Wa 'Adhānun Mina Allāhi Wa Rasūlihi 'Ilaá An-Nāsi Yawma Al-Ĥajji Al-'Akbari 'Anna Allāha Barī'un Mina Al-Mushrikīna Wa Rasūluhu Fa'in Tubtum Fahuwa Khayrun Lakum Wa 'In Tawallaytum Fā`lamū 'Annakum Ghayru Mu`jizī Allāhi Wa Bashshiri Al-Ladhīna Kafarū Bi`adhābin 'Alīmin (At-Tawbah: 3). |
3. Na ni tangazo kutokana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawana jukumu lolote kwa washirikina. Basi mkitubu itakuwa kheri kwenu, na mkigeuka basi jueni kuwa nyinyi hamumshindi Mwenyezi Mungu. Na wabashirie makafiri kuwa watapata adhabu chungu. |