37) Sūrat Aş-Şāffāt

Printed format

37) سُورَة الصَّافَّات

Wa Aş-Şāffāti Şaffāan 1. Naapa kwa wanao jipanga kwa safu. وَالصَّافَّاتِ صَفّا ً
Fālzzājirāti Zajan 2. Na kwa wenye kukataza mabaya. فَالزَّاجِرَاتِ زَجْرا ً
Fālttāliyāti Dhikrāan 3. Na kwa wenye kusoma Ukumbusho. فَالتَّالِيَاتِ ذِكْرا ً
'Inna 'Ilahakum Lawāĥidun 4. Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja. إِنَّ إِلَهَكُمْ لَوَاحِد ٌ
Rabbu As-Samāwāti Wa Al-'Arđi Wa Mā Baynahumā Wa Rabbu Al-Mashāriqi 5. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote. رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ الْمَشَارِقِ
'Innā Zayyannā As-Samā'a Ad-Dunyā Bizīnatin Al-Kawākib 6. Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. إِنَّا زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِزِينَة ٍ الْكَوَاكِب
Wa Ĥifžāan Min Kulli Shayţāninridin 7. Na kulinda na kila shet'ani a'si. وَحِفْظا ً مِنْ كُلِّ شَيْطَان ٍ مَارِد ٍ
Lā Yassamma`ūna 'Ilá Al-Mala'i Al-'A`lá Wa Yuqdhafūna Min Kulli Jānibin 8. Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande. لاَ يَسَّمَّعُونَ إِلَى الْمَلَإِ الأَعْلَى وَيُقْذَفُونَ مِنْ كُلِّ جَانِب ٍ
Duĥūrāan Wa Lahum `Adhābun Wa Aşibun 9. Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu. دُحُورا ً وَلَهُمْ عَذَاب ٌ وَاصِب ٌ
'Illā Man Khaţifa Al-Khaţfata Fa'atba`ahu Shihābun Thāqibāun 10. Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara. إِلاَّ مَنْ خَطِفَ الْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَه ُُ شِهَاب ٌ ثَاقِبا ٌ
Fāstaftihim 'Ahum 'Ashaddu Khalqāan 'Am Man Khalaqnā 'Innā Khalaqnāhum Min Ţīnin Lāzibin 11. Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata. فَاسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقاً أَمْ مَنْ خَلَقْنَا إِنَّا خَلَقْنَاهُمْ مِنْ طِين ٍ لاَزِب ٍ
Bal `Ajibta Wa Yaskharūna 12. Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara. بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ
Wa 'Idhā Dhukkirū Lā Yadhkurūna 13. Na wanapo kumbushwa hawakumbuki. وَإِذَا ذُكِّرُوا لاَ يَذْكُرُونَ
Wa 'Idhā Ra'aw 'Āyatan Yastaskhirūna 14. Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara. وَإِذَا رَأَوْا آيَة ً يَسْتَسْخِرُونَ
Wa Qālū 'In Hādhā 'Illā Siĥrun Mubīnun 15. Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri. وَقَالُوا إِنْ هَذَا إِلاَّ سِحْر ٌ مُبِين ٌ
'A'idhā Mitnā Wa Kunnā Turābāan Wa `Ižāmāan 'A'innā Lamabthūna 16. Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa? أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابا ً وَعِظَاماً أَئِنَّا لَمَبْعُوثُونَ
'Awa'ābā'uunā Al-'Awwalūna 17. Hata baba zetu wa zamani? أَوَآبَاؤُنَا الأَوَّلُونَ
Qul Na`am Wa 'Antumkhirūna 18. Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili. قُلْ نَعَمْ وَأَنْتُمْ دَاخِرُونَ
Fa'innamā Hiya Zajratun Wāĥidatun Fa'idhā Hum Yanžurūna 19. Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona! فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَة ٌ وَاحِدَة ٌ فَإِذَا هُمْ يَنظُرُونَ
Wa Qālū Yā Waylanā Hādhā Yawmu Ad-Dīni 20. Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo. وَقَالُوا يَاوَيْلَنَا هَذَا يَوْمُ الدِّينِ
dhā Yawmu Al-Faşli Al-Ladhī Kuntum Bihi Tukadhdhibūna 21. Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha. هَذَا يَوْمُ الْفَصْلِ الَّذِي كُنتُمْ بِه ِِ تُكَذِّبُونَ
Aĥshurū Al-Ladhīna Žalamū Wa 'Azwājahum Wa Mā Kānū Ya`budūna 22. Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu - احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ
Min Dūni Allāhi Fāhdūhum 'Ilá Şirāţi Al-Jaĥīmi 23. Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu! مِنْ دُونِ اللَّهِ فَاهْدُوهُمْ إِلَى صِرَاطِ الْجَحِيمِ
Wa Qifūhum 'Innahum Mas'ūlūna 24. Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa: وَقِفُوهُمْ إِنَّهُمْ مَسْئُولُونَ
Mā Lakum Lā Tanāşarūna 25. Mna nini? Mbona hamsaidiani? مَا لَكُمْ لاَ تَنَاصَرُونَ
Bal Humu Al-Yawma Mustaslimūna 26. Bali hii leo, watasalimu amri. بَلْ هُمُ الْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ
Wa 'Aqbala Ba`đuhum `Alá Ba`đin Yatasā'alūna 27. Watakabiliana wao kwa wao kuulizana. وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْض ٍ يَتَسَاءَلُونَ
Qālū 'Innakum Kuntum Ta'tūnanā `Ani Al-Yamīni 28. Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia. قَالُوا إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ الْيَمِينِ
Qālū Bal Lam Takūnū Mu'uminīna 29. Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini. قَالُوا بَلْ لَمْ تَكُونُوا مُؤْمِنِينَ
Wa Mā Kāna Lanā `Alaykum Min Sulţānin Bal Kuntum Qawmāan Ţāghīna 30. Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu. وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُمْ مِنْ سُلْطَان ٍ بَلْ كُنتُمْ قَوْما ً طَاغِينَ
Faĥaqqa `Alaynā Qawlu Rabbinā 'Innā Ladhā'iqūna 31. Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu. فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَا إِنَّا لَذَائِقُونَ
Fa'aghwaynākum 'Innā Kunnā Ghāwīna 32. Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu. فَأَغْوَيْنَاكُمْ إِنَّا كُنَّا غَاوِينَ
Fa'innahum Yawma'idhin Al-`Adhābi Mushtarikūna 33. Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja. فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذ ٍ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ
'Innā Kadhālika Naf`alu Bil-Mujrimīna 34. Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu. إِنَّا كَذَلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ
'Innahum Kānū 'Idhā Qīla Lahum Lā 'Ilāha 'Illā Allāhu Yastakbirūna 35. Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna. إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لاَ إِلَهَ~َ إِلاَّ اللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ
Wa Yaqūlūna 'A'innā Latārikū 'Ālihatinā Lishā`irin Majnūnin 36. Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu? وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُوا آلِهَتِنَا لِشَاعِر ٍ مَجْنُون ٍ
Bal Jā'a Bil-Ĥaqqi Wa Şaddaqa Al-Mursalīna 37. Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume. بَلْ جَاءَ بِالْحَقِّ وَصَدَّقَ الْمُرْسَلِينَ
'Innakum Ladhā'iqū Al-`Adhābi Al-'Alīmi 38. Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu. إِنَّكُمْ لَذَائِقُو الْعَذَابِ الأَلِيمِ
Wa Mā Tujzawna 'Illā Mā Kuntum Ta`malūna 39. Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya. وَمَا تُجْزَوْنَ إِلاَّ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
'Illā `Ibāda Allāhi Al-Mukhlaşīna 40. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa. إِلاَّ عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ
'Ūlā'ika Lahum Rizqun Ma`lūmun 41. Hao ndio watakao pata riziki maalumu, أُوْلَائِكَ لَهُمْ رِزْق ٌ مَعْلُوم ٌ
Fawākihu Wa Hum Mukramūna 42. Matunda, nao watahishimiwa. فَوَاكِه ُُ وَهُمْ مُكْرَمُونَ
Fī Jannāti An-Na`īmi 43. Katika Bustani za neema. فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ
`Alá Sururin Mutaqābilīna 44. Wako juu ya viti wamekabiliana. عَلَى سُرُر ٍ مُتَقَابِلِينَ
Yuţāfu `Alayhim Bika'sin Min Ma`īnin 45. Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem يُطَافُ عَلَيْهِمْ بِكَأْس ٍ مِنْ مَعِين ٍ
Bayđā'a Ladhdhatin Lilshshāribīna 46. Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao. بَيْضَاءَ لَذَّة ٍ لِلشَّارِبِينَ
Lā Fīhā Ghawlun Wa Lā Hum `Anhā Yunzafūna 47. Hakina madhara, wala hakiwaleweshi. لاَ فِيهَا غَوْل ٌ وَلاَ هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ
Wa `Indahum Qāşirātu Aţ-Ţarfi `Īnun 48. Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri. وَعِنْدَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ عِين ٌ
Ka'annahunna Bayđun Maknūnun 49. Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika. كَأَنَّهُنَّ بَيْض ٌ مَكْنُون ٌ
Fa'aqbala Ba`đuhum `Alá Ba`đin Yatasā'alūna 50. Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe. فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْض ٍ يَتَسَاءَلُونَ
Qāla Qā'ilun Minhum 'Innī Kāna Lī Qarīnun 51. Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki قَالَ قَائِل ٌ مِنْهُمْ إِنِّي كَانَ لِي قَرِين ٌ
Yaqūlu 'A'innaka Lamina Al-Muşaddiqīna 52. Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki يَقُولُ أَئِنَّكَ لَمِنَ الْمُصَدِّقِينَ
'A'idhā Mitnā Wa Kunnā Turābāan Wa `Ižāmāan 'A'innā Lamadīnūna 53. Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa? أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابا ً وَعِظَاماً أَئِنَّا لَمَدِينُونَ
Qāla Hal 'Antum Muţţali`ūna 54. Atasema: Je! Nyie mnawaona? قَالَ هَلْ أَنْتُمْ مُطَّلِعُونَ
Fāţţala`a Fara'āhu Fī Sawā'i Al-Jaĥīmi 55. Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu. فَاطَّلَعَ فَرَآهُ فِي سَوَاءِ الْجَحِيمِ
Qāla Ta-Allāhi 'In Kidta Laturdīni 56. Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza. قَالَ تَاللَّهِ إِنْ كِدْتَ لَتُرْدِينِ
Wa Lawlā Ni`matu Rabbī Lakuntu Mina Al-Muĥđarīna 57. Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningeli kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa. وَلَوْلاَ نِعْمَةُ رَبِّي لَكُنتُ مِنَ الْمُحْضَرِينَ
'Afamā Naĥnu Bimayyitīna 58. Je! Sisi hatutakufa, أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ
'Illā Mawtatanā Al-'Ūlá Wa Mā Naĥnu Bimu`adhdhabīna 59. Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa. إِلاَّ مَوْتَتَنَا الأُولَى وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ
'Inna Hādhā Lahuwa Al-Fawzu Al-`Ažīmu 60. Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa. إِنَّ هَذَا لَهُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ
Limithli Hādhā Falya`mali Al-`Āmilūna 61. Kwa mfano wa haya nawatende watendao. لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ
'Adhalika Khayrun Nuzulāan 'Am Shajaratu Az-Zaqqūmi 62. Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum? أَذَلِكَ خَيْر ٌ نُزُلاً أَمْ شَجَرَةُ الزَّقُّومِ
'Innā Ja`alnāhā Fitnatan Lilžžālimīna 63. Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu. إِنَّا جَعَلْنَاهَا فِتْنَة ً لِلظَّالِمِينَ
'Innahā Shajaratun Takhruju Fī 'Aşli Al-Jaĥīmi 64. Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu. إِنَّهَا شَجَرَة ٌ تَخْرُجُ فِي أَصْلِ الْجَحِيمِ
Ţal`uhā Ka'annahu Ru'ūsu Ash-Shayāţīni 65. Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet'ani. طَلْعُهَا كَأَنَّه ُُ رُءُوسُ الشَّيَاطِينِ
Fa'innahum La'ākilūna Minhā Famāli'ūna Minhā Al-Buţūna 66. Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo. فَإِنَّهُمْ لَآكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ
Thumma 'Inna Lahum `Alayhā Lashawbāan Min Ĥamīmin 67. Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka. ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبا ً مِنْ حَمِيم ٍ
Thumma 'Inna Marji`ahum La'ilá Al-Jaĥīmi 68. Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu. ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى الْجَحِيمِ
'Innahum 'Alfaw 'Ābā'ahum Đāllīna 69. Hakika waliwakuta baba zao wamepotea. إِنَّهُمْ أَلْفَوْا آبَاءَهُمْ ضَالِّينَ
Fahum `Alá 'Āthārihim Yuhra`ūna 70. Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao. فَهُمْ عَلَى آثَارِهِمْ يُهْرَعُونَ
Wa Laqad Đalla Qablahum 'Aktharu Al-'Awwalīna 71. Na bila ya shaka walikwisha potea kabla yao wengi wa watu wa zamani. وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ الأَوَّلِينَ
Wa Laqad 'Arsalnā Fīhim Mundhirīna 72. Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji. وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِمْ مُنذِرِينَ
nžur Kayfa Kāna `Āqibatu Al-Mundharīna 73. Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa walio onywa. فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُنذَرِينَ
'Illā `Ibāda Allāhi Al-Mukhlaşīna 74. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa. إِلاَّ عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ
Wa Laqad Nādānā Nūĥun Falani`ma Al-Mujībūna 75. Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji. وَلَقَدْ نَادَانَا نُوح ٌ فَلَنِعْمَ الْمُجِيبُونَ
Wa Najjaynāhu Wa 'Ahlahu Mina Al-Karbi Al-`Ažīmi 76. Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa. وَنَجَّيْنَاه ُُ وَأَهْلَه ُُ مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ
Wa Ja`alnā Dhurrīyatahu Humu Al-Bāqīna 77. Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia. وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَه ُُ هُمُ الْبَاقِينَ
Wa Taraknā `Alayhi Fī Al-'Ākhirīna 78. Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye. وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الآخِرِينَ
Salāmun `Alá Nūĥin Al-`Ālamīna 79. Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote! سَلاَمٌ عَلَى نُوح ٍ فِي الْعَالَمِينَ
'Innā Kadhālika Naj Al-Muĥsinīna 80. Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema. إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ
'Innahu Min `Ibādinā Al-Mu'uminīna 81. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. إِنَّه ُُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ
Thumma 'Aghraq Al-'Ākharīna 82. Kisha tukawazamisha wale wengine. ثُمَّ أَغْرَقْنَا الآخَرِينَ
Wa 'Inna Min Shī`atihi La'ibrāhīma 83. Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake, وَإِنَّ مِنْ شِيعَتِه ِِ لَإِبْرَاهِيمَ
'Idh Jā'a Rabbahu Biqalbin Salīmin 84. Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima. إِذْ جَاءَ رَبَّه ُُ بِقَلْب ٍ سَلِيم ٍ
'Idh Qāla Li'abīhi Wa Qawmihi Mādhā Ta`budūna 85. Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini? إِذْ قَالَ لِأَبِيه ِِ وَقَوْمِه ِِ مَاذَا تَعْبُدُونَ
'A'ifkāan 'Ālihatan Dūna Allāhi Turīdūna 86. Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu? أَئِفْكا ً آلِهَة ً دُونَ اللَّهِ تُرِيدُونَ
Famā Žannukum Birabbi Al-`Ālamīna 87. Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote? فَمَا ظَنُّكُمْ بِرَبِّ الْعَالَمِينَ
Fanažara Nažratan An-Nujūmi 88. Kisha akapiga jicho kutazama nyota. فَنَظَرَ نَظْرَة ً فِي النُّجُومِ
Faqāla 'Innī Saqīmun 89. Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa! فَقَالَ إِنِّي سَقِيم ٌ
Fatawallaw `Anhu Mudbirīna 90. Nao wakamwacha, wakampa kisogo. فَتَوَلَّوْا عَنْهُ مُدْبِرِينَ
Farāgha 'Ilá 'Ālihatihim Faqāla 'Alā Ta'kulūna 91. Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli? فَرَاغَ إِلَى آلِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلاَ تَأْكُلُونَ
Mā Lakum Lā Tanţiqūna 92. Mna nini hata hamsemi? مَا لَكُمْ لاَ تَنطِقُونَ
Farāgha `Alayhim Đarbāan Bil-Yamīni 93. Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia. فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبا ً بِالْيَمِينِ
Fa'aqbalū 'Ilayhi Yaziffūna 94. Basi wakamjia upesi upesi. فَأَقْبَلُوا إِلَيْهِ يَزِفُّونَ
Qāla 'Ata`budūna Mā Tanĥitūna 95. Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe? قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ
Wa Allāhu Khalaqakum Wa Mā Ta`malūna 96. Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya! وَاللَّهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ
Qālū Abnū Lahu Bunyānāan Fa'alqūhu Fī Al-Jaĥīmi 97. Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo! قَالُوا ابْنُوا لَه ُُ بُنْيَانا ً فَأَلْقُوه ُُ فِي الْجَحِيمِ
Fa'arādū Bihi Kaydāan Faja`alnāhumu Al-'Asfalīna 98. Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini. فَأَرَادُوا بِه ِِ كَيْدا ً فَجَعَلْنَاهُمُ الأَسْفَلِينَ
Wa Qāla 'Innī Dhāhibun 'Ilá Rabbī Sayahdīni 99. Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa. وَقَالَ إِنِّي ذَاهِب ٌ إِلَى رَبِّي سَيَهْدِينِ
Rabbi Hab Lī Mina Aş-Şāliĥīna 100. Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema. رَبِّ هَبْ لِي مِنَ الصَّالِحِينَ
Fabashsharnāhu Bighulāmin Ĥalīmin 101. Basi tukambashiria mwana aliye mpole. فَبَشَّرْنَاه ُُ بِغُلاَمٍ حَلِيم ٍ
Falammā Balagha Ma`ahu As-Sa`ya Qāla Yā Bunayya 'Innī 'Ará Fī Al-Manāmi 'Annī 'Adhbaĥuka Fānžur Mādhā Tará Qāla Yā 'Abati Af`al Mā Tu'umaru Satajidunī 'In Shā'a Allāhu Mina Aş-Şābirīna 102. Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri. فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَابُنَيَّ إِنِّي أَرَى فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَى قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ سَتَجِدُنِي إِنْ شَاءَ اللَّهُ مِنَ الصَّابِرِينَ
Falammā 'Aslamā Wa Tallahu Liljabīni 103. Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji. فَلَمَّا أَسْلَمَا وَتَلَّه ُُ لِلْجَبِينِ
Wa Nādaynāhu 'An Yā 'Ibrāhīmu 104. Tulimwita: Ewe Ibrahim! وَنَادَيْنَاهُ~ُ أَنْ يَا إِبْرَاهِيمُ
Qad Şaddaqta Ar-Ru'uyā 'Innā Kadhālika Naj Al-Muĥsinīna 105. Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema. قَد صَدَّقْتَ الرُّؤْيَا إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ
'Inna Hādhā Lahuwa Al-Balā'u Al-Mubīnu 106. Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri. إِنَّ هَذَا لَهُوَ الْبَلاَءُ الْمُبِينُ
Wa Fadaynāhu Bidhibĥin `Ažīmin 107. Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu. وَفَدَيْنَاه ُُ بِذِبْحٍ عَظِيم ٍ
Wa Taraknā `Alayhi Fī Al-'Ākhirīna 108. Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye. وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الآخِرِينَ
Salāmun `Alá 'Ibrāhīma 109. Iwe salama kwa Ibrahim! سَلاَمٌ عَلَى إِبْرَاهِيمَ
Kadhālika Naj Al-Muĥsinīna 110. Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema. كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ
'Innahu Min `Ibādinā Al-Mu'uminīna 111. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. إِنَّه ُُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ
Wa Bashsharnāhu Bi'isĥāqa Nabīyāan Mina Aş-Şāliĥīna 112. Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema. وَبَشَّرْنَاه ُُ بِإِسْحَاقَ نَبِيّا ً مِنَ الصَّالِحِينَ
Wa Bāraknā `Alayhi Wa `Alá 'Isĥāqa Wa Min Dhurrīyatihimā Muĥsinun Wa Žālimun Linafsihi Mubīnun 113. Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi. وَبَارَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَى إِسْحَاقَ وَمِنْ ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِن ٌ وَظَالِم ٌ لِنَفْسِه ِِ مُبِين ٌ
Wa Laqad Manannā `Alá Mūsá Wa Hārūna 114. Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni. وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَى مُوسَى وَهَارُونَ
Wa Najjaynāhumā Wa Qawmahumā Mina Al-Karbi Al-`Ažīmi 115. Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa. وَنَجَّيْنَاهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ
Wa Naşarnāhum Fakānū Humu Al-Ghālibīna 116. Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda. وَنَصَرْنَاهُمْ فَكَانُوا هُمُ الْغَالِبِينَ
Wa 'Ātaynāhumā Al-Kitāba Al-Mustabīna 117. Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha. وَآتَيْنَاهُمَا الْكِتَابَ الْمُسْتَبِينَ
Wa Hadaynāhumā Aş-Şirāţa Al-Mustaqīma 118. Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. وَهَدَيْنَاهُمَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ
Wa Taraknā `Alayhimā Fī Al-'Ākhirīna 119. Na tukawaachia (sifa njema) katika watu walio kuja baadaye. وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِي الآخِرِينَ
Salāmun `Alá Mūsá Wa Hārūna 120. Iwe salama kwa Musa na Haruni! سَلاَمٌ عَلَى مُوسَى وَهَارُونَ
'Innā Kadhālika Naj Al-Muĥsinīna 121. Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema. إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ
'Innahumā Min `Ibādinā Al-Mu'uminīna 122. Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini. إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ
Wa 'Inna 'Ilyāsa Lamina Al-Mursalīna 123. Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume. وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ
'Idh Qāla Liqawmihi 'Alā Tattaqūna 124. Alipo waambia watu wake: Hamwogopi? إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ~ِ أَلاَ تَتَّقُونَ
'Atad`ūna Ba`lāan Wa Tadharūna 'Aĥsana Al-Khāliqīna 125. Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji, أَتَدْعُونَ بَعْلا ً وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ الْخَالِقِينَ
Allāha Rabbakum Wa Rabba 'Ābā'ikumu Al-'Awwalīna 126. Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani? اللَّهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ آبَائِكُمُ الأَوَّلِينَ
Fakadhdhabūhu Fa'innahum Lamuĥđarūna 127. Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa; فَكَذَّبُوه ُُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ
'Illā `Ibāda Allāhi Al-Mukhlaşīna 128. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa. إِلاَّ عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ
Wa Taraknā `Alayhi Fī Al-'Ākhirīna 129. Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye. وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الآخِرِينَ
Salāmun `Alá 'Il Yā -Sīn 130. Iwe salama kwa Ilyas. سَلاَمٌ عَلَى إِلْ يَا-سِين
'Innā Kadhālika Naj Al-Muĥsinīna 131. Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema. إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ
'Innahu Min `Ibādinā Al-Mu'uminīna 132. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini. إِنَّه ُُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ
Wa 'Inna Lūţāan Lamina Al-Mursalīna 133. Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume. وَإِنَّ لُوطا ً لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ
'Idh Najjaynāhu Wa 'Ahlahu 'Ajma`īna 134. Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote, إِذْ نَجَّيْنَاه ُُ وَأَهْلَهُ~ُ أَجْمَعِينَ
'Illā `Ajūzāan Al-Ghābirīna 135. Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma. إِلاَّ عَجُوزا ً فِي الْغَابِرِينَ
Thumma Dammarnā Al-'Ākharīna 136. Kisha tukawaangamiza wale wengineo. ثُمَّ دَمَّرْنَا الآخَرِينَ
Wa 'Innakum Latamurrūna `Alayhim Muşbiĥīna 137. Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi, وَإِنَّكُمْ لَتَمُرّ