Falawlā Kānat Qaryatun 'Āmanat Fanafa`ahā 'Īmānuhā 'Illā Qawma Yūnis Lammā 'Āmanū Kashafnā `Anhum `Adhāba Al-Khizyi Fī Al-Ĥayāati Ad-Dunyā Wa Matta`nāhum 'Ilaá Ĥīnin (Yūnis: 98). |
| 98. Kwa nini usiwepo mji mmoja ukaamini na Imani yake ikawafaa - isipo kuwa kaumu Yunus? Waliamini na Sisi tukawaondolea adhabu ya hizaya katika maisha ya dunia, na tukawastarehesha kwa muda. |