36) Sūrat Yā -Sīn

Printed format

36) سُورَة يَا-سِين

Yā -Sīn 1. Ya-Sin (Y.S.). يَا-سِين
Wa Al-Qur'āni Al-Ĥakīmi 2. Kwa Haki ya Qur'ani yenye hikima! وَالْقُرْآنِ الْحَكِيمِ
'Innaka Lamina Al-Mursalīna 3. Hakika wewe ni miongoni mwa walio tumwa, إِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ
`Alá Şirāţin Mustaqīmin 4. Juu ya Njia Iliyo Nyooka. عَلَى صِرَاط ٍ مُسْتَقِيم ٍ
Tanzīla Al-`Azīzi Ar-Raĥīmi 5. Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. تَنزِيلَ الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ
Litundhira Qawmāan Mā 'Undhira 'Ābā'uuhum Fahum Ghāfilūna 6. Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basi wao wamekuwa wenye kughafilika. لِتُنذِرَ قَوْما ً مَا أُنذِرَ آبَاؤُهُمْ فَهُمْ غَافِلُونَ
Laqad Ĥaqqa Al-Qawlu `Alá 'Aktharihim Fahum Lā Yu'uminūna 7. Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini. لَقَدْ حَقَّ الْقَوْلُ عَلَى أَكْثَرِهِمْ فَهُمْ لاَ يُؤْمِنُونَ
'Innā Ja`alnā Fī 'A`nāqihim 'Aghlālāan Fahiya 'Ilá Al-'Adhqāni Fahum Muqmaĥūna 8. Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu. إِنَّا جَعَلْنَا فِي أَعْنَاقِهِمْ أَغْلاَلا ً فَهِيَ إِلَى الأَذْقَانِ فَهُمْ مُقْمَحُونَ
Wa Ja`alnā Min Bayni 'Aydīhim Saddāan Wa Min Khalfihim Saddāan Fa'aghshaynāhum Fahum Lā Yubşirūna 9. Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni. وَجَعَلْنَا مِنْ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدّا ً وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدّا ً فَأَغْشَيْنَاهُمْ فَهُمْ لاَ يُبْصِرُونَ
Wa Sawā'un `Alayhim 'A'andhartahum 'Am Lam Tundhirhum Lā Yu'uminūna 10. Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini. وَسَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لاَ يُؤْمِنُونَ
'Innamā Tundhiru Mani Attaba`a Adh-Dhikra Wa Khashiya Ar-Raĥmana Bil-Ghaybi Fabashshirhu Bimaghfiratin Wa 'Ajrin Karīmin 11. Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman, Mwingi wa Rehema, kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema. إِنَّمَا تُنذِرُ مَنِ اتَّبَعَ الذِّكْرَ وَخَشِيَ الرَّحْمَنَ بِالْغَيْبِ فَبَشِّرْهُ بِمَغْفِرَة ٍ وَأَجْر ٍ كَرِيم ٍ
'Innā Naĥnu Nuĥyi Al-Mawtá Wa Naktubu Mā Qaddamū Wa 'Āthārahum Wa Kulla Shay'in 'Ĥşaynāhu Fī 'Imāmin Mubīnin 12. Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha. إِنَّا نَحْنُ نُحْيِ الْمَوْتَى وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ وَكُلَّ شَيْءٍ أحْصَيْنَاه ُُ فِي إِمَام ٍ مُبِين ٍ
Wa Ađrib Lahum Mathalāan 'Aşĥāba Al-Qaryati 'Idh Jā'ahā Al-Mursalūna 13. Na wapigie mfano wa wakaazi wa mji walipo wafikia walio tumwa. وَاضْرِبْ لَهُمْ مَثَلاً أَصْحَابَ الْقَرْيَةِ إِذْ جَاءَهَا الْمُرْسَلُونَ
'Idh 'Arsalnā 'Ilayhimu Athnayni Fakadhdhabūhumā Fa`azzaznā Bithālithin Faqālū 'Innā 'Ilaykum Mursalūna 14. Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu. إِذْ أَرْسَلْنَا إِلَيْهِمُ اثْنَيْنِ فَكَذَّبُوهُمَا فَعَزَّزْنَا بِثَالِث ٍ فَقَالُوا إِنَّا إِلَيْكُمْ مُرْسَلُونَ
Qālū Mā 'Antum 'Illā Basharun Mithlunā Wa Mā 'Anzala Ar-Raĥmānu Min Shay'in 'In 'Antum 'Illā Takdhibūna 15. Wakasema: Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uwongo tu. قَالُوا مَا أَنْتُمْ إِلاَّ بَشَر ٌ مِثْلُنَا وَمَا أَنزَلَ الرَّحْمَنُ مِنْ شَيْء ٍ إِنْ أَنْتُمْ إِلاَّ تَكْذِبُونَ
Qālū Rabbunā Ya`lamu 'Innā 'Ilaykum Lamursalūna 16. Wakasema: Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu. قَالُوا رَبُّنَا يَعْلَمُ إِنَّا إِلَيْكُمْ لَمُرْسَلُونَ
Wa Mā `Alaynā 'Illā Al-Balāghu Al-Mubīnu 17. Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi. وَمَا عَلَيْنَا إِلاَّ الْبَلاَغُ الْمُبِينُ
Qālū 'Innā Taţayyarnā Bikum La'in Lam Tantahū Lanarjumannakum Wa Layamassannakum Minnā `Adhābun 'Alīmun 18. Wakasema: Sisi tumeagua kuwa nyinyi ni wakorofi. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu. قَالُوا إِنَّا تَطَيَّرْنَا بِكُمْ لَئِنْ لَمْ تَنتَهُوا لَنَرْجُمَنَّكُمْ وَلَيَمَسَّنَّكُمْ مِنَّا عَذَابٌ أَلِيم ٌ
Qālū Ţā'irukum Ma`akum 'A'in Dhukkirtum Bal 'Antum Qawmun Musrifūna 19. Wakasema: Ukorofi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu walio pindukia mipaka. قَالُوا طَائِرُكُمْ مَعَكُمْ أَئِنْ ذُكِّرْتُمْ بَلْ أَنْتُمْ قَوْم ٌ مُسْرِفُونَ
Wa Jā'a Min 'Aqşá Al-Madīnati Rajulun Yas`á Qāla Yā Qawmi Attabi`ū Al-Mursalīna 20. Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini, akasema: Enyi watu wangu! Wafuateni hawa walio tumwa. وَجَاءَ مِنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ رَجُل ٌ يَسْعَى قَالَ يَاقَوْمِ اتَّبِعُوا الْمُرْسَلِينَ
Attabi`ū Man Lā Yas'alukum 'Ajrāan Wa Hum Muhtadūna 21. Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka. اتَّبِعُوا مَنْ لاَ يَسْأَلُكُمْ أَجْرا ً وَهُمْ مُهْتَدُونَ
Wa Mā Liya Lā 'A`budu Al-Ladhī Faţaranī Wa 'Ilayhi Turja`ūna 22. NA KWA NINI nisimuabudu yule aliye niumba na kwake mtarejeshwa? وَمَا لِيَ لاَ أَعْبُدُ الَّذِي فَطَرَنِي وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
'A'attakhidhu Min Dūnihi 'Ālihatan 'In Yuridni Ar-Raĥmānu Biđurrin Lā Tughni `Annī Shafā`atuhum Shay'āan Wa Lā Yunqidhūni 23. Je! Niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani, Mwingi wa Rehema, akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa. أَأَتَّخِذُ مِنْ دُونِهِ آلِهَة ً إِنْ يُرِدْنِ الرَّحْمَنُ بِضُرّ ٍ لاَ تُغْنِ عَنِّي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئا ً وَلاَ يُنقِذُونِ
'Innī 'Idhāan Lafī Đalālin Mubīnin 24. Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotovu ulio dhaahiri. إِنِّي إِذا ً لَفِي ضَلاَل ٍ مُبِين ٍ
'Innī 'Āmantu Birabbikum Fāsma`ūni 25. Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni! إِنِّي آمَنْتُ بِرَبِّكُمْ فَاسْمَعُونِ
Qīla Adkhuli Al-Jannata Qāla Yā Layta Qawmī Ya`lamūna 26. Akaambiwa: Ingia Peponi! Akasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua قِيلَ ادْخُلِ الْجَنَّةَ قَالَ يَالَيْتَ قَوْمِي يَعْلَمُونَ
Bimā Ghafara Lī Rabbī Wa Ja`alanī Mina Al-Mukramīna 27. Jinsi Mola wangu Mlezi alivyo nisamehe, na akanifanya miongoni mwa walio hishimiwa. بِمَا غَفَرَ لِي رَبِّي وَجَعَلَنِي مِنَ الْمُكْرَمِينَ
Wa Mā 'Anzalnā `Alá Qawmihi Min Ba`dihi Min Jundin Mina As-Samā'i Wa Mā Kunnā Munzilīna 28. Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha. وَمَا أَنزَلْنَا عَلَى قَوْمِه ِِ مِنْ بَعْدِه ِِ مِنْ جُند ٍ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا كُنَّا مُنزِلِينَ
'In Kānat 'Illā Şayĥatan Wāĥidatan Fa'idhā Hum Khāmidūna 29. Hakukuwa ila ukelele mmoja tu; na mara walizimwa! إِنْ كَانَتْ إِلاَّ صَيْحَة ً وَاحِدَة ً فَإِذَا هُمْ خَامِدُونَ
Yā Ĥasratan `Alá Al-`Ibādi Mā Ya'tīhim Min Rasūlin 'Illā Kānū Bihi Yastahzi'ūn 30. Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli. يَاحَسْرَةً عَلَى الْعِبَادِ مَا يَأْتِيهِمْ مِنْ رَسُول ٍ إِلاَّ كَانُوا بِه ِِ يَسْتَهْزِئُون
'Alam Yaraw Kam 'Ahlaknā Qablahum Mina Al-Qurūni 'Annahum 'Ilayhim Lā Yarji`ūna 31. Je! Hawaoni umma ngapi tulizo ziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao. أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُمْ مِنَ الْقُرُونِ أَنَّهُمْ إِلَيْهِمْ لاَ يَرْجِعُونَ
Wa 'In Kullun Lammā Jamī`un Ladaynā Muĥđarūna 32. Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu. وَإِنْ كُلّ ٌ لَمَّا جَمِيع ٌ لَدَيْنَا مُحْضَرُونَ
Wa 'Āyatun Lahumu Al-'Arđu Al-Maytatu 'Aĥyaynāhā Wa 'Akhrajnā Minhā Ĥabbāan Faminhu Ya'kulūna 33. Na Ishara hiyo kwao - ardhi iliyo kufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanazila! وَآيَة ٌ لَهُمُ الأَرْضُ الْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَاهَا وَأَخْرَجْنَا مِنْهَا حَبّا ً فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ
Wa Ja`alnā Fīhā Jannātin Min Nakhīlin Wa 'A`nābin Wa Fajjarnā Fīhā Mina Al-`Uyūni 34. Na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemchem ndani yake, وَجَعَلْنَا فِيهَا جَنَّات ٍ مِنْ نَخِيل ٍ وَأَعْنَاب ٍ وَفَجَّرْنَا فِيهَا مِنَ الْعُيُونِ
Liya'kulū Min Thamarihi Wa Mā `Amilat/hu 'Aydīhim 'Afalā Yashkurūna 35. Ili wale matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru? لِيَأْكُلُوا مِنْ ثَمَرِه ِِ وَمَا عَمِلَتْهُ أَيْدِيهِمْ أَفَلاَ يَشْكُرُونَ
Subĥāna Al-Ladhī Khalaqa Al-'Azwāja Kullahā Mimmā Tunbitu Al-'Arđu Wa Min 'Anfusihim Wa Mimmā Lā Ya`lamūna 36. Subhana, Ametakasika, aliye umba dume na jike vyote katika vinavyo mea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyo vijua. سُبْحَانَ الَّذِي خَلَقَ الأَزْوَاجَ كُلَّهَا مِمَّا تُنْبِتُ الأَرْضُ وَمِنْ أَنفُسِهِمْ وَمِمَّا لاَ يَعْلَمُونَ
Wa 'Āyatun Lahumu Al-Laylu Naslakhu Minhu An-Nahāra Fa'idhā Hum Mužlimūna 37. Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani. وَآيَة ٌ لَهُمُ اللَّيْلُ نَسْلَخُ مِنْهُ النَّهَارَ فَإِذَا هُمْ مُظْلِمُونَ
Wa Ash-Shamsu Tajrī Limustaqarrin Lahā Dhālika Taqdīru Al-`Azīzi Al-`Alīmi 38. Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua. وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرّ ٍ لَهَا ذَلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ
Wa Al-Qamara Qaddarnāhu Manāzila Ĥattá `Āda Kāl`urjūni Al-Qadīmi 39. Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe. وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاه ُُ مَنَازِلَ حَتَّى عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ
Ash-Shamsu Yanbaghī Lahā 'An Tudrika Al-Qamara Wa Lā Al-Laylu Sābiqu An-Nahāri Wa Kullun Fī Falakin Yasbaĥūna 40. Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao. لاَ الشَّمْسُ يَنْبَغِي لَهَا أَنْ تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَلاَ اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ وَكُلّ ٌ فِي فَلَك ٍ يَسْبَحُونَ
Wa 'Āyatun Lahum 'Annā Ĥamalnā Dhurrīyatahum Al-Fulki Al-Mashĥūni 41. Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuriya zao katika jahazi ilio sheheni. وَآيَة ٌ لَهُمْ أَنَّا حَمَلْنَا ذُرِّيَّتَهُمْ فِي الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ
Wa Khalaqnā Lahum Min Mithlihi Mā Yarkabūna 42. Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyo vipanda. وَخَلَقْنَا لَهُمْ مِنْ مِثْلِه ِِ مَا يَرْكَبُونَ
Wa 'In Nasha' Nughriqhum Falā Şarīkha Lahum Wa Lā Hum Yunqadhūna 43. Na tukitaka tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi, وَإِنْ نَشَأْ نُغْرِقْهُمْ فَلاَ صَرِيخَ لَهُمْ وَلاَ هُمْ يُنقَذُونَ
'Illā Raĥmatan Minnā Wa Matā`āan 'Ilá Ĥīnin 44. Isipo kuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda. إِلاَّ رَحْمَة ً مِنَّا وَمَتَاعا ً إِلَى حِين ٍ
Wa 'Idhā Qīla Lahumu Attaqū Mā Bayna 'Aydīkum Wa Mā Khalfakum La`allakum Turĥamūna 45. Na wanapo ambiwa: Jilindeni na yalioko mbele yenu na yalioko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa... وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّقُوا مَا بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَمَا خَلْفَكُمْ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
Wa Mā Ta'tīhim Min 'Āyatin Min 'Āyāti Rabbihim 'Illā Kānū `Anhā Mu`rīna 46. Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi ila wao huwa ni wenye kuipuuza. وَمَا تَأْتِيهِمْ مِنْ آيَة ٍ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِمْ إِلاَّ كَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ
Wa 'Idhā Qīla Lahum 'Anfiqū Mimmā Razaqakumu Allāhu Qāla Al-Ladhīna Kafarū Lilladhīna 'Āmanū 'Anuţ`imu Man Law Yashā'u Allāhu 'Aţ`amahu 'In 'Antum 'Illā Fī Đalālin Mubīnin 47. Na wanapo ambiwa: Toeni katika aliyo kupeni Mwenyezi Mungu, walio kufuru huwaambia walio amini: Je! Tuwalishe ambao Mwenyezi Mungu angependa angeli walisha mwenyewe? Nyinyi hammo ila katika upotofu ulio dhaahiri. وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ أَنفِقُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّهُ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنُطْعِمُ مَنْ لَوْ يَشَاءُ اللَّهُ أَطْعَمَهُ~ُ إِنْ أَنْتُمْ إِلاَّ فِي ضَلاَل ٍ مُبِين ٍ
Wa Yaqūlūna Matá Hādhā Al-Wa`du 'In Kuntum Şādiqīna 48. Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli? وَيَقُولُونَ مَتَى هَذَا الْوَعْدُ إِنْ كُنتُمْ صَادِقِينَ
Mā Yanžurūna 'Illā Şayĥatan Wāĥidatan Ta'khudhuhum Wa Hum Yakhişşimūna 49. Hawangojei ila ukelele mmoja tu utakao wachukua nao wamo kuzozana. مَا يَنظُرُونَ إِلاَّ صَيْحَة ً وَاحِدَة ً تَأْخُذُهُمْ وَهُمْ يَخِصِّمُونَ
Falā Yastaţī`ūna Tawşiyatan Wa Lā 'Ilá 'Ahlihim Yarji`ūna 50. Basi hawataweza kuusia, wala kwa watu wao hawarejei. فَلاَ يَسْتَطِيعُونَ تَوْصِيَة ً وَلاَ إِلَى أَهْلِهِمْ يَرْجِعُونَ
Wa Nufikha Fī Aş-Şūri Fa'idhā Hum Mina Al-'Ajthi 'Ilá Rabbihim Yansilūna 51. Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi. وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَإِذَا هُمْ مِنَ الأَجْدَاثِ إِلَى رَبِّهِمْ يَنسِلُونَ
Qālū Yā Waylanā Man Ba`athanā Min Marqadinā Hādhā Mā Wa`ada Ar-Raĥmānu Wa Şadaqa Al-Mursalūna 52. Watasema: Ole wetu! Nani aliye tufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyo yaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume. قَالُوا يَاوَيْلَنَا مَنْ بَعَثَنَا مِنْ مَرْقَدِنَا هَذَا مَا وَعَدَ الرَّحْمَنُ وَصَدَقَ الْمُرْسَلُونَ
'In Kānat 'Illā Şayĥatan Wāĥidatan Fa'idhā Hum Jamī`un Ladaynā Muĥđarūna 53. Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watahudhuruishwa mbele yetu. إِنْ كَانَتْ إِلاَّ صَيْحَة ً وَاحِدَة ً فَإِذَا هُمْ جَمِيع ٌ لَدَيْنَا مُحْضَرُونَ
Fālyawma Lā Tužlamu Nafsun Shay'āan Wa Lā Tujzawna 'Illā Mā Kuntum Ta`malūna 54. Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa ila yale mliyo kuwa mkiyatenda. فَالْيَوْمَ لاَ تُظْلَمُ نَفْس ٌ شَيْئا ً وَلاَ تُجْزَوْنَ إِلاَّ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
'Inna 'Aşĥāba Al-Jannati Al-Yawma Fī Shughulin Fākihūna 55. Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi. إِنَّ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ الْيَوْمَ فِي شُغُل ٍ فَاكِهُونَ
Hum Wa 'Azwājuhum Fī Žilālin `Alá Al-'Arā'iki Muttaki'ūna 56. Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya fakhari. هُمْ وَأَزْوَاجُهُمْ فِي ظِلاَلٍ عَلَى الأَرَائِكِ مُتَّكِئُونَ
Lahum Fīhā Fākihatun Wa Lahum Mā Yadda`ūna 57. Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakacho kitaka. لَهُمْ فِيهَا فَاكِهَة ٌ وَلَهُمْ مَا يَدَّعُونَ
Salāmun Qawlāan Min Rabbin Raĥīmin 58. "Salama!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu. سَلاَم ٌ قَوْلا ً مِنْ رَبّ ٍ رَحِيم ٍ
Wa Amtāzū Al-Yawma 'Ayyuhā Al-Mujrimūna 59. Na enyi wakosefu! Jitengeni leo! وَامْتَازُوا الْيَوْمَ أَيُّهَا الْمُجْرِمُونَ
'Alam 'A`had 'Ilaykum Yā Banī 'Ādama 'An Lā Ta`budū Ash-Shayţāna 'Innahu Lakum `Adūwun Mubīnun 60. Je! Sikuagana nanyi, enyi wanaadamu, kuwa msimuabudu Shet'ani? Hakika yeye ni adui dhaahiri kwenu. أَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَابَنِي آدَمَ أَنْ لاَ تَعْبُدُوا الشَّيْطَانَ إِنَّه ُُ لَكُمْ عَدُوّ ٌ مُبِين ٌ
Wa 'Ani A`budūnī Hādhā Şirāţun Mustaqīmun 61. Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka. وَأَنِ اعْبُدُونِي هَذَا صِرَاط ٌ مُسْتَقِيم ٌ
Wa Laqad 'Ađalla Minkum Jibillāan Kathīrāan 'Afalam Takūnū Ta`qilūna 62. Na bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri? وَلَقَدْ أَضَلَّ مِنْكُمْ جِبِلّا ً كَثِيراً أَفَلَمْ تَكُونُوا تَعْقِلُونَ
Hadhihi Jahannamu Allatī Kuntum Tū`adūna 63. Hii basi ndiyo Jahannamu mliyo kuwa mkiahidiwa. هَذِه ِِ جَهَنَّمُ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ
Aşlawhā Al-Yawma Bimā Kuntum Takfurūna 64. Ingieni leo kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru. اصْلَوْهَا الْيَوْمَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ
Al-Yawma Nakhtimu `Alá 'Afwāhihim Wa Tukallimunā 'Aydīhim Wa Tash/hadu 'Arjuluhum Bimā Kānū Yaksibūna 65. Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyo kuwa wakiyachuma. الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ
Wa Law Nashā'u Laţamasnā `Alá 'A`yunihim Fāstabaqū Aş-Şirāţa Fa'anná Yubşirūna 66. Na tungeli penda tungeli yafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wange ionaje? وَلَوْ نَشَاءُ لَطَمَسْنَا عَلَى أَعْيُنِهِمْ فَاسْتَبَقُوا الصِّرَاطَ فَأَنَّى يُبْصِرُونَ
Wa Law Nashā'u Lamasakhnāhum `Alá Makānatihim Famā Astaţā`ū Muđīyāan Wa Lā Yarji`ūna 67. Na tungeli taka tunge wageuza sura hapo hapo walipo, basi wasinge weza kwenda wala kurudi. وَلَوْ نَشَاءُ لَمَسَخْنَاهُمْ عَلَى مَكَانَتِهِمْ فَمَا اسْتَطَاعُوا مُضِيّا ً وَلاَ يَرْجِعُونَ
Wa Man Nu`ammirhu Nunakkis/hu Fī Al-Khalqi 'Afalā Ya`qilūna 68. Na tunaye mzeesha tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je! hawazingatii? وَمَنْ نُعَمِّرْهُ نُنَكِّسْهُ فِي الْخَلْقِ أَفَلاَ يَعْقِلُونَ
Wa Mā `Allamnāhu Ash-Shi`ra Wa Mā Yanbaghī Lahu 'In Huwa 'Illā Dhikrun Wa Qur'ānun Mubīnun 69. Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur'ani inayo bainisha. وَمَا عَلَّمْنَاهُ الشِّعْرَ وَمَا يَنْبَغِي لَهُ~ُ إِنْ هُوَ إِلاَّ ذِكْر ٌ وَقُرْآن ٌ مُبِين ٌ
Liyundhira Man Kāna Ĥayyāan Wa Yaĥiqqa Al-Qawlu `Alá Al-Kāfirīna 70. Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri. لِيُنْذِرَ مَنْ كَانَ حَيّا ً وَيَحِقَّ الْقَوْلُ عَلَى الْكَافِرِينَ
'Awalam Yaraw 'Annā Khalaqnā Lahum Mimmā `Amilat 'Aydīnā 'An`āmāan Fahum Lahā Mālikūna 71. Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyo fanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki. أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا خَلَقْنَا لَهُمْ مِمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَا أَنْعَاما ً فَهُمْ لَهَا مَالِكُونَ
Wa Dhallalnāhā Lahum Faminhā Rakūbuhum Wa Minhā Ya'kulūna 72. Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanao wapanda, na baadhi yao wanawala. وَذَلَّلْنَاهَا لَهُمْ فَمِنْهَا رَكُوبُهُمْ وَمِنْهَا يَأْكُلُونَ
Wa Lahum Fīhā Manāfi`u Wa Mashāribu 'Afalā Yashkurūna 73. Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru? وَلَهُمْ فِيهَا مَنَافِعُ وَمَشَارِبُ أَفَلاَ يَشْكُرُونَ
Wa Attakhadhū Min Dūni Allāhi 'Ālihatan La`allahum Yunşarūna 74. Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati wapate kusaidiwa! وَاتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ آلِهَة ً لَعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ
Lā Yastaţī`ūna Naşrahum Wa Hum Lahum Jundun Muĥđarūna 75. Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio watakuwa askari wao watakao hudhurishwa. لاَ يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَهُمْ وَهُمْ لَهُمْ جُند ٌ مُحْضَرُونَ
Falā Yaĥzunka Qawluhum 'Innā Na`lamu Mā Yusirrūna Wa Mā Yu`linūna 76. Basi maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisi tunayajua wanayo yaweka siri na wanayo yatangaza. فَلاَ يَحْزُنْكَ قَوْلُهُمْ إِنَّا نَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ
'Awalam Yara Al-'Insānu 'Annā Khalaqnāhu Min Nuţfatin Fa'idhā Huwa Khīmun Mubīnun 77. Kwani mwanaadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndio amekuwa ndiye mgomvi wa dhaahiri! أَوَلَمْ يَرَ الإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاه ُُ مِنْ نُطْفَة ٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيم ٌ مُبِين ٌ
Wa Đaraba Lanā Mathalāan Wa Nasiya Khalqahu Qāla Man Yuĥyī Al-`Ižāma Wa Hiya Ramīmun 78. Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika? وَضَرَبَ لَنَا مَثَلا ً وَنَسِيَ خَلْقَه ُُ قَالَ مَنْ يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيم ٌ
Qul Yuĥyīhā Al-Ladhī 'Ansha'ahā 'Awwala Marratin Wa Huwa Bikulli Khalqin `Alīmun 79. Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba. قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّة ٍ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيم ٌ
Al-Ladhī Ja`ala Lakum Mina Ash-Shajari Al-'Akhđari Nārāan Fa'idhā 'Antum Minhu Tūqidūna 80. Aliye kujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha. الَّذِي جَعَلَ لَكُمْ مِنَ الشَّجَرِ الأَخْضَرِ نَارا ً فَإِذَا أَنْتُمْ مِنْهُ تُوقِدُونَ
'Awalaysa Al-Ladhī Khalaqa As-Samāwāti Wa Al-'Arđa Biqādirin `Alá 'An Yakhluqa Mithlahum Balá Wa Huwa Al-Khallāqu Al-`Alīmu 81. Kwani aliye ziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi. أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَى أَنْ يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ بَلَى وَهُوَ الْخَلاَّقُ الْعَلِيمُ
'Innamā 'Amruhu 'Idhā 'Arāda Shay'āan 'An Yaqūla Lahu Kun Fayakūnu 82. Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa. إِنَّمَا أَمْرُهُ~ُ إِذَا أَرَادَ شَيْئاً أَنْ يَقُولَ لَه ُُ كُنْ فَيَكُونُ
Fasubĥāna Al-Ladhī Biyadihi Malakūtu Kulli Shay'in Wa 'Ilayhi Turja`ūna 83. Basi Ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa. *   فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِه ِِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْء ٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
Next Sūrah