Wa Mimman Ĥawlakum Mina Al-'A`rābi Munāfiqūna Wa Min 'Ahli Al-Madīnati Maradū `Alaá An-Nifāqi Lā Ta`lamuhum Naĥnu Na`lamuhum Sanu`adhdhibuhum Marratayni Thumma Yuraddūna 'Ilaá `Adhābin `Ažīmin (At-Tawbah: 101). |
| 101. Na katika mabedui walio jirani zenu wamo wanaafiki; na katika wenyeji wa Madina pia wapo walio bobea katika unaafiki. Wewe huwajui. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa. |