Wa Akhtāra Mūsaá Qawmahu Sab`īna Rajulāan Limīqātinā Falammā 'Akhadhat/hum Ar-Rajfatu Qāla Rabbi Law Shi'ta 'Ahlaktahum Min Qablu Wa 'Īyāya 'Atuhlikunā Bimā Fa`ala As-Sufahā'u Minnā 'In Hiya 'Illā Fitnatuka Tuđillu Bihā Man Tashā'u Wa Tahdī Man Tashā'u 'Anta Walīyunā Fāghfir Lanā Wa Arĥamnā Wa 'Anta Khayru Al-Ghāfirīna (Al-'A`rāf: 155). |
155. Na Musa akawateuwa watu sabiini katika kaumu yake kwa miadi yetu. Na ulipo fika mtetemeko mkubwa alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ungeli taka ungeli wahiliki wao na mimi zamani! Unatuhiliki kwa waliyo yafanya wajinga katika sisi? Haya si chochote ila ni mtihani wako, umpoteze umtakaye na umhidi umtakaye. Wewe ndiye Rafiki Mlinzi wetu. Basi tughufirie na uturehemu. Na Wewe ndiye mbora wa kughufiria. |