31. Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni
Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha walio kufuru,
wapate kuwa na yakini walio pewa Kitabu, na wazidi Imani wale walio amini,
wala wasiwe na shaka walio pewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye
maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa
mfano huu? Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na
humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anaye jua majeshi ya Mola wako Mlezi
ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu.
|