Fī Al-Buţūni 45. Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ
Kaghalyi Al-Ĥamīmi 46. Kama kutokota kwa maji ya moto. كَغَلْيِ الْحَمِيمِ
Khudhūhu Fā`tilūhu 'Ilá Sawā'i Al-Jaĥīmi 47. (Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu! خُذُوه ُُ فَاعْتِلُوهُ~ُ إِلَى سَوَاءِ الْجَحِيمِ
Thumma Şubbū Fawqa Ra'sihi Min `Adhābi Al-Ĥamīmi 48. Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka. ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِه ِِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ
Dhuq 'Innaka 'Anta Al-`Azīzu Al-Karīmu 49. Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu! ذُقْ إِنَّكَ أَنْتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ
'Inna Hādhā Mā Kuntum Bihi Tamtarūna 50. Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka. إِنَّ هَذَا مَا كُنتُمْ بِه ِِ تَمْتَرُونَ
'Inna Al-Muttaqīna Fī Maqāmin 'Amīnin 51. Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani, إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِين ٍ
Fī Jannātin Wa `Uyūnin 52. Katika mabustani na chemchem, فِي جَنَّات ٍ وَعُيُون ٍ
Yalbasūna Min Sundusin Wa 'Istabraqin Mutaqābilīna 53. Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana, يَلْبَسُونَ مِنْ سُندُس ٍ وَإِسْتَبْرَق ٍ مُتَقَابِلِينَ
Kadhālika Wa Zawwajnāhum Biĥūrin `Īnin 54. Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini. كَذَلِكَ وَزَوَّجْنَاهُمْ بِحُورٍ عِين ٍ
Yad`ūna Fīhā Bikulli Fākihatin 'Āminīna 55. Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani. يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَة ٍ آمِنِينَ
Lā Yadhūqūna Fīhā Al-Mawta 'Illā Al-Mawtata Al-'Ūlá Wa Waqāhum `Adhāba Al-Jaĥīmi 56. Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu, لاَ يَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلاَّ الْمَوْتَةَ الأُولَى وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ
Fađlāan Min Rabbika Dhālika Huwa Al-Fawzu Al-`Ažīmu 57. Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa. فَضْلا ً مِنْ رَبِّكَ ذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ
Fa'innamā Yassarnāhu Bilisānika La`allahum Yatadhakkarūna 58. Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka. فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاه ُُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ
Fārtaqib 'Innahum Murtaqibūna 59. Ngoja tu, na wao wangoje pia. *   فَارْتَقِبْ إِنَّهُمْ مُرْتَقِبُونَ
Next Sūrah