35. Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi.
Mfano wa Nuru yake ni kama shubaka lenye kuwekwa ndani yake taa. Taa ile
imo katika tungi. Tungi lile ni kama nyota inayo meremeta, inayo washwa
kwa mafuta yanayo toka katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wa mashariki
wala magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung'aa wenyewe ingawa moto haujayagusa
- Nuru juu ya Nuru. Mwenyezi Mungu humwongoa kwenye Nuru yake amtakaye.
Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua
kila kitu.
|