61. Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa
kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu nyinyi, mkila katika nyumba
zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za kaka
zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba za shangazi
zenu, au nyumba za wajomba zenu, au nyumba za dada wa mama zenu, au za
mlio washikia funguo zao, au rafiki yenu. Si vibaya kwenu mkila pamoja
au mbali mbali. Na mkiingia katika nyumba, toleaneni salamu, kuwa ni maamkio
yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu, yenye baraka na mema. Hivyo ndivyo Mwenyezi
Mungu anavyo kubainishieni Aya zake mpate kuelewa.
|