22. Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu
na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume
wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao.
Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo
kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa
daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi,
Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa.
*
|