29. Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio
pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao.
Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi
Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio
mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio
toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu
ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao
makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika
wao msamaha na ujira mkubwa.
*
|