Sayaqūlu Laka Al-Mukhallafūna Mina Al-'A`rābi Shaghalatnā 'Amwālunā Wa 'Ahlūnā Fāstaghfir Lanā Yaqūlūna Bi'alsinatihim Mā Laysa Fī Qulūbihim Qul Faman Yamliku Lakum Mina Allāhi Shay'āan 'In 'Arāda Bikum Đarrāan 'Aw 'Arāda Bikum Naf`āan Bal Kāna Allāhu Bimā Ta`malūna Khabīrāan (Al-Fatĥ: 11). |
11. Watakuambia mabedui walio baki nyuma: Yametushughulisha mali yetu na ahali zetu, basi tuombee msamaha. Wanasema kwa ndimi zao yasiyo kuwamo katika nyoyo zao. Sema: Ni nani awezaye kukusaidieni chochote kwa Mwenyezi Mungu akitaka Yeye kukudhuruni au akitaka kukunufaisheni? Bali Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. |