15) Sūrat Al-Ĥijr

Printed format

15) سُورَة الحِجر

'Alif-Lām-Rā Tilka 'Āyātu Al-Kitābi Wa Qur'ānin Mubīnin 1. Alif Lam Ra. (A.L.R). Hizi ni Aya za Kitabu na Qur'ani inayo bainisha. أَلِف-لَام-رَا تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ وَقُرْآن ٍ مُبِين ٍ
Rubamā Yawaddu Al-Ladhīna Kafarū Law Kānū Muslimīna 2. HUENDA ikawa walio kufuru wakatamani wange kuwa Waislamu. رُبَمَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ كَانُوا مُسْلِمِينَ
Dharhum Ya'kulū Wa Yatamatta`ū Wa Yulhihimu Al-'Amalu Fasawfa Ya`lamūna 3. Waache wale, na wastarehe, na iwazuge tamaa. Watakuja jua. ذَرْهُمْ يَأْكُلُوا وَيَتَمَتَّعُوا وَيُلْهِهِمُ الأَمَلُ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
Wa Mā 'Ahlaknā Min Qaryatin 'Illā Wa Lahā Kitābun Ma`lūmun 4. Na hatukuuangamiza mji wowote ule ila ulikuwa na muda wake maalumu. وَمَا أَهْلَكْنَا مِنْ قَرْيَة ٍ إِلاَّ وَلَهَا كِتَاب ٌ مَعْلُوم ٌ
Mā Tasbiqu Min 'Ummatin 'Ajalahā Wa Mā Yasta'khirūna 5. Hawawezi watu wowote kuitangulia ajali yao, wala kuchelewa. مَا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ
Wa Qālū Yā 'Ayyuhā Al-Ladhī Nuzzila `Alayhi Adh-Dhikru 'Innaka Lamajnūnun 6. Na walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu. وَقَالُوا يَا أَيُّهَا الَّذِي نُزِّلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُون ٌ
Law Mā Ta'tīnā Bil-Malā'ikati 'In Kunta Mina Aş-Şādiqīna 7. Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli? لَوْ مَا تَأْتِينَا بِالْمَلاَئِكَةِ إِنْ كُنْتَ مِنَ الصَّادِقِينَ
Mā Nunazzilu Al-Malā'ikata 'Illā Bil-Ĥaqqi Wa Mā Kānū 'Idhāan Munžarīna 8. Sisi hatuwateremshi Malaika ila kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula. مَا نُنَزِّلُ الْمَلاَئِكَةَ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَمَا كَانُوا إِذا ً مُنْظَرِينَ
'Innā Naĥnu Nazzalnā Adh-Dhikra Wa 'Innā Lahu Laĥāfižūna 9. Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda. إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَه ُُ لَحَافِظُونَ
Wa Laqad 'Arsalnā Min Qablika Fī Shiya`i Al-'Awwalīna 10. Na hakika tulikwisha watumia Mitume mataifa ya mwanzo. وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِنْ قَبْلِكَ فِي شِيَعِ الأَوَّلِينَ
Wa Mā Ya'tīhim Min Rasūlin 'Illā Kānū Bihi Yastahzi'ūna 11. Na hakuwafikia Mtume ila walimkejeli. وَمَا يَأْتِيهِمْ مِنْ رَسُول ٍ إِلاَّ كَانُوا بِه ِِ يَسْتَهْزِئُونَ
Kadhālika Naslukuhu Fī Qulūbi Al-Mujrimīna 12. Na kama hivi ndivyo tunavyo ingiza katika nyoyo za wakosefu. كَذَلِكَ نَسْلُكُه ُُ فِي قُلُوبِ الْمُجْرِمِينَ
Lā Yu'uminūna Bihi Wa Qad Khalat Sunnatu Al-'Awwalīna 13. Hawayaamini haya, na hali ya kuwa umekwisha wapitia mfano wa watu wa kale. لاَ يُؤْمِنُونَ بِه ِِ وَقَدْ خَلَتْ سُنَّةُ الأَوَّلِينَ
Wa Law Fataĥnā `Alayhim Bābāan Mina As-Samā'i Fažallū Fīhi Ya`rujūna 14. Na lau tungeli wafungulia mlango wa mbingu, wakawa wanapanda, وَلَوْ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَابا ً مِنَ السَّمَاءِ فَظَلُّوا فِيه ِِ يَعْرُجُونَ
Laqālū 'Innamā Sukkirat 'Abşārunā Bal Naĥnu Qawmun Masĥūrūna 15. Basi wangeli sema: Macho yetu yamelevywa, bali sisi wenyewe tumerogwa. لَقَالُوا إِنَّمَا سُكِّرَتْ أَبْصَارُنَا بَلْ نَحْنُ قَوْم ٌ مَسْحُورُونَ
Wa Laqad Ja`alnā Fī As-Samā'i Burūjāan Wa Zayyannāhā Lilnnāžirīna 16. Na hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye kuangalia. وَلَقَدْ جَعَلْنَا فِي السَّمَاءِ بُرُوجا ً وَزَيَّنَّاهَا لِلنَّاظِرِينَ
Wa Ĥafižnāhā Min Kulli Shayţānin Rajīmin 17. Na tumezilinda na kila shetani afukuzwaye. وَحَفِظْنَاهَا مِنْ كُلِّ شَيْطَان ٍ رَجِيم ٍ
'Illā Mani Astaraqa As-Sam`a Fa'atba`ahu Shihābun Mubīnun 18. Isipo kuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa na kijinga cha moto kinacho onekana. إِلاَّ مَنِ اسْتَرَقَ السَّمْعَ فَأَتْبَعَه ُُ شِهَاب ٌ مُبِين ٌ
Wa Al-'Arđa Madadnāhā Wa 'Alqaynā Fīhā Rawāsiya Wa 'Anbatnā Fīhā Min Kulli Shay'in Mawzūnin 19. Na ardhi tumeitandaza na humo tumeweka milima, na tumeotesha kila kitu kwa kiasi chake. وَالأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْبَتْنَا فِيهَا مِنْ كُلِّ شَيْء ٍ مَوْزُون ٍ
Wa Ja`alnā Lakum Fīhā Ma`āyisha Wa Man Lastum Lahu Birāziqīna 20. Na tumekujaalieni humo vitu vya maisha yenu, na ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku. وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ وَمَنْ لَسْتُمْ لَه ُُ بِرَازِقِينَ
Wa 'In Min Shay'in 'Illā `Indanā Khazā'inuhu Wa Mā Nunazziluhu 'Illā Biqadarin Ma`lūmin 21. Na hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi ila kwa kipimo maalumu. وَإِنْ مِنْ شَيْء ٍ إِلاَّ عِنْدَنَا خَزَائِنُه ُُ وَمَا نُنَزِّلُهُ~ُ إِلاَّ بِقَدَر ٍ مَعْلُوم ٍ
Wa 'Arsalnā Ar-Riyāĥa Lawāqiĥa Fa'anzalnā Mina As-Samā'i Mā'an Fa'asqaynākumūhu Wa Mā 'Antum Lahu Bikhāzinīna 22. Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayo yaweka. وَأَرْسَلْنَا الرِّيَاحَ لَوَاقِحَ فَأَنْزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاء ً فَأَسْقَيْنَاكُمُوه ُُ وَمَا أَنْتُمْ لَه ُُ بِخَازِنِينَ
Wa 'Innā Lanaĥnu Nuĥyī Wa Numītu Wa Naĥnu Al-Wārithūna 23. Na Sisi ndio tunao huisha na tunao fisha. Na Sisi ndio Warithi. وَإِنَّا لَنَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَنَحْنُ الْوَارِثُونَ
Wa Laqad `Alim Al-Mustaqdimīna Minkum Wa Laqad `Alim Al-Musta'khirīna 24. Na tunawajua walio tangulia katika nyinyi, na tunawajua walio taakhari. وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنْكُمْ وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَأْخِرِينَ
Wa 'Inna Rabbaka Huwa Yaĥshuruhum 'Innahu Ĥakīmun `Alīmun 25. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye atakaye wakusanya. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mjuzi. وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحْشُرُهُمْ إِنَّه ُُ حَكِيمٌ عَلِيم ٌ
Wa Laqad Khalaq Al-'Insāna Min Şalşālin Min Ĥama'iin Masnūnin 26. Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. وَلَقَدْ خَلَقْنَا الإِنسَانَ مِنْ صَلْصَال ٍ مِنْ حَمَإ ٍ مَسْنُون ٍ
Wa Al-Jānna Khalaqnāhu Min Qablu Min Nāri As-Samūmi 27. Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto. وَالْجَانَّ خَلَقْنَاه ُُ مِنْ قَبْلُ مِنْ نَارِ السَّمُومِ
Wa 'Idh Qāla Rabbuka Lilmalā'ikati 'Innī Khāliqun Basharāan Min Şalşālin Min Ĥama'iin Masnūnin 28. Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلاَئِكَةِ إِنِّي خَالِق ٌ بَشَرا ً مِنْ صَلْصَال ٍ مِنْ حَمَإ ٍ مَسْنُون ٍ
Fa'idhā Sawwaytuhu Wa Nafakhtu Fīhi Min Rūĥī Faqa`ū Lahu Sājidīna 29. Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia. فَإِذَا سَوَّيْتُه ُُ وَنَفَخْتُ فِيه ِِ مِنْ رُوحِي فَقَعُوا لَه ُُ سَاجِدِينَ
Fasajada Al-Malā'ikatu Kulluhum 'Ajma`ūna 30. Basi Malaika wote pamoja walimsujudia, فَسَجَدَ الْمَلاَئِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ
'Illā 'Iblīsa 'Abá 'An Yakūna Ma`a As-Sājidīna 31. Isipo kuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na walio sujudu. إِلاَّ إِبْلِيسَ أَبَى أَنْ يَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ
Qāla Yā 'Iblīsu Mā Laka 'Allā Takūna Ma`a As-Sājidīna 32. (Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na walio sujudu? قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا لَكَ أَلاَّ تَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ
Qāla Lam 'Akun Li'sjuda Libasharin Khalaqtahu Min Şalşālin Min Ĥama'iin Masnūnin 33. Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yenye sura. قَالَ لَمْ أَكُنْ لِأسْجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقْتَه ُُ مِنْ صَلْصَال ٍ مِنْ حَمَإ ٍ مَسْنُون ٍ
Qāla Fākhruj Minhā Fa'innaka Rajīmun 34.(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni! قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيم ٌ
Wa 'Inna `Alayka Al-La`nata 'Ilá Yawmi Ad-Dīni 35. Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo. وَإِنَّ عَلَيْكَ اللَّعْنَةَ إِلَى يَوْمِ الدِّينِ
Qāla Rabbi Fa'anžirnī 'Ilá Yawmi Yub`athūna 36. Akasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watapo fufuliwa. قَالَ رَبِّ فَأَنْظِرْنِي إِلَى يَوْمِ يُبْعَثُونَ
Qāla Fa'innaka Mina Al-Munžarīna 37. (Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika walio pewa muhula قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ الْمُنْظَرِينَ
'Ilá Yawmi Al-Waqti Al-Ma`lūmi 38. Mpaka siku ya wakati maalumu. إِلَى يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ
Qāla Rabbi Bimā 'Aghwaytanī La'uzayyinanna Lahum Al-'Arđi Wa La'ughwiyannahum 'Ajma`īna 39. Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote, قَالَ رَبِّ بِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمْ فِي الأَرْضِ وَلَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ
'Illā `Ibādaka Minhumu Al-Mukhlaşīna 40. Ila waja wako walio safika. إِلاَّ عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ
Qāla Hādhā Şirāţun `Alayya Mustaqīmun 41. Akasema: Hii Njia ya kujia kwangu Iliyo Nyooka. قَالَ هَذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيم ٌ
'Inna `Ibādī Laysa Laka `Alayhim Sulţānun 'Illā Mani Attaba`aka Mina Al-Ghāwīna 42. Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata. إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَان ٌ إِلاَّ مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ
Wa 'Inna Jahannama Lamaw`iduhum 'Ajma`īna 43. Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote. وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ
Lahā Sab`atu 'Abwābin Likulli Bābin Minhum Juz'un Maqsūmun 44. Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa. لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَاب ٍ لِكُلِّ بَاب ٍ مِنْهُمْ جُزْء ٌ مَقْسُوم ٌ
'Inna Al-Muttaqīna Fī Jannātin Wa `Uyūnin 45. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّات ٍ وَعُيُون ٍ
Adkhulūhā Bisalāmin 'Āminīna 46. (Wataambiwa:) Ingieni kwa salama na amani. ادْخُلُوهَا بِسَلاَم ٍ آمِنِينَ
Wa Naza`nā Mā Fī Şudūrihim Min Ghillin 'Ikhwānāan `Alá Sururin Mutaqābilīna 47. Na tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana. وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِمْ مِنْ غِلّ ٍ إِخْوَاناً عَلَى سُرُر ٍ مُتَقَابِلِينَ
Lā Yamassuhum Fīhā Naşabun Wa Mā Hum Minhā Bimukhrajīna 48. Humo hayatawagusa machofu, wala hawatatolewa humo. لاَ يَمَسُّهُمْ فِيهَا نَصَب ٌ وَمَا هُمْ مِنْهَا بِمُخْرَجِينَ
Nabbi' `Ibādī 'Annī 'Anā Al-Ghafūru Ar-Raĥīmu 49. Waambie waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. نَبِّئْ عِبَادِي أَنِّي أَنَا الْغَفُورُ الرَّحِيمُ
Wa 'Anna `Adhābī Huwa Al-`Adhābu Al-'Alīmu 50. Na kwamba adhabu yangu ndio adhabu iliyo chungu! وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ الْعَذَابُ الأَلِيمُ
Wa Nabbi'hum `An Đayfi 'Ibrāhīma 51. Na uwape khabari za wageni wa Ibrahim. وَنَبِّئْهُمْ عَنْ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ
'Idh Dakhalū `Alayhi Faqālū Salāmāan Qāla 'Innā Minkum Wajilūna 52. Walipo ingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunakuogopeni. إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلاَما ً قَالَ إِنَّا مِنْكُمْ وَجِلُونَ
Qālū Lā Tawjal 'Innā Nubashshiruka Bighulāmin `Alīmin 53. Wakasema: Usiogope. Sisi tunakubashiria kijana mwenye ujuzi. قَالُوا لاَ تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلاَمٍ عَلِيم ٍ
Qāla 'Abashshartumūnī `Alá 'An Massaniya Al-Kibaru Fabima Tubashshirūna 54. Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanibashiria? قَالَ أَبَشَّرْتُمُونِي عَلَى أَنْ مَسَّنِيَ الْكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ
Qālū Bashsharnāka Bil-Ĥaqqi Falā Takun Mina Al-Qāniţīna 55. Wakasema: Tunakubashiria kwa haki; basi usiwe miongoni mwa wanao kata tamaa. قَالُوا بَشَّرْنَاكَ بِالْحَقِّ فَلاَ تَكُنْ مِنَ الْقَانِطِينَ
Qāla Wa Man Yaqnaţu Min Raĥmati Rabbihi 'Illā Ađ-Đāllūna 56. Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi ila wale walio potea? قَالَ وَمَنْ يَقْنَطُ مِنْ رَحْمَةِ رَبِّهِ~ِ إِلاَّ الضَّالُّونَ
Qāla Famā Khaţbukum 'Ayyuhā Al-Mursalūna 57. Akasema: Hebu nini amri yenu, enyi wajumbe? قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ
Qālū 'Innā 'Ursilnā 'Ilá Qawmin Mujrimīna 58. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wakosefu! قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَى قَوْم ٍ مُجْرِمِينَ
'Illā 'Āla Lūţin 'Innā Lamunajjūhum 'Ajma`īna 59. Isipo kuwa walio mfuata Luut'i. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote. إِلاَّ آلَ لُوط ٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ
'Illā Amra'atahu Qaddarnā 'Innahā Lamina Al-Ghābirīna 60. Ila mkewe. Tunakadiria huyo atakuwa miongoni watao bakia nyuma. إِلاَّ امْرَأَتَه ُُ قَدَّرْنَا إِنَّهَا لَمِنَ الْغَابِرِينَ
Falammā Jā'a 'Āla Lūţin Al-Mursalūna 61. Basi wale wajumbe walipo fika kwa Luut'i, فَلَمَّا جَاءَ آلَ لُوط ٍ الْمُرْسَلُونَ
Qāla 'Innakum Qawmun Munkarūna 62. Alisema (Luut'i): Hakika nyinyi ni watu msio juulikana. قَالَ إِنَّكُمْ قَوْم ٌ مُنْكَرُونَ
Qālū Bal Ji'nāka Bimā Kānū Fīhi Yamtarūna 63. Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyo kuwa wakiyafanyia shaka. قَالُوا بَلْ جِئْنَاكَ بِمَا كَانُوا فِيه ِِ يَمْتَرُونَ
Wa 'Ataynāka Bil-Ĥaqqi Wa 'Innā Laşādiqūna 64. Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi tunasema kweli. وَأَتَيْنَاكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ
Fa'asri Bi'ahlika Biqiţ`in Mina Al-Layli Wa Attabi` 'Adbārahum Wa Lā Yaltafit Minkum 'Aĥadun Wa Amđū Ĥaythu Tu'umarūna 65. Basi ondoka na ahli zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao, wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende mnapo amrishwa. فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْع ٍ مِنَ اللَّيْلِ وَاتَّبِعْ أَدْبَارَهُمْ وَلاَ يَلْتَفِتْ مِنْكُمْ أَحَد ٌ وَامْضُوا حَيْثُ تُؤْمَرُونَ
Wa Qađaynā 'Ilayhi Dhālika Al-'Amra 'Anna Dābira Hā'uulā' Maqţū`un Muşbiĥīna 66. Na tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa kesha katiliwa mbali. وَقَضَيْنَا إِلَيْهِ ذَلِكَ الأَمْرَ أَنَّ دَابِرَ هَاؤُلاَء مَقْطُوع ٌ مُصْبِحِينَ
Wa Jā'a 'Ahlu Al-Madīnati Yastabshirūna 67. Na wakaja watu wa mji ule nao furahani. وَجَاءَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ يَسْتَبْشِرُونَ
Qāla 'Inna Hā'uulā' Đayfī Falā Tafđaĥūni 68. Akasema: Hakika hawa wageni wangu, basi msinifedheheshe. قَالَ إِنَّ هَاؤُلاَء ضَيْفِي فَلاَ تَفْضَحُونِ
Wa Attaqū Allāha Wa Lā Tukhzūni 69. Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi. وَاتَّقُوا اللَّهَ وَلاَ تُخْزُونِ
Qālū 'Awalam Nanhaka `Ani Al-`Ālamīna 70. Wakasema: Sisi hatukukukataza usimkaribishe yeyote? قَالُوا أَوَلَمْ نَنْهَكَ عَنِ الْعَالَمِينَ
Qāla Hā'uulā' Banātī 'In Kuntum Fā`ilīna 71. Akasema: Hawa binti zangu, ikiwa nyinyi ni watendaji. قَالَ هَاؤُلاَء بَنَاتِي إِنْ كُنْتُمْ فَاعِلِينَ
La`amruka 'Innahum Lafī Sakratihim Ya`mahūna 72. Naapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo. لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ
Fa'akhadhat/humu Aş-Şayĥatu Mushriqīna 73. Ukelele ukawatwaa wakipambaukiwa. فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُشْرِقِينَ
Faja`alnā `Āliyahā Sāfilahā Wa 'Amţarnā `Alayhim Ĥijāratan Min Sijjīlin 74. Na tukaigeuza nchi juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa Motoni. فَجَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِمْ حِجَارَة ً مِنْ سِجِّيل ٍ
'Inna Fī Dhālika La'āyātin Lilmutawassimīna 75. Hakika katika hayo zipo ishara kwa waaguzi. إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَات ٍ لِلْمُتَوَسِّمِينَ
Wa 'Innahā Labisabīlin Muqīmin 76. Na miji hii ipo kwenye njia inayo pitiwa. وَإِنَّهَا لَبِسَبِيل ٍ مُقِيم ٍ
'Inna Fī Dhālika La'āyatan Lilmu'uminīna 77. Hakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini. إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَة ً لِلْمُؤْمِنِينَ
Wa 'In Kāna 'Aşĥābu Al-'Aykati Lažālimīna 78. Na hakika watu wa Kichakani walikuwa wenye kudhulumu. وَإِنْ كَانَ أَصْحَابُ الأَيْكَةِ لَظَالِمِينَ
ntaqamnā Minhum Wa 'Innahumā Labi'imāmin Mubīnin 79. Kwa hivyo tukawaadhibu. Na nchi mbili hizi ziko kwenye njia ilio wazi. فَانْتَقَمْنَا مِنْهُمْ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَام ٍ مُبِين ٍ
Wa Laqad Kadhdhaba 'Aşĥābu Al-Ĥijri Al-Mursalīna 80. Na bila ya shaka wakaazi wa Hijr waliwakanusha Mitume. وَلَقَدْ كَذَّبَ أَصْحَابُ الْحِجْرِ الْمُرْسَلِينَ
Wa 'Ātaynāhum 'Āyātinā Fakānū `Anhā Mu`rīna 81. Na tuliwapa ishara zetu, nao wakazipuuza. وَآتَيْنَاهُمْ آيَاتِنَا فَكَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ
Wa Kānū Yanĥitūna Mina Al-Jibāli Buyūtāan 'Āminīna 82. Nao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani. وَكَانُوا يَنْحِتُونَ مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتا ً آمِنِينَ
Fa'akhadhat/humu Aş-Şayĥatu Muşbiĥīna 83. Basi ukelele ukawatwaa asubuhi. فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُصْبِحِينَ
Famā 'Aghná `Anhum Mā Kānū Yaksibūna 84. Hayakuwafaa waliyo kuwa wakiyachuma. فَمَا أَغْنَى عَنْهُمْ مَا كَانُوا يَكْسِبُونَ
Wa Mā Khalaq As-Samāwāti Wa Al-'Arđa Wa Mā Baynahumā 'Illā Bil-Ĥaqqi Wa 'Inna As-Sā`ata La'ātiyatun Fāşfaĥi Aş-Şafĥa Al-Jamīla 85. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ila kwa ajili ya Haki. Na hakika Kiyama kitafika. Basi samehe msamaha mzuri. وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلاَّ بِالْحَقِّ وَإِنَّ السَّاعَةَ لَآتِيَة ٌ فَاصْفَحِ الصَّفْحَ الْجَمِيلَ
'Inna Rabbaka Huwa Al-Khallāqu Al-`Alīmu 86. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji Mjuzi. إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْخَلاَّقُ الْعَلِيمُ
Wa Laqad 'Ātaynāka Sab`āan Mina Al-Mathānī Wa Al-Qur'āna Al-`Ažīma 87. Na tumekupa Aya saba zinazo somwa mara kwa mara, na Qur'ani Tukufu. وَلَقَدْ آتَيْنَاكَ سَبْعا ً مِنَ الْمَثَانِي وَالْقُرْآنَ الْعَظِيمَ
Lā Tamuddanna `Aynayka 'Ilá Mā Matta`nā Bihi 'Azwājāan Minhum Wa Lā Taĥzan `Alayhim Wa Akhfiđ Janāĥaka Lilmu'uminīna 88. Usivitumbulie macho yako vitu tulivyo waneemesha makundi fulani kati yao, wala usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini. لاَ تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَى مَا مَتَّعْنَا بِهِ~ِ أَزْوَاجا ً مِنْهُمْ وَلاَ تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ
Wa Qul 'Innī 'Anā An-Nadhīru Al-Mubīnu 89. Na sema: Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha. وَقُلْ إِنِّي أَنَا النَّذِيرُ الْمُبِينُ
Kamā 'Anzalnā `Alá Al-Muqtasimīna 90. Kama hivyo tuliwateremshia walio gawa, كَمَا أَنْزَلْنَا عَلَى الْمُقْتَسِمِينَ
Al-Ladhīna Ja`alū Al-Qur'āna `Iđīna 91. Ambao wakaifanya Qur'ani vipande vipande. الَّذِينَ جَعَلُوا الْقُرْآنَ عِضِينَ
Fawarabbika Lanas'alannahum 'Ajma`īna 92. Basi Naapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawahoji wote, فَوَرَبِّكَ لَنَسْأَلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ
`Ammā Kānū Ya`malūna 93. Kwa waliyo kuwa wakiyatenda. عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Fāşda` Bimā Tu'umaru Wa 'A`riđ `Ani Al-Mushrikīna 94. Basi wewe yatangaze uliyo amrishwa, na jitenge na washirikina. فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ
'Innā Kafaynāka Al-Mustahzi'īna 95. Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanao kejeli. إِنَّا كَفَيْنَاكَ الْمُسْتَهْزِئِينَ
Al-Ladhīna Yaj`alūna Ma`a Allāhi 'Ilahāan 'Ākhara Fasawfa Ya`lamūna 96. Hao wanao fanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu yupo mungu mwingine. Basi, watakuja jua! الَّذِينَ يَجْعَلُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَها ً آخَرَ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
Wa Laqad Na`lamu 'Annaka Yađīqu Şadruka Bimā Yaqūlūna 97. Na Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo. وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدْرُكَ بِمَا يَقُولُونَ
Fasabbiĥ Biĥamdi Rabbika Wa Kun Mina As-Sājidīna 98. Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanao msujudia. فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُنْ مِنَ السَّاجِدِينَ
Wa A`bud Rabbaka Ĥattá Ya'tiyaka Al-Yaqīnu 99. Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini. *   وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّى يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ
Next Sūrah