Wa Jā'ahu Qawmuhu Yuhra`ūna 'Ilayhi Wa Min Qablu Kānū Ya`malūna As-Sayyi'āti Qāla Yā Qawmi Hā'uulā' Banātī Hunna 'Aţharu Lakum Fa Attaqū Allāha Wa Lā Tukhzūnī Fī Đayfī 'Alaysa Minkum Rajulun Rashīdun (Hūd: 78). |
78. Wakamjia kaumu yake mbio mbio. Na kabla ya haya walikuwa wakitenda maovu. Yeye akasema: Enyi watu wangu! Hawa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi mbele ya wageni wangu. Hivyo, hamna hata mtu mmoja miongoni mwenu aliye ongoka? |