4. Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim
na wale walio kuwa pamoja naye, walipo waambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga
nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; na
umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini
Mwenyezi Mungu peke yake. Isipo kuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake:
Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele
ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea,
na kwako ndio marejeo.
|