|
50. Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako ulio
wapa mahari yao, na ulio wamiliki kwa mkono wako wa kulia katika alio kupa
Mwenyezi Mungu, na mabinti ami zako, na mabinti wa shangazi zako, na mabinti
wa wajomba zako, na mabinti wa dada za mama yako walio hama pamoja nawe;
na mwanamke Muumini akijitoa mwenyewe kwa Nabii, kama mwenyewe Nabii akitaka
kumwoa. Ni halali kwako wewe tu, si kwa Waumini wengine. Sisi tunajua tuliyo
wafaridhia wao katika wake zao na wanawake ilio wamiliki mikono yao ya
kulia. Ili isiwe dhiki kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye
kurehemu.
|