Wa Naza`nā Mā Fī Şudūrihim Min Ghillin Tajrī Min Taĥtihim Al-'Anhāru Wa Qālū Al-Ĥamdu Lillāhi Al-Ladhī Hadānā Lihadhā Wa Mā Kunnā Linahtadiya Lawlā 'An Hadānā Allāhu Laqad Jā'at Rusulu Rabbinā Bil-Ĥaqqi Wa Nūdū 'An Tilkum Al-Jannatu 'Ūrithtumūhā Bimā Kuntum Ta`malūna (Al-'A`rāf: 43). |
43. Na tutaondoa chuki vifuani mwao, na mbele yao iwe inapita mito. Na watasema: Alhamdulillah! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye aliye tuhidi kufikia haya. Wala hatukuwa wenye kuhidika wenyewe ingeli kuwa Mwenyezi Mungu hakutuhidi. Hakika Mitume wa Mola wetu Mlezi walileta Haki. Na watanadiwa kwamba: Hiyo ndiyo Pepo mliyo rithishwa kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyafanya. |