Wa 'Idh Zayyana Lahum Ash-Shayţānu 'A`mālahum Wa Qāla Lā Ghāliba Lakum Al-Yawma Mina An-Nāsi Wa 'Innī Jārun Lakum Falammā Tarā'ati Al-Fi'atāni Nakaşa `Alaá `Aqibayhi Wa Qāla 'Innī Barī'un Minkum 'Innī 'Araá Mā Lā Tarawna 'Innī 'Akhāfu Allāha Wa Allāhu Shadīdu Al-`Iqābi (Al-'Anfāl: 48). |
48. Na pale Shet'ani alipo wapambia vitendo vyao, na akawaambia: Hapana watu wa kukushindeni hii leo, na hali mimi ni mlinzi wenu. Yalipo onana majeshi mawili, akarudi nyuma, na akasema: Mimi si pamoja nanyi. Mimi naona msiyo yaona. Mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu. |