Yā 'Ayyuhā Al-Ladhīna 'Āmanū Liyasta'dhinkum Al-Ladhīna Malakat 'Aymānukum Wa Al-Ladhīna Lam Yablughū Al-Ĥuluma Minkum Thalātha Marrātin Min Qabli Şalāati Al-Fajri Wa Ĥīna Tađa`ūna Thiyā Bakum Mina Až-Žahīrati Wa Min Ba`di Şalāati Al-`Ishā'i Thalāthu `Awrātin Lakum Laysa `Alaykum Wa Lā `Alayhim Junāĥun Ba`dahunna Ţawwāfūna `Alaykum Ba`đukum `Alaá Ba`đin Kadhālika Yubayyinu Allāhu Lakum Al-'Āyāti Wa Allāhu `Alīmun Ĥakīmun (An-Nūr: 58). |
58. Enyi mlio amini! Nawakutakeni idhini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaalighi miongoni mwenu mara tatu - kabla ya Sala ya alfajiri, na wakati mnapo vua nguo zenu adhuhuri, na baada ya Sala ya isha. Hizi ni nyakati tatu za faragha kwenu. Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kuelezeni Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. |