'Inna Al-Ladhī Farađa `Alayka Al-Qur'āna Larādduka 'Ilaá Ma`ādin Qul Rabbī 'A`lamu Man Jā'a Bil-Hudaá Wa Man Huwa Fī Đalālin Mubīnin (Al-Qaşaş: 85). |
| 85. Hakika aliye kulazimisha kuifuata Qur'ani hapana shaka atakurudisha pahala pa marejeo. Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuja na uwongofu, na nani aliyomo katika upotofu ulio dhaahiri. |