5. Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa
basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na
manii, kisha kutokana na kipande cha damu ilio gandana, kisha kutokana
na kipande cha nyama chenye umbo na kisicho kuwa na umbo, ili tukubainishieni.
Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio
wekwa. Kisha tunakutoeni kwa hali ya mtoto mchanga, kisha mfikie kutimia
akili. Na wapo katika nyinyi wanao kufa, na wapo katika nyinyi wanao rudishwa
kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijua.
Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake
husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri.
|