Allāhu Yatawaffaá Al-'Anfusa Ĥīna Mawtihā Wa A-Atī Lam Tamut Fī Manāmihā Fayumsiku Allatī Qađaá `Alayhā Al-Mawta Wa Yursilu Al-'Ukhraá 'Ilaá 'Ajalin Musamman 'Inna Fī Dhālika L'āyātin Liqawmin Yatafakkarūna (Az-Zumar: 42). |
42. MWENYEZI MUNGU huzipokea roho zinapo kufa. Na zile zisio kufa wakati wa kulala kwake, huzishika zilizo hukumiwa kufa, na huzirudisha nyengine mpaka ufike wakati uliowekwa. Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri. |