43) Sūrat Az-Zukhruf

Printed format

43) سُورَة الزُّخرُف

Ĥā-Mīm 1. H'a Mim حَا-مِيم
Wa Al-Kitābi Al-Mubīni 2. Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha. وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ
'Innā Ja`alnāhu Qur'ānāan `Arabīyāan La`allakum Ta`qilūna 3. Hakika Sisi tumeifanya Qur'ani kwa Kiarabu ili mfahamu. إِنَّا جَعَلْنَاه ُُ قُرْآناً عَرَبِيّا ً لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ
Wa 'Innahu Fī 'Ummi Al-Kitābi Ladaynā La`alīyun Ĥakīmun 4. Na hakika hiyo imo katika Asili ya Maandiko yalioko kwetu, ni tukufu na yenye hikima. وَإِنَّه ُُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيم ٌ
'Afanađribu `Ankumu Adh-Dhikra Şafĥāan 'An Kuntum Qawmāan Musrifīna 5. Je! Tuache kukukumbusheni kabisa kwa kuwa nyinyi ni watu mlio pita mipaka kwa ukafiri? أَفَنَضْرِبُ عَنكُمُ الذِّكْرَ صَفْحاً أَنْ كُنتُمْ قَوْما ً مُسْرِفِينَ
Wa Kam 'Arsalnā Min Nabīyin Al-'Awwalīna 6. Na Manabii wangapi tuliwatuma kwa watu wa zamani! وَكَمْ أَرْسَلْنَا مِنْ نَبِيّ ٍ فِي الأَوَّلِينَ
Wa Mā Ya'tīhim Min Nabīyin 'Illā Kānū Bihi Yastahzi'ūn 7. Na hawajii Nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli. وَمَا يَأْتِيهِمْ مِنْ نَبِيّ ٍ إِلاَّ كَانُوا بِه ِِ يَسْتَهْزِئُون
Fa'ahlaknā 'Ashadda Minhum Baţshāan Wa Mađá Mathalu Al-'Awwalīna 8. Na tuliwaangamiza walio kuwa na nguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani umekwisha pita. فَأَهْلَكْنَا أَشَدَّ مِنْهُمْ بَطْشا ً وَمَضَى مَثَلُ الأَوَّلِينَ
Wa La'in Sa'altahum Man Khalaqa As-Samāwāti Wa Al-'Arđa Layaqūlunna Khalaqahunna Al-`Azīzu Al-`Alīmu 9. Na ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi, وَلَئِنْ سَأَلْتَهُمْ مَنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ لَيَقُولُنَّ خَلَقَهُنَّ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ
Al-Ladhī Ja`ala Lakumu Al-'Arđa Mahdāan Wa Ja`ala Lakum Fīhā Subulāan La`allakum Tahtadūna 10. Ambaye amekufanyieni ardhi kama tandiko, na akakufanyieni ndani yake njia mpate kuongoka. الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الأَرْضَ مَهْدا ً وَجَعَلَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلا ً لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ
Wa Al-Ladhī Nazzala Mina As-Samā'i Mā'an Biqadarin Fa'ansharnā Bihi Baldatan Maytāan Kadhālika Tukhrajūna 11. Na ambaye ndiye aliye teremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi, na kwa hayo tukaifufua nchi iliyo kufa. Na namna hivi ndivyo mtakavyo tolewa. وَالَّذِي نَزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاء ً بِقَدَر ٍ فَأَنشَرْنَا بِه ِِ بَلْدَة ً مَيْتا ً كَذَلِكَ تُخْرَجُونَ
Wa Al-Ladhī Khalaqa Al-'Azwāja Kullahā Wa Ja`ala Lakum Mina Al-Fulki Wa Al-'An`ām Mā Tarkabūna 12. Na ambaye ndiye aliye umba katika kila kitu jike na dume, na akakufanyieni marikebu na wanyama mnao wapanda. وَالَّذِي خَلَقَ الأَزْوَاجَ كُلَّهَا وَجَعَلَ لَكُمْ مِنَ الْفُلْكِ وَالأَنعَام مَا تَرْكَبُونَ
Litastawū `Alá Žuhūrihi Thumma Tadhkurū Ni`mata Rabbikum 'Idhā Astawaytum `Alayhi Wa Taqūlū Subĥāna Al-Ladhī Sakhkhara Lanā Hādhā Wa Mā Kunnā Lahu Muqrinīna 13. Ili mkae vizuri migongoni mwao, kisha mkumbuke neema za Mola wenu Mlezi mnapokaa sawa sawa juu yao na mseme: Ametakasika aliye mfanya huyu atutumikie, na tusingeli weza kufanya haya wenyewe. لِتَسْتَوُوا عَلَى ظُهُورِه ِِ ثُمَّ تَذْكُرُوا نِعْمَةَ رَبِّكُمْ إِذَا اسْتَوَيْتُمْ عَلَيْهِ وَتَقُولُوا سُبْحانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَه ُُ مُقْرِنِينَ
Wa 'Innā 'Ilá Rabbinā Lamunqalibūna 14. Na hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi. وَإِنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ
Wa Ja`alū Lahu Min `Ibādihi Juz'āan 'Inna Al-'Insāna Lakafūrun Mubīnun 15. Na wanamfanyia katika waja wake fungu. Kwa hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila aliye dhaahiri. وَجَعَلُوا لَه ُُ مِنْ عِبَادِه ِِ جُزْءا ً إِنَّ الإِنسَانَ لَكَفُور ٌ مُبِين ٌ
'Am Attakhadha Mimmā Yakhluqu Banātin Wa 'Aşfākum Bil-Banīna 16. Au amejichukulia watoto wanawake katika vile alivyo viumba, na akakuteulieni nyinyi watoto wanaume? أَمْ اتَّخَذَ مِمَّا يَخْلُقُ بَنَات ٍ وَأَصْفَاكُمْ بِالْبَنِينَ
Wa 'Idhā Bushshira 'Aĥaduhum Bimā Đaraba Lilrraĥmani Mathalāan Žalla Wajhuhu Muswaddāan Wa Huwa Kažīmun 17. Na anapo bashiriwa mmoja wao kwa yale aliyo mpigia mfano Mwenyezi Mungu, uso wake husawijika na hujaa hasira. وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُمْ بِمَا ضَرَبَ لِلرَّحْمَنِ مَثَلا ً ظَلَّ وَجْهُه ُُ مُسْوَدّا ً وَهُوَ كَظِيم ٌ
'Awaman Yunashsha'u Fī Al-Ĥilyati Wa Huwa Fī Al-Khāmi Ghayru Mubīnin 18. Ati aliye lelewa katika mapambo, na katika mabishano hawezi kusema kwa bayana...? أَوَمَنْ يُنَشَّأُ فِي الْحِلْيَةِ وَهُوَ فِي الْخِصَامِ غَيْرُ مُبِين ٍ
Wa Ja`alū Al-Malā'ikata Al-Ladhīna Hum `Ibādu Ar-Raĥmāni 'Ināthāan 'Ashahidū Khalqahum Satuktabu Shahādatuhum Wa Yus'alūna 19. Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao? Ushahidi wao utaandikwa na wao watahojiwa! وَجَعَلُوا الْمَلاَئِكَةَ الَّذِينَ هُمْ عِبَادُ الرَّحْمَنِ إِنَاثاً أَشَهِدُوا خَلْقَهُمْ سَتُكْتَبُ شَهَادَتُهُمْ وَيُسْأَلُونَ
Wa Qālū Law Shā'a Ar-Raĥmānu Mā `Abadnāhum Mā Lahum Bidhālika Min `Ilmin 'In Hum 'Illā Yakhruşūna 20. Nao husema: Angeli penda Mwingi wa Rehema tusingeli waabudu sisi. Hawana ujuzi wowote wa hayo! Hawana ila kusema uwongo tu! وَقَالُوا لَوْ شَاءَ الرَّحْمَنُ مَا عَبَدْنَاهُمْ مَا لَهُمْ بِذَلِكَ مِنْ عِلْم ٍ إِنْ هُمْ إِلاَّ يَخْرُصُونَ
'Am 'Ātaynāhum Kitābāan Min Qablihi Fahum Bihi Mustamsikūna 21. Kwani tuliwapa Kitabu kabla ya hichi, na ikawa wao wanakishikilia hicho? أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابا ً مِنْ قَبْلِه ِِ فَهُمْ بِه ِِ مُسْتَمْسِكُونَ
Bal Qālū 'Innā Wajadnā 'Ābā'anā `Alá 'Ummatin Wa 'Innā `Alá 'Āthārihim Muhtadūna 22. Bali wanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, basi na sisi tunaongoza nyayo zao. بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَى أُمَّة ٍ وَإِنَّا عَلَى آثَارِهِمْ مُهْتَدُونَ
Wa Kadhalika Mā 'Arsalnā Min Qablika Fī Qaryatin Min Nadhīrin 'Illā Qāla Mutrafūhā 'Innā Wajadnā 'Ābā'anā `Alá 'Ummatin Wa 'Innā `Alá 'Āthārihim Muqtadūna 23. Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake walio deka kwa starehe walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao. وَكَذَلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِنْ قَبْلِكَ فِي قَرْيَة ٍ مِنْ نَذِير ٍ إِلاَّ قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَى أُمَّة ٍ وَإِنَّا عَلَى آثَارِهِمْ مُقْتَدُونَ
Qāla 'Awalaw Ji'tukum Bi'ahdá Mimmā Wajadtum `Alayhi 'Ābā'akum Qālū 'Innā Bimā 'Ursiltum Bihi Kāfirūna 24. Akasema (Mwonyaji): Hata nikikuleteeni yenye uwongofu bora kuliko mlio wakuta nao baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa tu hayo mliyo tumwa. قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكُمْ بِأَهْدَى مِمَّا وَجَدْتُمْ عَلَيْهِ آبَاءَكُمْ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُمْ بِه ِِ كَافِرُونَ
ntaqamnā Minhumnžur Kayfa Kāna `Āqibatu Al-Mukadhdhibīna 25. Basi tukawalipizia. Angalia ulikuwaje mwisho wa walio kadhibisha! فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ
Wa 'Idh Qāla 'Ibrāhīmu Li'abīhi Wa Qawmihi 'Innanī Barā'un Mimmā Ta`budūna 26. Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yaabudu, وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيه ِِ وَقَوْمِهِ~ِ إِنَّنِي بَرَاء ٌ مِمَّا تَعْبُدُونَ
'Illā Al-Ladhī Faţaranī Fa'innahu Sayahdīni 27. Isipo kuwa yule aliye niumba, kwani Yeye ataniongoa. إِلاَّ الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّه ُُ سَيَهْدِينِ
Wa Ja`alahā Kalimatan Bāqiyatan Fī `Aqibihi La`allahum Yarji`ūna 28. Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee. وَجَعَلَهَا كَلِمَة ً بَاقِيَة ً فِي عَقِبِه ِِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Bal Matta`tu Hā'uulā' Wa 'Ābā'ahum Ĥattá Jā'ahumu Al-Ĥaqqu Wa Rasūlun Mubīnun 29. Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia Haki na Mtume aliye bainisha. بَلْ مَتَّعْتُ هَاؤُلاَء وَآبَاءَهُمْ حَتَّى جَاءَهُمُ الْحَقُّ وَرَسُول ٌ مُبِين ٌ
Wa Lammā Jā'ahumu Al-Ĥaqqu Qālū Hādhā Siĥrun Wa 'Innā Bihi Kāfirūna 30. Na ilipo wafikia Haki wakasema: Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa. وَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ قَالُوا هَذَا سِحْر ٌ وَإِنَّا بِه ِِ كَافِرُونَ
Wa Qālū Lawlā Nuzzila Hādhā Al-Qur'ānu `Alá Rajulin Mina Al-Qaryatayni `Ažīmin 31. Na walisema: Kwa nini Qur'ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii? وَقَالُوا لَوْلاَ نُزِّلَ هَذَا الْقُرْآنُ عَلَى رَجُل ٍ مِنَ الْقَرْيَتَيْنِ عَظِيم ٍ
'Ahum Yaqsimūna Raĥmata Rabbika Naĥnu Qasamnā Baynahum Ma`īshatahum Al-Ĥayāati Ad-Dunyā Wa Rafa`nā Ba`đahum Fawqa Ba`đin Darajātin Liyattakhidha Ba`đuhum Ba`đāan Sukhrīyāan Wa Raĥmatu Rabbika Khayrun Mimmā Yajma`ūna 32. Kwani wao ndio wanao gawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wenginewe wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya. أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَةَ رَبِّكَ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُمْ مَعِيشَتَهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْض ٍ دَرَجَات ٍ لِيَتَّخِذَ بَعْضُهُمْ بَعْضا ً سُخْرِيّا ً وَرَحْمَةُ رَبِّكَ خَيْر ٌ مِمَّا يَجْمَعُونَ
Wa Lawlā 'An Yakūna An-Nāsu 'Ummatan Wāĥidatan Laja`alnā Liman Yakfuru Bir-Raĥmani Libuyūtihim Suqufāan Min Fađđatin Wa Ma`ārija `Alayhā Yažharūna 33. Na lau isinge kuwa watu watakuwa kundi moja tungeli wajaalia wanao mkufuru Rahmani wana nyumba zao zina dari ya fedha, na ngazi zao pia wanazo pandia, وَلَوْلاَ أَنْ يَكُونَ النَّاسُ أُمَّة ً وَاحِدَة ً لَجَعَلْنَا لِمَنْ يَكْفُرُ بِالرَّحْمَنِ لِبُيُوتِهِمْ سُقُفا ً مِنْ فَضَّة ٍ وَمَعَارِجَ عَلَيْهَا يَظْهَرُونَ
Wa Libuyūtihim 'Abwābāan Wa Sururāan `Alayhā Yattaki'ūna 34. Na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyo egemea juu yake, وَلِبُيُوتِهِمْ أَبْوَابا ً وَسُرُراً عَلَيْهَا يَتَّكِئُونَ
Wa Zukhrufāan Wa 'In Kullu Dhālika Lammā Matā`u Al-Ĥayāati Ad-Dunyā Wa Al-'Ākhiratu `Inda Rabbika Lilmuttaqīna 35. Na mapambo. Lakini hayo si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na Akhera iliyoko kwa Mola wako Mlezi ni ya wenye kumchamngu. وَزُخْرُفا ً وَإِنْ كُلُّ ذَلِكَ لَمَّا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَالآخِرَةُ عِنْدَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ
Wa Man Ya`shu `An Dhikri Ar-Raĥmāni Nuqayyiđ Lahu Shayţānāan Fahuwa Lahu Qarīnun 36. Anaye yafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea Shet'ani kuwa ndiye rafiki yake. وَمَنْ يَعْشُ عَنْ ذِكْرِ الرَّحْمَنِ نُقَيِّضْ لَه ُُ شَيْطَانا ً فَهُوَ لَه ُُ قَرِين ٌ
Wa 'Innahum Layaşuddūnahum `Ani As-Sabīli Wa Yaĥsabūna 'Annahum Muhtadūna 37. Na hakika wao wanawazuilia Njia na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka. وَإِنَّهُمْ لَيَصُدُّونَهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ مُهْتَدُونَ
Ĥattá 'Idhā Jā'anā Qāla Yā Layta Baynī Wa Baynaka Bu`da Al-Mashriqayni Fabi'sa Al-Qarīnu 38. Hata atakapo tujia atasema: Laiti ungeli kuwako baina yangu na wewe kama umbali baina ya mashariki na magharibi. Rafiki mwovu mno wewe! حَتَّى إِذَا جَاءَنَا قَالَ يَالَيْتَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ بُعْدَ الْمَشْرِقَيْنِ فَبِئْسَ الْقَرِينُ
Wa Lan Yanfa`akumu Al-Yawma 'Idh Žalamtum 'Annakum Al-`Adhābi Mushtarikūna 39. Na kwa kuwa mlidhulumu, haitakufaeni kitu leo kwamba nyinyi mnashirikiana katika adhabu. وَلَنْ يَنفَعَكُمُ الْيَوْمَ إِذْ ظَلَمْتُمْ أَنَّكُمْ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ
'Afa'anta Tusmi`u Aş-Şumma 'Aw Tahdī Al-`Umya Wa Man Kāna Fī Đalālin Mubīnin 40. Je! Unaweza kuwasikilizisha viziwi, au unaweza kuwaongoa vipofu na waliomo katika upotofu ulio wazi? أَفَأَنْتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ أَوْ تَهْدِي الْعُمْيَ وَمَنْ كَانَ فِي ضَلاَل ٍ مُبِين ٍ
Fa'immā Nadh/habanna Bika Fa'innā Minhum Muntaqimūna 41. Na hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi chetu kwao. فَإِمَّا نَذْهَبَنَّ بِكَ فَإِنَّا مِنْهُمْ مُنْتَقِمُونَ
'Aw Nuriyannaka Al-Ladhī Wa`adnāhum Fa'innā `Alayhim Muqtadirūna 42. Au tutakuonyesha tulio waahidi. Nasi bila ya shaka tuna uweza juu yao. أَوْ نُرِيَنَّكَ الَّذِي وَعَدْنَاهُمْ فَإِنَّا عَلَيْهِمْ مُقْتَدِرُونَ
Fāstamsik Bial-Ladhī 'Ūĥiya 'Ilayka 'Innaka `Alá Şirāţin Mustaqīmin 43. Basi wewe yashike yaliyo funuliwa kwako. Hakika wewe uko kwenye Njia Iliyo Nyooka. فَاسْتَمْسِكْ بِالَّذِي أُوحِيَ إِلَيْكَ إِنَّكَ عَلَى صِرَاط ٍ مُسْتَقِيم ٍ
Wa 'Innahu Ladhikrun Laka Wa Liqawmika Wa Sawfa Tus'alūna 44. Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa. وَإِنَّه ُُ لَذِكْر ٌ لَكَ وَلِقَوْمِكَ وَسَوْفَ تُسْأَلُونَ
Wa As'al Man 'Arsalnā Min Qablika Min Rusulinā 'Aja`alnā Min Dūni Ar-Raĥmāni 'Ālihatan Yu`badūna 45. Na waulize Mitume wetu tulio watuma kabla yako: Je! Tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rah'mani? وَاسْأَلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِنْ قَبْلِكَ مِنْ رُسُلِنَا أَجَعَلْنَا مِنْ دُونِ الرَّحْمَنِ آلِهَة ً يُعْبَدُونَ
Wa Laqad 'Arsalnā Mūsá Bi'āyātinā 'Ilá Fir`awna Wa Mala'ihi Faqāla 'Innī Rasūlu Rabbi Al-`Ālamīna 46, Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu ende kwa Firauni na waheshimiwa wake, na akasema: Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote! وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَى بِآيَاتِنَا إِلَى فِرْعَوْنَ وَمَلَئِه ِِ فَقَالَ إِنِّي رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ
Falammā Jā'ahum Bi'āyātinā 'Idhā Hum Minhā Yađĥakūna 47. Lakini alipo wajia na Ishara zetu wakaingia kuzicheka. فَلَمَّا جَاءَهُمْ بِآيَاتِنَا إِذَا هُمْ مِنْهَا يَضْحَكُونَ
Wa Mā Nurīhim Min 'Āyatin 'Illā Hiya 'Akbaru Min 'Ukhtihā Wa 'Akhadhnāhum Bil-`Adhābi La`allahum Yarji`ūna 48. Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyenginewe. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee. وَمَا نُرِيهِمْ مِنْ آيَة ٍ إِلاَّ هِيَ أَكْبَرُ مِنْ أُخْتِهَا وَأَخَذْنَاهُمْ بِالْعَذَابِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Wa Qālū Yā 'Ayyuhā As-Sāĥiru Ad`u Lanā Rabbaka Bimā `Ahida `Indaka 'Innanā Lamuhtadūn 49. Na wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyo kuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka. وَقَالُوا يَاأَيُّهَا السَّاحِرُ ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِنْدَكَ إِنَّنَا لَمُهْتَدُون
Falammā Kashafnā `Anhumu Al-`Adhāba 'Idhā Hum Yankuthūna 50. Basi tulipo waondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja ahadi. فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ
Wa Nādá Fir`awnu Fī Qawmihi Qāla Yā Qawmi 'Alaysa Lī Mulku Mişra Wa Hadhihi Al-'Anhāru Tajrī Min Taĥtī 'Afalā Tubşirūna 51. Na Firauni alitangaza kwa watu wake, akisema: Enyi watu wangu! Kwani mimi sinao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu? Je! Hamwoni? وَنَادَى فِرْعَوْنُ فِي قَوْمِه ِِ قَالَ يَاقَوْمِ أَلَيْسَ لِي مُلْكُ مِصْرَ وَهَذِهِ الأَنْهَارُ تَجْرِي مِنْ تَحْتِي أَفَلاَ تُبْصِرُونَ
'Am 'Anā Khayrun Min Hādhā Al-Ladhī Huwa Mahīnun Wa Lā Yakādu Yubīnu 52. Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi? أَمْ أَنَا خَيْر ٌ مِنْ هَذَا الَّذِي هُوَ مَهِين ٌ وَلاَ يَكَادُ يُبِينُ
Falawlā 'Ulqiya `Alayhi 'Aswiratun Min Dhahabin 'Aw Jā'a Ma`ahu Al-Malā'ikatu Muqtarinīna 53. Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu, au hawakuja Malaika pamoja naye wakamwandama? فَلَوْلاَ أُلْقِيَ عَلَيْهِ أَسْوِرَة ٌ مِنْ ذَهَبٍ أَوْ جَاءَ مَعَهُ الْمَلاَئِكَةُ مُقْتَرِنِينَ
Fāstakhaffa Qawmahu Fa'aţā`ūhu 'Innahum Kānū Qawmāan Fāsiqīna 54. Basi aliwachezea watu wake, na wakamt'ii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu. فَاسْتَخَفَّ قَوْمَه ُُ فَأَطَاعُوهُ~ُ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْما ً فَاسِقِينَ
Falammā 'Āsafūnā Antaqamnā Minhum Fa'aghraqnāhum 'Ajma`īna 55. Walipo tukasirisha tuliwapatiliza tukawazamisha wote! فَلَمَّا آسَفُونَا انتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ
Faja`alnāhum Salafāan Wa Mathalāan Lil'ākhirīna 56. Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye. فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفا ً وَمَثَلا ً لِلآخِرِينَ
Wa Lammā Đuriba Abnu Maryama Mathalāan 'Idhā Qawmuka Minhu Yaşiddūna 57. Na alipo pigiwa mfano Mwana wa Mariamu, watu wako waliupiga ukelele. وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلا ً إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ
Wa Qālū 'A'ālihatunā Khayrun 'Am Huwa Mā Đarabūhu Laka 'Illā Jadalāan Bal Hum Qawmun Khaşimūna 58. Wakasema: Miungu yetu kwani si bora kuliko huyu? Hawakukupigia mfano huo ila kwa ubishi tu. Bali hao ni watu wagomvi! وَقَالُوا أَآلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ مَا ضَرَبُوه ُُ لَكَ إِلاَّ جَدَلا ً بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ
'In Huwa 'Illā `Abdun 'An`amnā `Alayhi Wa Ja`alnāhu Mathalāan Libanī 'Isrā'īla 59. Hakuwa yeye (Isa) ila ni Mtumwa tuliye mneemesha na tukamfanya ni mfano kwa Wana wa Israili. إِنْ هُوَ إِلاَّ عَبْدٌ أَنْعَمْنَا عَلَيْهِ وَجَعَلْنَاه ُُ مَثَلا ً لِبَنِي إِسْرَائِيلَ
Wa Law Nashā'u Laja`alnā Minkum Malā'ikatan Al-'Arđi Yakhlufūna 60. Na tungeli penda tungeli wafanyia miongoni mwenu Malaika katika ardhi wakifuatana. وَلَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَا مِنْكُمْ مَلاَئِكَة ً فِي الأَرْضِ يَخْلُفُونَ
Wa 'Innahu La`ilmun Lilssā`ati Falā Tamtarunna Bihā Wa Attabi`ūnī Hādhā Şirāţun Mustaqīmun 61. Na kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka. وَإِنَّه ُُ لَعِلْم ٌ لِلسَّاعَةِ فَلاَ تَمْتَرُنَّ بِهَا وَاتَّبِعُونِي هَذَا صِرَاط ٌ مُسْتَقِيم ٌ
Wa Lā Yaşuddannakumu Ash-Shayţānu 'Innahu Lakum `Adūwun Mubīnun 62. Wala asikuzuilieni Shet'ani. Hakika yeye ni adui yenu wa dhaahiri. وَلاَ يَصُدَّنَّكُمُ الشَّيْطَانُ إِنَّه ُُ لَكُمْ عَدُوّ ٌ مُبِين ٌ
Wa Lammā Jā'a `Īsá Bil-Bayyināti Qāla Qad Ji'tukum Bil-Ĥikmati Wa Li'abayyina Lakum Ba`đa Al-Ladhī Takhtalifūna Fīhi Fa Attaqū Allāha Wa 'Aţī`ūni 63. Na alipo kuja Isa na dalili zilizo wazi, alisema: Nimekujieni na hikima, na ili nikuelezeni baadhi ya yale mliyo khitalifiana. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na mnit'ii mimi. وَلَمَّا جَاءَ عِيسَى بِالْبَيِّنَاتِ قَالَ قَدْ جِئْتُكُمْ بِالْحِكْمَةِ وَلِأَبَيِّنَ لَكُمْ بَعْضَ الَّذِي تَخْتَلِفُونَ فِيه ِِ فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ
'Inna Allāha Huwa Rabbī Wa Rabbukum Fā`budūhu Hādhā Şirāţun Mustaqīmun 64. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na ni Mola wenu Mlezi. Basi Muabuduni Yeye tu. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka. إِنَّ اللَّهَ هُوَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوه ُُ هَذَا صِرَاط ٌ مُسْتَقِيم ٌ
khtalafa Al-'Aĥzābu Min Baynihim Fawaylun Lilladhīna Žalamū Min `Adhābi Yawmin 'Alīmin 65. Lakini makundi kwa makundi yao yalikhitalifiana wao kwa wao. Ole wao walio dhulumu kwa adhabu ya siku chungu. فَاخْتَلَفَ الأَحْزَابُ مِنْ بَيْنِهِمْ فَوَيْل ٌ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْ عَذَابِ يَوْمٍ أَلِيم ٍ
Hal Yanžurūna 'Illā As-Sā`ata 'An Ta'tiyahum Baghtatan Wa Hum Lā Yash`urūna 66. Je! Nini wanangojea ila Saa iwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui? هَلْ يَنظُرُونَ إِلاَّ السَّاعَةَ أَنْ تَأْتِيَهُمْ بَغْتَة ً وَهُمْ لاَ يَشْعُرُونَ
Al-'Akhillā'u Yawma'idhin Ba`đuhum Liba`đin `Adūwun 'Illā Al-Muttaqīna 67. Siku hiyo marafiki watakuwa ni maadui, wao kwa wao, isipo kuwa wachamngu. الأَخِلاَّءُ يَوْمَئِذ ٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوّ ٌ إِلاَّ الْمُتَّقِينَ
Yā `Ibādi Lā Khawfun `Alaykumu Al-Yawma Wa Lā 'Antum Taĥzanūna 68. Enyi waja wangu! Hamtakuwa na khofu siku hiyo, wala hamtahuzunika. يَاعِبَادِ لاَ خَوْفٌ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ وَلاَ أَنْتُمْ تَحْزَنُونَ
Al-Ladhīna 'Āmanū Bi'āyātinā Wa Kānū Muslimīna 69. Ambao waliziamini Ishara zangu na walikuwa Waislamu. الَّذِينَ آمَنُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا مُسْلِمِينَ
Adkhulū Al-Jannata 'Antum Wa 'Azwājukum Tuĥbarūna 70. Ingieni Peponi, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo. ادْخُلُوا الْجَنَّةَ أَنْتُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ تُحْبَرُونَ
Yuţāfu `Alayhim Bişiĥāfin Min Dhahabin Wa 'Akwābin Wa Fīhā Mā Tashtahīhi Al-'Anfusu Wa Taladhdhu Al-'A`yunu Wa 'Antum Fīhā Khālidūna 71. Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele. يُطَافُ عَلَيْهِمْ بِصِحَاف ٍ مِنْ ذَهَب ٍ وَأَكْوَاب ٍ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الأَنفُسُ وَتَلَذُّ الأَعْيُنُ وَأَنْتُمْ فِيهَا خَالِدُونَ
Wa Tilka Al-Jannatu Allatī 'Ūrithtumūhā Bimā Kuntum Ta`malūna 72. Na hiyo ni Pepo mliyo rithishwa kwa hayo mliyo kuwa mkiyafanya. وَتِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Lakum Fīhā Fākihatun Kathīratun Minhā Ta'kulūna 73. Mnayo humo matunda mengi mtakayo yala. لَكُمْ فِيهَا فَاكِهَة ٌ كَثِيرَة ٌ مِنْهَا تَأْكُلُونَ
'Inna Al-Mujrimīna Fī `Adhābi Jahannama Khālidūn 74. Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannamu. إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُون
Lā Yufattaru `Anhum Wa Hum Fīhi Mublisūna 75. Hawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa. لاَ يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيه ِِ مُبْلِسُونَ
Wa Mā Žalamnāhum Wa Lakin Kānū Humu Až-Žālimīna 76. Wala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio walio kuwa madhaalimu. وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَكِنْ كَانُوا هُمُ الظَّالِمِينَ
Wa Nādaw Yā Māliku Liyaqđi `Alaynā Rabbuka Qāla 'Innakum Mākithūna 77. Nao watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi! Naye aseme: Hakika nyinyi mtakaa humo humo! وَنَادَوْا يَامَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ قَالَ إِنَّكُمْ مَاكِثُونَ
Laqad Ji'nākum Bil-Ĥaqqi Wa Lakinna 'Aktharakum Lilĥaqqi Kārihūna 78. Kwa yakini tulikuleteeni Haki, lakini wengi katika nyinyi mlikuwa mnaichukia Haki. لَقَدْ جِئْنَاكُمْ بِالْحَقِّ وَلَكِنَّ أَكْثَرَكُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ
'Am 'Abramū 'Amrāan Fa'innā Mubrimūna 79. Au waliweza kupitisha amri yao? Bali ni Sisi ndio tunao pitisha. أَمْ أَبْرَمُوا أَمْرا ً فَإِنَّا مُبْرِمُونَ
'Am Yaĥsabūna 'Annā Lā Nasma`u Sirrahum Wa Najwāhum Balá Wa Rusulunā Ladayhim Yaktubūna 80. Au wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong'ono yao? Wapi! Na wajumbe wetu wapo karibu nao, wanayaandika. أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لاَ نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُمْ بَلَى وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ
Qul 'In Kāna Lilrraĥmani Waladun Fa'anā 'Awwalu Al-`Ābidīna 81. Sema: Ingeli kuwa Rahmani ana mwana, basi mimi ningeli kuwa wa kwanza kumuabudu. قُلْ إِنْ كَانَ لِلرَّحْمَنِ وَلَد ٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ
Subĥāna Rabbi As-Samāwāti Wa Al-'Arđi Rabbi Al-`Arshi `Ammā Yaşifūna 82. Ametakasika Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, Mola Mlezi wa A'rshi, na hayo wanayo msifia. سُبْحَانَ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ
Fadharhum Yakhūđū Wa Yal`abū Ĥattá Yulāqū Yawmahumu Al-Ladhī Yū`adūna 83. Basi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao waliyo ahidiwa. فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّى يُلاَقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ
Wa Huwa Al-Ladhī Fī As-Samā'i 'Ilahun Wa Fī Al-'Arđi 'Ilahun Wa Huwa Al-Ĥakīmu Al-`Alīmu 84. Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hikima, Mwenye ujuzi. وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَه ٌ ٌ وَفِي الأَرْضِ إِلَه ٌ ٌ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ
Wa Tabāraka Al-Ladhī Lahu Mulku As-Samāwāti Wa Al-'Arđi Wa Mā Baynahumā Wa `Indahu `Ilmu As-Sā`ati Wa 'Ilayhi Turja`ūna 85. Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo ndani yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa. وَتَبَارَكَ الَّذِي لَه ُُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَعِنْدَه ُُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
Wa Lā Yamliku Al-Ladhīna Yad`ūna Min Dūnihi Ash-Shafā`ata 'Illā Man Shahida Bil-Ĥaqqi Wa Hum Ya`lamūna 86. Wala hao mnao waomba badala yake Yeye hawana uweza wa kumwombea mtu, isipo kuwa anaye shuhudia kwa haki, na wao wanajua. وَلاَ يَمْلِكُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِنْ دُونِهِ الشَّفَاعَةَ إِلاَّ مَنْ شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ
Wa La'in Sa'altahum Man Khalaqahum Layaqūlunna Allāhu Fa'anná Yu'ufakūna 87. Na ukiwauliza ni nani aliye waumba? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu! Basi ni wapi wanako geuziwa? وَلَئِنْ سَأَلْتَهُمْ مَنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّهُ فَأَنَّى يُؤْفَكُونَ
Wa Qīlihi Yā Rabbi 'Inna Hā'uulā' Qawmun Lā Yu'uminūna 88. Na usemi wake (Mtume) ni: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hawa ni watu wasio amini. وَقِيلِه ِِ يَارَبِّ إِنَّ هَاؤُلاَء قَوْم ٌ لاَ يُؤْمِنُونَ
Fāşfaĥ `Anhum Wa Qul Salāmun Fasawfa Ya`lamūna 89. Basi wasamehe, na uwambie maneno ya salama. Watakuja jua. *   فَاصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلاَم ٌ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
Next Sūrah