Wa 'In Ta`jab Fa`ajabun Qawluhum 'A'idhā Kunnā Turābāan 'A'innā Lafī Khalqin Jadīdin 'Ūlā'ika Al-Ladhīna Kafarū Birabbihim Wa 'Ūlā'ika Al-'Aghlālu Fī 'A`nāqihim Wa 'Ūlā'ika 'Aşĥābu An-Nāri Hum Fīhā Khālidūna (Ar-Ra`d: 5). |
5. Na kama ukistaajabu, basi cha ajabu zaidi ni huo usemi wao: Ati tukisha kuwa mchanga kweli tutakuwa katika umbo jipya? Hao ndio walio mkufuru Mola wao Mlezi. Na hao ndio watao kuwa na makongwa shingoni mwao, na hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu. |