Wa Allāhu Fađđala Ba`đakum `Alaá Ba`đin Fī Ar-Rizqi Famā Al-Ladhīna Fuđđilū Birāddī Rizqihim `Alaá Mā Malakat 'Aymānuhum Fahum Fīhi Sawā'un 'Afabini`mati Allāhi Yajĥadūna (An-Naĥl: 71). |
71. Na Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki. Na wale walio fadhilishwa hawarudishi riziki zao kwa wale ilio wamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika riziki hiyo. Basi je, wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu? |