20. Hakika Mola wako Mlezi anajua ya kuwa hakika
wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi
yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Mwenyezi Mungu
ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu,
basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur'ani. Anajua
ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi
wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia
ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na mshike Sala,
na toeni Zaka, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema. Na kheri yoyote
mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa
bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu.
Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
*
|